MWANAMKENDEGE ; USHAIRI

 hadith hadith njoo
simulizi lake sikio
naanza safisha koo
nikupe langu tukio
eneo nikariakoo
sikujua mwanamkendege

ushungi, umbo na guu
mahabani kazamia
kiunoni kichuguu
moyoni nikaridhia
yalonisibu makuu
sikujua mwanamkendege

tabasamu lake lahaja
nikaona njia nyeupe
amejazia mapaja
si mweusi si mweupe
Radhia jina kataja
sikujua mwanamkendege

lafudhi yake yalamu
tamko lake murua
midomo yake adhimu
kicheko kajaaliwa
kumbe mja haramu
sikujua mwanamkendege

sikujua mwanamkendege
kuuza yake tabia
ucheshi wake nizengwe
pesa kushadadia
ukiwa nacho twende
mwanzoni sikutambua

kwa miguu miwili
nikazama nae hubani
sikutaka subiri
kumfikisha nyumbani
kumbe ndumilakuwili
sikujua mwanamkendege

alianzia kwa kaka
ushemeji kukataa
akasema anataka
nayeye kuzima taa
mwenzenu yamenifika
sikujua mwanamkendege

ndugu kunihabarisha
nimepotea gizani
mie nikakanusha
kwamba haiwezekani
kaka uongo kazusha
sikujua mwanamkendege

sakata jengine bosi
kiongozi wangu kazini
jamani nina mkosi
bosi kazama tegoni
wakayatenda matusi
sikujua mwanamkendege

ajabu kwangu heshima
havui ndio vazi lake
ana aibu kusema
aficha makucha yake
mwanzoni nilimtetea
sikujua mwanamkendege

penzi lake na bosi
mie nijulie wapi
huyu binti mkosi
sijui ana mangapi
nahisi ana virusi
sikujua mwanamkendege

uzuri wake hadaa
mwepesi wakulaghai
mie hadi nashangaa
kumuacha mpenzi zai
kwake hadi kukaa
sikujua mwanamkendege

Tamaa yake si pesa
hata ukiwa na mvuto
utaanzaje kumtosa
jinsi alivyo mrembo
utulivu ndio kakosa
masikini mwanamkendege

Mwengine rafiki yangu
tamaa ikamuingia
falagha chumbani kwangu
shemejie kamuingia
meona kwa macho yangu
hakika mwanamkendege

Kaiponza kazi yangu
bosi aliponogewa
kafuta ajira yangu
apate kumchumbia
masikini moyo wangu
kauponza mwanamkendege

Sihadaike na uzuri
uzuri gamba la nje
fukuto huwa uturi
harufu isikuponze
maisha ni sura mbili
sikujua mwanamkendege


 usiku uingiapo
nyota hupendezea
kwa ule wake mweko
lakini mchana jua
nisawa mwanamkendege

MUHIMU KUJUA @ukweli unaumbua

Ukweli unapotaka kudhihirika kamwe hauwezi kuzuiliwa na nguvu ama utashi wowote alionao mwanadamu.

amini nakwambia ukweli una nguvu adimu ambayo haizuiliwi kamwe na vitu kama Pesa, maneno mengi, cheo, huruma wala kujuana.

Ukweli ni jambo la kuajabia maana lina 40 zake kama ilivyo kwa siku za mwizi.

Ukweli unapotaka kudhihirika haupokei rushwa wala hongo tena humchagua yoyote hata awe ndio bingwa wa uongo siku hiyo hujikuta akianika sura ya ukweli mbele za watu.

Ni ukweli pekee ndio ambao huruhusu wenyewe kufichwa lakini unapotaka kujidhihiri hujidhiri wenyewe kwa njia zake.

ukweli jambo balaa ambalo nalistaajabia lilivyokaa! maana lenyewe ndio linaruhusu kukumbatiwa na waongo tena wakiruhusu vitu kama Chuki, Uadui, Mauaji, Ubinafsi, Rohombaya na choyo vivae vazi la Upendo, Urafiki, Wema na Kusaidiana na siku ukweli ukijiachia hubaki aibu kwa watu hao waongo.

Mra nyingi sifa za ukweli huumiza na ndio maana wengi wetu hatupendi kusadiki mambo ya kweli mbaya zaidi tupo radhi kuruhusu uzushi utufurahishe kwa kuhofia ukweli utatudhoofisha.

kwasasa wakati unasoma ujumbe huu nina uhakika kuna watu mud huu wanakutana na ukweli na wanaumia lakini hawana namna ya kuupinga

sijui kama na wewe ni miongoni mwao ila hapa nitawataja baadhi tu wanaoonja dhoruba ya ukweli

1: mgonjwa hospitalini au nyumbani au hata aliye njiani kwasasa anajua mwili wake unaumwa na huo ndio ukweli wenyewe ambao kamwe hawezi kuukataa.

2: Fukara asiye na kitu nae ni miongoni mwa watu ambao wanakutana na ukweli wahali zao na wanaumia mno wanatamani vitu vizuri wavimiliki nyumba nzuri, gari na hata pesa za kujikimu, familia bora na mengineyo mataamu yakidunia lakini ukweli ni kwamba muda huu hana ivo vitu na hawezi kuvipata kwa muda huu.

huo ndio ukweli wa hali zao na wanajua lakini watafanyaje sasa na wakati ukweli unawaambia HAKUNA NAMNA ukiiba utapigwa, ukiomba utanyimwa au utapewa masharti ambayo huyawezi huo ndio ukweli ambao maskini huwezi kuubadili kwa muda huu! ukweli bado unakutaka usubiri, naukweli zaidi ni kuwa unaweza ukaja ukapata au usipate ukafa na ndoto zako! kwani ni makaburi mangapi tumeyazika yamesheheni ndoto ambazo hazikuwahi kufanyakazi duniani.

HUU NDIO UKWELI AMBAO HAUFICHIKI!

Mwengine anayekutana na ukweli muda huu ni

3: Mtu anayekufa, huyu kwa muda huu anajua kabisa kuwa hana chake duniani anaacha kila kitu na hakuna namna yakuendelea kuishi hata kwa dakika kumi zijazo.

masikini ukweli kuwa ndio anakufa muda huu hawezi kuubadili, niukweli unaomuumiza lakini utashi wake hauna mabavu yakupinga.

nafikiri mifano hiyo inatosha.

Shughulisha akili yako ugundue mengine mengi ya ukweli yaliyo ndani yako na ambayo kwa jinsi yalivyo machungu huwezi hata kumwambia jirani yako, rafiki au ndugu.

tambua kuwa wapo watu wanaoficha ukweli kuwahusu kama vile WACHAWI, WASALITI, WANAFIKI N.k nahawa ndio mabingwa wa kuonesha huruma, tabasamu la uongo na upendo wa kughushi.

laana iwe juu yao watu hawa! ni wauaji wa kimyakimya tena ndio haswaa wale mazimwi wenye kukujua, hawakuli wakakumamiliza!

Mungu awashushie gharika, ukweli uwaumbue kabla ya vifo vyao!.

lakini hivi umeshajiuliza utaiweka wapi sura yako siku ukweli kukuhusu ukiamua kujidhihirisha wenyewe mbele ya unaowaficha.

tambua kuwa Ukweli ni kama mbegu unaweza kuificha kwa kuchimba shimo refu ardhini na miaka mingi ikapita mbegu hiyo ikachipua na ikazaa matunda yenye kukufedhehesha wewe uliyeificha lakini kuwanufaisha wale uliowafichia ambao maskini ya mungu huenda kipindi hicho wanakaribia kufa kwa kukosa lishe ya mbegu hiyo uliyoificha na ilikuwa ni halali yao.

Ukweli haufichiki Rafiki, kujaribu kuzuia na kuuficha ukweli ni mithili ya kuzuia mafuriko kwa viganja vyako viwili.

Hakuna Muongo ambaye hajawahi kuitwa mara ya pili kufafanua jambo alilowahi kulielezea huko nyuma.

hii ikiwa ni dalili ya kwamba Uongo mara zote una ulakini na maswali mengi yasiyo na majibu kwa wadadisi.

Mkweli ni mara chache sana kuulizwa jambo ambalo alishawahi kulizungumzia huko nyuma.

Hii ikiwa namaana ya kwamba ukweli una tabia yakujibu maswali yote ya anayedadisi vitu kwa kina hivyo anakosa haja yakumuita mtu kumuuliza labda tu kama anataka kujiridhisha zaidi.

na ubora wa ukweli ni kwamba mkweli akija ataeleza vitu sawa na alivyoeleza mwanzo kwasababu kila kitu kipo wazi na kina ushahidi.

udhaifu wa uongo nikwamba ukimuita mtu aeleze tena maelezo yake lazima ubabaishaji utakuwa mwingi na maelezo yatakuwa na kajiutofauti kidogo na yale ya mwanzo.

Mtafakari kwa kina mtu aliyekufundisha kusema ukweli kisha muone kuwa ni mwenye haki yakutukuzwa.

kwangu mimi ni MUNGU kwenye vitabu vyake ndio amesisitiza ukweli.

yeye ndiye mwenye haki na ndio maana ukweli unapoamua kudhihirika hakuna duniani mwenye uwezo wakuupinga.

mtafakari muovu anayekushawishi useme uongo kisha ona njia yake ilivyo fupi hana mwisho mzuri kamwe zaidi ya aibu nakudhalilika mbeleya uliowaficha ukweli kwa sababu ya maslahi yako au chuki zako.

kwangu mimi shetani pekee ndio bingwa wakuhadaa nakuongopa na kufanya wengine waongope pia.

muone uongo wake ulivyotuponza mpaka kushushwa huku tutafute kwa jasho na wenzetu wazae kwa uchungu.

Tafakari sasa ninani anayekutawala duniani kwasasa MUNGU au SHETANI?

kwa mimi naona wengi sasa mtawala wao ni shetani sababu dunia imepambwa na vazi la uongo lenye taswira ya ukweli.

kwasasa uongo ndio mali, utajiri na kila kitu chenye mvuto.

ukweli maafa, chuki, umasikini na kila kitu chenye kuumiza.

kitu pekee kinachonifariji nikwamba ukweli hauna sifa yakufichwa labda upende tu wenyewe au watu waamue kutofatilia kwa kuridhishwa na ukweli wa kughushi.

nafirijika pia ninapobaini nakuamini kuwa haitafika tamati hii dunia bila UKWELI kubainika.
itakuwa ni siku ambayo waongo watakuwa wamechelewa na wakweli watafarijika kwa kusimamia ukweli wao.

Somo langu kwako leo hii ni hili:

Ukiona kitu chochote kinawavutia wengine wengi nakukitukuza kwa kukifanya ni sehemu ya maisha yao basi rudi nyuma ukitafakati kwa kina kitu hicho.

tafakari kwa kuzingatia mambo yafuatayo
kwanza ni dunia hii ndio ambayo wengi ni wafuasi wa shetani wachache sana wenye imani ya MUNGU.

pili vitu vya kuvutia ambavyo huleta furaha kwenye dunia hii vingi hutokana na dhulma, udanganyifu na niukweli kwamba wanaosimamia haki wanapingwa vikali na ni watu wahali ya chini kabisa yaani madhalili wakutupwa.

sasa chaguo ni lako uishi kifalme duniani kwa kutangaza uadui mbele ya muumba wako au uishi kama dhalili duniani kwa kusimamia maagizo namafundisho ya Mungu wako.

SHETANI AMESHIKA MPINI WA KISU KILICHO FAKE LAKINI MUNGU AMESHIKA MPINI WA KISU KIKALI NA CHENYE KUKATA!

CHAGUO NI LAKO NANI WAKUMSIHI ASIKUKATE.

Utasadiki tu siku moja!
Na
Omar Zongo

Dear Septemba....

 "Mwezi ambao nimezaliwa mimi, Mwezi ambao nauthamini, sijui kwanini hua unakuja nakuondoka mwezi huu, September"

 Na.
Omar Zongo
 
Unaelekea wapi mpendwa!?

iweje unishushe hapa duniani kisha uniache kama hunijui!

ninani mwenyeji wangu!?

inamaana lengo lako nikunileta kisha unitelekeze!!

Jibu lako la jana usiku wakati ukifungusha nguo zako bado nalifikiria eti "nitakomazwa na octoba, novemba na december"

hivi mie nawajulia wapi watu hao! niwewe ndio umenileta hapa duniani niwewe ndio nimekuandika kwenye historia!

niwewe ndio nakufahamu bosi wangu kwanini lakini unanifanyia hivi!!

basi ungeniambia mapema kuwa lengo lako nikunishusha tu duniani halafu utaniacha!
ndio

ungeniambia namimi nikajiandaa kisaikolojia!

nani atanidekeza kama wewe! nani atajua kuwa nimezaliwa katika moja ya siku zako!
ninani atajua kuwa nina vinasaba vya baraka zako!

hujisikii vibaya labda siku ile unanishusha duniani watu walishangilia kila mmoja akisema "Wakiume kazaliwa" wengine wakiandika kifupi kwenye mitandao yao neno HBD.

neno ambalo lilinifariji mno maana wapo waliosema kuwa kirefu chake ni HAPPY BIRTH DAY..

leo unanishangaza mpendwa yaani unaondoka huku ukinifumbulia fumbo la neno hilo eti maana yake HAKUNA BINAADAMU DUNIANI.

Dear septemba kwanini lakini unaniacha wakati kumbe unalijua hilo kuwa hawapo binaadamu nakwanini umewaacha wanifumbie maneno yao ya mafumbo.

bado nahitaji unikuze kifikra usiondoke septemba! unakuwaje radhi kuniacha uyatimani mwenzako!!
Tafadhali septemba usiondoke bwana hebu niambie ninani nitamdekea kama wewe.

Angalau wewe ndio uliwapa nafasi watu wanipendao waeleze hisia zao kwangu!
wengi walileta dua na maombi ya kutimia kwa ndoto zangu.

Unaniacha!?

unaenda wapi lakini! kwanini usibaki namimi unaniachaje kwenye dunia ya dhiki namna hii!
majaribu yakuzidi! fitina mpaka pomoni! uchawi na mikosi! dhiki na ufukara huku raha ikimezwa na shida za aina mbalimbali.

hakika septemba ulioufanya kwangu ni ukatili kunihadaa nami nikahadaika ukanishusha duniani huku wewe ukiendelea.

ahadi yako yakuwa utarudi tena nimeielewa ila tambua kuwa wewe sio mpangaji hivyo sema 'Ishaallah'.

nisalimie uendako maana sina namna yoyote yakukuzuia!

Sitakwambia kwaheri maana neno hilo huua kabisa tamaa yakukutana tena.

Gud bye....
Dear Sept.....
Wako
Mr.Experience

chuki shairi

chuki imekuwa vazi,
 limewakaa mwilini.
kulivua kwao kazi,
haling'oki mauongoni
kama dunia twapita
chuki ya kazi gani.

imewakaa mwilini
imetuwama nyoyoni.
yajionyesha machoni,
imegeuka miwani.
kama dunia twapita
chuki ya kazi gani.

chuki pini nyembamba
yapenya kotekote
si baba wala mjomba
atakuchuki yoyote
kama dunia twapita
chuki ya kazi gani

chuki ikikuhadaa
pigana kuiambaa
ni jumba la karaha
sio kiti chakukaa
kama dunia twapita
chuki ya kazi gani.

chuki ina hila zote
haingojei sababu
ikukuzidia kete
itakuvaa taabu
hii dunia twapita
chuki ya kazi gani

dunia hii twapita
hatutaishi dawamu
litakufika gharika
chuki haina nidhamu
swali nakuswalika
chuki ya kazi gani

ulimwengu una adha
njiaze kadha wakadha
itakupata bughudha
fakiri wakujifunza
kama dunia twapita
chuki ya kazi gani.

SHAIRI: JAWA

"Ni baada tu ya rafiki yangu fulani wakati nipo chuo kuniomba nimuandikie utenzi kumuhusu, kila siku nilikuwa namuahidi nitamuandikia ila siku moja abra ikanishukia na tenzi nikamtungia...."

Na.
BIN ZONGO

Jawa
Malkia
Zawadiwa
Jaaliwa

Jawa
Tunukiwa
pendelewa
Zidishiwa

Jawa kwani nani
mtu gani, ana nini?
jawa mwenye hadhi
sio mpuzi ni azizi

roho yake nyeupe
theluji mithili yake
sema nini akupe
kilicho uwezo kwake

haiba ni vazi lake
stara jaala yake
ucheshi sifa yake
maringo hayapo kwake

Wa UBAVU WAKO

Wazungu wanamuita  soulmate

je unamjua mtu huyu? umeshakutana nae? unadhani yuko wapi??

anza sasa kumfikiria wa ubavu wako maana ni muhimu sana mtu huyu!

kama umempata hewallah laa kama bado fanya hima umtafute mashariki na magharibi usiache akaendelee kuteseka nawe kuteseka kwa nyinyi watu kuishi mbalimbali.

huyo ndiyo sahihi kwako, katika mahusiano yako ya urafiki, mapenzi mpaka ndoa.
yeye ni muendelezo wa akili zako zinapogota kufikiri! yeye ni msaada wa dhati unapokwama katika hali yoyote!

yeye nifaraja unapotokwa na machozi!

amini nakwambia ni mtu aaziz sana huyu.

hatoruhusu ulie! udhoofishwe na mawazo mabaya na ujihisi mpweke.

atakufanya useme "kwanini sikumpata tangu mwanzo mtu huyu!"

hata ujinga wake utakuwa ni burudani kwako!
yote sababu ni ubavu wako umetokana na yeye
wanaoamini uumbaji wa Adam na hawa watasadiki hili

kwanini uendelee kuteseka na mtu ambaye hamuendani? kwako wewe moja jumlisha moja ni mbili kwake yeye ni kumi na moja.

kwanini unalazimishs mtu ambaye hamrandani kimtazamo eti! kwanini unajisahau na unasahau kuwa yupo mwenza wako, wa ubavu wako na ambaye ni sahihi kwako.

sikia, sio rahisi kumpata waubavu wako!

ndio, sio rahisi hata kidogo.

sababu Mungu alipokuumba nakisha kumuumba aliwaamrisha mje duniani lakini sio pamoja amewaamrisha kila mmoja aje kwa mtindo wake.

huenda we umezaliwa Dar es salsam halafu waubavu wako amezaliwa Magila huko muheza Tanga ndanindani.

ila kwasasa yupo kikazi muhinduro!

bado hamjakutana!! wala hamna dalili, na huenda msikiutane!
usipokuwa makini.

usilisahau hili, lizingatie na uongeze umakini katika maombi ili ukutane na waubavu wako.

acha nikukumbushe! baba etu Adam na Mama etu Hawa! walipoamrishwa kushuka hapa duniani nao pia walitenganishwa na ilimchukua muda mwingi Adam kutembea akimtafuta Hawa.

hatimaye akampata!

ilikuwa ni siku ya furaha mno kwa wawili hawa kukutana!

Hapa tena naomba nikumbushe vitu muhimu ambavyo ni asili ya mwanamke ingawa kwasasa vinapuuzwa!
kwanza Umeona hapo juu Adam ndio alihustle kumtafuta Hawa! huezi amini Hawa yeye ivyoshushwa akatulia tuli mahala aliposhushwa hakujishughulisha kamwe kumtafuta mwenzie.

Dah wanawake Mungu anawaona!

Pili siku ambayo Adam anamuona Hawa baada yakutembea maili nyingi kuchomwa na miba, kukimbia wanyama wakali na dhoruba kadha wa kadha Huezi amini Hawa alikuwa anajificha kwa aibu.

wala hakufanya maigizo ya "waooh jamani tumeonana tena! nimekumis wewe!!"

No, hajafanya hivyo kabisa..! ndio kwanza alikuwa anajificha ficha kwa aibu na niyeye ndiye wakwanza kumuona Adam lakini hakumshtua kabisa kwa aibu mpaka Mzeebaba alipomuona mwenyewe.

Aibu ni asili ya mwanamke na sio uchakaramu wakuropoka hovyo kama umekunywa maji ya chooni.
mxxxxiiiieee!

Turudi kwenye mada! tambua kuwa waubavu wako yupo!

somo hili limewapita watu kushoto ndio maana maumivu ya mapenzi kwasasa mengi mno.
yamejaa pomoni!

maumivu lazima yawepo sababu watu wanachukuana chukuana tu bila kujua kuwa unayemchukua sio aliyotokana na ubavu wako.

sasa unadhani asikuumize kwakuwa wewe nani!

atakuumiza tu! na tena mie nasema uumizwe tu maana hakuna namna sasa.

ni lazima akuumize sababu haoni uchungu wowote maana wewe sio wake kwa hivyo nafsi yake haimsuti hata kidogo kukutenda.

ni tofauti na waubavu wako! yeye akikuumiza hata kwa bahati mbaya atajutia kosa hilo na litamuumiza sana kama vile ameumizwa yeye.

ina raha ukimpata mwenza wako! acha tu yani...

ukilia atalia na wewe hata kama hajui kinachokuliza!
tatizo lako litamgusa kama vile lakwake

kiukweli ni somo pana hili kuhusu waubavu wako na kwa vipi utamjua kama huyu ndiye.
kwakweli inahitaji umakini sana maana sasa wamejaa wengi kila mmoja akijifanya ndiye yule wa ubavu wako.

ndiyo! wengi huweza kuja kwako wakiwa wamesheheni sifa lukuki za waubavu wako.
nina uhakika laiti kama wangelijua jina lake basi WANGEKUJA KWA JINA LAKE! pia.

tena huigiza nakujikuta wakizidisha mbwembwe za mambo mazuri kua
shinda hata waubavu wako!

hawa wapo na kwasasa wamezidi ulimwenguni!
utawajuaje!?

hili ni swali zuri najibu lake ni ngumu kuwajua hivyo umakini unahitajika na kusubiri huku ukimuomba MUNGU ni njia iliyo sahihi zaidi.

acha tamaa ya gari zuri, pesa na maisha mazuri!

huenda siku moja waubavu wako akaja na vitu hivyo!

au vitafute kwa njia nzuri ya halali ili siku moja uvitumie ukiwa na wa ubavu wako.

maana athari zakuhadaika na waubavu wako wauongo ni nyingi nitakutajia chache.

kwanza hatakuthamini kutoka moyoni bali ataigiza tena zaidi akiwa mbele ya macho yako tu, ukiondoka atakung'ong'a nakukupuuza.

atakuwa tayari kufanya lolote zuri ili aendelee kukutumia, kukuchezea nakukunyonya vyote anavyovitamani kutoka kwako,

amini au usiamini ukipatwa natatizo kubwa utalia na ndugu zako yeye hataguswa, abadan.
pia mazuri yake yana mwisho yaani inafika kipindi hafanyi tena aliyokuwa anayafanya mwanzo mazuri yaliyokuwa yanakuvutia.

na hiyo ni tofauti na waubavu wako! kamwe narudia tena kamwe hawezi kuacha kusimamia furaha yako.
hata asiposema lakini vitendo utaviona na vitakudhihirishia kuwa yeye kwako ni Washida na raha, shibe na njaa, uzima na maradhi umasikini na utajiri.

