Ipo siku ambayo nilikupiga sana, nilikupiga kipigo cha pakaMwizi! ulitetea uso wako nisiuharibu, ukalia kwa uchungu nikuhurumie lakini sikukusikiliza nikaongeza madoido katika kuushambulia mwili wako.
kosa lilikuwa ni wewe kuniuliza kwanini nimechelewa kurudi nyumbani, nakumbuka niling'aka kwa hasira nikakuhoji kwa chuki "kwanini unanifuatilia!?" nilisahau kabisa kuwa wewe nimke wangu unapaswa kuniuliza chochote ukipendacho.
nakumbuka baada ya kipigo kile kilichokuletea homa kali ulikosa kabisa huruma yangu, nilikutelekeza bila kuacha pesa nyumbani ya matumizi, nilidiriki kumuachia pesa mwanangu ili akanunue chipsi ale njaa ikimuuma.
mwanao aliponiuliza kuhusu wewe nilimtolea maneno makali kumuonya! masikini mtoto akaogopa ikawa inampasa pesa ndogo ninayomuachia akukabidhi wewe ili mtafute kitu chakula pamoja.
siku tatu mfululizo hali ilikuwa ni hii kumbe ulikuwa unajikaza ndani yako ulikuwa unaumwa kupita kiasi, ulipoona sikujali na hata pesa yakwenda hospitali nimekunyima.
maskini mke wangu ukaamua kurudi nyumbani kwenu ili ukapate tiba kisha ukipona urudi.
uliponigusia kuwa unataka kwenda nyumbani hukuniambia kuwa unaenda kutafuta nusura ya afya yako mgogoro iliyotokana na kipigo changu, nakumbuka uliniambia unaenda tu kusalimia ila utakaa wiki moja! nilikujibu kwa kiburi "nenda ila mwanangu muache wewe hata usiporudi ni sawa tu" masikini haukukasirika wala kubishana namimi zaidi ulinishukuru kwa kukuruhusu na uliponiomba nauli nikakutukana nakutaka kukupiga tena ukawahi kupiga magoti chini ukinisihi nisikupige tena maana hali yako si nzuri!
kwa mbaali sana huruma ikaniingia mwanangu alipokuja nae akasema "baba usimpige tena mama anaumwa sana...msamehe!" kauli hii ilinichoma kidogo hivyo nikaambulia kukupiga kofi moja tu.
nakumbuka niliingia ndani usiku ule nikakutolea pesa nakumbuka sijakukabidhi mkononi bali nilikutupia kiasi chakutosha nauli yako kisha nikamwambia mtoto ajiandae usiku ule nikaondoka nae.
nilikuacha nyumbani ukitamani kuniuliza naenda wapi na mtoto usiku ule, bila shaka uliogopa pengine labda naweza nikakushambulia tena na kipigo.
Mwanangu nilimpeleka kwa mwanamke wangu wa nje, ni mwanammke huyu ndiye aliyefanya niuze lile gari lako nililokununulia kisha pesa nikaongezea kumnunuli yeye gari.
niyeye ndiye aliyenifanya siku ile nikakulaza ukumbini kisa mimi nayeye tunataka kutumia chumba chako unacholala namimi kila siku.
ni huyu ndiye ambaye amenifanya kwa hiyari yangu niandike mali zote jina lake hata ambazo nimechuma nawewe.
Mwanamke huyu ndiye aliyenizuzua nakunifanya nisiione tena thamani yako iliyonishawishi nikuoe.
Uliponiaga unaenda kwenu niliona mwanangu hastahili kubaki nawewe hivyo nikampeleka kwa mwanamke huyu.
hata wiki ilipoisha bila kukuuliza kama umefika salama mimi kwangu niliona sawa tu!
mama yako mara kadhaa alikuwa akinipigia simu bila kujua anataka kusema nini niliikata mwisho nikamblock kabisa.
najishangaa sababu hata mwanangu afya yake ilipoanza kudhoofu sikushtuka niliona kawaida nikijiaminisha kuwa ni sababu tu hajamzoea mama yake mpya ila baada ya muda atakuwa kawaida.
mwezi mmoja tu mwanangu anafariki dunia bila hata kujua kuwa alikutana na madhila ya dhiki namateso makubwa.
mie ninapokuwa kazini kumbe mwanamke huyu alikuwa anamsimanga, anampiga nakumfanyia ukatili usiosemeka, alikuwa hampi chakula akashiba wala hampi uhuru wakufurahia mali za wazazi wake maana sikumkuta na kitu mwanamke huyu, naumia sana kugundua leo kuwa kumbe mwanamke huyu alikuwa anadiriki kutafuta vijana wahuni ili wamuingilie kinyume na maumbile mtoto wangu.
mwanangu mpendwa amefariki dunia kwa ujinga wangu ulionipa upofu wakuona ubaya wa mwanamke huyu.
ni muda huu ndio nagundua umuhimu wako najaribu kukutafuta napata taarifa kuwa nawe umeshafariki kumbe kile kipigo cha siku ile uliumia ndani na damu iliivilia huko hivyo madaktari walishindwa kuokoa maisha yako maana ulichelewa kutibiwa.
napiga simu nyumbani kwenu kuwapa taarifa za msiba wa mtoto ndipo nami napewa taarifa za msiba wako!
taarifa hizi zinanishtua mno na kufanya nishtuke pia usingizini, nafarijika kukuona mke wangu upo hai maana imeniumiza sana sauti ya mama ako kwenye ndoto ikiniambia umekufa.
kushtuka kwangu kumekushtua nawe usingizini, saa hizi ni usiku sana mke wangu isingekuwa wewe kunilazimisha nikuhadithie nimeota nini nisingekuhadithia maana usiku una mengi.
ila mke wangu hii ndoto imeniliza nakunihuzunisha sana nakuomba sana tumuombe MUNGU ya kwenye ndoto yasije yakajitokeza kwenye ndoa yetu na hata kama ikitokea naomba tena nakuomba sana USINISAMEHE kamwe..
Na........
Omar Zongo
Na........
Omar Zongo