Shaaban Robert Katabasamu

Shaaban Robert Katabasamu

Siku kadhaa zimepita tangu niandike barua kwa marehemu nguli wa Kiswahili na mtunzi wa mashairi Sheikh Shaabani Robert, Usiku naweweseka nashtuka nakiona kivuli cha  Shaaban Robet, kinanikabidhi Barua, kisha kinatoweka machoni mwangu , napigwa na butwaa, nakurupuka kana kwamba nimemwagiwa maji ya baridi naikimbilia taa naiwasha , mkononi  mwangu nauona  waraka ule wa barua niliyokabidhiwa, moyo unaenda mbio, macho yanakimbilia kusoma kilichoandikwa!
Maneo ya juu kabisa yameandikwa.

Shaaban Robert Katabasamu!

Naongeza umakini kusoma zaidi….

iliandikwa hiviii.

Asante sana, kilembwe changu, yumkini baadhi ya kizazi chenu chatambua niliwahi kuwapo duniani basi  najifaghiri sana huku nilipo.

Barua yako nimeipokea, ingawa hukuipa jina barua ile ila nikaona nisifanye kosa kama ulilofanya wewe  yakwangu mie nimeipa jina hilo hapo juu, Shaaban Katabasamu.

Kwa hakika umenifanya nitabasamuj kwa mara ya kwanza tangu kufariki kwangu, mwanzoni nilivyoanza kupigania lugha yangu nilianza kwa masikhara lakini baadae nikaona yapasa nigangamare ili niipatie heshima lugha hiyo, mchango wangu  nilikuja utambua dakika za mwisho kabisa za uhai wangu, lakini sikuwa na namna yakukwepa rungu la kifo ambalo liliishukia roho yangu.

Mauti yakanikabili kwa mabavu yake, nikawa mpole nikinyoosha mikono juu kusalimu amri, tangu hapo nilitaraji kuwapo hata na maadhimisho ya heshima kwa sisi wapigania hadhi ya lugha hiyo, lakini sikuwahi sikia, angalau barua yako imenifanya nitabasamu sababu mchango wangu umekuja kuenziwa nawe ambaye jina langu limekufikia kwa historia tu, naamini labda utakatifu huo utawashukia na vizazi vyako,pamoja na wenye mamlaka serikalini!

Tabasamu langu lanena maneno ya aina tatu, aina ya kwanza ni furaha yakupokea barua yako kilembwe changu, aina ya pili ya tabasamu hili ni  huzuni kuu itoakanayo na habari ulizo nipa kuhusu Fasihi simulizi ilivyo kwa sasa huko duniani, ama hakika ni pigo kwangu tena pigo takatifu kusikia hii leo duniani hatupo sisi wakina Shaaban Robert tena, zaidi ule mziki wa kina Bi Siti haupo tena, kimekumbwa na lana gani kizazi chenu Masikini! Haya huo mziki wakuruka nakuvua mashati ndio mziki wa aina gani mbona ni khabari ngeni hizi . Tena sio ngeni hivi hivi ni ngeni zakushangaza.

Ashaakum si matusi Uvaaji wenu huo wakushusha suruali chini ya makalio,  nimeustaajabia mara dufu, Karima awaponye yasije yakawakuta yalowakuta kizazi cha Nuhu,
Tabasamu langu hili lanena pia kuhusu sononeko langu la kazi zangu na wanagenzi wenzangu kuthaminiwa kwa mwendo wa kinyonga, lakini usitie shaka katika hilo, Kusahau ni sifa kuu ya binaadamu dhaifu, na ndio mana hakamiliki kuumbwa kabla hajafa! Ulizo nazo zitunze ni hadhina kwako na kwa wale watakaosadiki misemo yetu ya kwamba vyakale ni dhahabu,

Nimeona tamaa yako yakutaka kujua kinachoendela katika nchi yakusadikika, vizuri sana.
Nchi yakusadikika hii leo angalau imepata kiongozi thabiti,anadhibiti kweli mianya ya rushwa hatoi hata upenyo kwa mtumishi wa uma kukaa kizembe, anahimiza kazi, anajenga uzalendo na anafuata sheria kwa maana nchi ile ilishapoteza kabisa nidhamu yakiungozi. Usitie shaka ipo siku utafika nchini mule kwa maana hata wageni wanaweza kuingia hivi sasa bila kupata shida sababu, miundombinu inaendelea kuimarishwa hasa ya usafiri, kuna magari mareefu hivi sasa yanaingia abiria wengi.
Nakumbuka Niliacha Hati duniani, hati muktasi  kwa mabinti, nakumbuka ulikuwa ni wasia wangu mzuri kwao, hakikisha unaipata hati ile itakusaidia hata kumnyoosha mchumba wako kimaadili,
Zilikuwa beti 100, nitarejea chache  tu hapa,
Taabu zikikukuta waweza nazo kuteta, njia yakupita lazima zitakwachia.
Lakini zikikuona huwezi nazo pigana,zitakusumbua sana, hati hii yafunua
Tia katikamoyo nia ya maendeleo hati hii ni cheo kushinda ovu andaa.
Usishiriki hongo,ijara upate hongo, mtu muongo ni msungo, masuto mengi hupewa,
Jambo usiloliona haifai kunongona, hiyo ndio fitina mngwana ya kujitoa.
Hujaniambia katika barua ulonitumia nani hasa amevaa viatu vyangu katika utenzi wa mashairi, nilipenda sana mashairi, yalinimaliza hasira iliponikaribia na yalinipa burudani kila nilipoyasikia,
asante sana kwa kuukumbuka uwepo wangu, Ipokee barua hii Kilembwe changu,  nitahakikisha unapata Baraka zangu, ili uendelee kupigania lugha yangu, vitunze na uvisome vitabu vyangu angalau utaipata akili yangu. Na ukipata nafasi tembelea kaburi langu, watafute waliyo na chembe za damu yangu, na usisite kuwapa salamu zangu……
Ni mimi Mwanagenzi Shaaban Robert, Angali bado uhai usisite kutenda mema, maana Wema hauozi, hudumu huko duniani na huku nilipo akhera,
Wasalaam kilembwe changu Omar Zongo…
Namaliza kusoma barua hiyo Jasho lanitoka, napatwa na woga ghafla barua hiyo yatoweka mikononi mwangu, nashtuka usingizini loh kumbe nilikuwa ndotoni

…..ama hakika Mungu Ailaze roho yako mahala pema peponi Shaaban Robert, aamin.


Mafanikio Yatabaki Kwao!

Nafsi za wazee wao zinacheka kicheko cha majivuno, wanajivunia sana kuacha vizazi  ambavyo vinaenzi uwepo wao, sura za wazee wao zimepambwa na tabasamu wanagonga  glasi zao za mvinyo kwa furaha na hawaachi kubariki harakati za damu zao zinazoendelea kupumua na kuitumia hii hewa ya bure kabisa ambayo Mungu aliamua ujira wake uwe ni kumcha yeye tu. kwa hakika mafanikio lazima yawe kwao.

hata kama ugumu upo wakuyafikia mafanikio lakini kwao ugumu unageuka kuwa ulaini, ulaini ambao unatokana na furaha na amani ya wazazi wao kutokana na kuenziwa kwa juhudi zote nakutangazwa kwa michango yao katika historia ya waliopo sasa na hata wa kesho, lazima wafanikiwe.

najua busara zi pamoja nawe na ndio mana unasadiki kuwa mafanikio yataendelea kuwa kwao sababu hata makazi ya wazazi wao ya milele bado yangali na thamani na wanayaenzi kwa marefu na mapana, sasa kuna kipi kinaweza fanya laana ya umasikini iwe kwao! nasisitiza ni lazima wafanikiwe!

tutaendelea kutamani kutibiwa kwao, kula vyakula wanavyokula wao, kuishi nyumba kama zao na hata tamaduni zao kwetu zitakuwa lulu sababu zetu zimeshasuswa na baraka za wazazi wetu, mababu zetu ambao waliihifadhi heshima yetu mahala wakitaraji tuitafute kwa kuienzi nakuwatunuku joho la heshima katika ukamilifu wote wa maisha yetu, lakini haya ya wapi? ni kinyume na uhalisia wenyewe, kazi zao, damu zao na hata michango yao imepuuzwa huku harakati zikiwa kutafuta maendeleo ya kiuchumi.

hakika haya ni mastaajabio yangu bin Zongo, mastaajabio makuu katika muda wangu huu wa pumzi iliyo hai, mastaajabio ya mafanikio bila baraka za wazazi wetu, wazee wetu na waliowahi kuweka nakshi katika haya tunayojivunia hii leo!

ni nani asiyesadiki ya wahenga waliotukuka kwa misemo na tafakari zakuona mbali ambao walipata muda nakunena kwamba Vyakale Dhahabu, ni nani? jibu ni sisi tuloikuta hii dunia kisha tukawa mbio, tukaharakatia matumbo yetu na vizazi vyetu huku tukisahau utu wa wazee wetu, waliokuwa na michango kwenye tamaduni zetu, nchi yetu na kila kitu kutuhusu
 Sehemu ya kumbukumbu ya mwanafasihi Wilium Shakespear

Natafakari kwa kina huku nafsi ikilalama naliona tabasamu la maridhio lililo usoni mwa aliyekuwa nguli wa mashairi na mtunzi wa vitabu wa uingereza WILLIUM SHAKESPEAR, naliona kaburi lake linaloenziwa nakutunukiwa Mashada ya pongezi huku taswira chungu yenye sononeko nikiiona kwa Mwanagenzi aliyekuwa mashuhuri ukanda wa Afrika mashariki SHAABANI ROBERT huku kaburi lake likiona aibu kwa kutelekezwa kule Tanga ilhali kazi zake zikiendelea kudumisha utu na uelewa kwa vizazi vyoote tangu na baada ya kifo chake.

