kwa wewe mwanaume utakae kuja kunioa basi nakuomba jina ambalo utabatizwa na viumbe vitakavyotoka tumboni kwangu ulitumie vizuri sababu wako baadhi ya watu wa jinsia yako wanasahau kulitendea haki jina hilo.
kila siku najiuliza nini maana ya neno "BABA" sababu kwangu sijawahi kabisa kupata tafsiri ya neno hili ijapokuwa nilizaliwa na baba tena mungu akajaalia nikapata baba wapili.
fikra na ndoto zangu zilikuwa nitakuwa mwenye furaha isiyo kifani lakini kumbe niilikuwa nikijidanganya sababu sikujua kitakachokuja kutokea mbele yangu.
kwako baba mzazi ni kweli ni ugumu wa maisha ndo unaokufanya usahau kama unamtoto?au ndo unamsingizia mungu kwamba eti binadamu tumeubwa na chembechembe za kusahau ambazo zinasababisha kutokumbuka kama unamtoto?nijibu basi baba nikupendae kwa dhati.
kwani nini kosa langu kwako baba yangu.wewe huoni uchungu pale unapoona rafiki yako juma anapompigia simu na kuongea na binti yake kila iitwayo leo!!!!.wewe hutamani ule utani wa rafiki yako saidi na binti yake saida kila wanapokutana!!.basi sawa baba pengine hao hawakuhamasishi vipi kuhusu marehemu baba yako aliyokuwa akikaa na kushauriana na yule dada yako mama Asma pia hujavutiwa na matendo hayo kutoka kwa baba yako.
ni kweli nakukosea baba kwa hatua niliyofikia leo ya kunyanyua silaha yangu ambayo ni kalamu na kukuadhibu kwenye jukwaa hili la SIMULIZI ZINAISHI.
ila ni uchungu wa maumivu makali ninayoyapata kwenye moyo wangu ndo yanayosababisha kutoa adhabu hii kwako baba yangu,kukuchapa kwa bakora ni dhambi kubwa kwa mola wangu sababu wewe ni mzazi wangu .
pengine hujui ni kwanini maneno yote haya yananitoka kwenye kinywa changu labda tu nikukumbushe kuwa sababu ni upendo ulionipandikiza toka mwaka 1995 hadi leo na utaendelea kukomaza mizizi hadi kufa kwangu.
lakini nitakuwa ni mchoyo wa fadhila kutokupa shukrani sababu pale mama alipokutaarifu kwamba anakiumbe chako kwenye tumbo lake hukukikataa ulionyesha hali ya furaha hadi mimi niliyekuwa tumboni nilihisi furaha uliyokuwa nayo.
kwa upande wako baba mlezi..nakumbuka kabla hujamuoa mama ulimuahidi kuwa utamlea yeye na na mimi kama binti yako wa kunizaa.
sitoacha kukushukuru kwa yote uliyonitendea na unayoendelea kunitendea sababu ni watu wachache sana wenye upendo kama wako.
lakini baba kwanini unionyeshee kunibagua kwa kipindi hiki ambacho najua kung'amua baya na zuri.
ni wewe ambaye ulianza kunipa maana halisi ya baba lakini kwanini uwe kigeu geu kiasi hiki.
nawaomba baba zangu msinifanyia haya maana mimi binti yenu ni mdhaifu sana kwenu hakika naitaji uwepo na upendo wenu sana....
Na. Esher Swahib