Miguu yake ilizongwa na kihoro, jinamizi la laana yakuua lilijichora mbele ya ubongo wake nakumfanya akumbwe na kimbunga cha majuto, sasa alikuwa akikimbia kwa juhudi kwenda pasipojulikana!
jinai ya mauaji ilimsuta suto kuu, tamaa ya kisasi kisicho na sababu ilimgeuka nakumfanya ajutie juhudi zake zamuda mrefu zakutaka kumuua SIMULIZI.
alipita vichochoro kadhaa, mwili wake ulitweta, jasho lilimmiminika kama maji, licha ya kwamba alikuwa hajui anakimbilia wapi wala anamkimbia nani bado ari yakukimbia alikuwa nayo lakini ghafla mbele yake akashuhudia jambo lililomfanya ashtuke maradufu.
akiwa amejibanza kwa umakini kwenye uchochoro mmoja alijionea msafara waheshima ukipita barabarani, Ngamia watatu wa fahari walioshiba vema waliongozana.
ngamia aliyekuwa kati alivutia zaidi!
msafara ule uliongozwa na wanyama hao wapole na wastahamilivu jangwani.
nyuma yao walikuwepo watu idadi isiyoyosemeka, nyuso zao zilipambwa na furaha huku tabasamu la amani na upendo likiwatambulisha kwa yoyote kuwa msafara ule ni wa Bwana SIMULIZI ZINAISHI
ndiyo! alikuwa ni bwana Simulizi, alivalia kanzu na balaghashea, alikuwa juu ya ngamia akitembezwa kwa madaha kana kwamba hana haraka na aendako.
ngamia wawili waliosalia walifungwa bendera iliyoandikwa
ommyzongo.blogspot.com
SIMULIZI ZINAISHI!
kupepea kwa bendera zile kuliashiria Tumaini ya msafara ule.
Jamaa muuaji alipigwa na butwaa, hakuamini alichokiona alijisemea
"nimetoka kumuua iweje awe huku!!? tena mzima bukheri wa Afya!!!" mastaajabio yalimkumba jamaa huyu muuaji, yaani kwa mikono yake alimteketeza SIMULIZI tena wewe msomaji ukiwa shahidi, sasa iweje muda ule Bwana SIMULIZI awe kwenye msafara wa amani na usio nakilio cha aina yoyote! Au zinaishi kwa mazingara!?.
licha ya kwamba majuto yalimkabili baada yakufanikiwa kumdondosha SIMULIZI lakini msafara ule hakuupenda ghafla chuki ikarejea upya.
swali gumu lililojirudia kichwani mwake ni JE simulizi zimeponaje? iweje ziwe pale muda ule??
maswali yote haya yalijirudia kichwani mwake kwa kasi isiyomithilika.
akiwa pale uchochoroni aliendelea kushuhudia msafara ule ukiendelea kwa marefu na mapana.
kwa mbaali alisikia watu wakipaza sauti zao kwa nguvu nakushangilia "ZINAISHIIIIIII...."
akiwa makini huku masikio yake yakisikia na macho yakiona, aliwaona vijana wawili washabiki wa SIMULIZI wakiufuata ule msafara huku wakizungumza kwa sauti.
" nataka kushuhudia hiyo karamu, nasikia huku tuendako kuna mazuri mengi, simulizi za sauti pamoja na zile za picha tutaziona" aliongea kwa shauku kijana huyu huku mwenzake aliyeonekana hajui chochote akimsikiliza kwa umakini.
" nasikia imepewa jina sherehe hii! ningependa kujua yaitwaje????" alihoji kwa tamaa yakujua jamaa yule, mwenzake ambaye alionekana kujua mengi alijibu kwa papara.
" ulianza mchakato wakutafuta jina la sherehe hii, yakatolewa majina mawili 'SHEREHE YA KUGONGA GLAS' na jengine 'KUSHIKANA MIKONO' nasikia eti watu walilalamika wakisema kiswahili hakina maneno mazuru, wakitaka karamu hiyo ipewe majina ya kiingereza eti 'SHAKES HANDS PARTY' au 'CHEERS PARTY' ukiangalia kama kweli hivi lakini BWANA SIMULIZI aligoma akasema huo ni utumwa wa fikra akapitisha jina moja tu la kiswahili ' KARAMU YA KUGONGA GLAS' ndio leo tunaenda jionea"
maongezi haya yalipenya sawia masikioni mwa muuaji, angalau sasa alijua ule msafara unaenda wapi
aliendelea kusimama pale kwa taharuki kuu mpaka pale msafara ule ulipoisha ndipo wazo likamjia,
aliona ni sahihi arudi mahala alipotekeleza jinai.
alichomoka mbio mithili ya risasi, alitaka kwenda kuthibitisha kwa macho yake je aliyemuua ni nani.
kukimbia kwake kwa juhudi kulimfanya afike mapema, ajabu mwili wa SIMULIZI aliukuta bado umelala pale chini.
aliusogelea kwa tahadhari akaukaribia usoni Loh! alichoka..!!
hakuwa simulizi wa kweli ulikuwa ni mfano wake! alichezewa mchezo wa danganya jinga! aliwekewa sanamu lililofanana na SIMULIZI.
alikiri ujinga "kwanini sikushangaa SIMULIZI kuanguka kirahisi hivi! "alijihoji huku moyoni mwake akiuona ujinga ukizunguka sambamba na damu mwilini mwake.
"SIMULIZI ZINAISHI" alijikuta akijisemea mwenyewe hivi, huku akizidi kulikagua lile jitu mfano wa simulizi
"mnh inawezekana kweli zikawa ZINAISHI! Lakini ZITAISHI mpaka lini agh!!!"
wakati akijiuliza hivi huku akijipiga kichwani ghafla simu yake ya mkononi ikawa inaita, alipotazama nani anampigia alikuwa ni mpenzi wake.
aliipokekea akaiweka sikioni upande wapili binti akasikika " bae uko wapi nataka twende kwenye karamu ya Kugonga glas, au kama uko mbali naomba ruhusa niende, ila kumbuka party yenyewe inahusisha watu wawili wawili wapendanao so plz bae naomba uje kama inawezekana"
binti yule alisikika akizungumza kwa kudeka, jamaa alionekana wazi kuwa sauti ya yule mwanamke ndio udhaifu wake mkubwa hapa duniani, alijikuta akikubali kwenda bila kufikiri mara mbili.
alijikuta nayeye akipata shauku ya kuhudhuria ile KARAMU iliyoandaliwa na SIMULIZI ZINAISHI.
"karamu ya kugonga glas" alijisemea mwenyewe baada ya simu ya mpenzi wake kukata.
alirudisha ile simu mfukoni kisha macho yake yakarudi kwenye lile toi lililolala kama marehemu alilipiga teke kwa hasira huku tusi likimtoka kinywani.
taratibu akaanza kuondoka eneo lile akimuwahi mpenzi wake waende kwenye Karamu........
waingereza wanasema.
Itaendeleaaa......
BIN ZONGO