Fumba macho umuombee waubavu wako popote alipo asogee karibu yako akutoe mikononi mwa walaghai.
pia asiendelee kutumiwa na watu ambao sio wake.

ni mahusiano machache sana duniani yamekamilishwa na wawili ambao wameumbwa wawe wao
na utawagundua kwa historia zao, itikadi zao na namna ambavyo walivyo tu utawagundua na utawafurahia!
watakuvutia!

mtandaoni shairi

 Na
Bin Zongo

karibu mtandaoni
uyaone ya duniani
karibu keti makini
ujue nani ana nini

bando la uhakika
bando halina shaka
insta kunafikika
twitter nakadhalika

simu yangu smart
tabu tabu sipati
maridadi internet
karibuni tuchart

naanza nae Kimambi
Mage haeshi vitimbi
leo kapost mengi
post zake hupingi

alaani serikali
ina nyingi dosari
viongozi dhoflehali
insta kote zohari

mateja wazodolewa
polisi wanatakiwa
mkuu kashaamua
mkoa kusimamia

apost vita vyaanza
biashara
tokomeza
harakati ndo imeanza
madawa kuyamaliza

wengine niwapinzani
wameanzisha tafrani
eti mkuu hajulikani
amesoma shule gani

mengi ya mtandaoni
hufurahisha moyoni
eti mchungaji gani
amezaa kwa kuzini

yule na wimbo mpya
huyu na demu mpya
mondi kaibua jipya
bifu limeanza upya

PANDE MBILI ZAZOZANA

Pande moja imevaa gauni ishara ya mwanamke nyengine imetinga kanzu ishara ya mwanaume!
moja ya kanzu yasema wake waharibifu uaminifu hawana wamejawa mapungufu.

gauni lataharuki almanusura livuke lasema hayasadiki waume wanachosema wao ndio mamruki uaminifu hawana.

kanzu yatetemeka mate kinywani yatoka maneno yaropoka waume wametukuka, wanawake kwa vibweka duniani wasifika.

Gauni latabasamu kwa dharau na kiburi lasema huna nidhamu mwanaume baradhuli ukishaishiwa hamu mwanamke humjali
hauna ubinadamu wanaume ni zohari.

Kanzu yakunja ndita mijicho yachomoka, kukupiga sitosita hivi ndivyo yaropoka
sema nami kwa nukta dharau sitazitaka.

Mwanamke gauni asema sikuogopi sitoshuka chini maneno yangu silipi
tena yana thamani wanaume ni makapi.

kanzu yagadhibika busara yamtoka matusi aropoka gauni lamcheka.

Bi Gauni : tukana utukanavyo ila habari unayo, hivyo ndvyo mlivyo waume mapoyoyo, hasira zenye ujazo ni mapungufu hayo.

Bwana Kanzu : wanitafutia kesi mwanamke hayawani nyinyi bidhaa nyepesi twawaona mtaani siku izi mna kasi sio kama wazamani.

Bi Gauni : sisi ni mama zako tazama mdomo wako huo udume wako ukome matusi yako zungumza kwa staha nione udume wako.

maneno hayo mkuki yamchoma bwana kanzu ukweli haukwepeki umemvua kwa nyavu.

Bwana Kanzu : nisamehewe kwa hilo mie kanzu kweli juha lakini mnapotea kutanga tanga najua waja msotulia gauni nakuambia.

Bi Gauni : ninyi apo ndio chanzo chasisi kuhangaika, mmetufanya chotezo nyie maji mwamwagika mbinu zenu hamnazo kulaghai mwasifika.

Bwana Kanzu : tatizo uaminifu ndio kitu mnakosa waume walinganifu hatujaiga usasa
usagaji maradufu
eti mambo yakisasa.
hamnayo tena hofu
kujibadili kabisa.

Bi Gauni : ushoga nao wanani waume mwaaibisha
hayakuwepo zamani
mambo haya kabisa
aibu hebu oneni dunia itawakosa
marijali hatiani
wamejaa wakibisa.

Bwana Kanzu : umenionya matusi sasa mbona watukana mwanamke wewe nuksi tafsida hata huna
utakupata mkosi baba akikupa lana.


Bi Gauni : ukweli unaumiza mithili ya tusi kuu
nikweli nakueleza
wanaume mpo juu
tamaa zinawaponza
kutaka mambo ya juu.


Bwana Kanzu : midomo yenu jeuri ndio mana hatuwaoi
kimewajaa kiburi tunawatoa nishai
maisha yenu dhalili
acheni kujidai.

Bi Gauni : kuolewa kazi gani waoaji siwaoni wasasa ni matufani simuoni wathamani
mwanamke pambo ndani ataka mtu makini.

Bwana Kanzu : siwezi bishana nawe waweza nipa kesi bora niachane nawe hoja zako nyepesi.

Bi Gauni : toa zakwako nzito mwanaume huna haya mmegeuka watoto siku izi twawalea mambo yenu mpito mmezidisha mabaya.

Bwana Kanzu : nanyinyi hamjioni mavazi yenu dhalili.
mwakatiza mtaani
utupu juu ya mwili
tena hatuwatamani
kwasasa hamna dili

Bi Gauni : nacheka cheko la haja mwanaume hujijui tumeumbwa kwa lahaja nzuri huitambui tena andiko likaja kujiremba tanabai.

Bwana Kanzu : urembo gani ujinga utupu wenu thamani
urembo huo napinga
haupo maandikoni mwanamke we mjinga kutetea ushetani.


Bi Gauni : tumeumbwa tofauti usituhukumu wote
mwanamke humkuti
kaacha maungo yote
hao uwasemao sio wanaake wote.


Bwana Kanzu : kumbe walijua hilo sasa porojo zanini
hata sisi nasi pia tumeumbwa kwa makini wapo tulotunukiwa urijali mauongoni na wapo waliopewa ukike kike fulani.

Bi Gauni : basi kama hivyo ndivyo lawama weka pembeni sote tumeumbwa hivyo tofauti ni kichwani!
tuache habari hizo nakuhitaji chumbani nataka muendelezo
wa hoja tukiwa ndani....

Gauni latabasamu huku likijisemea "wanaume bwana yakwao ni haya tu haya hoja gani za chumbani.....hahahaaa makubwa haya acha nikamsikilize...!"

Na
Omar Zongo
SIMULIZI ZINAISHI

USISAHAU CHANGAMOTO @UjanaMajiYamoto

Na.
 Omar Zongo

Ishi nami kwa furaha ila tambua siku moja kuna karaha hivyo usisahau kujiandaa!
Usisahau changamoto ambazo kwa jicho langu naziona zimejaa pomoni!
kupendana angali vijana ni suala lamaana lina taadhima na kubwa heshima!
lakini usisahau kuwa ujana ni laana, jumba la usahaulifu na upotofu na kwa taarifa yako wengi waliouvamia sasa hivi ni wafu!
walio hai wanasubiri andiko litimie!, afya zao dhalili, wakenda kama walevi, wamedhoofu mwili, nguvu zao kumbukizi, kwao naona dalili ya kupoteza nguvu kazi, ni baya suala hii UJANA kweli maradhi.
Usisahau changamoto ya kwanza kwetu Ni Ujana!
tena hii ni ya Moto yapasa kuomba sana.
tuvuke mito, vijito tukeshe kuombeana!
kwenye baridi na joto tubaki tumeshikana.
Tena tuache utoto laa sivyo tutaachana.
Ujana ni changamoto naomba kumbuka sana!
wengi eti tulizo wanasema lipo kwa wazee! eti "vijana mzozo bora tuwapotezee" mapenzi sio mchezo yanaumiza
aisee!
singeni khabari hizo mchumba uzirejee, sikio lako chotezo changamoto zipokee
tena silete mchezo amani nisogezee!
ujana una kiburi dhahiri chaonekana! tena dakika sifuri tayari tumegombana ninani wakusubiri ujana subira hauna.
kijana bado nalipa nguvu tele maungoni.
ukizingua nasepa wasemavyo wa mjini.
anitakae nampa damu changa mauongoni, ujana unayo pupa
tulia na wako ndani.
mwisho wa ujana aibu kwa wale waso busara!
tulia wangu muhibu tuichore wote dira!
kesho tukiwa mababu simulizi yetu bora.
ujana wangu nalewa jaribu kunielewa pambana na hali yako katika kunikomboa
tumia utashi wako nipate kujielewa nimimi ndio mwenzako sahihi wa rika lako watoto nitakugea iweje uende zako sihadaike na wakubwa, wazee watakufia.
navaa nguo dhalili maungo yangu yawazi
na hizi ndizo dalili za ujana ipo wazi endelea kuhubiri nibadilishe mavazi usiseme wasubiri kitafakari kizazi.
watoto wetu wawili wataurithi ushenzi.
watu wazima muhimu wanajua kukutunza.
mie kijana nidhamu yangu yakuokoteza. haya yote nafahamu ila changamoto tunza.
hata wao walikuwa enzi zao kama mimi chamsingi vumilia tupendane kama nini.
wazee watakufia usalie kilioni ipite miaka mia ujutie mauongoni maradhi kashakugea na watoto yatimani.
chamsingi vumilia mimi na wewe pamoja
makosa kujirudia ujanani si kioja heshima kuzingatia ndio jambo nalingoja,
endapo kinipatia watatuzika pamoja,
kupendana ujanani ni suala lapendezea kutulia mahabani ni jambo adimikia alaaniwe shetani balaa katuletea wazee wakazi gani acha kuwasujudia.
ujana wao wanani mpaka uzee wa kwako epuka uhayawani tulia nami mwenzako.
enzi zao ni zamani walikuwa rika lako,
ujana wako ni shani
tumia na rika lako.
wao watu adhimu, adimu na wa muhimu kupata kwao wosia ni jambo la tabasamu,
na sio kukuchumbia kwangu ni jambo dhalimu.
ndio nina changamoto rika langu potofu sijauacha utoto mambo yangu pungufu,
kichwani nina ndoto ya kuwa maarufu
na kumiliki watoto warembo walinganifu.
haya yote yataisha ukiwa mkamilifu,
usiache kunikumbusha usichoke uvumilivu.
Usiufate mkumbo tengeneza nyumba yako!
watakupiga kumbo wakung'ong'e wenzako!
hili sio fumbo nasema na nafsi yako!
sasa kamata nyundo uponde ujana wako.
nami napanda upendo uote pembeni yako.
Usisahau Hii Changamoto nikubwa isiyo mithilika tena sio ya kitoto imesheheni vibweka!
moshi kugeuka moto ni jambo latambulika
tone kijito na mto hatua zahesabika,
haiwi bahari kuu bila ziwa kuvukika.
Andiko hili ni lako wahuba nikupendae wala sio la mwenzako ni wewe nikutakae samehe makosa yangu ujana wangu uelewe nataka nibaki kwako wivu wako uondoe.
najitambua mwenzako ujana kuudhibiti ingawa wanizidia una nyingi tashtiti Mungu kumrudia ni mbinu tuidhatiti
Muhimu kudhamiria tufike wote Tamati.

USINIACHE MUNGU WANGU!

Naandika kwa mtindo wa kuomba, maombi ambayo yametawaliwa na unyenyekevu na sura yangu ina dalili zote za kuonesha kuwa nina uhitaji wa ninachikiomba! tena sio uhitaji mdogo nina uhitaji mkubwa wa nikiombacho leo.

Yupo mpumbavu mmoja, ambaye daima sura lake analikunja kwa jazba kila anaposikia nataja jina lako kwa unyenyekevu nakumuita yeye kwa kiburi tena nikimtukana kumuita Mwanakharamu.
ni yeye ndiye ambaye ananitamani kuninyakua nakuniadhibu vikali, anatamani niwe mtumwa wake, ananiwinda kwa juhudi zake zote na hata siku moja hajachoka kunifatilia.

ni huyu maaluni ndio leo amenifanya ninyooshe mikono yangu kwako nikiomba kwa unyenyekevu nikikusihi kamwe usiniache maana dude hili linanitamani leo kesho niwe rafiki ake.
lengo lake nikuasi Mungu wangu na nifanye yale uloyakataza

hakika nakuambia sijawahi kumpenda kiumbe huyu tangu nilipoijua dhamira yake kwangu.
leo nina machache nataka kukwambia MUNGU wangu na nakuomba sana unipe msaada wako kwa kuniitikia Amina.

kwanza naomba ujue kuwa nina uhasama mkubwa na huyu Mpumbavu mwenye majina mengi yalaana.

niyeye ndio anaitwa Shetani, ibilisi na pia ndio huyu kiongozi wa waovu ambaye daima anapenda kunishawishi nitende uovu.

Ponya yangu ni jina lako MUNGU wangu na kinga yangu ni Imani ya dhati kwako Mungu wangu.
kwa sababu yako nimetangaza vita na mjinga huyu na simuogopi kamwe lakini chamsingi tambua MUNGU wangu bila wewe siziwezi hila zake.

usiniache Mungu wangu hata kwa sekunde moja maana nina hofu anaweza kuitumia sekunde hiyo kuniangamiza daima.

mimi nina kiburi kwake napingana na matakwa yake na niyeye pekee ndiye ambaye naweza kutangaza mbele za watu kuwa simpendi! namchukia mfanowe hakuna.

ninapowaza safari hii bila wewe kiukweli hofu yangu dhidi yake yanizidi mauongoni lakini ujasiri hunizidi kila ninapokumbuka uwepo wako kwangu.

usiniache mungu wangu hakika nina hofu na shari za kiumbe huyu bila wewe siwezi kumudu kupingana nae maana nia yake ovu nikunigombanisha nawewe.

Mungu wangu usiniache ili niendelee kumtukana nakumlaani mpumbavu huyu mwenye nia yakunipeleka jahanamuni.

natunishiana nae misuli kwasasa nikitegemea wewe upo, namtemea mate usoni kwa dharau na kumkejeli kwa maneno ya shombo yeye hanifanyi kitu sababu anajua upo na wewe ndio mtetezi wangu

sura lake baya lenye jazba dhidi yangu naliona na nina uhakika akipata hata kajiupenyo kadogo tu kakunizuru basi atafanya hima ili niangamie.

mwanzoni alinirimbikizia mikosi, nikakosa hata vinavyonistahili.

akanidhulumu haki zangu nikaishi kwenye udhalili na pia haitoshi akanifanya muovu mwenzake.
ni uwezo wako Mungu wangu na huruma zako ulizo nazo ghafla anashagaa yale yote aliyonilimbikizia yamegeuka neema zinazonifanya nikusujudie nakukutukuza wewe MUNGU wangu.

anashangaa ukarimu wako, umenipokea! ukanisamehe nakunijaza nguvu na kinga! anashangaa ule mzoga wake aliokuwa anautumikisha umekingwa na malaika wazuri kutoka kwako.
Usiniache MUNGU wangu maana mie sijui hata sura ya mpumbavu huyo lkn sifa zake zenye kutu nimezijua kupitia wewe.

usiniache MUNGU wangu nakuomba endelea kunikinga na huyu kiongozi wa wachawi wenye kuroga, mahasidi wenye kuhasidi, makafiri wenye kukufuru na waovu wenye kusujudia maovu.

Usiniache MUNGU wangu maana bila wewe naogopa kwakweli maana huyu MJINGA atanigeuza kiti chake kule Motoni na kunifanya tena MTAJI wake hapa duniani.

Ninajikinga kwako Nashetani Mungu wangu! usiniache kamwe.

@IshiKikamilifu
          2017

MASIKINI "MSAMAHA" @thamani yako haipo!!


uko wapi rafiki yangu msamaha, kusema kweli nimegundua leo kuwa haupo katika dunia hii maana mimi mwenyewe nimeshindwa kujisamehe mpaka muda huu kwa uzembe wakupoteza andiko langu la mwanzo.
Na
Omar Zongo
Andiko langu lakwanza kukuhusu lilikuwa zuri lapendeza nililipamba kwa vazi la mafumbo juu yake nikalivika joho zuri la tenzi kisha nikalipulizia marashi yenye misamiati ya lugha adhimu ya kiswahili!
ndio!!
andiko kukuhusu wewe MSAMAHA nililipamba likawa kamili kwa kusomwa lakini sijui ninini masikini ya MUNGU ghafla bin vuu tsunami la teknolojia ya simu inayohitaji chaji kuwa pomoni muda wote likanivaa simu ikazima kabla ya andiko langu kukuhifadhi ukahifadhika.
kwa namna ambavyo nilikupangilia ukapangika wallah naapa sikuwahi kupangilia vizuri andiko lolote kabla yako!
nafsi ikiwa imejawa lawama yakutokuwa makini na chaji yangu nikakumbuka kujiomba msamaha na nilipofanya hivyo angalau nafsi ikawa huru lakini nikaja gundua kisasi na simu yangu hakikuniisha moyoni nilitamani kuibamiza chini.
ufukara ndio ukanionya nakuniambia niibamize nione kama nitapata tena simu nyengine hivi karibuni.
tuachane na hayo leo nimedhamiria kuweka sononeko langu kwako wewe MSAMAHA!
Hivi ulizaliwa lini na kipindi gani uliishi duniani hapa na kifo chako kama kimetokea ilikuwaje na kama ulizikwa ulizikwa makaburi ya wapi???
nakuuliza hivi nikiwa na sababu lukuki maana kwasasa thamani yako siioni!
waja tumekuwa wagumu kusamehe! kwasasa ukikosea jiandae kulipiziwa na tena unafiki wenye sura ya msamaha umetawala hivyo kufanya mtu awe rahisi kusema amekusamehe ilhali roho yake ikiwa na dukuduku lisiloisha.
uko wapi rafiki yangu msamaha, kusema kweli nimegundua leo kuwa haupo katika dunia hii maana mimi mwenyewe nimeshindwa kujisamehe mpaka muda huu kwa uzembe wakupoteza andiko langu la mwanzo.
nijuavyo mimi MSAMAHA wewe nineno la thamani sana tena hautamkwi kiholela kwa mtu aso namaana.
mfano mie sidhani kama watu kumi wameshafika ambao nimewahi kuwatamkia neno hilo.
nikirudisha fikra nyuma nagundua niwachache mno ambao niliwakosea na kutokana na utu wao na thamani kubwa walio nayo nikawatamkia neno wewe MSAMAHA!
huwezi kuamini kuna wengine kama bado wapo hai kamwe hawawezi tena kupata neno hilo kutoka kwangu na hiyo yote nikwasababu enzi za thamani yao kwangu huenda imeshaisha.
huo ni mfano wakukujulisha kuwa wewe ni miongoni mwa mja uliye na thamani utokapo kinywani! na sio wote wanastahili kukupokea.
kama mtu huna mpango nae wala hauna umuhimu nae itawezekana vipi kumkosea nimegundua leo tena baada yakukutafakari sana nimeona kuwa tunawakosea tulio nao karibu kwasababu ndio watu wetu wamuhimu katika kukamilisha furaha yetu nandio maana umuhimu wa neno MSAMAHA huwahusu sana watu hawa.
lakini pia katika tafakuri yangu leo nimegundua kuwa ni watu hawa ambao nao hawaoni tena thamani ya neno wewe MSAMAHA.
wanakudharau vijana wa kileo wanasema UNACHUKULIWA POAH sana siku hizi.
enzi za wahenga msamaha ni tamko ambalo lilikuwa limebeba majabari mazito matatu Hekima, Busara na Uvumilivu.
majabari hayo yalikuwa ngao kwa anayeomba msamaha na anayepokea msamaha huo nakusamehe! tofauti na sasa.
enzi za dot.com msamaha ni neno ambalo analitoa mtu dhalili, mwenye uhitaji na fakiri mbele ya anayemuomba Msamaha.
nimetumia staha lakini kutokana na kuwa ashahkum si matusi basi acha nifunguke kuwa wakileo msamaha hutafsiri kuwa ni lofa, mzembe ambaye hawezi kujizuia kukosea.
thamani yako haipo Msamaha! watu waleo wamekosa uvumilivu kamwe hawataki kuvumilia makosa!
wapo wachache ambao mara moja watakusamehe lakini hawatasahau na ukiteleza mara ya pili hukumu kali ya machungu itakuhusu tena usije ukathubutu kuleta falsafa za Isaah Bin Maryam eti Samehe Saba mara sabini, watakutukana matusi yanguoni.
iko wapi thamani yako rafiki yangu msamaha mbona ninaowathamini hawashtuki tena hata nikikukimbilia wewe nakukutamka mbele yao.
mbona wananihukumu wakati wewe umeletwa ili kufidia mapungufu tuliyoumbwa nayo wanadamu.
kwani nani asojua kuwa nisisi waja ndio hujifunza kwa wingi kutokana na makosa na pia asiyetambua kuwa ni dunia hii ndio haina kiwango maalumu cha makosa yaani yapo tuu yameumbwa kwa mtindo tofauti tofauti na wakati mwengine unaloona wewe kosa mwenzako analiona ni sahihi kabisa.
Msamaha jitokeze basi kuokoa dunia hii ikibidi kukosoa pia zile sheria ambazo kiini chake ni UMOJA WA MATAIFA.
zikosoe na uziambie kuwa katika kanuni na taratibu za kumuadhibu mtu wangeweka pia sheria yakusamehe maana sio wote wakosefu kutoka ndani mioyo yao.
natamani ungejidhiri machoni mwangu MSAMAHA ningechukua hata harufu ya jasho lako nikaiweka chumbani kwa mwanamke wangu ili aione thamani ya kusamehe na anisamehe hata kwa makosa ya kesho na keshokutwa.
ningechana hata upande wa vazi lako nikawaonesha wote ninaohitaji msamaha wao wa makosa yote yaliyo na yanayokuja ili wanisamehe kwa dhati ya moyo wao.
KUMBUKA KUWA UMEUMBWA KWA MAKOSA NA UTAKOSEA, LEO KESHO NA HATA KESHOKUTWA KAMA UTAKUWEPO UTAKOSEA TU.
KAMWE HUWEZI KUYAEPUKA MAKOSA MPAKA UKAMILIFU WAKO UTAKAPODHIHIRIKA KATIAKA ILE SIKU YA MWISHO YA PUMZI YAKO!
USICHOKE KUSAMEHE SAMEHE KADIRI YA UWEZO WAKO!
NAWEWE UTASEMEHEWA SIKU MOJA!
tena utasemehewa siku ambayo una uhitaji kweli MSAMAHA!

KESHO HAIJULIKANI @Ishi Ki kamilifu

Na
Omar Zongo

Siku za mwisho kabla ya kifo chako nakiri niliona mabadiliko ya kitabia! ulipenda kukaa mwenyewe! upole ulikuvaa na hata chakula kilikuwa hakipandi jambo ambalo silakawaida kwako, kiukweli upweke niliuona kupitia macho yako na sijui kwanini nilikupuuza.

leo natamani kujua nini chanzo cha wewe kuwa hivyo lakini sina namna yakusikia sauti yako ikinieleza.

je ni hali ngumu ya maisha ulikosa dira na muongozo???

mimi sijui..

je ni mapenzi yalikuvuruga kiasi kwamba ukakosa ushauri wangu mimi kaka ako hivyo ukaamua kujimaliza???

hili pia mimi sijui

wakati mwengine nawaza labda kutokuwa karibu tena nawewe tukibadilishana mawazo, kucheka na kutaniana ndio chanzo maana ni ukweli kuwa ulinizoea sana na ni mimi pekee ndio nilikuwa kaka na rafiki yako pia.

bado hili nalo sina uhakika nalo pia.

kwa ufupi nateseka kwa kutaka kujua kilichokufanya ukakatisha pumzi yako.

sijui kwanini sikutilia maanani nilikupuuza uliponiomba kuzungumza nami hata sauti yako ikiniomba kuzungumza nami bado inajirudia masikioni mwangu "bro nina shida naomba tuongee kidogo" ulikuwa huchoki kuniomba kwa kusema aina hii ya maneno.

ukubwa kweli jalala sikujua najutia!

leo hii nagundua kuwa mimi ndiye sababu ya kifo chako ukweli nina hatia!

uliniganda kwakweli mpaka nikaona kero, ukaka nikasahau nikajawa na kiburi nikakukwepa waziwazi nikidai niko busy laiti kama ningejua ningekuacha tuwe wote,nikusikilize na nijue unakabiliwa na nini mdogo wangu.

nimimi na wewe tuu mama etu katuzaa mdogo angu kipenzi huzuni inanijaa laiti kama ningejua ningekuazima sikio.

sio kawaida yako kuja kwangu asubuhi, ulikuwa mpole sana furaha hukuwa nayo, utani na shem wako hata haukuwa nao na haikuwa tabia yako upole ulio nao sikuyajua mwenzako maisha ni mapitio nakumbuka sura yako mdogo wangu Kihiyo.

hukutaka chakula changu wala hata senti yangu, hukutaka kulala kwangu wala chochote chakwangu ulitaka faraja yangu sikujua mdogo wangu kwanini hukuniambia nikaacha ujinga wangu.

nahisi maisha yalikupiga mbele yako giza tupu dili zote hazitiki ukata ulikuzonga, kila unachotamani kukipata vigumu hakuna matumaini ninani wakumwambia!?

mitihani ya maisha msomi ila masikini, kazi zakubahatisha kesho yako haijulikani nimimi ndio kaka yako ulitaka nikupe moyo ndio mana ukaja kwangu nami nikawa mchoyo kukupa tu muda wangu nikaona ni gharama masikini mdogo wangu ulizidi kukosa dira.

sikupata muda asilani wakusema nawe japo kidogo usiku niliporudi nilijifungia chumbani kwangu tena ulinisikia nikicheka na mke wangu.

kudamka mapema ikawa tabia yangu mradi nisisikie una nini mdogo wangu nilipo nina kilio nasutwa na nafsi yangu!

nilisahau kabisa vifo vya wazazi wetu aliyeanza ni mama na baba akamalizia hivyo mimi kubaki nawe sikuweza kupinga.

mimi nikawa baba na mama kukufariji namlaani shetani kunisahaulisha wajibu.

ghafla nikapuuza kwamba mimi ndio mfariji wako mwanzo nilikuwa nakupa moyo usome kwabidii nakukusihi usikate tamaa utafanikiwa lakini mara nikasahau kabisa kuwa nimimi ndio nilikuwa nguvu yako pale unapokwama.

kiburi cha pesa kilinifanya nisahau kuwa wewe bado mdogo hujakomaaa na ungehitaji muongozo wangu hasa unapokosa muelekeo.

nilisahau kabisa kuwa maisha ni magumu mno na yana mitihani na yoyote anastahili kupewa moyo!
nilisahau kabisa kuwa neno langu la faraja ni tumaini kwako kuliko pesa na chakula.

leo hii sijui hata nini kilikusibu mpaka ukakosa raha na ukakata tamaa nakuamua kujiua!


muda wangu niliuona una thamani sana na hata ulipoomba kuzungumza nami nilisema "tutaongea baadae dogo" bila shaka ulishangazwa na tabia yangu hii maana siku zote za ukuaji wako nimimi ndiye nilikuwa wakwanza kukufuta machozi ukilia na ulipoanguka nimimi ndiye nilikuwa pale kukuokota.

maisha yamenibadili yamenifanya nijidanganye kuwa umekuwa na sipaswi kuwa karibu yako bila kujua kuwa mimi pekee duniani ndio ndugu yako.

nilizoea kugusa nywele zako kwa upendo nikikubembeleza ulale enzi za udogo wako siamini leo kama nagusa majani namchanga kwenye hili kaburi lako.

nisamehe mdogo wangu! nisamehe sana kwakutokupa nafasi yakusikiliza kile kinachokutatiza maishani!

siamini kama sipo nawe tena leo nimepata funzo!

NI VEMA KUMUAZIMA SIKIO KILA ANAYEKUOMBA KUONGEA NAWEWE PENGINE KATIKA MAONGEZI YENU NENO LAKO MOJA LIKAWA MSAADA MKUBWA KATIKA MAISHA YAKE NA LIKAMUONGEZEA SIKU ZA KUISHI AU LIKAMBADILISHIA MAISHA YAKE!

TUMAINI LA WANAOTUPENDA LIPO KWETU TUSILIZUIE KUWAFIKIA HASA WANAPOLIOMBA!

MAISHA NI MAFUPI MNO HAKUNA KINACHOUMIZA KAMA KUGUNDUA HAYUPO TENA DUNIANI ULIYEPESA KUMFANYA AWEPO NI DHAHIRI UTAKUWA MWENYE HATIA MAISHA YAKO YOTE UTAJIONA MUUAJI!.

tabasamu lako, ucheshi, upendo na maneno mazuri yatokayo kinywani kwako ni zaidi ya majumba, magari na vyote ujuavyo vina thamani, amini na uweke akilini kuwa sio muda wote watu wako wakaribu hasa walio chini yako wanataka pesa kumaliza matatizo yao, faraja nisuluhisho na muongozo wenye sababu nyingi za kumfanya mwanadamu asonge mbele bila woga wa magumu yaliyo mbele yake.

kamwe usipuuze kutoa tumaini kwa wanaokutamainia!

TWENDAPO WAZEE HAWATAKUWEPO!!!

"Huko twendako, siku baada ya hizi nina uhakika wazee watakuwa viumbe adimu kuonekana katika sura ya dunia hii! sababu ni nyingi lakini chache kati ya hizo ndizo nitakazoziwekea mkazo katika andiko langu la leo!"

Na
Omar Zongo

Baridi kali inayopuliza mwilini inasababisha mwili usisimke kwa woga vinyweleo visimame, hali hii ya hewa ni sababu tosha kwa wavivu kuvuta shuka hasa mishale hii ya asubuhi lakini kwangu ni tofauti, saa kumi kamili za alfajiri niko macho natafakari utashi wa MUNGU.

tafakuri yangu hiyo inaenda sambamba na vitendo vyangu takatifu vyakujiandaa kwenda masjid kumsujudia mwenye dunia hii, mwenzenu imani yangu ni muislamu lakini namshukuru MUNGU sijawahi kukashifu imani za wengine.

vitendo vyangu vya maandalizi yakujiweka safi kimwili na kiimani vinachukua kama dakika kumi na tano hivi, najipuliza marashi, navaa msuli wangu kwa kuukunja vema mkwiji, shati langu safi nililoliandaa kwa ajili ya swala ile kisha nalisindikizia na koti kubwa ili angalau kuzuia ubaridi usiendelee kunipa adhabu!

Sasa nimekalimika kwenda kumsujudia aliyeniumba mimi na kuumba kila unachokifahamu ulimwenguni hapa! msikiti uko mbali kidogo hivyo nina kama mwendo wa hatua elfu mbili mia tano ili kuufikia lakini nitafanyaje na wakati nina nia yakuswali na waumini wenzangu, Njiani nipitapo waja wachache mno.

ndio, lazima wawe wachache maana sio wote wenye ujasiri wakudamka mishale ile hasa kama hawana sababu za msingi!

ni kunguru na ndege wengine ndio nawaona kwa wingi kwenye misitimu ya umeme wakijibizana kwa sauti zao, kichwani kwangu natafsiri sauti zao kuwa ni kelele za kumtukuza MUNGU muweza vyote! nami kimoyoni namtukuza MUNGU maana nimeambiwa kitabuni kuwa ameniumba kwa ajili hiyo tu.

hatua kadhaa mbele ghafla mwili wangu unanisisimka mno! najiuliza ni kwanini hali hii!? hisia mbaya zanivaa, wazo kuhusu uchawi na hila za majini na binaadamu wabaya lanivaa!

naingiwa na woga kwa mbaali lakini ghafla ndani yangu sauti ya imani kwa MUNGU inanijaa! nakumbuka kukimbilia mikononi kwa mungu kuomba ulinzi wake! napiga dua za kujihami na shari za ubaya wa aina yoyote unaotaka kunidhuru asubuhi ile.

Naam! MUNGU ni mwema ghafla tumaini lanivaa, woga waniepuka sina tena wasiwasi,
imani yangu kwa MUNGU bila shaka imeniweka mbali na mabaya yote yaliyokuwa yananisisimua mwili wangu, kiukweli muda ule sikuona lolote baya lakini waswahili husema kuwa ukihisi mwili wako unakusisimka ujue kuna shari karibu yako, hivyo mie nikaona busara kujikinga kwa MUNGU wangu mlezi.

kama una imani nawe nakushauri kufanya hivyo! kila unaposisimkwa na mwili katika mazingira hatarishi

Hatua zangu Imara hatimaye zikakomea msikitini, Kabla yakuingia ndani ya nyumba hii tukufu namshukuru Mungu kwa kunifikisha salama, maana kutopishana hata na vibaka,wezi au majambazi ni baraka tosha kwakweli.

Jicho langu sasa laangaza msikitini, uzuri ni kwamba tayari nilishachukua udhu nyumbani hivyo nikaingia tuu nakuketi msikitini kusubiria adhana ili niswali sunna!

wakati nimekaa kitako mule msikitini navuta uladu taratabu kumtaja MUNGU wangu kwa wingi ndipo wazo likanijia, wazo muktasi ambalo nikaona si sahihi kuliacha linipite, wazo lakuwatazama watu wachache waliowahi asubuhi ile msikitini kama mimi!

Nikaruhusu jicho langu liangaze kwa kila mmoja, hakika walikuwa sio wengi hata kama ningetaka kuwahesabu ningeibuka na idadi ya watu saba au nane lakini sio zaidi ya kumi, nakiri katika mtazamo wangu kwa waumini wenzangu wale kuna kitu nilikibaini kuwa ni mimi pekee ndiye nilikuwa kijana kati yao!

wengi walikuwa watu wazima, wazee kabisa wenye umri sawa na baba yangu na wengine babu zangu kabisa! wazo langu likakwamia hapa nikajikuta najiuliza kwanini wazee tuu ndio wana muamko wakufanya ibada kwa wingi???

swali langu hili likaibuka na majibu yangu mepesi ambayo naamini kama tukiyatafakari kwa kina labda huenda tukayafanya yawe mazito.

jibu langu kubwa kati ya mengi niliyoyajibu ni kwamba tunapoelekea wazee hawatakuwepo!!
Ni tafakuri yangu ambayo sina shaka itapigwa vita nakuonekana laana kwa vijana lakini kamwe sitaifuta kirahisi na itaendelea kusalia wazoni mwangu labda ikitokea niyaonayo yakibadilika!
huko twendako, siku baada ya hizi nina uhakika wazee watakuwa viumbe adimu kuonekana katika sura ya dunia hii! sababu ni nyingi lakini chache kati ya hizo ndizo nitakazoziwekea mkazo katika andiko langu la leo!

Kwa mahesabu ya haraka haraka yasiyo hitaji akili kubwa kufikiria utabaini kuwa kwa kipindi kirefu sasa misiba mingi tunayoisikia ni ya vijana wadogo ambao bado damu zao zingali mbichi na zenye nguvu yakuzunguka mwilini kwa kasi iliyo kuu.

hali hii ni tofauti na hapo kale, sitashangaa vijana wa leo wakileta mzaha katika neno langu hili wakiniita Mhenga! lakini ukweli nitausimamia daima sitauacha uniponyoke nafsini mwangu.

nahisi sababu ya vijana kufa kwa wingi katika karne hii ni kutokana na dhambi zetu nakuhatarisha maisha yetu kwa kufanya kwa wingi yale ambayo MUNGU ametukataza kuyafanya.

Uzinzi, Uasherati, Ulevi, Utovu wa Nidhamu na Starehe zilizo kinyume kabisa na maandiko kutoka kwake Jabbar.

Uzinzi huo niliyoutaja matokeo yeke mengi ni sambamba na Maradhi yanayosababisha kifo.

Uasherati pia nimeujumuisha ingawa hauna tofauti na uzinzi lakini nahisi huu umepita mipaka ndipo tunapoona hata matendo yaliyoangamiza kizazi cha Nuhu, hakika hili nalo matokeo yake ni kifo.

Ulevi nao huchangia kwa asilimia kubwa Ajali na mengine mengi yanayokatisha maisha ya vijana, kama vile matumizi ya dawa za kulevya yanayonyonya nguvu na ushababi wa mamia kwa maelfu ya vijana duniani kote.

Utovu wa nidhamu na starehe zilizo kinyume na maandiko haya yote kwa ujumla na mengine yanayofanana na haya huzalisha wivu, visasi, tamaa na mabalaa yanayosababisha wenyewe kwa wenyewe kuuana.

Vijana kwasasa tunaisha kwa kasi inayoogopesha ni nadra sasa mtu kufika umri walau wa miaka 40, yaani thelathini na tano yenyewe mtu amekwepa mengi yaliyotaka kummaliza au kama sio hivyo ndio yuko mbioni kufa aidha kwa virusi vilivyo mwilini mwake au kwa visasi alivyowekewa na wenzake kutokana na kuiba mwanamke wa watu au kuzulumu mali ya mtu.

Nionavyo Mimi miaka ijayo Dunia haitakuwa na wazee au kama watakuwepo basi wachache sana! hawa tulio naso sasa masikini ya Mungu wanadondoka taratiibu sana ukilinganisha na vijana lakini utaratibu huo nina uhakika utawamaliza wote na hakutakuwa na wazee tena maana tunaotakiwa tukawe wazee ndio hivyo tena tumezongwa na vikwazo vyakukanyaga anga hilo la uzee.

Masikini ya Mungu bila shaka wazee wana ile hofu ya kuwa umri wao umeenda mbele, nguvu zao zinawaisha mauongoni mwao kwa hivyo wameamua kujikurubisha kwa MUNGU wao walau watubu dhulma walizozifanya kipindi chote cha ujana wao.

dhana hii inawasaidia wazee wengi kufanya ibada na natamani vijana nao tungekuwa tunajijengea hofu hii kwamba sasa izrael anatuwinda sisi kwa hiyo tuanze kumrudia MUNGU, maana hatuijua saa wala dakika.

lakini Masikini vijana sisi tupo tofauti kabisa na dhana ya wazee, daima tunajiona wenye nguvu na tunaweza kufanya lolote kwa kipidi hiki, mbaya zaidi wakati mwengine tukidiriki kusema kuwa "Muda wakutumia ndio huu, kutubu tutaanza uzee ukitufikia"

Hakika kizazi hiki kinapotea kwa kukosa maarifa! uvivu wakufikiri na kuzifuata hadaa za mpumbavu, mjaa lana, maaluni ibilisi, shetani kiumbe ninayemchukia kuliko wote duniani! MUNGU anilinde na kuniepusha na shari zake mjinga huyu.

Tafakari sasa na unipe jibu jee unadhani TUENDAKO WAZEE WATAKUWEPO??? baada ya hawa waliopo kuisha!

MUNGU atujaalie mwisho mzuri! atuondoe gizani na atufanye tuwe wenye kumtukuza kwa kufuata amri zake!

amen!!!

Muda wa swala umefika, acha nisimame na waumini wachache waliofika msikitini leo, vijana nao tupo ila wengi wazee.

nakuahidi nitakutaja katika swala yangu hasa muda wakusujudi ili uwe mwenye kukumbuka kuwa duniani Tunapita!

SAUTI YA MUNGU


 Anaandika 
Omar Zongo

wakati mwengine ukiwaza sanaaaa utagundua kuwa hauna faida yoyote kwa mwenzio wala yeye hana faida yoyote kwako!

ukiendelea kuwaza sanaa utagundua ni MUNGU pekee ndio mwenye faida kwenu wote, na ukiendelea kuwaza sanaa utagundua mnashobokeana, kufuatiliana kujuliana hali na kujaliana kutokana na Amri ya huyo  MUNGU ambaye ametuamrisha tupendane na ni dhambi kuchukiana.

ukiwa unaendelea kuwaza sanaa utazidi kubaini kuwa anaekupuuza kutojali uwepo wako na kukupotezea hauna sababu yoyote yakumshobokea, kumfutalia nakumjali lakini ajabu ukiendelea kuwaza sanaa utagundua kuwa kufanya hivyo nikumuudhi MUNGU wako ambaye anakujali wewe kwa ukarimu mkuu! na niyeye ndiye aliyekuamrisha umpende adui yako!

ukiwa hujachoka kuwaza utagundua kuwa kuna kitu kinaitwa uvumilivu kinahitajika sana ili uwende sawa na watu wote maana wameumbwa kwa mitihani usipoangalia unaweza ukaamka asubuhi moja nakuwatukana wote kwa kuwa hawana faida kwako!

ukiwa unaendelea kuumiza kichwa kuwaza utagundua kuwa hata uvumilivu wenyewe kwa sasa haupo bali ni maigizo ya uvumilivu kuchekeana kinafki na upendo wenye joho la fitina ndani yake!
ukiwa unaendelea na juhudi yako yakuwaza utagundua kuwa hata wewe umeshaanza kurithi kajiunafki hako ambako kanakufanya ucheke wakati moyoni una jiduku duku! huo ni mwanzo wake mwisho wake unakuwa na jiroho jikubwa kama bara la afrika!

Utajiona hakika ukiwa unaendelea kuwaza na utabaini kuwa wakati mwengine kile unachokisema moyoni mwako sicho kabisa kinachotoka mdomoni mwako, lakini kutokana na kuwa hutaki vita na kuchukiwa ndio maana unajitahidi kujichekesha na kujifanya uko karibu na watu!

endelea kuwaza na kama hutaki mimi nitakuwazisha ili ujione kuwa kuna kajiunafki umeumbwa nako na kanakufanya wakati mwengine umchukie mtu bila sababu lakini kutokana na kuwa hutaki wengine wajue unajifanya unabaki na siri yako moyoni!

naitamani ile siku ya dhahiri ifike! siku ambayo mioyo ya watu itafunguliwa nakuwekwa wazi kilichojificha humo, naamini siku hiyo itashibisha mawazo yangu ya leo ya kwamba sura unazozioana zikikuchekea nakutabasamu ukikutana nazo sio sura zinazokufurahia kwa dhati kabisa kwa kile ulichojaaliwa!

usichoke kuwaza rafiki angu endelea ili uone kuwa Binaadamu ukiwepo wewe pia namimi tumeumbwa na siri na wakati mwengine tunasingizia eti damu yangu na yake haijaendana! nani kasema kumchukia mtu kunasababishwa na damu, huu ni ufinyu wa fikra ambao unakufanya uhisi kuwa una haki yakutafuta sababu zakumchukia mja mwenzako!

laiti kama ungekuwa unajua kuwa kuna wakati mwili wako utaishiwa nguvu, utasikia lakini hutaweza kujibu, utaona lakini hutaweza kuamka na utabebwa lakini hutaweza kujisogeza! naamini ungejua kuwa huna thamani na wewe ni kitu kidogo sana katika dunia hii na unapaswa kutokuwa mnafki na kuizulumu nafsi yako kwa kumchukia mwenzako hata kwa siri.

hakuna mkubwa wala mwenye hadhi kuliko mwenzake duniani wote ni sawa! kuna vitu tuu vidogo sana ndio vimetufanya leo hii tuone fulani ni wa muhimu na fulani ni dhalili na hana thamani!

nikivitaja naamini vitakufanya uendelee kuwaza nakugundua kuwa binaadamu tuna ujinga ambao unatufanya fikra zetu chanya tulizoumbwa nazo tusizitumie maana haiwezekani, Muonekano wa mtu uwe ni tija katika kumtukuza huyu na kumdunisha yule.

au utajiri uwe ni chanzo chakumuona huyu ni wa maana na yule ni dhalili aso na tija! haiwezekani hata ukiniamsha usiku nikiwa na miusingizi nitakijubu haiwezekani, na nitasisitiza tena haiwezekani kumfanya fulani awe chini kisa ana kitu unahisi kitamnufaisha nawe kitakuangusha nasema HAIWEZEKANI!
Sikuwa MREXPERIENCE kabla, nilikuwa Zongo wakawaida lakini ukubwa, malezi na kuishi na waja wenzangu vyote vinanipa maneno yanayoshibisha andiko langu hili leo ambalo naamini ni SAUTI YA MUNGU!
ingepata shida nafsi yangu kama siku ingedondoka bila kuonya kuhusu maisha haya yenye utabaka,  maisha yenye umimi na ubaguzi wa hali ya juu! maisha yaliyojaa wivu, husda, uchawi na kila aina ya takataka!
hayana faida maisha haya kama waja wasiposhtuka nakugundua kuwa shetani ametutawala katika fikra zetu, anatuendesha katika maamuzi yetu na anayasimamia vema mawazo na maamuzi yetu, ni huyu mpumbavu shetani ndiye ambaye aliapa kutuingiza motoni sisi binaadamu na mungu alituamrisha tumchukie na tujikinge naye maana ni ADUI YETU.

Ukiwa bado hujachoka kuwaza utamuona huyu mjaa lana shetani anavyokupa wivu kwa kilicho bora kinachopatikana kwa mwenzako, niyeye ndiye ambaye anakupa nguvu yakumchukia kimoyomoyo na muda mwengine hukushinda nakukufanya mpaka ushiriki shirki na udiriki kuroga!

laiti kama ningekuwa sijachoka kuwaza ningeendelea kukufanya nawewe uwaze sema nahisi nimechoka na kichwa kinaniuma kwa kuwaza udhalili wetu binadamu, fikra hasi na matendo yakinafki tuliyojigubika nayo mithili ya vazi zito kwenye msimu wa baridi.

laiti kama ningekuwa sijachoka kuwaza ningeendelea kukufanya nawewe uwaze sema nahisi nimechoka na kichwa kinaniuma kwa kuwaza udhalili wetu binadamu, fikra hasi, husda na matendo yakinafki tuliyojigubika nayo mithili ya vazi zito kwenye msimu wa baridi.

Imefika muda sasa tugundue kuwa waliokufa kuwapata ni ngumu na mazuri yao, upekee wao na kila kitu kilichowafanya wawe wao wameenda navyo, hivyo sisi tuliobaki tupendane na kufurahia vizuri vilivyopo ndani yetu, maana hatutaweza kuvitoa tena andiko likitimia.

