Idadi kubwa ya watu wake kwa waume, wazee kwa watoto, wasichana kwa wavulana.
eneo ni porini ni nyasi tu ndio zimesambaa kote, watu hawa wamekaa chini ya mti wa muembe.
mwenyekiti wa mkutano wao alikuwa ni mfupi kuliko wote waliokuwa pale.
alivaa koti kubwa kuliko kimo chake, hakuwa na kipaza sauti hivyo alilazimika kuipaza sauti yake isikike kuwafikia watu wote waliokusanyika pale.
watu wakiwa makini kumsikiliza ghafla jamaa fulani ambaye mwili wake ulikuwa mkubwa (mnene) akasikika akipumua kwa nguvu jambo lililozua tafurani na watu kuguna nakupoteza umakini wakumsikiliza mwenyekiti wao.
hali ya hewa ilibadilika ghafla katika eneo lile, jamaa bonge huku akiona aibu akajikuta akijikaza kuamka ili aombe radhi lakini kabla yakufanikisha zoezi hilo alijikuta akipumua tena mfululizo tena kwa sauti kuu iliyopenya masikioni mwa wote waliokusanyika pale, masikini ya Mungu mtu mnene yule sijui alishiba maharagwe mpaka yakamfanya ashindwe kujizuia kupumua hovyo nakuharibu hali ya hewa.
baadhi ya watu waliokuwa pale walianza kucheka kwa sirisiri lakini mwisho wakashindwa kujizuia wakajikuta wanaangua kicheko kikubwa akiwemo mwenyekiti wa kikao kile.
mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa karibu na yule mtu mnene alijikuta akiingiwa na aibu, aliyekuwa akichekwa ni mume wake. alijisikia aibu sana alitamani ardhi ipasuke aingie ndani.
"jamani basi yaishe tuendeleeni na kikao..!" alisikika mwenyekiti akizungumza na watu wote wakakaa kimya kumsikiliza.
"lengo lakukusanyika hapa nikutafuta namna yakuzidhoofisha simulizi, nasikia wanasema zinaishi inawesekana kuna ukweli maana nimezitafutia sumu ya panya nikazinywesha lakini wapi bado zinahema na wala hazionekani kuwa na dalili yakufa...bila shaka wote hapa tuliopo ni wapinga simulizi sasa kila mmoja atoe maoni yake..."
alipaza sauti mwenyekiti yule ambaye meno yale yalikuwa meupe sana hivyo kumfanya akizungumza angalau aonekane kutokana na kuwa mweusi kuliko ulivyo mkaa.
"mnh huyu nae mwenyewe mweusi bado akajivika koti jeusi watu wengine hawajijui loh"
alijisemea nafsini mwanamke mmoja ambaye alikaa pembeni kabisa akifuatilia kikao cha Wapinga Simulizi.
watu sasa walikuwa wamenyoosha vidole wakionekana kila mmoja ana shauku yakutoa maoni ya namna gani nzuri yakudhoofisha Simulizi.
mwenyekiti akiwa makini kuchagua nani aanza kuzungumza ndani yake alikuwa akijisemea " hawa watu wangejua hapa kuwa nina njaa tangu asubuhi sijala hata wasingenipa uenyekiti"
alijisemea hivi huku akisindikizwa na miayo ya njaa huku yeye mwenyewe akilazimisha ionekane ni uchovu.
"acha nichague wanawake wazuri wazuri tu, mijianaume najifanya kama siioni" alijisemea tena mwenyekiti huku akimchagua mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa katikati ya kundi la watu.
mwanamke yule alisimama alikuwa amesuka mtindo wa haraka niwahi maarufu kama nywele za msibani chini alivaa kandambili kuubwa kuliko miguu yake. alisimama kwa mbwembwe akilazimisha kuonekana mzuri kwa kusimama akijitingisha ilhali mwili wenyewe hakujaaliwa yaani alipendelewa mifupa zaidi ya nyama.
sauti yake ndio iliwashangaza watu zaidi hakuna aliyetegemea kuwa mwanamke yule angekuwa na sauti nzito kama mwanaume.
mbaya zaidi alizungumza kwa jazba kama mtu angekuwa hamuoni angesema aneyezungumza ni mwanaume.
"kwakweli siwapendi sana hawa watu wa simulizi,wananinkera kuanzia chini yao mpaka juu yao, nawachukia sana"
aling'aka mwanamama yule huku kitaalamu akiwa hajazungumza kitu chamaana hata kimoja, alizunguka tu kwa maneno meengi lkn akiwa na maana moja tu kuwa Hazipendi Simulizi Zinazoishi.
katika kuonesha wote waliokuwa pale akili zao zilifanana walijikuta wanampigia makofi kwa wingi.
na mwenyekiti bila kujua kuwa alichouliza hakijajibiwa alijikuta anamruhusu mwanamama yule kukaa baada yakuthibitisha kuwa amemaliza kuchangia.
"vizuri sana haya mwengine mwenye mawazo yakudhoofisha si....." kabla mwenyekiti hajamaliza kuzungumza yule mwanadada mwenye sautu nzito alisimama tena akidai eti amesahau kitu muhimu chakuzungumza, watu wote wakanyamaza nakumgeukia.
"katika simulizi Kuna kale kadada kutoka nyanda za kati kanajiita Wendo yaani sikapendi kanajiona kazuuuri kutwa mitandaoni na picha picha zao za Simulizi, yaani bahati yake me simu yangu mbovu yakuingia huko fesibuku!"
alizungumza tena yule mwanamama huku pia bado akiwa hajachangia njia yakudhoofisha Harakati za Simulizi lkn bahati mbaya hakuna pia aliyegundua hili wote walijikuta wakipiga makofi wakimsifia amechangia vizuri.
"haya asante kwa kuchangia kaa chini mwengine aamke achangie" aliamrisha mwenyekiti huku akipiga miayo mara kwa mara.
safari hii aliamka mwanaume alikuwa amevaa kanzu nyeupe lakini ilibadilika rangi kutokana na kuchakaa na ilikuwa na viraka kila sehemu.
baraghashea aliyovaa ndio ilikuwa vituko zaidi ilirarukararuka kama imeshambuliwa na bomu, jamaa huyu alikuwa mrefu kiasi, mwembamba kwa umbo, pengine kutokana na urefu wake ndio maana watu walielekeza umakini wao kwake.
jamaa alianzakwa kusalimia
loh! ilikuwa ni ajabu sauti yake yaani ilikuwa nyembamba mno, kama ya kike.
ilistaajabisha sana maana mchangiaji wakwanza wakike alikuwa ana sauti nzito yakiume sasa huyu wakiume inakuaje awe na sauti nyembamba ya kike.
mwenyekiti akahisi anadharauliwa, bila hata kufikiri mara mbili akasimama akamuamrisha jamaa akae,
"ndugu yangu mwenyekanzu kama unaenda kwenye mualiko, tafadhali kaa chini hakikisha sauti yako inakuwa yakiume, nzito yakishababi kisha utazungumza. haiwezekani mwanaume uwe na sauti hiyo, eboo!!"
watu wote wakajikuta wanaangua kicheko, masikini baba wa watu mwenyekanzu akajikuta akikumbwa na huzuni na aibu ndani yake, mwenyekiti alimdhalilisha, alijiandaa kukaa chini huku akisikika akijikohoza kuweka koo lake vizuri, kumbe wakati anasimama kuna mtu aliondoa kiti alichokuwa amekalia hivyo jamaa yule wakanzu alijikuta anaanguka kama mzigo baada yakukosa pakukaa, ilikuwa ni bahati mbaya sana kwake maana hakutazama anapokaa,
ilikuwa ni ajabu sana yaani badala ya watu kumpa pole walijikuta wakimcheka baba wa watu.
muda huu mwenyekiti alikuwa akijipongeza kimoyoni "nimemuweza, halafu sijui imekuaje nikamruhusu mwanaume asimame.hapa ni mwendo wa wanawake tu" alijisemea hivi mwenyekiti bila kujua anazungumza kwa nguvu na sauti yake imesikika na katibu wake aliyekuwa amekaa nae meza kuu.
"hee kumbe ndio njama yako !?" alisema Katibu mtu mwenye sharubu nyingi kuwahi kutokea hapa duniani! alikuwa mfupi na kitambi chake cha pombe za kienyeji kilimfanya aonekane mfupi pengine labda angelikuwa mwembamba angelikuwa mrefu kidogo.
"njama? njama gani!?" alihamaki mwenyekiti hakutaka kabisa kuamini kuwa amesikika alichokuwa amedhamiria, macho yataharuki yalimtazama katibu wake wa masharubu.
" nimekusikia kuwa umepanga kuchagua wanawake tu hapa" alisema katibu safari hii kwa sauti kubwa iliyomfikia jamaa wakupumua, mtu bonge kuliko wote waliokuwako pale.
"ndio zake huyo, nina kesi nae mimi tena leo atanitambua" alisikika bonge akizungumza kutoka katikati ya watu, na tayari alikuwa ameamka na jazba, sijui hata alikuwa na mgogoro gani na mwenyekiti.
wakati hayo yakiendelea tifu zito liliibuka kwa jamaa wakanzu akiuliza ni nani aliyemtolea kiti mpaka kusababisha aanguke.
tafurani ikazuka katika eneo, utulivu na maelewano vikatoweka kwa kasi yaajabu sasa eneo la mkutano likageuka soko la kelele
na wakati hayo yakiendelea ghafla tukio la ajabu likatokea pale taharuki ikwakumba wote waliopo pale na kila mmoja akichanguka kuelekea upande wake ili mradi kunusuru roho yake.
NINI KIMETOKEA KATIKA KIKAO HIKI CHA WAPINGA SIMULIZI??
INAENDELEA.....
jiunge nasi
watsap simulizi: +255 782 181 862
Na.
BIN ZONGO
MR EXPERIENCE
SIMULIZI ZINAISHI...!