KUELEKEA SIKU YAKO YA KUZALIWA

Wewe hukumbuki kitu miaka ileee upo tumboni ndio unaelekea kuzaliwa.. Ila mama anakumbuka zaidi, Fanya hivi:

kama mama yupo hai Fanya juu chini utenge muda wakuzungumza nae, kama upo mbali simu sio mbaya ukimpigia lkn ingekuwa vizuri zaidi ungeonana nae macho kwa macho, ungempelekea Zawadi nzuuri ya tenge au khanga kisha ukafanya utani nae kwa kumwambia "mama unaendea kujifungua sasa jiandae kwa khanga hii" bila shaka atafurahia utani huu, atakumbuka mengi sana ya miaka ile kipindi hicho ujauzito wako umekomaa, na pengine mengine Yanaweza hata kumliza lkn usjali muache alie ili apunguze machungu asibaki nayo ndani yanaweza kumuumiza.
wakati huu ndio mzuri kumuomba mama akuhadithie anakumbuka nini kipindi hicho....

Ongea nae kwa mfumo wa utani mwingi, kula nae, mwambie malengo yako, muombe akushauri kwa linalokutatiza (JUNGU KUU HALIKOSI UKOKO)... Zaidi mwambie namna unavyompenda sana, dhihirisha hili kuelekea siku yakuzaliwa kwako.
Kama mama ni mgonjwa, mtu mzima sana au yupo katika hali yoyote ambayo haimpi amani, kuwa nae, tafuta maneno mazuri yakuongea nae hata kama hakusikii mzawadie na umuoneshe thamani yake, aone kuwa hakukosea hata kidogo kukuzaa...

Kama mama ametangulia mbele za haki, usjali hayupo nasi katika mgongo wa ardhi kwa mfumo wa mwili lkn roho yake inaishi nasi, rejea album yako tazama picha zake, ongea na sura uionayo kwenye picha hiyo, muelezee hisia zako namna unavyomkumbuka, unavyovikosa baada ya kifo chake, na jinsi gani unampenda, sema " MAMA BADO UNAISHI NDANI YANGU, NI NGUMU KUKUSAHAU, UPENDO WAKO BADO UNAISHI MAMA, NAKUPENDA SANA MAMA ANGU...NAAMINI IPO SIKU NAFSI ZETU ZITAKUTANA TENA" usizuie kulia lia tu, machozi ni dawa kubwa yakupunguza machungu, ukimaliza kuomboleza kwa picha Fanya taratibu zakumuombea mama apumzike kwa amani kama unaamini ktk MUNGU, tambua kuwa maombi ya mtoto kwa wazazi wake MUNGU huyapokea haraka sana, na amini kuwa mama atapumzika kwa amani kupitia maombi yako.

Usiende kwene kaburi lake kupeleka Maua naona kama ungefanya hivyo ukipata nafasi siku ile yakumbukumbu yakuzaliwa kwako ikifika (birthday).
Kuelekea birthday yako
Unaonaje ukitafakari juhudi zako za maisha, wapi umetoka, wapi ulipo na unapanga kuelekea wapi, katika tafakari hizo utagundua uliowakosea na waliokukosea pia, kuwa mwepesi kuomba msamaha na pia fikiria kuwasamehe waliokukosea na sio lazima uwaambie kuwa umewasemehe iambie tu nafsi yako inatosha.
dhamiria kuanza umri mpya na maisha mapya kwa kuyaacha yale mabaya.
Dah!! kuelekea birthday usitegemee sana kupata wishes nyiiingi kutoka kwa ndugu na marafiki wanaweza siku hiyo wakakuchunia kila mtu kwa sababu zake halafu ukajisikia vibaya hivyo Panga kufurahi mwenyewe na endapo marafiki wakijitokeza kukuunga mkono basi furahi nao na waoneshe kuwa umefurahia ukaribu wao, ni muhimu sana kuweka ratiba nzima ya siku hiyo ili usipate muda wakufikiria Nani kakukumbuka na Nani hajakukumbuka KAMWE USITEGEMEE FURAHA YAKO KUWA MIKONONI KWA WENGINE...
Naamini kuwa BINAADAMU NI MPANGAJI MUNGU NI MUAMUAJI hivyo unaweza ukapanga mengi mazuri katika birthday yako lkn kumbe MUNGU alishaamua kuwa kabla hujafika siku hiyo upatwe na janga lolote hivyo pigania utu wako kwa kumuomba yeye maana HAKUNA AIJUAE SIKU WALA DAKIKA!!
Kuelekea birthday yako......ahahaa!!!

NA ZONGO
‪#‎MREXPERIENCE‬

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »