MTUNZI : BIN ZONGO
Jina Lake aliitwa Jef alikuwa ni mrefu kwa kimo umbo lililoshiba na sura yake haikuwa ya mzaha.
Maisha yake yalikuwa mtaani, nguo zake zilimtambulisha kwa yoyote kuwa hakuwa timamu kiakili.
alizoeleka kuongea peke yake na kujichekesha mwenyewe bila sababu ya msingi.
alikuwa ni mwendawazimu lakini uzuri wake hakuzuru watu wala kugombana nao yeye alipenda kuwachekea na kila gari na nyumba nzuri aliyoiona alijinasibu kuwa ni ya kwake.
alipenda sana kuzungumza na watoto wadogo ambao wengi walimzoea jef nakumfanya rafiki.
bila shaka wazazi wa watoto wale walithibitisha kuwa Jef hakuwa mwendawazimu wakudhuru watoto ndio maana wakawaacha watoto wao wacheze nae kutwa nzima ingawa pia walikuwepo wazazi waliokuwa wakihofia kuwaacha watoto wao na Jef. wakihisi kuwa ipo siku atazidiwa na uchizi awafanye kitu kibaya.
Pengine labda isingekuwa Rafiki yake jef aitwae Salim hata pia nisingepata lakusimulia kuhusu Jef.
ni Salim ambaye alijaribu kuelezea tatizo linalomkumba Jef, tatizo ambalo wazazi wake na hata mpenzi wake alipambana kulitatua sababu lilimuanza kimasihara sana na hakuna aliyedhani kama angefikia hatua ile.
hakuna Daktari aliyefanikiwa kujua chanzo cha Jef kuwa vile wengi walitoa maoni yao kuwa Jef amerogwa.
lakini hakuna aliyethibitisha hilo wala pia hakuna aliyejitokeza kumuagua!
Baada ya salim kuachana na Jef miaka zaidi ya tano alistaajabishwa sana na hali aliyomkuta nayo mwenzake huyo.
miaka yote hiyo Salim alikuwa yupo nje ya nchi akisomea masuala ya afya ya akili.
kumuona mtaani rafiki yake akirandaranda kama mbuzi wa albadili lilikuwa ni pigo kwake.
alikumbuka mengi aliyowahi kufanya naye enzi akiwa timamu.
siku ya kwanza Salim kujaribu kumfuata Jef ilikuwa ni hatari kubwa!
ni siku hiyo ndio ambayo Jef alizidi kchanganyikiwa!
ilikuwa hivii..
baada ya Salim kumdadisi mama yake na ndugu zake kuhusu hali ya rafiki yake aliamua kwenda nyumbani kwa kina Jef kuwajulia hali na kuwapa pole kwa matatizo yaliyomkuta kijana wao.
ni siku hii ndio ambayo mama yake Jef alilia sana baada ya kumuona Salim.
kijana wake alikuwa makamo sawa na Salim ilimuumiza kichwa sana kwann apatwe na matatizo yale.
Salim alifanya juhudi zakumfariji kabla yakuomba ruhusa yakwenda kumuona Jef lakini aliambiwa kuwa muda ule jef hataki kabisakukaa nyumbani anaaga anaenra kazini.
"hataki kabisa kukaa ndani hasa mida ya mchana ila jioni anarudi mwenyewe nyumbani" alisema kwa uchungu Bi Getrude ambaye ndie mama mzazi wa Jef.
Salim aliumia sana kwa hali aliyomuona nayo mama yake Jef na taarifa alizopewa kuhusu Rafiki yake.
alijikuta anajiambiza mwenyewe kuwa ni lazima amsaidie Jef.
aliondoka nyumbani pale akiwa ana mawazo lukuki na nafsi yake ilimwambia kuwa anapaswa kutumia utaalamu wake aliosomea ili kumsaidia mwenzake.
wakati akikatiza mtaani nyumba tano kutoka nyumbani kwa kina Jef ghafla mbele akaona rundo la watoto wakiimba nakukimbizana na kijana ambaye alipomtazama kwa makini alimtambua kuwa ni Jef rafiki yake.
alijikuta akipigwa na butwaa nakumeza funda kubwa la mate huku akisimama kumtazama Jef, huruma ilimuingia, kumbukumbu za miaka kadhaa nyuma waliyokuwa wakisoma wote ikamrejea.
alimuona mawazoni Jef mwenye nidhamu, msafi mwenye akili na anayejipenda, Jef ambaye alikuwa tofauti kabisa na yule anayemuona mbele akiwa anacheza na watoto.
kwa hatua za tahadhari na umakini Salim alijongea kumsogelea Jef na watoto waliokuwa sasa wamekaa kwenye jumba bovu wakicheza nakucheka.
nafikiri nia ya Jef ilikuwa ni nzuri sana, alipanga kuyaaminisha macho yake kuwa kweli anayemuona ni Jef au amemfananisha.
lakini dhamira yake hiyo iliibua utata mkubwa sana pale Jef alipomuona Salim.
kwa mara ya kwanza tangu Jef awehuke siku hii ndio alionesha hasira yake.
kitendo cha kumuona Salim tu anamtazama kilikuwa ni kitendo cha kero kwake.
masikini ya MUNGU sijui alitafsiri nini kichwani mwake aliamka ghafla akawasukuma watoto waliokuwa wanamdandia dandia nakucheza nae. kisha akamsogelea Salim.
huku Salim akiwa amepigwa na butwaa kwa tukio hilo ghafla alishangaa akivamiwa nakuangushwa chini kama mzigo.
ilikuwa ni hatari Jef alianza kumshambulia kwa mawe na ngumi hila woga wala huruma.
wengi wapita njia walikuwa bado wameduwaa wasijue lakufanya mpaka pale walipoanza kushuhudia damu zikiruka kwa kasi kutoka pale chini.
ni dhahiri SALIM alikuwa yupo katika hatari ya kuuliwa wakati watu wakijishauri kumuokoa.
INAENDELEA....