SALAMU ZANGU

By ZONGO
MR. EXPERIENC

Huu ni mwisho wa wiki tamati ya juma hili,
hebu niacheni kwanza nitume salamu zangu!
juma hili linaenda kurudi ni abadani acha nitume salama ziende huko iendako sina shaka itazikuta na wiki nyingi za nyuma ambazo nazo zilikuja nakisha zikatoweka!

hili sio juma la kwanza yalikuja majuma mengi kwa mbwembwe nakisirani kila moja nahulka zake!

nakumbuka juma fulani nilisheheni mipesa, nikaweka vyakula ndani na vinywani vyakusaza leo nikitambo kingi juma lile tangu lije, nalikumbuka hakika lakini ndio basi tena.

ukiachana na hilo kuna moja ndio balaa wiki nzima mitihani, misiba dhiki na njaa! sitaki kukumbuka sana juma lile la machungu siku kadhaa nipo ndani niliumizwa na mapenzi.

alinizuga anaumwa kenda kwao kutibiwa kwakuwa ni mkoani nikabaki namngojea ajabu wiki ileile namuona mtaani akiwa na jamaa mwengine yani niliumia sana ila nashukuru yamepita!

Peleka salamu zangu kwa wiki fulani ivi ilikuja na mawazo mazuri ya maendeleo, nakumbuka nilianza baadhi kuyafanyia kazi lakini changamoto nyingi maungoni zikanikabili mpaka kesho sijafuzu kwa kile nilichowaza, ingawa bado sijachoka naamini nitafanikisha.

ukifika huko uendako itafute wiki fulani ilikuwa ni wiki ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja iambie ahsante sana kwa kuondoka na mama angu, imeniachia kidonda wakukiponya hakuna!
iambie nimekuwa mnyonge kwa ule ubabe wake kwa sasa naitwa yatima sitakaa kuisahau!
najua nawewe wenda kurudi huku hapana utabaki mawazoni mwetu kwa yale ulokuja nayo!
Unaondoka ukiwa na mengi mengine yanaumiza, baba wa rafiki yangu kimabavu umemchukua!

kinachoniuma zaidi kabla yako alikuwa mzima, maradhi umekuja nayo na ndio hayo yamemuua!

Zifike salamu hizi kwa wiki ile ya ajali! wiki ya maafa mfululizo na vilio kwa kila kaya, wiki ya tetemeko majanga ya kupatwa kwa jua! isalimie sana iambie isijirudie, Hatuitamani Asirani.

fikisha salamu pia kwa wiki ya panya road, kutuweka roho juu na mashaka yaso pimika bado sijaisahau wiki ya scopion, wiki ya walimu wababe na wiki ya uzinduzi wa SIMULIZI ZINAISHI!

kuna wiki moja hivi ilikuwa ya mitihani, kodi ya chumba, madeni mtaani mke anataka kula, watoto wanataka ada halafu maradhi yamenikabili!

wiki ile ni hatari Mungu ndie anaejua, kama siye yeye rahmani nahisi ningejiua.

wakati njiani unaenda ukikutana nawiki inayokuja iambie Habii ipunguze hasira iache maya ije kwa ustaarabu ijue kuwa mioyo yetu dhaifu.
iweke kando majaribu ikumbatie njia nzuri iliyonyooka na ituletee mabadiliko mazuri hasa ya yale tuyaotayo.

halafu nimesahau, ni hivi majuzi juzi tu imepita wiki ya Tanzia
wiki ya kifo chake Fidel Castro shujaa!
cuba yote simanzi bendera nusu mlingoti, jamaa amekufa huru sababu nafsi yake ilisimamia ilichoamini, mungu ailaze Roho mahala pema peponi.

wiki gani tena waungwana nikumbusheni, achaneni na ile ya bomoabomoa kule mkwajuni kuna wiki fulani ivi miamba mingi ilianguka, miamba ya siasa za Bongo Samwel Sitta na wengine!
hii ardhi ina maajabu haikinai miili ya watu!!! kutwa ina wapokea na bado inahitaji tena.

nachoka sana na hizi wiki na hasa utendaji wake, zinakuja kimabavu zinafuata ratiba zake, zinafanya zilichoagizwa nakuondoka bila kuaga, wapo wanaojiita wababe, wababe wa dunia hii lakini kuzuia wiki isiondoke wamegonga mwamba!

"nafarijika sana hasa nafsi yangu inapobaini kuwa upo mkono wahaki unaotenda kazi yake kwa siri kubwa duniani hapa" Bin Zongo.

TAFADHALI WIKI HII NISALIMIE SANA WIKI NYENGINE ZILIZOWAHI KUJA!.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »