Sio kosa kukunyooshea kidole wewe hii leo,
nakumbuka niliwahi kukemewa kumnyooshea kidole mtu yeyote ama awe mkubwa kwangu
au mdogo lakini leo sitakiweka chini kidole hiki nitakinyoosha kwa uthabiti
tena bila kutetereka , nakunyooshea wewe kidole hiki.
Sio fahari hata kidogo na huwezi sifiwa kwa
tabia zako za ubinafsi, choyo na uzandiki, hufai kwa kulumangia wala kulia na
kachumbari, ni wewe ndio nakuwambia, unajisikiaje kuishi kifahari kama mfalme
ilihali waliokuzunguka ni dhalili, wamechoka na macho yao yanaongea shida na
ufakiri uliowagubika.
Eti wewe? Kwani wewe ni nani hasa katika hii dunia mpaka
watoto wa wenzako uwageuze punda kwa kuwabebesha madawa yakulevya na kuuza utu
wao? Eti wewe ni nani? Nani amekwambia kama dunia hii ni yakwako na kwamba una
haki yakutesa wenzako sababu ya pesa?
Wewe |
Kidole hiki kina beba mengi na labda tu
nikwambie huwezi kukikata licha ya kwamba unamiliki kila aina ya ,kifaa cha kukatia utu wa wenzio na thamani zao, lakini kamwe kidole hiki hakitakatika hata ukithubu kukinyofoa bado kitaendelea kukutazama wewe na kukuuliza maswali
haya tena uyajibu kwa ufasaha labda yupi limbukeni aliyothubutu kukuongopea
kuwa wewe upo sahihi kutembea na wake za watu, watoto wadogo na kuwadhalilisha
wenzio wanapojaribu kudai haki yao kwako,
Kwani wewe umeumbwaje labda mpaka ufikirie
kuwa rushwa ni sahihi na uweze kuitumia kudhulumu haki ya mnyonge, tuambizane
hapa nijue na pengine hata nihofie kukunyooshea kidole hiki kwani ni wapi hasa
panaposema kuwa cheo chako ndio umungu mtu wako unaopaswa kuutumia kuumiza
walio chini yako,
kidole changu hata ukitazame kwa chuki hakitasita wala kuona aibu kukukosoa kwa uyatendao, nani amesema mtu atapata radhi za wazazi asipofuata maadili mema ambayo wazazi wamemfunza, nani kakwambia kuwa uvivu, ulevi nakupenda starehe ndio ujana!
Hakizungumzi kidole unaoongea ni mdomo ila hiki kidole kinakuoneshea wewe ili ujue maneno yangu hayaatoki bure yanakulenga wewe, labda useme hapa nifahamu, ninani aliyewahi kuishi milele duniani hapa, hata pesa kama ulizo nazo haziwezi kukufanya uishi milele sasa kwanini usirudishe utu hata chakula unachomwaga uwagaie watoto wanaoshindia kipande kimoja cha mkate au wakati mwengine maji pekee, nani aliokwambia roho mbaya ndio mtaji wakujirimbikizia mali.
sitaacha kukunyooshea kidole wewe mpaka utakapoamua kubadilika nakuwa mwema, kuacha kumnyanyasa mkeo, wala kutelekeza familia, sitaacha kukunyooshea kidole mpaka utakapoamua kuacha kuvuta mihadarati, kunywa pombe nakutembea na wake za watu, sitaacha kamwe kukunyooshea kidole hiki mpaka pale utakapoamua kusaidia wazazi wako kijijini. kidole hiki hakitashuka chini mpaka pale utakapoona neno la busara nikuwaomba msamaha ulio wakosea nakuishi nao kwa utu!
wewe! wewe! wewe msanii unaedhani kipaji chako ni fursa yakupotosha jamii, sio kweli, simamia haki za wanyonge kemea, ufisadi na rushwa sababu wewe ni kioo cha jamii,
wewe Kiongozi unaejali tumbo lako, mimi mwenzio siogopi wala sitaogopa cheo chako, nitakunyooshea kidole hiki kwa ujasiri, tambua kuwa uchu wako wa madaraka unagharimu maisha ya wakimbizi wengi kutoka nchini kwako, watoto wanateseka mpaka nafsi zao zinajuta kwanini zimefika hapa duniania, yote ni sababu ya wewe, badilika, laa sivyo kidole hiki kitaendelea kukusuta kwa kukufuata popte ulipo,
Wewe, mwanamke usiyetulia kwenye ndoa yako, ni ulimbukeni ulio nao wala mume hana tatizo, imeandikwa na ipo wazi kuwa mwanamke mjinga ndio anayeweza kuivunja ndoa yake tena kwa mikono yake mwenyewe, kidole hiki kinakunyooshea wewe kwa uthabiti kabisa ili ujue kuwa uyafanyayo ndio yanaakisi afanyacho mumeo. thamani ya mwanamke ni kulinda kufuli lake nakujiuliza mara mbili je ni sahihi kulifungua kwa unaemfungulia..
siwezi kukusahau wewe mwanaume, mzandiki, jeuri, kiburi usiyejua thamani ya mkeo, tambua kuwa kidole hiki hakina jinsia lakini kinatambua kuwa mwanaume ili uwe thabiti unapaswa kuwa na msimamo, upendo na huruma kwa mkeo na familia yako,
kuvaa suruali sio kipimo cha mwanaume, wala usijidanganye kuwa sauti yako nzito ndio uanaume pia labda useme kuwa na kifua kikubwa chenye bustani ya huba ndio uanaume, siku hizi hata wanawake wapo hivyo, chamsingi kitakachosimamia uanaume wako ni msimamo kuwa na msimamo, usikatae mtoto, usibadilishe wanawake kama nguo.
wewe kijana acha uzembe shule kwanza mengine yote yapo tu, utayakuta, hayo unayohadaika nayo yaliundwa na wasomi, soma uunde yako nawe ujivunie sio unacheza na shule utakuja kuwa MZEE MPUMBAVU baadae halafu ukose wakumlaumu, binti acha kuiga mitindo yakimagharibi bibi aliyomzaa mama yako hakuwahi kuwa hivyo na ndio maana aliheshimiwa sana na mpaka leo tunautumia msemo wake usemao TAMAA MBELE MAUTI NYUMA, wewe kijana acha kushusha suruali mlegezo kwa wajuaji wa mambo watakutafsiri vibaya ilhali sivyo ulivyo. fanya uoe usiogope maisha, tambua kuwa riziki ya mtu ipo kwa mtu, kuogopa kuoa wakati una wanawake zaidi ya mmoja unazini nao halafu unawatumia pesa zamatumizi yao madogo madogo ni uzembe usiovumiliwa na MUNGU! bado niko na wewe!

Kidole hiki kitaendelea tu kukunyooshea mpaka pale utakaponyooka.