Nina ipata
faraja, kwa pendo la maulana
Sina gumizi
kutaja, kwa nguvu za Subuhana
Na giza
likisha kuja, kimbilio kwa Rabana
Kumbukumbu
sifa njema, sipokupa maumivu
Ukikumbuka
kilema, na ukalishika kovu
Mwili utakuzizima,
na kupata ukamavu
Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana
Vunjiko kuu
la moyo, halinipi majutio
Mengi
yavunjikayo, nayaziba masikio
Ninayafuata
hayo, kupata mafanikio
Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana
Mimi wa kuvaa moja,siwezi lilia mbili
Ninavikwepa
vioja, wanione wa akili
Naliuita
umoja, wakaja tukajadili
Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana
Tukasemezana
kucha, lakini hawaku afiki
Walifunga na
mabucha, utii wa kinafiki
Walibaki
kula kucha, ni njia za kizandiki
Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana
Wakabomoa
daraja, lilo jengwa vitabuni
Na bado wana
bwabwaja, hawajui nina nini
Wananiona
buwaja, mzamaji wa ziwani
Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana
Zile ngumi
za fahari,na nyika zikaumia
Kwa yangu
tafakari, aridhi zakaukia
Kutulambisha
shubiri, huku watupulizia
Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana
By
Fulgence Makayula