AHSANTE MUNGU


Mimi ni Kijana muafrika, nimezaliwa katika familia ya kimaskini lakini nasema ahsante MUNGU sababu sijawahi kutamani kuiba mkate nyumba ya jirani ili Nile.
Omar Zongo's photo. Nimekuwa nikijituma huku nikiamini kila siku uwepo wako na nguvu yako ya ajabu ambayo Mara zote imekuwa ikitenda muujiza Mkubwa kwangu na kwa vijana wengine wengi barani afrika.
Kuna siku nilishuhudia Kijana mwenzangu ambaye huku kwetu anatambulika zaidi kama 'ombaomba' akipigwa kikumbo na gari, bila shaka alikuwa anaomba pesa kwenye magari yaliyosimama kusubiria foleni, Taa zakuruhusu magari zilipowaka Dereva akawasha gari nakumkanyaga vidole vyake vya miguu iliyokuwa imekaa usawa wa matairi ya gari lile.
gari jengine likaja likamkumba nakuanguka kusababisha gari jengine kuja kumpandia, Maskini Kijana huyu hakuweza kupinga mauti yaliyosababishwa na ajali ile, hivi sasa nikisema ahsante MUNGU naiona nafsi yake angani ikielea, machozi yake yakianguka nakuchora maneno ardhini yanayosomeka neno moja tu NILITAMANI!
ndio najua alitamani kuendelea kuishi licha yakwamba maisha yake yalikuwa ni UKATA usioelezeka, najua ni mpambanaji aliyekuwa akiamini kuwa kuzaliwa masikini haimaanishi kuwa ndio utakufa masikini, najua kuwa alitamani kuja kuishi maisha ambayo wanaishi wale waliomkanyaga barabaran nakuidhulumu nafsi yake, najua alitamani kuja kubadilisha maisha ya familia yake.
Ahsante MUNGU kwa pumzi, bado naendelea kupambana naamini Mimi ni Starring katika hii movie(MAISHA) .
Naamini watoto nyumbani, ndugu marafiki watakuja lienz jina langu kwa Zawadi yakuwonesha njia nakuwawashia Taa kwenye hii BARABARA YA KIZA!
Ahsante MUNGU kwa uwezo ulionipa wa kutoa FARAJA mpya kwa ujumbe huu naamini yupo ambaye sasa anaiona thamani yake na sababu zakupambana ili kutimiza malengo yake bila kujali yeye ni Nani na amezaliwa na familia ya aina gani....
AHSANTE MUNGU WANGU!

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »