TANZIA....



Siupendi huu utenzi
shairi hili machozi
rafiki wangu waenzi
kanitoka majonzi

sikumjua utotoni
tumejuana chuoni
rafiki wa darasani
alikuwa mwandani

taaluma yetu habari
mtangazaji hodari
chipukizi mashuhuri
amenitoka kwakweli

baada ya mitihani
alienda mkoani
kazi za redioni
alazwe pema peponi

mahafali yamefika
taarifa zikamfika
safari ikapangika
kurudi kufurahika

wakati yupo njiani
ajali barabarani
maafa ya huzuni
tanzia kote chuoni

rafiki hayupo nasi
huzuni ya mwendokasi
majonzi yanatughasi
wote alosoma nasi.

Tanzia ilo pomoni
machozi mengi usoni
nashtuka usingizini
asante kumbe ndotoni.

Mungu baraka zako
ishushe neema yako
epusha balaa lako
utukufu wote wako

mahafali ya amani
jaalia Maanani
mikosi ya duniani
epusha kwetu chuoni.

Maombi ndio hekima
naomba nilale tena
ndoto iso na mana
naomba isije tena.

.Na. 
Bin Zongo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »