umepita muda mwingi sana sijarejea tena nilichoongea siku ile, nina imani utakuwa umekumbuka sana na unatamani hata siku ile ijirudie, nitakuwa mkosefu sana nikiendelea kukuacha utamani ule muda ilihali mimi ningali hai! acha niutumie muda huu sasa, kukwambia tena maneno sawa na niliyokwambia siku ile,
Sikuwahi hata siku moja kujua maana ya kupenda kabla sijakutana nawe, nilikuwa nabishana na waliowahi kupenda hasa walipokuwa wakidai kuwa maumivu ya mapenzi yana uhusiano na moyo, niliwabishia enzi zile sababu sikuwahi kuona hata siku moja moyo wangu ukipatwa na msukosuko eti sababu ya mapenzi! wapo waliosema kuwa mimi bado sijapenda nikawaambia nimependa sababu enzi zile alikuwepo wapembeni yangu lakini ukweli nikwamba hakuwahi hata siku moja kunifanya niumie moyo hata ikitokea amepitisha siku bila kunijulia hali, lakini hali ni tofauti tangu nikupate wewe kwakweli hunipa mawazo upitishapo siku bila kupokea salamu yako.
Nimepata nafasi Laazizi, nitaitumia viuzri kwa ajili yako |
unanimaliza zaidi ulitamkapo jina langu kwa lafudhi fulani ndani yake iliyobeba heshima inayoniambia kuwa wewe ni mke bora, yafaa kukuoa!.
wanimaliza zaidi hasa unaponihimiza mema, nakunifafanulia siri ya muda na namna unavyotembea kwa hiari bila kulazimishwa na mtu wala kusimamishwa hutembea kwa usahihi nakunitaka niusubirie muda kwa maana hauongopi utakapofika kila lililo jaala yangu litafika na ukinisisitiza kuwa kuusubiri muda huku nikijutuma ni Vazi avaalo mvumilivu na mwenye subira.
Busara zako zinifanya nikumbuke upendo fulani niliowahi kuuonja kutoka kwa mama na ndugu zangu, huwa natenga muda kuzungumza na mola wangu ili azidi kukupa afya tele, maarifa na uwezo wakufikiri zaidi kwa maana mafanikio yangu nayaona kupitia ushauri wako mzuuri na muongozo thabiti, kwa hakikia sijakosea hata siku moja kutumia muda wangu siku ile kukuomba uwe wangu.
Vijana ni wengi sana walionizidi vingi sababu ya ukweli wa watu wa pwani walosema ASO HILI ANA LILE, nikosalo mimi isiwe chanzo cha kuumia kwangu, naomba utambue kuwa mapenzi yangu ni yadhati na naamini yaliumbwa maalumu kwa ajili yako kwamaana ya kwamba yametosha kabisa hayana nafasi yakutoka wala kuongezeka, sina shaka dhamira ya mapenzi yangu yanalenga kufia mikononi mwako.
Ningeweza kusema neno moja tu 'NAKUPENDA' ili kufupisha muda na maelezo meengi ambayo sina uhakika sana kama yanakuchosha ila neno hilo nina mashaka nalo sababu mamluki wa mapenzi nao hulitumia neno hilo tena siku hizi hulitamka kwa kiingereza ili kuvuruga kabisa akili zenu mabinti, ubaya zaidi wakishatamka kwa lugha hiyo ngeni huambatanisha na tabasamu kisha kutoa pochi zao zilizonona pesa.
Kipato tunatofautiana laazizi nina mashaka leo utakataa SHILINGI kisa ni yakitanzania haya akijiminya nakukutolea DOLA ya marekani!? nina hakika atavuruga saikolojia yako sababu siku hizi maisha gharama na kauli za kileo ndio zinanivuruga sana eti laazizi NIKWELI MAPENZI BILA PESA HAYENDI???
naitazama mbele yangu naiona familia yangu ikiwa na mama thabiti, ambaye leo hii nimepata nafasi naongea nawe huku nikiyatazama kwa umakini macho yako ambayo yananieleza namna ambavyo unanizingatia na hiki ninachokwambia, naomba usidhihaki hata neno moja sababu ni ukweli kwamba nafsi inanisuta kuongea sana sababu naona kama utaniona miongoni mwa wale wanazungumza sana ili uingie kwenye kumi na nane zao zakukuongopea,
Naomba niishie hapa Mchumba nikikukabidhi hili busu ambalo naamini halina tofauti na lile busu ambalo nilikukabidhi siku ya kwanza katika midomo yako hii minene inayotema maneno mataamu yanayoionesha thamani yangu ya uanaume kila siku iitwayo leo!
nimepata nafasi mpenzi wangu zipokee hizi hisia zangu, nakupenda sana!.