Allah mkarimu sana, ana nifanya
nahema
Nakushukuru kwa sana, kunijazia
neema
Wewe uliye bayana, hutujuza
baya jema
Dunia tambala gani, na
nimeghafirika
Sikio lazidi kichwa, wahenga
hawapo tena
Vibiongo vimefichwa, uwazi haupo tena
Vinaliwa tu na mchwa, kwasababu
ya hiyana
Dunia tambala gani, na
nimeghafirika
Wanaitana vyumbani, mda wa kula fikapo
Kwa minong’ono ya chini,
wanafungua makopo
Na tena pasipo soni,
wanazizuia pepo
Dunia tambala gani, na
nimeghafirika
Dunia sio tambala, halifai hata
dekio
Ukizubaa kulala, utabaki na masikio
Pima umri kabla, ni mingapi
masalio
Dunia tambala gani, na
nimeghafirika
Msikia la mkuu, nini amefaidika
Amevunjika guu, au hakukumbuka
Kuhesabu toka juu, kukwepa
kughadhabika
Dunia tambala gani, na nimeghafirika
Hiyari ni ndoto njema, ukiiota
mchana
Uking’amua mapema, achana na
kubishana
Ya nini ukilema, kwa yasiyo na
maana
Dunia tambala gani, na
nimeghafirika
By
Fulgence Makayula