IGIZI UKAMILIFU2017

NIHESHIMU MKE WANGU

Unakumbuka maisha yako kabla sijakuoa??

ulikuwa hauna tofauti na bidhaa yakukodiwa ambayo ilikuwa ikitumiwa nakurudishwa ili mwengine aje aikodi tena.

maisha yako yalikuwa na uhuru wakukudharaulisha.
wapo wanaume wengi kama mimi walikufata nakukutumia bila hata kuwaza kuwa unastahili kuolewa.
kitendo cha mimi leo kutimiza ahadi yangu nakukuoa kinatosha kabisa kufanya wewe uniheshimu.
sio kama sijaona mapungufu yako au wewe ndio mwanamke mkalimilifu kuliko wote laa hasha! nimekuoa kwasababu nimeamua kukupokea kwa jinsi ulivyo so inatosha kabisa wewe kuniheshimu.
kwani hujasikia fununu kuwa duniani wanawake mpo wengi kuliko wanaume sasa kwanini usione bahati kubwa kwako kuchaguliwa namimi nakuolewa eti huoni kuwa nastahili kuheshimiwa nawewe??
Niheshimu mke wangu sababu nahisi kuwa nimekuvisha stara nakukutofautisha na wanawake wengine wahuni wanaotumiwa nakuachwa kila siku, naamini kuwa hayo sio maisha mazuri yanayompendeza binti yeyote hivyo niheshimu mume wako maana ni mimi ndiye niliyekukinga na mwamvuli ili usinyeshewe na mvua ya dharau wala usichomwe na jua la uhuni.

niheshimu mke wangu maana nimimj ndiye niliyewahifadhi wanao kwenye mgongo wangu bila mimi usingepata jina la heshima nakutambulika kama mama duniani hapa hivyo wakati unamshukuru Mungu kwahilo naomba unifurahishe pia kwa kuniheshimu mume wako.

ni mimi ndiye ambaye nikilala nawaza kesho niamkie wapi na nikafanye nini ili wewe ule, uvae na upendeze, tafadhali mke wangu niheshimu basi hata kwa sababu hii nitaridhika.

ndio wakati mwengine huenda nakukwaza kwa mapungufu yangu, lakini sio sababu yakunishusha thamani nakunidharau nakusihi niheshimu maana mimi sifanani na mwanaume yoyote unae na uliyewahi kumjua.

ni mimi ndiye niliyeshinda ndumba za vimada nikaruka vizuizi vyakukuoa nikafumba masikio ili nisisikie maneno ya wanafki wasiopenda nikuoea jee hii haitoshi wewe kuniheshimu mke wangu??
niheshimu mke wangu tafadhali maana wakati mwengine sina hamu yakula dona lakini kila ninapowaza natakiwa nijenge nguvu mwilini zakukulinda nakukuridhisha haja zako basi nafakamia vyote vinavyosaidia afya yangu nanguvu kuimarika.

Niheshimu mumeo maana nimeumbwa na nyama zisizopenda dharau abadan na tena dharau kutoka kwa wewe mwanamke wangu niliyejitoa kwako kwahali na mali.

Niheshimu tu kwakweli maana nafanya juhudi kubwa mwenzio ili kushinda vishawishi vya wanawake wengine wanaojipamba makusudi ili kuiba waume za watu, wanaojidai kunijali kushinda wewe na wanaokesha kwenda na wakati kwa nguo za wazi zinazonijengea ushawishi wa tamaa sababu ya miili yao wazi isiyostirika.
nipatie heshima yangu mke wangu maana kushinda mitego ya shetani mtaani ninakopita sio wanaume wote wanaweza! huoni tu kuwa unapaswa kuniheshimu na kujizuia kunidharau hata kwa sekunde moja.

usiseme eti ukali wangu wakiume ndio sababu ya wewe kunibyedulia midomo, kama mumeo wakati mwengine napaswa kukufokea ninapohisi umenikosea na sio vema kunijibu kwa kiburi utanipandisha jazba halafu nikose chakufanya maana mkono wangu mimi ulipewa tahadhari na mama yakutomgusa kwa kibao mwanamke wangu.

niheshimu tu mke wangu nami nitakuheshimu maana heshima ndio kila kitu katika ujenzi wa utulivu wa familia yetu.
tena niheshimu si kwa maigizo niheshimu kwa dhati ya moyo wako maana akili zangu zina jicho lakutambua maigizo na uhalisia hivyo tafadhali mke wangu usinifanyie maigizo katika kunipa heshima yangu.
naongea nawewe mke wangu sasa kama usasa umekuzidi kiasi kwamba kila kitu wataka ushauri kutoka mitandaoni nenda kawaambie na hili najua wapo watakaosema kuwa nina mfumo dume hivyo kukujaza umaaluni kisha ukaanza kunipuuza haki vile nakwambia NITAKUFIKIRIA UPYA NA KURUDI KWA MUNGU WANGU NAKUMUULIZA NIKWELI NDIYE WEWE NILIYEMUOMBA AU ULILETWA NA SHETWANI MJAA LANA.

Tusifike huko mke wangu naomba NIHESHIMU MKE WANGU!

MWENYE SIFA HIZI AJE!!!

Awe na kinywa tulivu chenye ulimi asali, neno lake tulizo sauti yake gitaa.
umbo lake pambo, mvuto kwa jicho langu, rangi ladha tamu si mweupe si mweusi!
lafudhi yake wimbo lahaja iwe ya pwani, sikio lipumbazike aniitapo jina.

aniduwaze na mwendo mithili yake hapana kaumbwa kwa mapambo na Mungu wa sifa njema.
upole tabia yake si binti wa pekepeke imani vazi lake hofu kwa Mungu wake.

kajaaliwa midomo unene wa kitumbua jicho lake legevu MUNGU kalipaka kungu.
nijione Adamu naye ndiye Hawa Wangu tena anipe faraja tabasamu lake afya.

Ngozi yake mboga wala sio yakughushi mchicha na matembele si maji wala mchina.
kauli yake dira, upole ndo vazi lake wala hawezi kuzira subira tabia yake.

roho yake imani, uchamungu matendo yake, adui yake shetani tumaini lake MUNGU.
mwenye sifa hizi nani namgojea afike simtaki hayawani akija nifilisike.

sitaki jibu dhalili eti nimuumbe mwenyewe naahidi kumsubiri hata kama yu tumboni.
akijue kiswahili maneno yake matamu, kizungu sistahili mie sio lugha yangu.

usomi uwepo kwake tena umsaidie kunitunza mume wake sio anikimbie.
ugumu wa hali hii aje anipe msaada kazini iwe bidii ndio ngao sio mwili.

yeyote mwenye adili akili ilo kamili mtambuzi wa neno hili afike namsubiri.

JUNIOR

 "Sikuwahi kusimulia kisa cha kweli nikakiruhusu kusomwa na watu pengine hii inaweza kuwa simulizi yangu ya kwanza yenye ukweli ndani yake, ni zawadi kwa ndugu yangu Ramadhan Madebe ambaye kwa asilimia kubwa amechangia ukamilifu wa simulizi hii....ni sehemu ndogo pekee ndio yakubuni lakini mengi yana ukweli....."

JUNIOR

SEHEMU YA KWANZA

Niliona wivu sana baada ya rafiki yangu kupewa jina na dada yako, yeye aliitwa mwinjuma lakini alimbeza jina lake hilo na akasema kuwa anapendeza zaidi akiitwa Geminus!

Leo ndio nagundua kuwa aina ya familia bora kama ilivyo ya kwenu ndiyo huwaaribu watoto nakuwafanya wayachukie majina ya Kiswahili kutokana na wao kukesha wakitazama filamu za kizungu na kihispania.
Hata kama muhusika mkuu katika filamu ya kizungu akitokea anaitwa Zongo, mradi ni mzungu na anacheza vizuri kwenye nafasi yake basi jina hilo linaweza kuwa ni jina zuri kuliko yote duniani.

Kiukweli licha ya kuwa akili yangu ndogo lakini imebaini kuwa hili ni tatizo ingawa nakiri sina utaalamu wa kutatua tatizo hilo maana ni tatizo kubwa linalohusu saikolojia zetu waafrika.
Nakumbuka Rafiki yangu Mwinjuma alivyobadilika jina nakuitwa Geminus nilikuja kwenu bila haya nikakulalamikia nikakwambia namimi unitafutie jina.

Sauti ya jibu lako bado inajirudia kichwani mwangu “usijali, acha leo nikeshe nikiomba naamini kesho nitakuja na jina zurii ambalo litakufaa”
Hivi ndivyo ulinijibu, nakumbuka nilifarijika sana na nikarudi nyumbani kwetu kwa furaha nikiiomba kesho ifike nilisikie jina langu ambalo umenichagulia wewe.

Sikujali kuwa mimi nimekupita umri na wewe ni makamo ya mdogo wangu, hilo sikulijali kabisa niliona na kukiri kuwa umenizidi upeo.

Sikujali pia umbali wa kila siku kutoka kwetu uswahilini kuja maneneo ya kwenu uzunguni ambapo hii ni kawaida kwa nchi zetu za kiafrika mitaa kujitenga kutokana na vipato vya watu wake.
Nina uhakika kama familia yako ingekuwa na kiburi kutokana na neema ya utajiri basi mimi na rafiki zangu tusingeweza kabisa kukanyaga nyumbani kwenu lakini nashukuru sana na kila siku nauota ukarimu wa wazazi wako, na ucheshi wa ndugu zako.

Nakiri kuwa hii ni historia ya miaka mingi sana ya nyuma lakini bado inaishi kichwani mwangu zaidi siku hii ambayo uliviweka viganja vya mikono yako usoni mwangu.
Ulitaka kuhakikisha kuwa nimeyafumba macho yangu yaani sioni kitu, uliniambia hilo ndilo sharti la wewe kunitajia jina langu jipya ulililonichagulia.

“kuanzia leo utaitwa Junior” hii ni sauti yako ambayo naisikia mpa
ka leo ikitamka maneno hayo, tangu hapo namimi nikajivunia kuitwa Junior.

JUNIOR
SEHEMU YA PILI


Yote hayo yalikuwa yanajiri tukiwa shule ya msingi, mimi nikiwa nimekupita madarasa matatu, sijui kizazi chetu kimekumbwa na nini masikini yaani tunayajua mapenzi tangu tukiwa wadogo.

Ndio maana mpaka leo muda huu unasoma ujumbe wangu bado mwenzako nastaajabu na hila za mapenzi, ukweli ni kwamba kati yetu kulikuwa na upendo! Lakini utoto wetu ulikuwa chanzo cha sisi kushindwa kuelezana ya kwamba tunapendana tena sio kimasikhara yaani tunapendana sana.

Zaidi tuliishia kucheza pamoja huku kila mmoja akifurahia ukaribu wa mwenzake, kwangu mimi ilikuwa siku mbaya sana ikiisha bila kuiona sura yako sijui kwa upande wako.

Mdogo wangu ambaye ulikuwa unasoma nae darasa moja sijui kwanini alikuwa ananificha kuwa mkiwa pamoja hua unanisifia nakumwambia kuwa mimi ni mstaarabu sana, ndio! mimi ni msataarabu na sijui kwanini nilikuacha mwanamke ambaye uligundua ustaarabu wangu tangu nikiwa mdogo.

Nakumbuka zama zile na natamani zijirudie angalau niwe karibu nawe nikiwa na akili za sasa hivi ili nikwambie neno nililostahili kukwambia kipindi kile nikashindwa.
Ujinga wa utoto ulinifanya nikahadaika na binti mwengine ambaye aliibua wivu wako wa kitoto na ukaanza kujifunza kunichukia tangu hapo.

mwisho wakuiona sura yako ilikuwa ni mimi wakati namaliza kidato cha nne, maisha yalitutenga nakutuwekea mpaka mkubwa uliofanya hadi hii leo sura yako ibaki kuwa kumbukumbu tu.
Asante teknolojia walau sasa nakuona mtandaoni.

Sikuamini kabisa kuwa ungenijibu ujumbe wangu mfupi nilipokusalimia kwa mara ya kwanza Facebook, sikuamini pia uliponijibu kuwa ni wewe ndiye Yule mwanamke wangu wa kwanza kuvutiwa nae duniani hapa.
Ujio wako umekuja siku chache tu baada ya maombi yangu kwa mungu pamoja nakufunga ili anioneshee mke mwema. Sababu nataka kuoa mwenzako.

Kukutana tena kwa mara ya pili nawewe imekuwa ni faraja kwangu nikiamini kuwa umeletwa na Mungu.
Kauli yako ya jana ndio imenitoa kabisa kwenye imani yangu! Siamini kabisa kama ni kweli umeolewa na una watoto wawili.

Masikini mimi nilikuwa wapi! Kwanini sikuwahi kujua kuwa ni wewe ndio nilipaswa nikung’ang’anie.
Unasema hauishi kwa amani na mume wako, ni Malaya na hana kabisa upendo. Amekulaghai kwa pesa zake na sasa haioni thamani yako tena.

Ilikuchukua mud asana kunielezea haya, ulikuwa hutaki kwa sababu ya kuficha maovu ya baba watoto wako, lakini nilipokubembeleza sana ndipo siku moja ukanidokeza japo si kwa undani.
Uliniumiza zaidi uliponiambia kuwa jamaa hakupi haki yako ya ndoa,licha ya kuwa unambembeleza sana.
nafsi yangu ni nzito kukwambia utoroke uje maana najua watoto wako wanapaswa kupata haki ya kulelewa na baba na mama yao.
Naogopa kesho huenda wakanihukumu kuwa nilikuachanisha na baba yao, naogopa pia dhambi maana imani yenu haiwaruhusu kuachana kamwe na mnahitajika mpendane kwenye shida na raha kama mlivyoapa siku ile mnafunga ndoa kanisani.

Lakini kwanini urudi wewe mawazoni baada ya kumuomba Mungu anipe mke mwema! Tafadhali nijibu kama ukipatwa na fahamu maana nimeambiwa na rafiki yako kuwa mume wako amekupiga sana juzi na hivi sasa upo chumba cha wagonjwa mahututi, hali yako ni yakuombewa! Maana humjui aingiaye wala atokaye.
Kwanini wanaume tuko hivi, amewezaje kuutendea maovu mti mbichi namna hii au nikwasababu haijui asili yako,
Nakumbuka kuna siku ulizungumza na baba yangu kwenye simu, mzee wangu ni mtaalamu sana wakugundua tabia ya mtu hata kupitia simu, na nilisubiria maoni yake baada ya kuongea nawewe, sikuongopei alikusifia sana na ajabu alipokutaja kwa mama ndio sifa nzuri juu yako zikazidi, wadogo zangu bado wanakumbuka zawadi na upendo wako kwao, kwa mfano mdogo angu Naa mpaka leo kuna gauni lake ulilomzawadia amelitunza sana licha ya kuwa limemruka na halivai tena lakini anasema ni kumbukumbu ya mdada mkarimu aliyewahi kumjua maishani mwake.

Kiukweli najikaza tu nisilie hasa wazazi wangu wanaponiuliza habari zako ninapoenda kuwatembelea, nashindwa kuwaambia kuwa nilikupoteza.

Sasa nafahamu kuwa kweli mimi ni JUNIOR! Ulikuwa mkubwa kwangu kiupeo na ulijua thamani ya upendo licha ya kuwa umri nilikuzidi na ndio maana uliniambia kuwa “huezi kuendelea kuwa namimi maana nimesoma na wewe unahitaji kusoma” aya maneno yako yalikuja baada yakugundua kuwa mimi nina mwanamke mwengine.

Naomba upone haraka unisaidie kunijibia maswali yangu nini nifanye maana niwewe ndiye nimeonyeshewa baada ya kumuomba mungu lakini ni wewe ndiye ambaye kwa sasa ni mke wamtu.
Tafadhali amka Anna kwa sasa mimi sio Junior Tena mtaani wananiita MR experience, nina uzoefu mkubwa na haya maisha na ninajua pia thamani ya upendo.

Plz Anna amka, nipo na wanao hapa Mumeo amesafiri mchana huu kikazi, ndivyo alivyodai wakati amepigiwa simu kuelezewa hali yako lakini kwenye mtandao wake wa kijamii namuona amepost yuko hoteli flani Arusha na mwanadada mrembo lakini hakuzidi wewe Anna,
Plz naomba uamke unipe dira yangu Katika mapenzi…nahitaji kuoa mwenzako.
Na
Omar Zongo

Inaendelea….
SEHEMU YA TATU

UMESAHAULIKA BABA WA KISWAHILI

Imekuwa ni desturi yangu kuenzi harakati zako kila siku hasa kipindi ambacho ni kumbukizi ya kifo chako mithili yakuzima kwa mshumaa uliokuwa ukimulika fasihi andishi yenye tija na akili kubwa kwa miongo kadhaa sasa yaani tangu na baada ya kifo chako.

Baba wa kiswahili, Shaaban Robert  (kuzaliwa 1 January 1909 – kufa 20 June 1962)

Nionacho leo kuhusu kuenzi mchango wako ni USAHAULIFU MKUU, kiukweli UMESAHAULIKA BABA WA KISWAHILI! 

Anasimulia
Omar Zongo 

Naona aibu kusema kuwa natamani ule utashi wako walau ungeuacha sehemu kisha ukaniagiza hata ndotoni nikauchukue niutumie kuendeleza falsafa zako na utamu wa Kiswahili uliopo ndani yako.
Nasikitika ninapogundua kuwa 20 june wakati unafariki ulikusanya kila kilicho chako nakuelekea nacho kaburini, sitaki kusema kuwa hilo limetokea kutokana na uchoyo wako laa hasha ila nakulaumu kwanini hukutaka kumuachia mtu arithi angalau robo ya unguli wako wa kutumia vema hii lugha Kiswahili katika maandishi.
Ni juzi tu nimemrejea Adili na wasifu wake uliomchora nao kwenye ile riwaya yako ya adili na nduguze,hakika nafurahishwa sana na jaala ya mfalme Rai ambaye aliweza kuwa na upendo kwa kila kitu anachokitawala si mnyama, binaadamu hata mmea, alidiriki kujinyima yeye ili vitu hivyo vineemeke.
Umesahaulika Baba wa Kiswahili na sijui kwanini limewezekana hilo kwenye ardhi hii ambayo kwa sasa busara zako zingepaswa zitumike zaidi ili kujenga maudhui sahihi ya utu wema na uongozi bora ndani ya bara letu Afrika.
Naugua maradhi ya kusonona moyo kila nipigapo soga na mabarobaro rika langu ni wachache kati yao wanaokujua,  tena kwa kupapasa papasa.  wengi husalia kuuliza “ni nani huyo baba wa Kiswahili?” nazidi kuamini kuwa umesahaulika nguli wewe ambaye akili yako nikiitathimini kupitia kazi zako naiona imezidi ukawaida.
Enzi zako upo hai wapo waliodiriki kukufananisha na Wilium Shakespare lakini vifo vyenu vimedhihirisha kuwa yale yalikuwa maneno tuu, maana wewe kaburi lako limetelekezwa kule kwenu Tanga, wanaokujali kwa kung’oa  walau majani tu kwenye kaburi lako ni wale waja wenye nasaba nawewena hilo kusema kweli  nitofauti na  Yule mwenzio uliyekuwa ukifananaishwa nae bado kaburi lake ni alama inayosimama kama historia katika anga la waandishi mahiri wa mashairi na riwaya nchini uingereza na duniani kwa ujumla.
Kinachonifanya niugue maradhi yakusononeka moyo ni kwamba wewe ni wajuzi tuu labda kama nakosea au sijui mahesabu, lakini ukweli ni kwamba Willium Shakespare ni wamiaka ya  1564, naomba nirejee tena  elfu 1 mia 5 na sitini na 4 na akafariki mwaka 1616 ingawa inakisiwa lakini ukweli ni kwamba nguli huyo wa uingereza ni wa makarne mengi yaliyopita iweje bado anaenziwa na alama yake bado ni dira kwa vizazi vipya vyote vinavyozaliwa uingereza.
Mwenzangu namimi wewe baba wa Kiswahili ni wajuzi tuu masikini lakini umesahaulika kwakweli! Kuzaliwa kwako ni 1909 na kufa kwako 1962 lakini juhudi zako zimezikwa nawe siku ile kule kwenu mwambani Tanga.

Mwandishi nae ni mtu wa desturi kama walivyo watu wengine hawezi ishi kwa kunywa upepo nakutafuna mawe, bila shaka nukuu yako hii ulitaka kudhihirisha mgogoro wako wa nafsi uliokuwa nao katika kupigania mafao yaendane na kazi zako, kwa maono yangu ni kuwa hapana siku uliyowahi kunufaika na kuridhishwa na ubaba wa Kiswahili.
Naiona lana kwenye anga hili ulilotokea lana itokanayo na sononeko lako la tangu ungali hai na hata miaka mingi tangu kufariki kwako.
Umesahaulika Mzee wangu, baba wa Kiswahili!
Niseme nini namimi sina mamlaka yakuamrisha kuwepo siku ya kuwaenzi ninyi wenye michango yenu katika fani ya ushairi na riwaya.
Nahisi siku hizo zipo lakini kwako wewe ingepaswa kuteuliwe siku maalumu ya kumbukizi kwa Baba wa Kiswahili lakini bado swali linabaki kuwa mimi ninani hasa??
Mchango wako si tu mashuleni kukuza bongo za watoto wetu bali pia ulipigania uhuru kupitia karma yako, zipo sababu zaidi ya bilioni zakukumbukwa lakini iweje uwe umesahaulika hivi.
Naomba niishie hapa maana niendapo naenda kukufuru,
 leo sijaandika barua kwako bali nimepanda kilimani nikiuagiza upepo ufike na sauti yangu uisikie nikikwambia habari hii UMESAHAULIKA BABA WA KISWAHILI.
Nilipo naugua maradhi ya kusononeka moyo sababu kama wewe na utashi wako ule wote umetelekezwa kiasi hicho mimi ninani katika fani ya uandishi mpaka nije angalau kutajwa tu mdomoni mwa waja wa kesho ambao watakuja baada ya mimi, kama sisi tulivyokuja baada ya wewe!.
Habari niliyokupa kupitia upepo uvumao kutoka nilipo kufika huko ulipo bila shaka ni habari mbaya maana hata mimi nisingetabasamu kamwe kusikia nimesahauliwa licha yakupigania hadhi ya lugha wanayojinasibu nayo watu hii leo.
Lakini ningefanyaje wakati niwewe ndio uliwahi kuniasa kuhusu kuwa mkweli, uliwahi sema
Siche kweli kuisema, hata kwa mfalme,
Ingawa inauma, sema kweli atazame,
Kweli ina heshima, wajibu wa mwanamume,
Uongo una lawama, ufukuzeni uhame.

Kweli ina thawabu, wametumia mitume,
Japo wamepata tabu, wamerithi ufalme,
Na waliowaadhibu, hawakumbukwi kamwe,
Kweli ina thawabu, kila mtu aseme.

Hakika sitakuwa mwema kama nikiacha sononeko liendelee kukusumbua naomba tabasamu sasa kwa uetnzi wako huu!

Wadogo kuwa wakuu, kwa watu ndio tabia,
Na wa chini kuwa juu, ni jambo la mazoea,
Mwenendo wao ni huu, wanao kama sheria,
Watu duni na wakuu, katika hii dunia.

Katika dunia hii, ya machungu na matamu,
Na rafiki na adui, na mepesi na magumu,
Viumbe walio hai, hubadilishana zamu,
Lakini hawatambui, kwa uchache wa fahamu.

Sina shaka utenzi huo umekufanya ukafarijika kuona kuwa kazi zako bado zingali nasi zikitusuta suto kuu kwa kukusahau baba wa Kiswahili.

Pumzika kwa amani vijana wenye chembechembe za karma aina yako bado twaendelea pambana ingawa twajua kusahauliwa kwako ni sawa nakunyolewa hivyo nasi tumetia maji nywele.