Usiku wa Kuamkia siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya
uhuru wa mtanganyika, ndio mwanzo wa simulizi yangu inapoanzia, na itakapoishia.
Ilikuwa ni alhamisi Fulani yenye ukame wa hali ya
juu mifukoni mwangu, mishale ya saa mbili usiku narudi zangu kwangu njaa ikiliadhibu
vilivyo tumbo langu tena bila hata chembe ya huruma , kinywa kililichacha
nakufanya kitoe harufu kwa mbaali maana hakikupata riziki ya kitu chochote tangu
kulipokucha.
“Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu” faraja ya msemo
huu siioni mwenzenu maana ni kitambo sasa nakaba golini lakini sioni mbivu za
wateja yaani uzuri wa bidhaa zangu
wanidodea mwenyewe, unga unga mwana yaani kwa neno moja tu lakusema kwa herufi
kubwa HALI NI NGUMU,Siju nikwangu tu au na wenzangu kwakweli hilo sijui.
Utangulizi huo sio lengo la simulizi hii! Acha nitie
udhu kuanza kukupa kisa hiki ambacho babu yangu alinisihi sana akisema hata kama akiwa
hayupo nihakikishe ndani ya miaka 55 nimuandikie ujumbe niwakabidhi wachunga
mbuzi wakienda chunga makaburini wataenda kumsomea naye atapata kujua hali
halisi ya uhuru wa mtanganyika ndani ya miaka 55.
Hasira ya njaa kali ya kutwa nzima nisingeweza
kulala siku ile bila kutumia akiba ya viunga na mchele villivyopo ndani kwangu,
kabla yakupika nikajishauri, “ninayo mia nne ya nauli ya kesho ya kwenda golini
kwangu, nikisema nikanunue nyanya na vitunguu ili niunde kachumbali ni dhahiri
nitakosa nauli, kwahivyo ugali hauna nafasi acha nipike wali maana ndio chakula
pekee ambacho unaweza kula bila mboga,” wali ndio lawa kimbilio langu.
nawaza sasa hatua zakupika wali, nagundua mafuta yakula yameabaki kidogo mno! Lakini najifariji kuwa yatatosha , changamoto ilikuwa kwenye maji yakupikia, ndoo zote zilinizomea, hazikuwa na maji!, Maji ni shilingi mia moja na hamsini kwa jirani, nikiitoa mia moja na hamsini kesho nauli nitakosa! Acha nikatumie ujirani mwema nikakope ndoo moja! Najishauri hivyo.
nawaza sasa hatua zakupika wali, nagundua mafuta yakula yameabaki kidogo mno! Lakini najifariji kuwa yatatosha , changamoto ilikuwa kwenye maji yakupikia, ndoo zote zilinizomea, hazikuwa na maji!, Maji ni shilingi mia moja na hamsini kwa jirani, nikiitoa mia moja na hamsini kesho nauli nitakosa! Acha nikatumie ujirani mwema nikakope ndoo moja! Najishauri hivyo.
Hivyohivyo kwa kuungaunga nakamilisha mapishi,
ubwabwa na chai, naweka mziki wa
mwanamuziki wa kurap nchini Tanzania anaitwa Darasa, wimbo wake ndio ulikuwa
unatamba kote ndani ya siku hizi za maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru, Maisha na
muziki, midundo na maneno yake mepesi yananifanya natabasamu, natikisa kichwa
nikisahau shida na matatizo yakushinda na njaa kutwa nzima, ubwabwa unaenda
kufariji tumbo langu, namaliza namshukuru MUNGU.
Kwa mara ya kwanza sasa ndio nahisi kumbe Dar ina
joto, maana wakati nina njaa hata jasho lilinisusa, nabangaiza maji niliyoyakopa
kwa jirani nachota kidogo mengine nabakisha nikijiambiza “yalobaki nitaoga
kesho”.
Namalizia kuoga narudi ndani najitupa kitandani,
napiga goti kumshukuru MUNGU kwa kunilinda kutwa nzima, nilipoenda kutafuta tonge
sikurudi nalo lakini nilirudi na uzima hivyo tumaini la kulipata tonge langu
kesho lilikuwa lipo na lilitegemea Baraka za Mungu.
Katikati ya maombi mawazo yanirudi nakumbuka tena
ile ilikuwa ni alhamisi, tayari usiku uliingia kuamkia ijumaa ya tarehe 9 mwezi
wa kumi na mbili mwaka wa 2016, Siku adhimu ya watanganyika kusheherekea miaka 55
ya Uhuru! Tabasamu lanijaa, nikiwa bado nipo ndani ya maombi, tabasamu lakuwa
miongoni mwa watanganyika wanaoishi kwenye Amani na Mshikamano.
Ningemkopa nani maji yakupikia kama Ukabila
ungetutenga watanganyika? Jirani yangu ni musilamu haya na huu ulokole wangu
angenipokea nakunikopesha ndoo ile ya maji kweli, nafarijika na najvunia miaka 55
ya UHURU, AMANI na MSHIKAMANO.
Kuhusu UPENDO sina uhakika sana maana naamini wapo miongoni
mwa Watanganyika wakati mimi nakula ubwabwa nakuifanya chai kuwa mboga wao
wanavinjari kwa vyakula vyakusaza, wanakunywa mvinyo na kila aina ya juisi
zenye ladha mbalimbali, Upendo huu wa aina gani? kwanini miaka 55 kuwe na
utofauti huu wakimaisha?
Yaani wakati Mimi nawazia mia nne ya nauli kesho,
wao tayari gari lakusafiria kesho limeshafanyiwa maandalizi yote, haya yote
niliyawaza nikiwa katika maombi ajabu ghafla lile tabasamu langu la awali likaanza kufutika
taratiibu, likafutika baada ya kuuona uhuru wa miaka 55 kukiwa na tabaka kubwa
sana la wenye nacho na wasio nacho.
Labda nikujulishe tuu sababu ya siku hii kufanya
maombi ya muda mrefu, ni kwasababu ya babu yangu, aliyepigania uhuru miaka hiyo
na ambaye alifariki mikononi mwangu akiniambia shauku yake yakutaka kujua
Tanganyika ndani ya miaka 55 ya uhuru itakuwaje.
Nilipiga magoti kumuomba msamaha Babu maana sikupata
namna yakumfikishia ujumbe, hivyo nikawa nayawaza haya nikiamini nafsi yake
inayapokea, niliamua kumfikishia ujumbe kwa njia ya maombi.
Maombi yangu yalikoma baada ya usingizi kuanza
kunighasi, sasa mwili ulihitaji kulala ukijiandaa na sherehe za maadhimisho ya
Uhuru wa Tanganyika baada ya miaka 55,
hatimaye nikalala, mawazo yangu yakaleta ndoto, ndoto ambayo ilitokana nakufikiria sana kuhusu babu yangu!
hatimaye nikalala, mawazo yangu yakaleta ndoto, ndoto ambayo ilitokana nakufikiria sana kuhusu babu yangu!
Babu alinijia, akaniamsha nakunitaka twende
tukaadhimishe miaka 55 ya Uhuru wa taifa letu kwa kutembea tujionee, usiku ule
babu yangu alinitembeza nilishangaa sana mipaka ya mikoa na wilaya tukiipita
kwa kutembea tu kwa miguu na bila hata ya uchovu,
Mwisho wa safari yetu babu akanitelekeza mbali sana
hata sipajui, alidai ametosheka, alinishukuru kwa kumsindikiza akanitaka nirudi
alisema “Zamani sisi popote ukiachwa mradi ndani ya mipaka ya Tanganyika basi
wewe upo salama, bado nina imani hiyo naamini utafika salama nyumbani”
kabla yakuondoka nikamzuia, nikamwambia tumetembea umejionea mengi lakini hukunipa nafasi nizungumze, babu akanitazama, sijamjali nikaanza kuongea.
"Taifa letu kila kukicha utawasikia watanzania wakisema Afadhali ya jana, tafsiri yangu ni kuwa Taifa letu linapiga hatua bila wenyewe kujua! maana kama jana ilikuwa afadhali basi hata leo pia itakuwa afadhali, kesho na kesho kutwa mwisho siku zote zitakuwa afadhali, naona miundombinu inaimarika si haba, nina uhakika Tanganyika hii ya leo sio sawa na ile mlioiotoa kwa mkoloni.
kitu kimoja nikiri bado hakijakaa sawa, umasikini kwa walio wengi, ajira ni changamoto, hali ngumu ya maisha milo mitatu ni ndoto, miwili ni hadithi na huo mmoja ni bahati nasibu.
mchawi wetu ni nani ni swali gumu bado halijapatiwa jibu maana raslimali zetu ni tunu inayoninyima sababu ya Watanzania kuendelea kuteseka na kulipa kodi zisizo zaa shule bora, hospitali nzuri, na vyengine vyenye manufaa kwao.
sikatai tunaendelea lakini siridhishwi na mwendo huu tunaotembea kuyafuata hayo maendeleo, tupeni baraka wazee wetu mliotangulia ili tumnase mchawi ,aadhibiwe na awaachie ahueni watanganyika wafurahie uhuru wao.
Awamu zote za uongozi zilizopita ni Bora, Mungu awalinde viongozi wetu, wale waliopita, aliyopo sasa na atakayekuja wote waweke alama ya heshima kuu ya Taifa hili lenye baraka zote kutoka kwa MUNGU wetu.
niliropoka mfululizo kumuelezea babu ninachoweza sema ndani ya miaka 55 lakini ajabu babu akaninyamazisha, akadai anataka kuondoka, kabla sijamjibu akaanza piga hatua
nilidhani masikhara lakini huwezi amini babu akaniacha kweli, muda mchache
baadae askari wakanikuta natembea wakanikamata kwa kosa la uzururaji usiku,
nilitupwa sero kinyama na nikashtuka kwa woga kutoka ndotoni, asante mungu nilikuwa
kwangu, Umeme ulikatika, lakini kwa jirani ulikuwepo!! jibu nikalipata kuwa luku
imekata, nitafanyaje sasa ndani hakulaliki, zamu yangu kununua umeme lakini
pesa sina, niliamua kwenda nje kukesha nikipigwa
na baridi kungojea Siku ya maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika
ambayo hivi sasa inapendeza zaidi na inatambulika kote ikiitwa TANZANIA.