yani ni matatizo bila chuki, sasa unadhani utamchukia nani?
maana unayedhani anapaswa kuchukiwa yeye mwenyewe anatafuta wakumchukia! Hatari, Hatari.
ukata umekithiri, hakuna tumaini, inasemekana kila mmoja anakula kazini kwake lakini inaumiza unapogundua wapo ambao hawana hiyo kazi yaani wapowapo tu kama mikia wakifuata uelekeo wa kichwa!
kwakweli maisha haya ni AFANALEKI!!! jana haikuwa afadhali leo ndio balaa kabisa!
kutokana na hadithi zao, eti wao waliwahi kushindia mlo mmoja na kulalia maji.
inaonekana kwa sasa ngoma ni ngumu zaidi
maana hata huo mlo mmoja ni shida shaka yangu ni maji nayo yakianza kuuzwa, sijui hata itakuwaje!
Wengi wanaigiza kuridhika lakini miili yao inawaumbua, machozi yanayobubujika kwa siri mioyoni mwao inazinyausha sura zao nakuonekana wazi kuwa wanajilazimisha tu kutabasamu!
mzazi aliyetegemea nuru itapatikana baada ya mwanaye kumaliza kusoma bado shushu la kiza cha umasikini linamshushua likitokana na ugumu wa ajira!
baba alipatwa na mshtuko akashikwa na degedege baada yakusikia SIKU HIZI AJIRA ZINAUZWA!
ndio, mwanae ametakiwa atoe pesa apate kazi halafu mbaya zaidi hawataki mkopo wanataka tit fo tat!
Sa zingine unaweza hata ukapaza sauti kwa kiingereza ukiuliza GOD WHERE U'RE????
Huwezi kunielewa wakishua kalamu hii kamwe haitakusisimua sababu wakati bado ukiwa hujazaliwa tayari ajira yako ilishaandaliwa!.
Hapa wananielewa washkaji zangu fulani ambao nafsi zao zimekinai kutamani maisha mazuri ambayo kila siku wanaamini yatafika kesho huku kesho ikiwa haifiki. kwambaali washkaji zangu wanaanza kuhisi dunia haiko sawa sababu elimu zao, vipaji vyao na karama nyengine walizojaaliwa hazijawanufaisha kitu zaidi yakusota kwenye mkeka wa umasikini wenye viraka dhalili vinavyowafanya wasiione thamani yao.
utanielewaje wewe wakati maisha yako yote umezoea kuona Utajiri ukikuzunguka haujui kitu kuhusu umasikini shukuru MUNGU wazazi wako waliwazidi ujanja wazee wengine hivyo wao wakawa vinara na ndio mana wewe huelewi kabisa kuwa huku mtaani wapo watu wanaokota vyakula vilivyowashinda ninyi mkavitupa na kuna wengine wanashindia vikombe kadhaa vya maji yakunywa huku wakiamini mapinduzi yatakuja kesho ukata utageuka ukwasi na watasahau yote.
Maisha Songombingo, ni heri wanaoangukia kuwa wacha mungu kuliko wale wanaoamua kujidunga dawa haramu za kulevya na kuwaibia masikini wenzao.
maisha sasa yamekuwa vichekesho watu wanalalamikia viongozi,
zile juhudi zakuimarisha uchumi wao wanaziona ndio UGUMU wa MAISHA hasira zakukosa shilingi wanazihusisha na siasa! wengine wanabweteka kabisa hata kazi hawafanyi wanalaani maisha magumu! kwakweli ni vichekesho!
ubunifu sasa unatafsiriwa kuwa ni usumbufu
maana watu hawana pesa ya kukuunga mkono wanaona unawachanganya tu.
wewe ukilalama huna lile lipe ruhusa sikio lako lisikie mwengine utabaini analalamikia kukosa hilo ulilo nalo wewe hivyo shukuru MUNGU licha ya kwamba nikweli MAISHA NI SONGOMBINGO!.
Na
BIN ZONGO