Mafanikio Yataendelea kuwa kwao, licha ya mapungufu mengine waliyonayo lakini katika hilo lazima vinara wawe wao! licha ya kwamba inaniuma lakini sitathubutu kusema Mungu wabariki wao na uzidi kutupa laana sie, sitathubutu na hata mdomo ukitaka kusema hivyo nitaukemea kwa sauti kuu na fikra zikianza kuwaza hilo nitazitenga kabisa, sababu nanua laana sio mbaya na daima nitaendelea kusema Mungu simamia imani zetu, tusiendelee kudharau ya wahenga wetu, tuwaenzi kwa yale yakwao yaliyojaa utu ili tuyaone mafanikio yetu.


Kuanzishwa, kuishi na kuanguka kwa Taifa Daladala!


Taifa lenye kila aina ya sifa lakuitwa taifa lenye maendeleo, ajabu haliishi mtu ndani yake, limeumbwa kwa mvuto wa hali ya juu, linavutia ndani na nje, kwa upande wa nje limechorwa maandishi makubwa mbele, maandishi yaliyonakshiwa kwa rangi za bendera ya tiafa hilo, maandishi hayo yanasomeka DALADALA.
Watu wawili wanaonekana wakishangaa uzuri wa taifa hilo, wanastaajabu kwanini taifa zuri kama hilo haliishi watu, wanalisogelea, wanalikagua mwisho wanaambizana
Daladala
            ''tunaweza kuwa viongozi wa taifa hili, tutawakusanya wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya dunia nakuwafanya wawe raia ambao wataishi ndani ya Taifa hili kwa kulipa kodi maalumu, inapoisha wanaachana na taifa letu tunatafuta raia wengine, hii itasaidia kuongoza nchi hii sababu ikitokea hata tunatakiwa tukarabati miundombinu na makaazi ya watu inakuwa ni rahisi kutumia kodi zao''

wanaweka mikakati, kanuni yakuendesha Taifa hilo, wanaridhika mmoja anajipa madaraka ya urais mwengine waziri mkuu, waziri mkuu anasimama mlangoni nakuanza kuita watu, huku aliyejipa cheo cha urais akikalia kiti chake cha enzi, mbele kabisa akizingatia usukani wake na namna atakavyoutumia kuongozea nchi ile, usukani unakuwa ndio katiba yake yakuongoza taifa lile liitwalo daladala.
shughuli yakuwapata raia, wananchi waje kulipia kodi kwenye taifa ile inakuwa ngumu kidogo, waziri mkuu mlangoni anatumia lugha nzuri, kuwalaghai wananchi waweze kuingia kwenye taifa hilo linalotembea. wengi wanahadaika nakuzama ndani kuwa raia halali kwa kulipa kodi zao.

Raia wanaanza kuingia wale wamwanzo, wanawahi makaazi yao na rafiki zao, wengine wanaochelewa wanakosa mahala pakukaa wanasimama kinyonge huku wakimtazama Rais wao wakikosa namna yakumwambia kuwa anawasaidiaje. waziri mkuu mlangoni anaonekana akiwanyanyasa vijana wadogo ambao wamevaa sare wakijitambulisha kuwa wao ni wanafunzi, anawaambia wanatosha hataki wengine.

vijana wale wanajipima nguvu zao na waziri yule aliye mlangoni wanabaini hawamuwezi hata kidogo kwani yeye amewazidi nguvu. kwa unyonge wanamuacha kwa siri kubwa laana ya wanafunzi wale inadokndoka kwenye taifa lile hasa rais wake na waziri wake, lakini wao hawajui wanaendelea kujaza watu...

sababu ya kuwakataa wanafunzi ni kwamba wametosha watu na hakuna nafasi nyengine lakini bado anaonekana akiwaita watu wengine waingie ndani ya Taifa lile, hajali namna ambavyo wamebanana mule ndani mpaka kelele zinaanza kusikika ndani ya taifa hilo HAKUNA NAFASI, JAMANI SITUMETOSHA... BASI SOGEA HUKO, JAMANI WE KAKA UNANIKANYAGA........DEREVA TWENDE.

Raisi wa taifa lile akiwa amekamata katiba yake hajali wala hageuki nyuma kuwatazama raia wake kazi hiyo kamuachia waziri wake ambaye sasa ameanza kuwa na lugha chafu  akiwatukana raia bila kujali aliwaita mwenyewe, rais yeye hasemi kitu lakini kichwanii mwake anajua kuwa taifa lake lina changamoto za sehemu za kukaa watu wakajinafasi bila kubanana na kukanyagana, kichwa chake kinarudi katika historia za mataifa mbalimbali yanayopiganis ardhi lakini hatilii maanani sana anaendelea kunyonganyonga katiba yake ikiwa kama ndio namna yakuendesha nchi ile masikio yake yanafuata sana muongozo kutoka kwa waziri wake, mara kadhaa akiambiwa waache hapo Anaruhusu taifa lile linalozunguka kutafuta abiria lisimame ili liwaache abiria waliokwisha lipa kodi ili kupandisha wengine ambao hawajalipa.

anawaza namna yakuboresha taifa lake ili angalau makaazi yawe mengi raia wake wasipate shida yakukanyagana lakini anakosa hivyo anaona kile anachokifanya waziri wake ni sahihi, bila kujua Masikini ya Mungu wamekusanya laana ya kwanza kutoka kwa wanafunzi ambao wanakosa namna yakufika shuleni kupata haki elimu sababu taifa lile halitaki wanafunzi kisa wanalipa kodi ndogo.

Hapa rais wa taifa hili DALADALA hafikirii kuwa wale ndio marais wa kesho wa kuongoza taifa lile lakini pia wataweza kutumika kubuni mataifa mengine yenye eneo kubwa ambalo raia hawatapata shida kukanyagana nakugombea makaazi kwa kutumia elimu zao.
waziri mkuu mwenye kiburi anawatukana kina mama wafanyabiashara wenye mizigo yao anawaambia kwa kejeli ''hakuna nafasi ya mizigo hiyo''.

kina mama wajasiriamali wengine wajane waume zao wamefariki wanakosa namna yakufanya wanazidi kuchelewa kufika waendako, taifa lile limewakataa, wanazidi kusubiria hifadhi kutoka kwenye taifa lenye waziri mkuu mwenye imani ambalo ni nadra sana kutokea.

ndani ya taifa hili ambalo raia wanachaguliwa mlangoni na waziri mkuu, kuna watu wa ajabu mno, wao wanajiita staff..watu ambao wana ukaribu na rais, wamepata makao huku wazee watu wazima wakiwa wamening'inia, nakukanyagwa bila huruma. hakuna anaewajali taifa linaangalia kodi tu!
hewa nzito, watu ni wengi wapo wajawazito ambao hawapewi haki zao, waziri mkuu bila huruma anachangisha kodi zake huku akiwaambia sogea huko nipite.

Laana inazidi kulikumba taifa hili, laana kutoka kwa wamama watu wazima, watoto, na wazee ambao walihitaji wapishwe kukaa ikibidi hata waishi bure mule lakini matokeo yake wananufaika wachache tu kisa wanajuana na mwenye nchi, mara kadhaa wana usalama wa kimataifa walipojaribu kuisimamisha nakuiwekea vikwazo kwa kufuatilia uhalali na haki pamoja usalama wa wananchi katika nchi hiyo daladala waliambulia kuzungumza kwa siri kubwa na waziri mkuu, halafu hakuna hatua zinazochukuliwa, udhalimu unaendelea, huku sasa jasho la mbanano

likifukuta, na taratibu hofu ya maradhi ya mlipuko kwa kuambukizana ikiianza kutanda miongoni mwa wananchi wa taifa lile.

Daladala
Maisha ndani ya taifa hili lenye waziri mkuu aso na nidhamu yanazidi kuwa magumu kutokana na laana, ghafla kunaibuka mgogoro ndani ya Nchi, raia mmoja kalipa kodi yake waziri mkuu anasema hajalipa, wanajibizana machafuko yanatokea huku waziri mkuu akijinasibu kuwa anaweza kumshusha katika taifa lile, raia anasema nina haki yakuishi humu nakufika niendako sababu nimelipia kodi yangu,

Rais anaona kero vurugu zinazoibuka katika nchi yake anaamua kusimamisha shughuli ya uendeshaji nchi kwa kufuata katiba, raia wanashangaa kwanini Rais asimamishe Taifa lile lisitembee kufika waendako, wote wanadhani labda Mheshimiwa Rais  amekerwa na mivutano ndani ya taifa lake kumbe la hasa! anaonekana akimgeukia Waziri wake " Naomba Buku", rais anaomba pesa watu wote wananyamaza mzozo unasimama kwa muda, moja ya abiria anajisemea " pesa zetu hizi, sijui anaenda kununua nini'' sauti hii inasikika moyoni mwake tu, na hata hivyo anajisemea hivyo huku wazi akijua kuwa hana tena mamlaka na zile pesa sababu alilipia kuishi mule ndani nakufika aendako, waziri mkuu anamkabidhi rais wake noti ya shilingi elfu moja, rais kauzu hacheki hata kidogo, anashuka kukiacha kiti chake cha urais, raia mmoja anatamani kukikalia akiendeshe yeye lakini anahofia watu watamuona fisadi na mwizi.

laana zitokanazo na uonevu na ubabe wa waziri wake mkuu mtendaji wake langoni ndio zimempata hadi yeye, na pale aliamua kwenda kununua na  kunywa kinywaji cha laana Maarufu kwa jina la Kiroba, eti alijiambiza kuwa huenda akinywa kinywaji kile ndio hataona bughda yale makelele ya Wananchi wake.

Raia wake nyuma wanapiga kelele kila mmoja akidai anacheleweshwa kufika aendako. Dereva hajali anapotelea kwenye duka moja lililo pembezoni mwa ramani ya taifa lake. anatumia dakika saba dukani pale,anarudi akiwa ameshika chupa ya maji safi ndani inaonekana ni maji lakini ukweli sio huo, ile  ni pombe kali yenye rangi ya maji lakini ladha ya dawa chungu kama vile muarobaini,
anarudi anakaa kwenye kiti chake cha enzi anakamata tena katiba yake maarufu kwa jina la Usukani, anainyonga nyonga Taifa lile liitwalo Daladala linaanza kuondoka.

Laana  walioachiwa na wazee waliokosa kukirimiwa kwa kupishwa wakae linawakumba Dereva anaanza kuyumba yumba, Abiria wanaanza kupayukwa " hujabeba makopa humu ndani tafadhali bwana endesha taratibu".

Dereva haelewi taratibu kilevi kilishaanza kupenya kwenye mifupa yake ya fahamu, raia walio kaa jirani yake ndio wanagundua kuwa kiongozi wao yule anatumia kilevi, wana patwa na mashaka na uhai wao, hata uendeshaji wa Taifa lile umebadilika, Wanapitisha maamuzi ya busara. wanaambizana washuke.
mmoja anasimama anapaza sauti yake " jamani hawa wanacheza na akili zetu, daladala lenyewe konda hana ustaarabu, dereva wake ndio chizi kabisa amelewa, watoto wadogo kule amewakatalia kupanda wazee hawawathamini wananing'inia kwenye mabomba huku siti zikiwa zimekaliwa na mastaf wao, tushukeni atatuua huyu bwege!'"

Maneno haya yanapokelewa kwa hisia tofauti na raia wote, lakini wote wanaunga mkono hoja ile mwengine anasimama nakusema '' hatuwezi shuka hivihivi lazima waturudishie pesa zetu, wapumbavu hawa, la sivyo tuwapeleke mbele ya sheria,"

Daladala
Umoja huo wa abiria ndani ya Nchi ile Daladala unajenga hofu kwa Waziri mkuu Konda kama vile anashtuka kutoka usingizini, ghafla Daladala inasimama, konda anafungua mlango anataka kukimbia, abiria wanamkamata wanamvuta ndani, wanamshambulia wakitaka awarudishie pesa, wanamkalia kooni nakufanikiwa kumpokonya pesa zote,wale awananchi waliokuwa wakijita mastaf wanashindwa kutetea kutokana na umoja wa raia wale wenye hasira kali. zoezi la dakika chache tu wanafanikiwa kumpokonya pesa zote yule waziri mkuu, mjeuri.
wanashuka,kwenye gari wanabaki konda na Dereva wake na vijana wawili waliojiita mastaf, Konda anajikagua anagundua sare zake za uwaziri mkuu zimechanwa chanwa, akijikagua zaidi anagundua hakuachwa hata na shilingi hamsini, anamtazama Dereva wake, hana habari, anasinzia kutokana na viroba anavyoendelea kujidunga navyo.

"umeyataka wewe, ona sasa! tumetumia mafuta ya bure kuendeshea daladala, hatujarudisha kitu, wamechukua pesa zao, acha mimi niendeshe hii gari, wewe kaa mlangoni,"
 dereva hajielewi anakubaliana na hoja hiyo, huku akipepesuka anasoge mlangoni, yule waziri mkuu mjeuri, anakalia kiti cha kuendeshea taifa lile, sio mzoefu na masuala ya uongozi, anajipa moyo kwamba ataweza, anafanikiwa kuwasha gari, linawaka, anaanza safari, wanafanikiwa kutembea kidogo tu, abiria wanakataa kupanda gari linayumba muendeshaji sio mzoefu, konda amelewa hawaiti kistaarabu, Dereva ambaye alikuwa waziri mkuu anaamua kurudisha Daladala walipotoka lakini wakati akijaribu kukunja kona arudi alipotoka anakumbana uso kwa uso na gari kubwa, ajali isiyoesemeka, wanagongana uso kwa uso,  Daladala lao linaminywa hakuna anaefanikiwa kutoka mzima,

 wengi wanaoshuhudia ajali ile wanasema kosa lilikuwa kwa dereva hakustahuili kugeuzia pale kwa maana sio mahala pakugeuzia,

WEWE,


Sio kosa kukunyooshea kidole wewe hii leo, nakumbuka niliwahi kukemewa kumnyooshea kidole mtu yeyote ama awe mkubwa kwangu au mdogo lakini leo sitakiweka chini kidole hiki nitakinyoosha kwa uthabiti tena bila kutetereka , nakunyooshea wewe kidole hiki.

Sio fahari hata kidogo na huwezi sifiwa kwa tabia zako za ubinafsi, choyo na uzandiki, hufai kwa kulumangia wala kulia na kachumbari, ni wewe ndio nakuwambia, unajisikiaje kuishi kifahari kama mfalme ilihali waliokuzunguka ni dhalili, wamechoka na macho yao yanaongea shida na ufakiri uliowagubika.

 Eti wewe? Kwani wewe ni nani hasa katika hii dunia mpaka watoto wa wenzako uwageuze punda kwa kuwabebesha madawa yakulevya na kuuza utu wao? Eti wewe ni nani? Nani amekwambia kama dunia hii ni yakwako na kwamba una haki yakutesa wenzako sababu ya pesa?

Wewe

Kidole hiki kina beba mengi na labda tu nikwambie huwezi kukikata licha ya kwamba unamiliki kila aina ya ,kifaa cha kukatia utu wa wenzio na thamani zao, lakini kamwe kidole hiki hakitakatika hata ukithubu kukinyofoa bado kitaendelea kukutazama wewe na kukuuliza maswali haya tena uyajibu kwa ufasaha labda yupi limbukeni aliyothubutu kukuongopea kuwa wewe upo sahihi kutembea na wake za watu, watoto wadogo na kuwadhalilisha wenzio wanapojaribu kudai haki yao kwako,

Kwani wewe umeumbwaje labda mpaka ufikirie kuwa rushwa ni sahihi na uweze kuitumia kudhulumu haki ya mnyonge, tuambizane hapa nijue na pengine hata nihofie kukunyooshea kidole hiki kwani ni wapi hasa panaposema kuwa cheo chako ndio umungu mtu wako unaopaswa kuutumia kuumiza walio chini yako,
kidole changu hata ukitazame kwa chuki hakitasita wala kuona aibu kukukosoa kwa uyatendao, nani amesema mtu atapata radhi za wazazi asipofuata maadili mema ambayo wazazi wamemfunza, nani kakwambia kuwa uvivu, ulevi nakupenda starehe ndio ujana!
Hakizungumzi kidole unaoongea ni mdomo ila hiki kidole kinakuoneshea wewe ili ujue maneno yangu hayaatoki bure yanakulenga wewe, labda useme hapa nifahamu, ninani aliyewahi kuishi milele duniani hapa, hata pesa kama ulizo nazo haziwezi kukufanya uishi milele sasa kwanini usirudishe utu hata chakula unachomwaga uwagaie watoto wanaoshindia kipande kimoja cha mkate au wakati mwengine maji pekee, nani aliokwambia roho mbaya ndio mtaji wakujirimbikizia mali.

sitaacha kukunyooshea kidole wewe mpaka utakapoamua kubadilika nakuwa mwema, kuacha kumnyanyasa mkeo, wala kutelekeza familia, sitaacha kukunyooshea kidole mpaka utakapoamua kuacha kuvuta mihadarati, kunywa pombe nakutembea na wake za watu, sitaacha kamwe kukunyooshea kidole hiki mpaka pale utakapoamua kusaidia wazazi wako kijijini. kidole hiki hakitashuka chini mpaka pale utakapoona neno la busara nikuwaomba msamaha ulio wakosea nakuishi nao kwa utu!
wewe! wewe! wewe msanii unaedhani kipaji chako ni fursa yakupotosha jamii, sio kweli, simamia haki za wanyonge kemea, ufisadi na rushwa sababu wewe ni kioo cha jamii,
wewe Kiongozi unaejali tumbo lako, mimi mwenzio siogopi wala sitaogopa cheo chako, nitakunyooshea kidole hiki kwa ujasiri, tambua kuwa uchu wako wa madaraka unagharimu maisha ya wakimbizi wengi kutoka nchini kwako, watoto wanateseka mpaka nafsi zao zinajuta kwanini zimefika hapa duniania, yote ni sababu ya wewe, badilika, laa sivyo kidole hiki kitaendelea kukusuta kwa kukufuata popte ulipo,
Wewe, mwanamke usiyetulia kwenye ndoa yako, ni ulimbukeni ulio nao wala mume hana tatizo, imeandikwa na ipo wazi kuwa mwanamke mjinga ndio anayeweza kuivunja ndoa yake tena kwa mikono yake mwenyewe, kidole hiki kinakunyooshea wewe kwa uthabiti kabisa ili ujue kuwa uyafanyayo ndio yanaakisi afanyacho mumeo. thamani ya mwanamke ni kulinda kufuli lake nakujiuliza mara mbili je ni sahihi kulifungua kwa unaemfungulia..
siwezi kukusahau wewe mwanaume, mzandiki, jeuri, kiburi usiyejua thamani ya mkeo, tambua kuwa kidole hiki hakina jinsia lakini kinatambua kuwa mwanaume ili uwe thabiti unapaswa kuwa na msimamo, upendo na huruma kwa mkeo na familia yako,
kuvaa suruali sio kipimo cha mwanaume, wala usijidanganye kuwa sauti yako nzito ndio uanaume pia labda useme kuwa na kifua kikubwa chenye bustani ya huba ndio uanaume, siku hizi hata wanawake wapo hivyo, chamsingi kitakachosimamia uanaume wako ni msimamo kuwa na msimamo, usikatae mtoto, usibadilishe wanawake kama nguo.
wewe kijana acha uzembe shule kwanza mengine yote yapo tu, utayakuta, hayo unayohadaika nayo yaliundwa na wasomi, soma uunde yako nawe ujivunie sio unacheza na shule utakuja kuwa MZEE MPUMBAVU baadae halafu ukose wakumlaumu, binti acha kuiga mitindo yakimagharibi bibi aliyomzaa mama yako hakuwahi kuwa hivyo na ndio maana aliheshimiwa sana na mpaka leo tunautumia msemo wake usemao TAMAA MBELE MAUTI NYUMA, wewe kijana acha kushusha suruali mlegezo kwa wajuaji wa mambo watakutafsiri vibaya ilhali sivyo ulivyo. fanya uoe usiogope maisha, tambua kuwa riziki ya mtu ipo kwa mtu, kuogopa kuoa  wakati una wanawake zaidi ya mmoja unazini nao halafu unawatumia pesa zamatumizi yao madogo madogo ni uzembe usiovumiliwa na MUNGU! bado niko na wewe!
Kidole hiki kitaendelea tu kukunyooshea mpaka pale utakaponyooka.

Nimepata Nafasi.

Sitaki ifike sehemu nikukose eti kisa sijaitumia hii nafasi, nakumbuka vizuri kuna siku fulani niliwahi kupata nafasi kama hii..ulifurahi sana ukapata sababu za kuwa namimi karibu, ukanipenda sana, ukaniamini nakunipa dhamana yakuubeba nakuutunza moyo wako.

umepita muda mwingi sana sijarejea tena nilichoongea siku ile, nina imani utakuwa umekumbuka sana na unatamani hata siku ile ijirudie, nitakuwa mkosefu sana nikiendelea kukuacha utamani ule muda ilihali mimi ningali hai! acha niutumie muda huu sasa, kukwambia tena maneno sawa na niliyokwambia siku ile,

Sikuwahi hata siku moja kujua maana ya kupenda kabla sijakutana nawe, nilikuwa nabishana na waliowahi kupenda hasa walipokuwa wakidai kuwa maumivu ya mapenzi yana uhusiano na moyo,  niliwabishia enzi zile sababu sikuwahi kuona hata siku moja moyo wangu ukipatwa na msukosuko eti sababu ya mapenzi! wapo waliosema kuwa mimi bado sijapenda nikawaambia nimependa sababu enzi zile alikuwepo wapembeni yangu lakini ukweli nikwamba hakuwahi hata siku moja kunifanya niumie moyo hata ikitokea amepitisha siku bila kunijulia hali, lakini hali ni tofauti tangu nikupate wewe kwakweli hunipa mawazo upitishapo siku bila kupokea salamu yako.

Nimepata nafasi Laazizi, nitaitumia viuzri kwa ajili yako
Nilikuwa sijui, kumbe ni kweli mimi nilikuwa sijawahi kupenda, hivi sasa napenda na nikupendae ni wewe naona namna ambavyo mapigo yangu ya moyo huenda mbio hasa nikuonapo katika vazi lako la staha, sura yako ya Haiba na mwendo wako wa madaha,
unanimaliza zaidi ulitamkapo jina langu kwa lafudhi fulani ndani yake iliyobeba heshima inayoniambia kuwa wewe ni mke bora, yafaa kukuoa!.
wanimaliza zaidi hasa unaponihimiza mema, nakunifafanulia siri ya muda na namna unavyotembea kwa hiari bila kulazimishwa na mtu wala kusimamishwa hutembea kwa usahihi nakunitaka niusubirie muda kwa maana hauongopi utakapofika kila lililo jaala yangu litafika na ukinisisitiza kuwa kuusubiri muda huku nikijutuma ni Vazi avaalo mvumilivu na mwenye subira.

Busara zako zinifanya nikumbuke upendo fulani niliowahi kuuonja kutoka kwa mama na ndugu zangu, huwa natenga muda kuzungumza na mola wangu ili azidi kukupa afya tele, maarifa na uwezo wakufikiri zaidi kwa maana mafanikio yangu nayaona kupitia ushauri wako mzuuri na muongozo thabiti, kwa hakikia sijakosea hata siku moja kutumia muda wangu siku ile kukuomba uwe wangu.

Vijana ni wengi sana walionizidi vingi sababu ya ukweli wa watu wa pwani walosema ASO HILI ANA LILE, nikosalo mimi isiwe chanzo cha kuumia kwangu, naomba utambue kuwa mapenzi yangu ni yadhati na naamini yaliumbwa maalumu kwa ajili yako kwamaana ya kwamba yametosha kabisa hayana nafasi yakutoka wala kuongezeka, sina shaka dhamira ya mapenzi yangu yanalenga kufia mikononi mwako.

Ningeweza kusema neno moja tu 'NAKUPENDA' ili kufupisha muda na maelezo meengi ambayo sina uhakika sana kama yanakuchosha ila neno hilo nina mashaka nalo sababu mamluki wa mapenzi nao hulitumia neno hilo tena siku hizi hulitamka kwa kiingereza ili kuvuruga kabisa akili zenu mabinti, ubaya zaidi wakishatamka kwa lugha hiyo ngeni huambatanisha na tabasamu kisha kutoa pochi zao zilizonona pesa.

Kipato tunatofautiana laazizi nina mashaka leo utakataa SHILINGI kisa ni yakitanzania haya akijiminya nakukutolea DOLA ya marekani!? nina hakika atavuruga saikolojia yako sababu siku hizi maisha gharama na kauli za kileo ndio zinanivuruga sana eti laazizi NIKWELI MAPENZI BILA PESA HAYENDI???

naitazama mbele yangu naiona familia yangu ikiwa na mama thabiti, ambaye leo hii nimepata nafasi naongea nawe huku nikiyatazama kwa umakini macho yako ambayo yananieleza namna ambavyo unanizingatia na hiki ninachokwambia, naomba usidhihaki hata neno moja sababu ni ukweli kwamba nafsi inanisuta kuongea sana sababu naona kama utaniona miongoni mwa wale wanazungumza sana ili uingie kwenye kumi na nane zao zakukuongopea,
Naomba niishie hapa Mchumba nikikukabidhi hili busu ambalo naamini halina tofauti na lile busu ambalo nilikukabidhi siku ya kwanza katika midomo yako hii minene inayotema maneno mataamu yanayoionesha thamani yangu ya uanaume kila siku iitwayo leo!

nimepata nafasi mpenzi wangu zipokee hizi hisia zangu, nakupenda sana!.

Barua kwako Mzee wangu Shaaban Robert

                Salaam ama baada ya salaam, Ni matumaini yangu umelala pema peponi, naamini hivo na naendelea kumuomba Mungu aendelee kukupa pepo sababu ya mchango wako mkubwa wakusimamia nakuipa heshima lugha yetu ya kiswahili nakuinyoosha jamii kupitia kipaji chako adhimu ulichokuwa umejaaliwa,          

               Umezaliwa miaka ambayo sio mimi tu hata baba yangu na mama walikuwa hawana dalili yakuzaliwa, lakini nalipa heshima sana tukio lakuzaliwa kwako,ilikuwa ni zamani sana, zamani isiyosemeka, zamani ya mwaka 1909.
nalipa heshima tukio lakuzaliwa kwako sababu zikiwa ni nyingi lakini kubwa ni heshima uliyowahi kuiwekea nchi yangu pamoja na lugha yangu ninayoitumia,

kwa dhati ya moyo wangu kabisa napata muongozo kupitia wewe ingawa sijui ni muongozo gani sababu umefariki kipindi ambacho mimi hata sijawa na dalili yakuiona hii sura ya dunia nimekujua kupitia historia lakini historia hiyo ndio inafanya niseme ulikuwa wa pekee

sina mengi yakukujuza niseme tu kazi zako bado zinaendelea kuishi ingawa tunaamini kuwa asiyekuwepo na lake halipo lakini kwangu mimi licha yakuwa haupo lakini lako bado lipo kichwani mwangu ingawa ni kweli  hatua zakuhifadhi nakuthamini kazi zako zinapigwa lakini zinapigwa kwa mwendo wakinyonga mno,

ile nchi yako uliyoiita yakusadikika, sijui inaendeleaje kwa sasa nimekosa kabisa namna yakufika kule ili kuona namna ambavyo elimu ya sheria ilivyowanyoosha watu, pengine labda ule udhalimu, uonevu na matumizi mabaya ya madaraka umeisha ningeweza kutafuta namna nifike kule nijionee mwenyewe hali ya mambo ilivyo lakini nimejikuta natamani mno ungekuwepo wewe nafikiri ungeniongoza kufika huko au ungenipa ujumbe wa hali ilivyo sababu jicho lako lilikuwa ni pevu mno na mtu wakawaida asingeweza kuiona nchi ile inayoelea angani.

kazi za akili yako zipo bado zinaendelea kuishi, ubora wako haufutiki hata kidogo kichwani mwa mwerevu na mwenye busara yakujua kizuri ni nini,
kwa sasa mambo yamebadilika sana, kuna maghorofa, kuna barabara za kila mtindo na hata mavazi yetu vijana sio kama yale yenu, yale ya balaghashea na kanzu pamoja na bakora, siku izi vijana tunavaa t shirt na jeans, halafu tunashusha kidogo, mtindo wetu maarufu kwa jina la mlegezo, au kata k.
 sipati picha ungekuwepo sasa ingekuwaje sababu kuna mengi yakuyaweka kimaandishi, yenye dhima pana ya migogoro, mauaji, vita, ubaguzi, ukatili, rushwa, tamaa ya madaraka, ubabe na kwakweli haya yote yanahitaji muongozo thabiti, lakini watu kama ninyi hampo tena, tuliopo hatujui utu na thamani ya tamaduni zetu, tunachojali ni masuala mepesi mno ambayo yanaishi kwa muda mchache sana nakufa, mapenzi, starehe na umimi uliomwagika nakusambaa kila kona ya ardhi hii.

Hii ni Barua kwako mzee wangu Shaabani Robert
Naamini tunu yako ya tenzi za mashairi zingetumika kama fimbo kutuchapa vijana wa kiafrika ambao tunaishi katika mawazo ya mzungu, tumekuwa watumwa wa fikra, vyakwetu vyanini vya wageni ndio habari ya mjini,

uliwahi kumuona yule mwanamama siti binti saad ukamuandikia kitabu, lakini mwambie sasa mziki wake ambao ndani yake pia ulibeba ujumbe kuntu kwa jamii, hii leo hakuna kitu kama hicho, hatusikilizi kutikisa kichwa nakutunza, sasa hivi tunaruka kama vichaa, tunavua mashati,tunakanyagana nakupiga kelele hovyo, hatuna muelekeo wa muziki wa akili ambao ndani yake una mafumbo yatafakari na ujumbe wakuona mbali,

naadika barua hii nikiwa nalikumbuka shairi lako la ujana, ujana sio rafiki wakudumu, acha nirejee ubeti wa saba wa shairi lile.

7. Wazuri wenye uturi, na mikono yenye hina,
Kila mtu mashuhuri, alipenda kuniona,
Nilifaa kwa shauri, na sasa kauli sina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana 

najaribu kupata mwanga wa nini uliwaza mzee wangu mpaka kuandika shairi hili, lakini utu uzima wako unanipa jibu kuwa ulichoandika ulikuwa unakijua hasa, na ni somo kwa vijana kuhakikisha wanajipa muda wakuutumia vema ujana kwa maana hupita na nyuma haurudi tena,

nina mengi sana yakukuambia ndani ya waraka huu, lakini naamini nitakuchosha sababu MUNGU aliyekuumba alishaamua kukupumizisha, lakini nitakuwa sijatenda haki nisipokupa maendeleo ya lugha uliyokuwa ukiipigania nakuiendeleza sana kupitia karma yako,
hivi sasa vijana wamesoma sana, hawajui kuongea kiswahili moja kwa moja bila kuchanganya na kiingereza, linaniuma sana jambo hili lakini jinsi sina kwa sababu hivi sasa sio kama enzi hizo, siku hizi dunia ni kama kijiji.

uwezo sina wakupata kila ulichokiacha kama zawadi ya kipaji ulichojaaliwa lakini mara zote nimekuwa nikijiambiza kuwa vichache nitakavyokuwa navyo kukuhusu nitavilinda, kuviheshimu na kuvijali sana huku nikivipitia  majira yote ya mawio na machweo.

namaliza kuandika waraka huu, nikiwa na dalili yakulia, natazama huu mgongo wa ardhi nagundua kuwa umehifadhi watu wengi waliokuwa na maana katika dunia hii, napata somo kuwa hata mimi siku moja nitahifadhiwa ndani ya mgongo huu, nauona mkono wa mungu wenye maajabu, ambao unaishi nasi kila siku ukitenda maajabu yake, naukabidhi maisha ya taifa lako, lugha yako, na kazi zako, huku nikiukabidhi waraka huu ukufikie na mwisho kabisa nausindikiza na dua itakayokufanya wewe uendelee kulala salama, tena mahala palipo pema peponi. Amin

           wako mtiifu  katika kuenzi Fasihi simulizi nchini Tanzania
                                              Omar Zongo

Nitaomba muda wako 'Uisome'

Baadhi ya vitabu vyenye upekee wa Shaaban Robert katika uandishi
Kama utakosa kabisa muda basi tafadhali naomba niazime hata ule ambao unautumia kwa kunywa maji, laa kama huo pia utasumbua tafadhali sana naomba ule muda unaotumia kupokea simu ya umpendae, kama hiyo ngumu basi hata ule muda ambao unatumia kumeza mate tu, naahidi sitatumia muda mwingi sana kidogo tu nitakamilisha ninachotaka unisaidie,

Unamfahamu Shabani Robert, moja ya binaadamu waliowahi kuishi duniani ukanda wa afrika mashariki, alikuwa ni mfano wa lulu kutokana na utashi wake wakubuni kuandika mashairi na simulizi mbalimbali zenye kufunza na kwa hilo mitaala ya elimu yetu tanzania inajua umuhimu wa huyu mzee katika kufundishia lugha na fasihi simulizi kwa ujumla,

Ni heshima kubwa aliipa nchi yetu na bado hadi hivi leo kumekuwa na juhudi mbalimbali zakulienzi jina la Nguli huyu..

kama ingekuwa utashi na kubuni visa mbalimbali vyenye kuonya, kukosoa nakuelimisha ni kibali chakuishi milele sina shaka hadi hivi leo tungekuwa nae mzee huyu, lakini kutokana na ukweli kwamba Ubaguzi ni kitu haramu kwa kifo, ndio maana kila mmoja ataonja mauti, kama ilivyokuwa kwa marehemu Shaabani Robert....

tarehe 22 june  nitaomba muda wako uisome
barua niliyomuandikia  Mzee wangu huyu Shaabani Robert kama kumuenzi kutokana na mazuri mengi aliyoyafanya yaliyokuwa ndani ya kipawa chake,
barua ambayo nitapenda uisome kwa kina na ukimaliza uombe dua kwa mzee wetu alale mahala pema peponi, isome ili nafsi yako na yangu ipate fursa yakuibariki barua hiyo na imfikie mahala alipo, sababu naamini kuwa mwili wake haupo nasi ila nafsi yake bado inaelea katika anga la afrika mashariki na afrika kwa jumla....

Kama alivyo kuwa na huruma na lugha yetu ya kiswahili nakuitumia barabara basi na huruma ya mungu imponye na apate kupumzika kwa amani mahala pema peponi...amen!

Acheni Niandike

Nchi inaitwa WATAJIJU serikali yake inayoongoza nchi hii ina nguvu na inafahamika kote ulimwenguni ikiitwa WAPUUZAJI  watumishi wa nchi hii wote hujitambulisha kwa sare zao zenye nembo hiyo, WAPUUZAJI.

Miongoni mwa vijana waliozaliwa nchini humo  mmoja anakibaini  kipaji chakuandika lakini  kabla yakuanza kuandika anajikuta anarejea historia ya waandishi waliowahi kupita katika nchi ile, Naam! anajifahiri sana, anajikuta kuwa hayupo peke yake waliwahi kuzaliwa vigogo na manguli katika sanaa aliyoigundua kuwa ipo ndani yake, lakini katika kufuatilia historia za waandishi hao, simanzi inamkaba...wengi anaona kazi zao nzuri huku wanahistoria wakisifia uhodari wa waandishi hao wengine wakidiriki hata kusema namna ambavyo wamechangia kukuza lugha adhimu ya taifa la Watajiju, wananchi wa taifa hilo wamegawanyika kwa makabila tofauti lakini asilimia kubwa waliweza kuongea lugha ya taifa lao iliyoitwa TWAIZARAU,

Lazima Niandike
Asilimia kubwa ya vitabu vilivyowahi kuandikwa na waandishi wa Nchi ya Watajiju imeandikwa kwa lugha adhimu ya Twaizarau  lakini kutokana na ubora wa kinachoandikwa nchi mbalimbali walijikuta wakichapisha vitabu hivyo kwa lugha zao, na asilimia kubwa ya wageni wakijifunza lugha ya Twaizarau  na wengi wao wakiijua kuandika nakuongea nakuwazidi hata viongozi wa serikali ya Wapuuzaji  ambao mara nyingi walisikika wakiongea lugha nyengine au wakiongea lugha yao nakuchanganya maneno ya lugha nyengine,

kijana muandishi anasita kuandika anapofuatilia undani wa waandishi waliopita katika taifa la Watajiju, wengi wanakumbukwa kwa kazi zao tu, hakuna ambaye familia yake inanufaika na chochote..makaburi yao hayana uzito wowote na wengi ni kama wametelekezwa licha ya mchango wao kutambulika sana na viongozi Wapuuzaji hasa katika kuikuza lugha ambayo ni Twaizarau.

kijana anasita kuandika, anaachana kabisa na harakati zakutaka kuandika anaona haina faida yakuichangia nchi yake kupitia kipaji chake ni heri afanye kitu kingine..miaka inapita kuandika bado kuna muhitaji kila anavyopinga jinamizi lakuandika linamkaba nakumpa muongozo wakuandika na ndipo anapoamua kuandika, hajali tena kinachowakuta waandishi nchini mwake anajipa sababu zakuandika anaamini anatakiwa kuandika......na hivi ndivyo alivyoanza kuandika.


Nina kila sababu zakuandika, na hata wakati mwengine nikijizuia najikuta siwezi nataka tu niandike, nimejiruhusu sasa niacheni tu niandike..

Naandika kwa sababu nyingi hapa sitazitaja kwa namba nitazielezea kwa maneno..kuandika kwangu ndio njia pekee itakayofikisha ujumbe kuwa duniani ukanda huu usijulikana aliwahi kuzaliwa mimi, ambaye naandika! 

nikawaida sana kutothaminiwa ukiwa hai hata kama una ngozi ya dhahabu inayohitaji kuoshwa tu kuondolewa tope ili ing'ae imereremete nakutengeneza mvuto mkubwa wa heshima kwa jamii yako na taifa lakini naamini maandiko yako yatakuthamini na uzuri wa ulichokiandika na maana yake itawasuta kwa majivu waliojifanya hawaoni unachoandika kipindi upo hai.

inajulikana kuwa ikitokea umekufa wengi wanakuenzi kwa mtindo tofauti ikiwamo maneno ya "alikuwa" maneno ambayo hayatakufaa tena uendako, sasa naomba mniache tu niandike najua maneno yao ya " alikuwa"  yatakuja sindikizwa na ushahidi wa maandiko yangu...maandiko ambayo yatawasuta na kuwavua nguo zao kama yanavyowasuta maandiko ya wengine wengi ambao nao waliandika na kazi zao zinaishi lakini bado hawazithamini,

Maandiko haya yatadumu naamini lakini kutokujali kwao, ubinafsi na kutothamini kile tunachozaliwa nacho kamwe hakutadumu, watakufa kinywa wazi na nzi watawazomea kwa uzandiki wakujifanya hawaelewi kwanini waandishi walizaliwa katika taifa hili.

kwani wananufaika na nini wale ambao walizaliwa na watu mashuhuri waliosifika kwa kazi zao nzuri, kazi ambazo zilitangaza taifa, lugha na tamaduni za TUTAJIJU, eti wananufaika na nini? sioni wanachonufaika nacho ndio mana leo nataka niandike ili wajue kuwa kuna sababu za mtu kuandika ili vizazi vijavyo vyenye karma kama hii wasisite kuandika kwa kuogopa kuwa hawatanufaika na kuandika kwao. lazima waandike sababu kazi zao zitaishi nakuwapa sababu wengine waandike.

Acheni niandike, maandiko ndio muongozo thabiti ambao jamii inaufuata na kamwe jamii haiendi kinyume na maandiko, naamini katika maandiko, naamini katika kuandika sitaacha kuandika nimesema niacheni niandike sijali nini nitapata kutoka kwa WAPUUZAJI.

Naandika sababu kuna vingi vyakuandika ikiwemo hiki ninachoandika, lazima siku moja nchi hii ijivunie maandiko yangu.

Inataka Moyo

sio rahisi hata kidogo na inahitaji moyo na sio mradi moyo tu, moyo wenye ujasiri na usio mwepesi kutiririkwa na machozi, moyo wenye kustahimili na wenye kuelewa kuwa haya mambo ndivyo yalivyo na yanahitaji utashi na busara ili yaweze kukupa heshima kwa vizazi vyote vya sasa na vijavyo,

Waswahili walitukuka kwa misemo na walimaanisha waliposema ukiona vyaelea ujue vimeundwa, au ukitaka uzuri sharti uzurike.

Inataka Moyo
walikuwa na maana pana sana waliposema hayo lakini maana hiyo ililenga hasa maisha yetu ya kawaida.
Umezaliwa Kijijini hakuna nyezo za aina yoyote ile, shule ipo mbali sana inasababisha hata viatu vya shule visidumu nakufanya muda wote vionekane kama vinacheka mbele na soli ikiwa ina upara wa lazima unaotokana na kiguu na njia kila uchwao.

unajikuta una uwezo mkubwa wakuimba lakini kipaza sauti hujawahi hata siku moja kukiona, wenzako mjini wanatunga mashairi huku ala ikiwa inasikika aidha kwenye kinukulishi, au simu lakini wewe huna hata redio, baba mkali sana ukiikaribia redio yake hivyo unakuwa mpole tu ukiendelea kujifariji kuwa lazima siku moja utatoka.

mara moja moja tena kwa tabu sana huwa unawasiliana na rafiki zako kadhaa ambao tayari angalau wapo mjini, na zamani mlikuwa mnadanganyana kuwa wote lazima mtatoka, lakini wewe kwa sababu huna hata ndugu mjini wenzio wamekuacha ukiendelea kupalilia shamba la familia nakusaga dona ili wadogo zake wasikose ugali watakaporudi nyumbani.

Mara moja ulishawahi kukutana na rafiki yako mmoja kati ya wengi walioenda mjini alirudi mara moja kwenye msiba wa mama wa bibi yake anakwambia habari za mjini, unamsikiliza kwa makini sana licha ya kwamba pia unamshangaa jinsi alivyobadilika , nywele amenyoa kote katikati ameacha, shati limekatwa mikono yote na suruali imechanika chanika magotini, ana kitu ambacho mara zote unawaona Wanawake wanakiweka masikioni. Unajiuliza maswali mengi kwanini avae yeye puani na kwenye sikio lake moja lakulia,

Kutokana nawewe una kipaji sawa na chakwake na mlikuwa mnaimba sana shuleni kwenu kwenye sherehe za shule basi unajiweka nae karibu huku ukitaka sana kujua habari za mjini, dakika kumi tu za mwanzo unabaini kuwa ili kuendana na kipaji chako lazima uwe kama jamaa,

Unajikuta unachukia lakini huna jinsi nawe taratibu unaanza kujitengenezea picha ya baadae utakuwa kama vile, wazee wote wa kijiji wanalaani uvaaji na muonekano wa rafiki yako lakini wewe tayari ulishakolea na simulizi za mjini umeshadanganyika unatamani kwenda mjini nawe ukawe vile,

Masikini ya mungu una kiu kweli kweli, kiu yakuonesha uwezo wako uliojaaliwa na Mungu, bila kuwa karibu na jamaa utakosa njia yakutangaza kipaji chako mjini. Jamaa anakwambia kuwa mjini tayari anafahamiana na watangazaji kadhaa na madj maarufu ambao wanaweza kumtoa mtu kimuziki.

Unazidi kuchizika, lakini kutokana na busara za mzee wako baadae unakaa na echini ya mti anakurejesha kwenye utimamu wako, anakwambia busara tupu, zinazokufanya ujione mjinga kwa kumpa muda wako jamaa kumsikiliza nakutamani kuwa kama yeye…mzee anakwambia kwa upole na umakini huku akionekana kujua zaidi saikolojia yako inawaza nini

“Mwanangu, najua uwezo wako, kipaji chako na karma yako uliyopewa, miaka mingi ya nyuma niliwahi kuishi mjini, nilibahatika kukutana na watu wenye kipaji aina yako, nilibahatika kuzungumza nao sababu hawakuwa kama alivyo rafiki yako.

walikuwa wastaarabu, sio wahuni, walikuwa wasikivu waelewa na katika maneno yao Ishirini kumi na tano yote wanaelezea kiu yao yakutaka kujulikana, kutangaza kipaji chao nakutumia kalamu zao kukosoa, kuelimisha na kurekebisha jamii, niliwafanya rafiki na nikawaazima sikio lao pia kuwasikiliza wanachoimba,mashallah nyimbo zao zilifunza, zikanipa muongozo na zikanijengea uzalendo wa nchi yangu, tamaduni yangu na kila kitu kuhusu asili yangu.
nyimbo zao zilinyooshea vidole maadili ya kiafrika yanayomomonyoka mithili ya mvua inayomomomnyosha udongo mabondeni,  nyimbo zao zilibeba ujumbe thabiti uliokosoa viongozi walafi, lakini zaidi nyimbo zao ziliburudisha nakukukonga nyoyo sababu ya ala safi ya muziki uliopangiliwa ukapangika.
Sikuona kama walisuka nywele au walikata nywele kama rafiki yako, sikuona kama walikuwa na ufinyu wa akili nakuvaa nguo zinazobana na zilizochanika magotini kama alivyokuja nazo huyu mwenzio, lakini pia sikumbuki kama walitoboa pua zao sababu ni wao ndio walihimiza jamii kusimama imara katika tamaduni za kiafrika, na waafrika hawana maelekezo ya wanaume kuvaa urembo katika pua wala kwenye masikio,
Nakupa Baraka upambane kutangaza kipaji chako lakini mara zote jiulize nini unakifanya kwa jamii yako kupitia kipaji chako. Kumbuka kuwa Kesho lazima utaulizwa!”

Baba huyu ni miongoni mwa wazee ambao huamini kuongea sana ni dalili yakutojiamini, hivyo alipomaliza kusema hivyo alimuacha mwanae, na somo moja lililopita kama muhtasari kichwani kwake, UWEZO ULIO ZALIWA NAO NI JAMBO LA KWANZA, NAMNA YAKUITUMIKIA JAMII YAKO KUPITIA UWEZO HUO NI JAMBO LA PILI NA LA MUHIMU ZAIDI.
Maneno ya baba yake yalisimama kama muongozo tangu hapo lakini swali gumu likabaki kwake ni vipi atapata pesa, na wakati Aina ya muziki aliomuelekeza baba yake ni mziki ambao vijana abadani hawauelewi, wanapenda mapenzi, starehe na dhima nyengine nyingi rahisi kama vile majivuno na sifa.
Inataka moyo, kusimamia uzalendo wakati mfuko upo hoehae, inataka moyo zaidi kuielimisha jamii ambayo yenyewe inataka kukulipa ukiipotosha, Inataka moyo sana kuchagua Kulipwa kesho na Mungu wako kupitia alichokuzawadia kwa kuisadia jamii kuzinduka kutoka katika kiza cha ujinga, uonewaji, ukatili na kunyimwa haki zao au kulipwa leo kwa kuwapa chakula ulichokiandaa chenye dhima waipendayo lakini sumu iwamalizayo

Inataka moyo….
                                                     

NITAKUOA LAKINI SITASAIDIA NDUGU ZAKO!



Mchumba hili ni neno la sita katika kitabu changu  cha vitu ambavyo unapaswa kuvijua kabla sijakuoa,
Ni neno la sita lakini nimeanza nalo kutokana na umuhimu na pia lina fitina sana neno hili maana wabaya wetu wasio penda mahusiano yetu lazima watakwambia kuwa mimi mume gani, nina roho mbaya na sifahi kukuoa sababu ya neno hilo,

Mengine yaliyopo katika kitabu hicho na wala usilalamike kuanza na neno la sita sababu tayari nimeshakwambia hapo juu mchumba,
utayafahamu

Acha nikufafanulie ili wanafiki, wafitini wasipate kutumia neno langu hilo kunigombanisha nawe na mwisho tukaachana , Kwanza fahamu kuwa nitakuoa hilo ni lamuhimu sana na unapaswa kulijua, nafanya kila liwezekanalo na tayari nyumbani kwetu wameshajua, wazazi wamebariki wananingojea mimi tu, lazima nitakuoa mchumba tuseme ishaallah,

Lakini mchumba, kabla sijakuoa naomba ujue na utambue kabisa kuwa sitasaidia ukoo wako, nitakachofanya mimi nitahakikisha unakula vizuri unalala vizuri, unapata kila kitu ambacho mwanamke anastahili kukipata kutoka kwa mume wake, lakini zaidi nitahakikisha unapata kazi nzuri sana itakayokuingizia kipato.

Ninaahidi hayo mchumba yazingatie na ikitokea sijayatimiza ruksa kunihukumu, hata ikibidi ninyime vya msingi ambavyo mume anastahili kuvipata kwa mkewe, usijisikie vibaya mchumba eti kisa  labda hauna elimu yakutosha kusema utapata kazi nzuri, kazi sio lazima kuajiriwa mama, nitahakikisha hata mtaji nakupa kiasi chochote ufungulie biashara yako,

Nitakuoa
Nitakupa mimi mtaji kiasi chochote kitakachokuwa ndani ya uwezo wangu mradi upate biashara, hii biashara mchumba tambua kuwa haitanihusu mimi hata kidogo, hiyo biashara niyakwako, mimi nitakuwa nyuma yako kuhakikisha haiyumbi na inasimama kadiri iwezekanavyo.

Kama unavyeti ambavyo unaamini vitasaidia mimi kufanya upate kazi ofisini sitakuwa na hiyana nenda kafanye kazi mama, kafanye kazi kwa bidii zote huku ukiamini kuwa una Baraka kutoka kwa mumeo.

Sitakuzuia wewe kupata kipato chako nitahakikisha unapata nami nitakupa kila fursa ambayo nitathibitisha kuwa haitahatarisha ndoa yetu,

Lengo langu mchumba pesa hizo wewe ujue kwanamna gani unazitumia kusaidia ukoo wako na wale wote wanaokuhusu wewe, mimi sitakuwa na jukumu hilo, mimi nitakuwa na jukumu la familia yangu tu ambayo ni wewe mke wangu na watoto tutakaojaaliwa  kuhusu kwenu simamia miradi yako mama uweze kumudu shida na matatizo yanayowakabili watu wa ukoo wako, sjui unaninielewa mchumba mimi kusema kweli vile sitasaidia Familia yenu wala ukoo wenu, hilo litakuwa  jukumu lako,
kuhusu watotot wetu kurudishwa shule sijui wanadaiwa ada, hilo litakuwa lakwangu lakini sio mdogo wako amefukuzwa shule au bibi yako anaumwa, samahani sana mchumba sitakuwa tayari kuhudumia hilo.

Maisha ni magumu sana, nikisema nibebe majukumu yote yakuhudumia familia yangu na mengine yote yatakayoikumba familia yako hatutofika, niazalilika na yatanishinda mapema, hivyo tambua kabisa jukumu la ndugu zako ni lakwako mwenyewe mimi usinihusishe, labda kama ukinihitaji kwa ushauri kaibu sana tena karibu kwa mikono miwili maana mimi ni wako, na nakupenda sana!.
Pengine labda unajiuliza eti ikitokea ndugu zangu mimi wameshikwa na shida ufanyeje, ni swali zuri sana mchumba, na jibu lake ni jepesi tu..usiwasaidie nitalibeba mimi hilo jukumu,nikishindwa nitakuomba msaada na hakikisha unanisaidia kwa makubaliano yakukurudishia pesa yako, hiyo itakuwa ni halali yako mchumba.
pesa yako wewe haitakuwa na nafasi yoyote yakununua nguo zako, chakula wala chochote ambacho nastahili kukifanya mimi kama mumeo, pesa yako wewe  utaamua mwenyewe ufanye nini kwa hiari yako sitakulazimisha, mradi mwenyewe uridhie na uamue. lakini suala la msingi hakikisha unaweka akiba yakuwasaidia mama, baba, bibi zako wajomba na ndugu zako wengine wote wakihitaji msaada wakifedha  kwa maana mimi sitakuwa na bajeti nao, na huo ndio ukweli...NITAKUOA LAKINI SITASAIDIA NDUGU ZAKO KIFEDHA! WEWE MWENYEWE UTABEBA JUKUMU HILO!

Ni Kama Nyota

Majira yanabadilika, kuna muda anga linameremeta kwa uangavu wa jua, huku likiwa na matokeo ya joto kali na mvuke wa moto utokanao na hasira za kuwaka kwa jua hilo!

sijui lakini naamini kuna maana ya jua kuwaka mchana na watu kuhitajika wafanye kazi mchana ili kukamilisha ule msemo usemao, mtatafuta kwa jasho, ikiwa na mantiki ya kwamba hata kama kazi yako itakuwa ya kukaa tu, lakini kutokana na ukali wa jua lazima jasho likutoke labda kwa wale wenye viyoyozi katika maeneo yao ya kazi, lakini muda wote jua halitishwi wala kubabaishwa lenyewe linawaka tu na ukithubutu utoke nje utakutana nalo!.

lengo sikulisakama jua, la hasha!

lengo langu nikuzungumzia majira yanavyobadilika, kuna muda ukitazama anga utagundua kuwa halipo tena jua, giza linakuwa limetanda kote na anga lote linapambwa na vimeremeta vyenye kupendeza na huwa vingi sana angani, na kama ukivitazama kwa hisia kali lazima neno litakutoka, neno lakupongeza kazi ya MUNGU. kazi ambayo hufanyika kwa siri kubwa hivyo kuongeza maajabu katika tafakuri yako.

lakini ukiwa unatazama zaidi angani muda huo utagundua kuwa vimeremeta hivyo vinavyotambulika kama nyota vinatofautiana kwa kuwaka, ukipata muda tazama kwa umakini utaona zipo nyota ambazo huwaka zaidi na mwanga wake huonekana kuwa na nguvu kuliko nyota nyengine ya jirani yake, lakini utofauti huo wakuwaka haubadilishi jina la nyota zote zinaitwa nyota,

Ni kama Nyota
safari ya maelezo yangu inaelekea mwisho kwa kusadiki kichwa cha habari ya maelezo haya 'Ni kama Nyota' ndiyo wala hakuna tofauti maisha yetu sisi binadamu ni kama nyota angani, wapo ambao wanang'ara na wala hupati shida kubaini hilo pindi tu unapomuona unahisi ni rafiki, unatamani kuongea nae, unamuamini kwa haraka unamdhamini na hata unaweza kumpa chochote akiongea nawe na akaonesha nia thabiti ya kuhitaji kitu hicho. 

huyu hana tofauti na nyota zile zinazong'aa angani, na yupo tofauti kabisa na ambaye  hajengi mvuto wa aina yoyote kwa mtu, hata ukikutana nae haraka unajikuta unamdharau, kwa kujipa majibu ya hawezi, sio rafiki, wakazi gani na mengine mengi tu yakumshusha sababu tu hajajenga mvuto katika macho yako wala hajang'ara.

unaweza kumuona mbaya, havutii, mwizi, hana ushawishi wala hawezi kukusaidia chochote, hata ikitokea amekufanyia kitu kizuri, unahisi hastahili kupongezwa nawe, ni dhalili, fakiri na anakushusha kuwa nawe karibu, unamuona yupo chini yako, wewe una thamani kubwa kuliko yeye, unamuona anafaa kuwa mtumishi wako, NI KAMA NYOTA, huyu ni aina ya nyota isiyong'aa!

lakini suala la msingi zote ni nyota, na anga inapendezeshwa zaidi na nyota za aina mbili, zenye kung'aa sana, na zenye kung'aa kwa kufifia, nyota hizi ndizo zinakamilisha anga la nyota ambalo hukumbatwa na usiku wa kiza wenye kujenga ladha ya usingizi kwa wanadamu.

najaribu kulitathimi  Anga lenye nyota zooote zenye kung'aa, nikiri kwamba sijawahi kuliona, na kama siku likitokea usiku huo utakuwa wa ajabu na una upekee ndani yake, sitaki kusema kama anga hilo litapendeza ama la! labda siku ikitokea tutajionea,

Ni kama nyota, unapaswa kutambua hili, unapaswa kujijua wewe ni aina gani ya nyota, na hata kama ukibaini kuwa wewe ni dhalili mbele ya wengine, huna thamani wala hujengi mvuto kwa yoyote, hupongezwi wala ile thamani yako ambayo wewe mwenyewe unaamini ipo ndani yako lakini wengine hawaitambua usijisikie hovyo, tambua kuwa macho yanatofautiana,

Naamini mimi na wewe tukisimama usiku kutazama angani, nyota ambayo itajenga mvuto kwako pengine mimi inaweza isinijengee mvuto huo, hivyo tambua kuwa hatua zako unazopiga katika maisha unaweza usikutane na mtu akakupokea kwa shangwe, lakini amini kadiri unavyoendelea kupiga hatua utajikuta anajitokeza mtu tena mwenye thamani kubwa kuliko uliowahi kukutana nao, atakupokea, atakukirimu, atakukaribisha kwa tabasamu linaloimba shairi lenye kupendeza, lenye maneno yanayofariji na atakupamba kwa marashi yakunukia, atakufuta dharau zote uliozopakwa,
atakupangusa mikosi yote yakupuuzwa na atakukalisha kwenye kiti cha enzi,

Ni kama nyota lakini macho yetu yanatofautiana, wapo wenye uwezo wakuona mbali, na wapo wenye uwezo wakuona karibu, wakijitokeza wengi wasiione thamani yako, tambua atajitokeza mmoja tu mwenye thamani kuwazidi wote na akakupa vyeo vyote vinavyopita heshima ya ufalme,
umeumbwa kwa sababu, usiache kuiamni sauti inayokwambia kuwa wewe ni wapekee, na wewe ni mbora, amini hivyo mitazamo ya watu kamwe isikurudishe nyuma, macho yao ndio yana matatizo wewe umeumbwa vizuri, ni kweli hakuna mkamilifu, lakini mapungufu yako wewe sio sababu ya wao kuendelea kukushusha...uliumbwa hivyo ulivyo kwa sababu, 

usichoke kuitafuta sababu hiyo.

NILIWAHI

Niko ndani chumbani, ugenini,gizani, najihisi mpweke, aliyezima taa sijakua nae, simjui nimekutana nae ukubwani, nakumbuka utotoni niliwahi kuzoeana na mtu kama yeye lakini sio yeye, nabaini kuwa kila siku iitwayo leo hili neno niliwahi linaendelea kunizoea sababu naweka historia ya mambo mengi ambayo nayapitia
Nakumbuka vizuri kabisa kuwa niliwahi kuwa na wazazi, baba na mama yangu, alianza kufariki baba nikabaki na mama na mara zote nilikuwa najiambia kuwa niliwahi kuwa na baba, maisha yameenda sana hii leo sina mama, najiambia tena kuwa niliwahi kuwa na mama sababu sipo nae tena,
Niliwahi kulia nakubembelezwa kwa upendo huku nikiulizwa unataka nini mtoto, lakini sasa hivi imebaki simulizi tu na huku nikijiwazia mwenyewe kwa kusema kuwa niliwahi kupitia maisha hayo,
Niliwahi kuwa na ndugu zangu walinijali kama mdogo wao, kipindi hicho nasoma walihakikisha sikosi kitu na walinitetea pale nilipokuwa naonewa, lakini sasa hivi imebaki kumbukumbu tu  na nakubali kuwa kipindi kile familia ile iliunganishwa na wazazi wetu na sasa hivi kila mmoja ana familia yake yaani kaka zangu sasa ivi wameshakuwa mababa wa familia zao, na dada zangu wameshakuwa wake wa mtu Fulani na pia ni ma mama wa familia zao,
Nakumbuka sana kuwa niliwahi kuwa nanunuliwa nguo, chakula na kupewa hata mahala pakulala, lakini sasa hivi naita ni mapito na hata sikumbuki tena mambo hayo kufanyiwa mara ya mwisho ni lini,
Niliwahi kuwa na shida nikamlilia mama yangu, niliwahi kukosa nauli nikawaomba ndugu zangu, na niliwahi kutamani ukubwa bila kujua kuwa siku moja nitakuja kuukumbuka udogo.
Dah siamini kabisa kuwa niliwahi kuwa na marafiki wengi ambao tulikuwa tukifuatana kila mahali, lakini wako wapi sasa, kila mmoja ana familia yake, niliwahi kulaumu sana wazazi walipokuwa wananiambia kuwa nisubirie wakipata pesa wataninunulia kitu flani, nilihisi wanafanya makusudi , nakiri sasa sikuwa najua,niliwahi kuwa mjinga!
Niliwahi kutamani kuyaanza maisha nikiamnini kuwa  nimepesi mno, nakiri sasa kuwa nilipotea sana, nilikuwa mfupi mno, mfupi wa fikra!
Nakumbuka niliwahi kuwa na mpenzi wangu wakwanza kabisa katika mapenzi, nikamuona yeye ni wamuhimu kuliko hata elimu yangu, nikawa natumia muda mwingi kuwa nae huku wenzangu wakiwa darasani,  niliwahi kujidanganya kuwa huyu ndie waubavu wangu, nikadharau wazazi na ushauri wao, nikapuuzia masomo nakuyavalia njuga mapenzi nikiyaona ndio kitu pekee cha faraja duniani, nakumbuka mwisho wake niliambulia kuvunjika guu, sababu sikusikia ya mkuu, hivi sasa yeye ana maisha yake na wapenzi wake na mimi niko na maisha yangu huku muda huu nikikumbuka kuwa niliwahi kuhadaika kipindi Fulani na huyu kiumbe hatari aitwae  Balehe, niliwahi kuwa mtumwa, mtumwa wa mapenzi!
Niliwahi kuwaza maisha bila Mama yangu, maisha ambayo nayaishi hivi sasa wakati nilikuwa naamini kuwa hayawezekani, kwakweli nimewahi mambo mengi sana ambayo yananiimarisha ili niwe nyani mzee niliyekwepa mishale mingi, na niweze kuja kuwasimulia wajukuu zangu kuwa Niliwahi kitu Fulani aidha kwa kuwaza au kutenda, lakini niliwahi!
Naumia sana muda huu nikiwaza hayo niliyowahi kuyatenda , nakuyawaza, yote yamebaki story, niko mpweke sina rafiki niliyekuwa nae, mpenzi niliyeanzana nae wala mzazi niliyempenda kwa dhati, sina yeyote ambaye nilikuwa nae muda mwingi nikijadili nae masuala mengi ya mbele, najiona mimi pekee kwenye safari hii, wengi ni wapya ambao nao naamini nitakuja kuwafikiria kuwa niliwahi kukutana nao…
Simulizi ya maisha ina ladha mbili, chungu na tamu, ulimi wako unapaswa kujiandaa kuonja ladha hizo zote huku ukitambua kuwa maisha ni hatua inayojipiga yenyewe huku ikikuachia alama ya kumbukumbu, wako wapi uliokuwa nao mwanzo, yako wapi ulioyawaza mwanzo, na kwanini kila siku wanajitokeza watu wapya katika maisha yako na mambo mapya katika maisha yako, maisha yana maana kubwa na ni wajibu wa kila mtu kuishi kwa akili, wema na upendo ili ukiwaza yote uliyowahi kuyapitia ujikute unatabasamu, huku ukiamini kuwa uliyewahi kukutana nae pia huko aliko anatabasamu kila anapokukumbuka…

MIMI NILIWAHI KUWAZA IPO SIKU UTAYAAMINI MAWAZO YANGU  NAKUYAISHI SABABU YALISHAWEKEWE BARAKA NA TUNU YA PEKEE NA MUNGU MUWEZA!
NILIWAHI
ZONGO

MREXPERIENCE

TAFITI NDANI YA SIKU HATARI......


Nilitamani sana kupata mke mwema, hasa atakayeweza kusimamia familia yetu hata kama Mimi ikitokea sipo duniani.
Nimewaza mambo mengi sana ikiwemo namna yakumpata mke huyo,
KUCHAGULIWA MKE NA WAZAZI mnh!! Hapana kwakweli sababu Mara kadhaa wao wenyewe wakikawazana wanaropokeana KWANZA ISINGEKUWA WAZAZI NISINGEKUWA NAWEWE sasa ina maana gani niwape dhamana wanitafutie mke ilhali wenyewe wanajutia.
kitu pekee nilichoona ni sahihi nikufanya utafiti wa Nani wa kumuoa kitu kizuri nikwamba kumbe sio Mimi tu niliyeanza kufikiria suala hili Wapo vijana wengi sana na wengine ni watu wazima hawajaoa bado wanafanya tafiti....
 Lakini naanza kubaini kuwa njia yakufanya tafiti ni hatari sana sababu ili tafiti ikamilike na umpate wa sahihi inabidi ukae kidogo na mtoto wa watu! Utaanza urafiki wakuzawadiana cake na maneno mazuri kwenye birthday mwisho kukaribishana ndani kutazama movie, mwisho ukaribu usio na mipaka na mwisho kabisa majina yanabadilika wanaitana hubby, love, bae na majina mengine mengi tu ambapo kwa sisi ambao bado tunasimamia utamu wa lugha yetu utatusikia tukitamka 'laazizi' ' wa huba' 'ini mkalia nyongo' na mengine mengi tu, baada ya yote hayo macho yetu yanageukia kitandani mimi napenda kuuita UWANJA WA FUNDI SEREMALA...hapo ndipo tafiti inapopoteza mueleko, baada yakuutumia uwanja wa fundi seremala, kila mmoja anaanza kumuona mwenzie hafai sababu wameshatumiana, tamaa inasimama imara nakuyumbisha akili, unapitisha uamuzi kuwa huyu hakufai unatafuta mwengine, nae njia ni ileile mwisho mnaachana. 
Umri unaenda kuoa huoi..na kuna wengine tafiti zao wanazifanya muda mrefu kila siku akijidanganya atajiridhisha kesho kuwa aliye nae ni sahihi bila kujua kesho haijawahi kufika hata SIKU moja!
Nimegundua hizi ni tafiti katika siku hatari, zamani pengine kipindi ambacho maradhi ya zinaa kama UKIMWI yalikuwa hayapo kubadili wapenz ilikuwa nikuvunja tu maadili lkn hupati athari nyengine lkn hivi sasa ukibadili wanawake kwa gea yakutafuta wakuoa unaathirika kiafya, kiuchumi na hata kiakili.

KIAFYA: Utapata maradhi sababu SIKU hizi ni ngumu sana kumtambua mgonjwa, unakuwa na huyu unamuona sio wife material unampiga chini unamfata yule mwisho unakufa kabla hata hujakamilisha utafiti wa mtu sahihi wakuoa.
KIUCHUMI: hata kama unajidanganya humpi pesa lkn kuja kwako kama kaja mchana utagharamia msosi wa mchana, akishinda mpk jioni ujue unalo hilo na akiondoka omba mungu asihitaji bajaji ili awahi kufika akihitaji ujue itabidi ujikamue mzee, hivyo bajeti yako imeyumba kwa siku kama akifululiza kwa siku tatu ujue kujenga utakutazama kene vipindi vya luninga tu, na niseme tu haya ni kwa wale wenye mahusiano ya tuvumiliane tu kinyume na hapa watoto wakike wanahitaji simu kali, mavazi yakisasa, kubadili nywele za wahindi walokufa na mahitaji mengine mengi yakisasa! So utafiti wako una matokeo ya kukusababishia ukata wa milele.... Bora kuoa!
KIAKILI: nafikiri hata wenyewe tunaona mapenzi yanavyoipelekesha dunia, uliyempata unampenda unahisi ni sahihi wewe kuwa nae lkn yeye hana mpango, anaye anayempenda, chakula hakipandi, kazi hazifanyiki, unaongea peke yako njiani, msongo wa mawazo, unamfumania anakucheka unawaza kunywa sumu ya panya unaenda kwa Mangi unainunua, unarudi kwako unajifungia chumba kimekamilika kina fenicha nzuri, kitanda mpk wachawi wanaogopa kuingia,friji ndani lina kila aina ya vinywaji na matunda lkn vyoote unaona ni ujinga hata mama yako kijijini ambaye anategemea sana fungu lako ili asogeze maisha umemsahau eti unakoroga sumu ya panya ufe kisa mapenzi, tayari hapa saikolojia yako haipo vzr.
Hata kama hauna vitu vyote hivyo hapo juu lkn Nina uhakika zipo sababu bilioni zakukufanya uendelee kuishi, huna sababu yakujiua ni lazima una tatizo la akili, na tatizo hilo limesababishwa na Utafiti wako unaoufanya kumpata wakuoa, sasa umeingia kwa Toto lakitanga kakuroga kitandani nakunyunyiza limbwata kidogo kwenye chakula baba wa watu haulewi..ni saikolojia yako tu imeshavurugwa....
HIZI NI TAFITI KATIKA SIKU HATARI, Dunia imebadilika mno, wanawake woooote ni Zawadi yetu, kama kweli wewe ni mwanaume kamili jivunie kumbadilisha mwanamke awe unavyotaka, na sio kumtafuta aliye na hulka unazotaka utapotea na hautafikia lengo....
MAPENZI NI ZAIDI YA TUNACHOFIKIRIA...
Zongo
‪#‎mrexperience‬