Tupo tofauti sana

nimeamka na neno hilo tangu asubuhi, linajirudia mara kwa mara, napiga mswaki linajirudia, naoga mpaka namaliza linajirudia, najiandaa kwenda kazini linajirudia.
tupo tofauti sana
napigania usafiri mpka nafanikiwa kupanda gari lakini sipati siti bado tu hili neno linajirudia, "tupo tofauti sana" naning'inia na begi langu huku tukiwa tumebanana mno na abiria wenzangu, pemebeni yangu alisimama mama mjamzito, tumbo lilikuwa kubwa mno, nilikuwa namuangalia huku sauti hii ya tupo tofauti ikijirudia,  
huku safari ikiendelea bado sauti ya tupo tofauti ikawa inajirudia,
sehemu niliyosimama akaamka mzee moja aliyekuwa amepata siti akanitaka nikae yeye alikuwa amefika, nikakataa nakumuoneshea yule mwanamke mjamzito akae, akakaa huku akisema 'asante'
nilimuitikia kwa kichwa huku nikiendelea kujisemea tupo tofauti, kiukweli nilikuwa najisemea tu mwenyewe lakini sikuwa najua kwanini najisemea hivyo.
 vituo viwili mbele watu wengi wakashuka mimi safari ilikuwa bado inaendelea hivyo nikalazimika kukaa kwenye siti ambazo sasa zilikuwa zipo tupu, na nilipokaa ndipo nikapata fursa yakutathimni kwa kina kwanini sauti yakujisemea kuwa tupo tofauti sana inajirudia tangu nilipoamka asubuhu,
nafikiri kwa vile nilikuwa nimekaaa mawazo pia yakawa na uga mpana wakujiachia kufikiri, huwa najiamini sana katika kufikiri, nasema hivi sababu sikuchukua muda mrefu tayari nilishaanza kupata uhalisia wa kwanini sauti ile inajirudia,
ni kweli kabisa tupo tofauti, na tunatofautiana sana.
Wakati mimi nimeamka kwenye nyumba yakupanga tena ipo uswahilini kabisa buguruni malapa, yupo ambaye ameamka kwenye nyumba aliyojenga ipo mbezi beach, jana yake usiku nililala mtindo wakukumbatia mto, ila yupo ambaye alilala akiwa amekumbatiwa na mke wake mzuri na katoto kao kadogo ambako nako kazuri mno,
wakati mimi nagombania gari la daladala niwahi kazini, yupo ambaye alikuwa anachagua siku ile atoke na gari la rangi gani ili kuendana rangi ya suti yake ya rangi ya maziwa,
wakati, mimi nimeweza kukataa kukaa kwenye kiti cha daladala kwa ajili yakumpisha mwanamke mjamzito tumbo likimuelemea yupo ambaye alikuwa hana hata mpango wakumpisha licha yakumuona kuwa anahitaji kupewa kipaumbele maalumu kutokana na hali yake, haya ni machache kati ya mengi yanayonipa sababu sasa niseme kwa nguvu TUPO TOFAUTI SANA!
Ona kwenye mitandao ya kijamii, huyu amepost picha yupo kazini kwake, ofisi inaonekana imechoka, haina samani nzuri, lakini ,mwengine anapost akionekana yupo kwenye ofisi nzuri.
tupo tofauti sana kwa kweli, mimi wakati nawaza kuwa tupo tofauti yupo ambaye muda huu anawaza kuwa kama mwengine ili auondoe utofauti uliopo, 
swala la msingi nikuikubali hii dhana nakushukuru huu utoafuti uliopo mana dunia ingekuwa mahala pa ajabu sana kama kusingekuwa na huu utofauti.
huyu anaweka chakula mezani anakipiga picha nakupost mitandaoni mwengine analike huku njaa ikimuuma mno na akiwa hajui atapata wapi chakula.
TUPO TOFAUTI SANA!

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »