.KAMA NI KITU, HIKI CHA ARUSHA
















Anasimulia
Omar Zongo

Siku ni Ijumaa tarehe ni Nane mwezi wa Sita mwaka ni hu huu 2017 Ubongo wa Mtanzania ukiwa umetulia tuli ukitathmini
Uwasilishaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18....!

Macho ya Mtanzania huyo kada ya chini ambaye licha yakuwa akitajiwa trilioni anaona mapicha picha haelewi inakuaje kuaje wala inafananaje lakini hayakuchoka kabisa kutazama luninga na kusikiliza redio zikitangaza mujarabu kutoka Dodoma.

Waziri wa fedha Philip Mpango akijinasibu kwelikweli na Mkoba wake nadhifu wenye makarabrasha yaliyosheheni Taarifa muhimu kuhusu Bajeti hiyo aliweza kushangiliwa vilivyo na wabunge wengi wakipongeza bajeti hiyo wengine wakidiriki kusema "HAIJAWAHI TOKEA"

Nilikujuza mwanzo wa andiko langu hili kuwa zilizokuwa zinatajwa ni namba mara sjui trilioni, mara bilioni mara sjui mwaka wa fedha, vyote hivi yule jamaa angu Mtanzania kada ya chini anavisikia lakini kuvielewa ndio tatizo.
tumaini lake pekee ni kwa rafiki zake waandishi wa habari ambao anaamini watamsaidia kumtafutia wachambuzi wa masuala ya uchumi ambao angalau wao watatolea ufafanuzi mkubwa kuhusu Bajeti na pengine pia watawasha nuru kupitia usomi wao na mtanzania ataelewa udhaifu na ukamilifu wa bajeti hiyo ya Mtanzania ambayo inaakisi mustakabali wake wa kuishi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Masikini ya Mungu vyombo vya habari vikiwa makini kutafuta wasomi na wachambuzi wa masuala ya uchumi ili kuitathimini bajeti hiyo nakumrahisishia mtanzania kuweza kung'amua kinagaubaga bajeti yake ghafla tsunami zito lajitokeza siku tatu baadae!

Tsunami hilo linavuruga kabisa ubongo wa mtanzania nakumfanya ashindwe kustahimili, sumu ya usahaulifu inamvaa kote maungoni nakumfanya aamue kuachana na habari za Bajeti ili kuachia nafasi ubongo wake uwaze hatma ya tsunami hili.

tsunami hilo liitwalo RIPOTI YA PILI YA MCHANGA WENYE MADINI linavuruga kabisa vichwa vya watu nakuwafanya wasahau kabisa kuitathimi ile trilion 31.6 kuelekea 2018/2019.

Rafiki anayeaminiwa kabisa na Mtanzania aitwae VYOMBO VYA HABARI naye hupelekwa na matukio nakusahau kabisa wajibu wake wakuweka uwiano sawa wa kila tukio llinalojiri na umuhimu wake.

Vyombo vya habari vinayumba nakumfanya Mtanzania nae ayumbe na ubongo wake uishi kwenye Tukio jipya linalojiri kila siku bila kuzingatia lile la jana ambalo pengine ni chachu ya ukamilifu wa hili la leo.

YANAYOJIRI YANACHANGANYA, KAMA NI KITU HIKI CHA ARUSHA!!!

Na..
Omar Zongo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »