Nakushukuru Karima, umpendevu ajabu
Unanifanya nahema, kunipa nyingi thawabu
Ninaipata salama, sia yakutu bawabu
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Ikarima ya Imamu, shauku tunu amini
Ulinipatia salamu, kwa mikonoko kichwani
Ukaniita binamu, na majina ya utani
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Umenialika kwako, nakuja nafamilia
Nabeba yangu mifuko, na
vibwende navalia
Usije pata shituko, mi sina cha kulalia
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Una nyumba kubwa sana, tarifa nimepata
Yenye viwanja vipana, na kwa kufugia bata
Nina kuweka bayana, usipike vya mafuta
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Hapa nipo nimekonda, mzee kama kijana
Pika ninavyo vipenda, vya enzi zetu za jana
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Situmii vya dukani, vinanitoa malenge
Andaa na vya zamani, kama vya kwa mama bonge
Ule mkeka wa utani, ulosukwa kwa mkonge
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Unitandikie chini, nikila na kulalia
Na kiti cha makondeni, sebuleni ntakalia
Zile nyimbo za zamani, nitafurahi kusikia
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Nimesikia tetesi, kwa chombo ki onaona
Wabomoa mkakasi, alojengea Sabuna
Yeye ni fundi wa nyasi, aliyejifunza kushona
Ahsante mwanakuja, salamu nimezipata
Hakika juhudi nzuri, wembamba wakupongeza
Nina yaona dhahiri, na wala sitakubeza
Nakutambua Amiri, usiyejua teleza
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Mimi sipendi kasuku, nasikia unafuga
Uwafukuze na huku, wanaiba zetu soga
Uzifute na shabuku, usije nipe mizoga
Ahsante mwanakuja, salamu
nimezipata
Na,
Fulgence Makayula
1 comments:
commentsnimependa mirindimo,utashi na vibweka
Replyimenifika muguno,kiswahili kukiteka
shairi la mikuno,na ujumbe ukaweka
yakale ndio puno,sasa ni hekaheka
ahsanteni mwanakuja,salamu nimezipata