Bi Getrude anadondoka chini nakupoteza fahamu, watu wachache wanamzunguka na wengine wengi wakikimbilia kushuhudia ajali ya kugongwa kwa Jef_
SASA ENDELEA...
Wengi walioshuhudia ajali ya kugongwa kwa Jef waliona kuwa dereva hakuwa na makosa kabisa na alijitahidi kadiri awezavyo kumkwepa Jef lkn alishindwa kabisa sababu alikuwa anaendesha gari kwa kasi na hakutegemea kabisa kumuona mtu mbele yake.
utu ulikuwa umeumbwa pia kwa dereva yule, alijikuta anayumba sana lkn baadae aliweza kusimama. na alijitolea kumpakiza kwenye gari Jef kumkimbiza hospitini.
Jef alirushwa vibaya sana katika mtaro uliokuwa pembeni mwa barabara ilecya mtaani kwao.
kitendo cha kuukota mwili wake nakuupakia kwenye gari kabla yakuondoka kuelekea hospitali kilichukua dakika kumi tu.
kilichobaki pale ni idadi ya watu walioshuhudia na wapita njia pamoja na viatu vilivyochakaa vya jef pamoja na bahasha lake alilkuwa akipenda kutembea nalo.
aidha pia michirizi ya damu ilionekana yaani kwa muda mchache sana mtaa mzima ulikuwa umezizima kwa huzuni.
wengi wafanyabiashara na watu wa mtaa ule walikuwa wanamjua Jef na walimjua hata kabla hajaanza kupatwa na uwenda wazimu.
Alikuwa ni mtu wa watu, mcheshi na alipenda sana utani zaidi wazee katika mtaa ule walimpenda nakumtambua kwa nidhamu na heshima yake.
Jef sasa alikuwa amegongwa na gari!
taarifa hizi zilikuwa mwiba mkali mioyoni mwa ndugu na jamaa wa Bi getrude na Jef.
zaidi walichanganyikiwa waliposikia kuwa Bi Getrude ameanguka nakupoteza fahamu baada yakushuhudia tukio lile.
magari ya kuwapeleka hospitali yaliongozana huku wachache tu wakifahamu kuwa wale walikuwa ni mtu na mwanae, na wengi walivyofahamishwa haya walizidi kuguswa na ajali ya Jef.
Temeke Hospitali ndipo wote walipofikishwa.
baadae ndugu na watu wengine waliofika kujua maendeleo yao, walipokea habari tofauti na walizokuwa wanazitegemea wao.
taarifa zilikuja kinyume kabisa, Bi Getrude alipoteza maisha kutokana na mshtuko alioupata na madaktari walisema amecheleweshwa kufika hospitali.
kwa upande wa Jef yeye hali yake ilikuwa mbaya sana lakini hakufariki dunia.
taarifa hizi zilikuja kinyume kabisa kutokana na wengi walijua kuwa Jef tayari alishapoteza maisha palepale ilipotokea ajali.
Hili lilikuwa ni pigo takatifu kwa familia ya Bi Getrude, hakika ni mama yao ndio alikuwa nguzo kuu ya familia yao.
hawakuwa na baba, ni Jef ndio alikuwa kaka yao mkubwa wanaemtegemea, Jef alikuwa na wadogo zake wawili wakike aliitwa Suzan na Mwengine wakiume ambaye alikuwa wamwisho kuzaliwa aliitwa Roby.
Mama yao aliwalea kwa mkono ulio na juhudi katika biashara ya mgahawa.
ni biashara hii ndio iliyofanikisha kumsomesha Jef hadi kufika chuo ambapo alisomea biashara .
ni miaka minne alisota kutafuta kazi tangu kumaliza chuo, ni ndani ya miaka hiyo ndipo alipojaribu masuala kadha wa kadha yakujikimu kimaisha lakini aliambulia kutofanikiwa.
ndoto yake yakuja kuwa mfanyabiashara mkubwa na mwenye mafanikio ilikuwa inatokomea kila siku iitwayo leo.
Alishazunguka mara kadhaa pia kutafuta kazi lakini hakubahatika kupata zaidi ya kuitwa kwenye usaili nakisha kusahauliwa.
Siku ya kurukwa na akili hakuna aliyedhani kama asingepona maana alianza kimasihara sana.
ilikuwa ni siku ya alhamisi ambayo Jef alidhamiria kuhudhuria mafunzo mafupi kwa wajasiriamali ambayo yaliitishwa na watu mbalimbali mashuhuri na wenye mafanikio.
Jef alidhamiria siku hii akaitumie kujifunza mengi na kutathimini ni wapi anakosea katika harakati zake zakutafuta maisha.
Ni siku hii ndio aliitumia kuvunja kabati nakutoka nadhifu, shati la rangi ya maziwa, suruali nyeusi na alivaa na viatu vya kuchomeka vya rangi nyeusi huku tai yake ikimfanya aonekane mtu makini zaidi.
ni siku hii ndio ambayo Jef kabla yakutoka kuelekea kwenye mafunzo alianza kwa kuimba inde monie na kucheza kupita kiasi.
ni siku hii ndio aliyoanza kunywa maji mfululizo na kuyamwaga huku na kule.
ni siku hii ndiyo ambayo watu walibaini kuwa Jef amechanganyikiwa.
Ilikuwa ni habari mbaya zaidi kwa mama yake, Marehemu Bi Getrude na mpenzi wake aitwae Jesca.
mwanzo walihangaika sana kumtafutia tiba lakini hakukuwa na dalili yakupona na taratibu mapenzi yakaanza kuchuja kwa Jesca licha ya kujitahidi sana kupigania uzima wa Jef wake ambaye waliahidiana kuoana
lakini matumaini yalimtoka hasa alipomshuhudia Jef akiambatana na watoto nakujiita bosi.
* * *
Miongoni mwa walioguswa na msiba wa Bi Getrude ni Mama yake Salim.
nafsi ilimsuta sana mwanamke huyu alijihisi ni mwenye hatia kubwa katika kifo cha Bi Getrude.
alitamani siku zirudi nyuma ili dakika zile anagongewa mlango na Bi Getrude zijirudie amfungilie waongee na wasameheane na maisha yao yaendelee.
Pigo la kifo cha Bi Getrude lilikuwa ni zaidi hata ya kifo cha mwanae Salim.
ni hapa ndipo alipofikiria kuwa Pengine Salim hakuuliwa na Jef bali ni siku zake tu ziliwadia.
sononeko la nafsi yake lilimtuma ajitoe kwa hali na mali katika msiba na matibabu ya Jef.
Majuma mawili yalikatika huku akishiriki vema kuhakikisha Jef anapata huduma bora hospitalini.
Nafsi ya mwanae Salum ilimvaa mwanamama huyu na alijikuta anatamani zaidi kumsaidia Jef.
Ni MUNGU pekee ndio mtenda miujiza isiyowezekana na mwanadamu yoyote yule, na hii ilidhihirika kupitia ruhusa aliyopewa Jef kutoka hospitalini.
Jef aliruhusiwa akiwa hawezi kutembea kutokana na miguu yake yote miwili kuvunjika lkn kilichowashangaza zaidi Jef hakuwa Mwendawazimu tena!.
Alikuwa ni Jef timamu, mkimya na mwenye kuomba apone haraka ili akalitembele kaburi la mama yake.
Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa Jef aliumbwa tena.
Mama yake Salum alichukua jukumu la kumuhudumia kila kitu Jef mpaka anaanza mazoezi yakutembea bado alikuwa yupo kwakina Salim.
*********
Upo mkono ambao unafanya kazi kwa siri sana hapa duniani,
ni mkono huu ndio ambao huweza kumuangusha huyu nakumuinua yule,
na sina shaka ni mkono huu ndio ambao uliendelea kufanya kazi yakumponya Jef,
alipona kwa kufuata maagizo ya madaktari na mazoezi ya mara kwa mara.
ni Jef huyu ndiye ambaye alipata simu ya kazi katika taasisi moja ya mikopo ambayo aliwahi kuitumia maombi miezi nane iliyopita.
NI JEF HUYU NDIYE ANAYEPATIKANA KATIKA SIMULIZI YANGU NZURI IITWAYO *TSUNAMI LA HUBA*
Nafsi ya Salim na Bi Getrude zikiwa angani zilibisha hodi mbinguni huku zikijadili masuala mengi yaliyoabaki kitendawili vichwani mwa ndugu na jamaa zao.
Bi Getrude: Msamehe Jef hakujua atendalo
Salim: hapana mama Jef hakuhusika na kifo changu, nilijiua mwenyewe.
Bi Getrude : (kwa mshangao) ulijiua!!? ulijiua kwa sababu gani?
Salim: (akionekana kujutia) ni sababu ya mapenzi mama lakini ni simulizi ndefu sana! _Simulizi hii yenye siri ya kifo cha Salim inaitwa *Doa*
nafsi za wawili hawa zinapungiana mkono kila mmoja akielekea upande wake Bi getrude anaelekea mashariki mwa mbingu na Salim anaelekea magharibi kisha anga linafunga ishara kuwa kitabu cha historia yao ulimwenguni kimefunikwa.
Duniani Jef Alimgeuza Bi Hadija yaani mama ake Salim kuwa ni mlezi na mama yake aliyemsaidia.
licha ya kwamba alihama nakupanga chumba maeneo ya Magomeni Mikumi jijini dar es salaam lkn mara nyingi siku za mwisho wa wiki alipendelea kwenda temeke nyumbani kwao kuwasalimia wadogo na rafiki zake.
*CHIZI MAFANIKIO NI SEHEMU YA KWANZA YA SIMULIZI YANGU IITWAYO TSUNAMI LA HUBA NA PIA BAADHI YA WAHUSIKA KAMA VILE SALIM ANAPATIKANA KWENYE SEHEMU NDOGO YA SIMULIZI YANGU NYENGINE IITWAYO DOA*
kwa simulizi fupi tembelea ommyzongo.blogspot.com
watsap simulizi-0782181862
"ishi na kila mmoja kwa upendo ili siku moja akikukumbuka tabasamu liipambe sura yake" Bin Zongo
MWISHO..