_Mama yake Salim anaingia chumbani kumsalimia mwanae anamkuta amelala usingizi wa kifo, hakutaka kuamini kabisa kuwa Salim amefariki lakini ukweli ulikuwa huo maana hakuweza kuamka hata walipofanya juhudi zakumuamsha_
SASA ENDELEA...
Haikuwa rahisi kuamini kuwa Salim amefariki dunia, maswali mengi magumu yalikatiza kichwani mwa mama yake..
wengi ilibidi waamini kuwa labda chanzo cha kifo chake ni kushambuliwa na Jef,
hata walipoufikisha hospitali mwili ule wa marehemu hakuna kilichobainika kumuua Salim.
ukweli wa kifo ni ukweli ambao hakuna ambaye yupo tayari kuukubali hasa aliyekufa awe na mahusiano ya dhati nawewe.
Salim alikuwa ni kijana mdogo sana umri wa miaka 27 pekee anafariki ndani ya siku nne tu tangu atoke uingereza kusoma.
wengi waliguswa na msiba huu lakini Bi Getrude aliguswa zaidi, aliamini chanzo cha kifo cha kijana yule ni mwanae Jef.
alilia sana na aliumia pia.
alishiriki kwa hali na mali katika msiba wa Salim na alionekana kuguswa zaidi na msiba ule na zaidi alimuomba sana Mungu isipite chuki kati ya familia zile mbili.
* * *
kujitoa kwake na kuguswa na msiba ule kulitoa faraja kubwa pia kwa familia ya kina Salim, hawakupata nafasi yakujenga chuki.
walizoeana na kuimarisha mahusiano yao. muda mwingi Bi getrude alikuwa nyumbani kwa kina Salim akimfariji mwanamke mwenzie, alitambua maumivu yakuondokewa na mtoto hasa kijana mkubwa kama Salim.
Ni majuma kadhaa yalipita tangu shughuli za msiba zipite bado ukaribu wa Bi getrude na mama yale Salim uliimarika.
"nafikiri Salim alidhamiria kumsaidia mwenzie, siku ile ya msiba wake nilikuta karatasi flani ameandika, zinahusu matatizo yanayomkabili Jef"
majuma kadhaa kupita baada ya kifo cha Salim siku moja alizungumza hivi mama yake, alimueleza mama yake Jef kabla yakumuagiza mwanae mwengine wa mwisho kuleta zile karatasi, yeye aliitwa Sophy.
haikuchukua muda mwingi sana mpaka karatasi zile kuletwa.
na ni sekunde chache pia zilitumika mpaka zoezi lakuanza kuzipitia karatasi zile kuanza.
'Msongo wa mawazo ya namna gani utafanikisha malengo yako na magumu unayopitia wakati mwengine huwa chanzo cha mtu kurukwa na akili.
utamgundua mwenye tatizo hili kwa kumsikiliza nini anatamka mara kwa mara na anajichukuliaje.
tafsiri ya alichokuwa nacho Jef ni matokeo ya kile alichokuwa anakiwaza nakukitamani muda mwingi.
changamoto na vikwazo vya kumfikisha anapopataka bila shaka ndio chanzo cha jef kuwa vile.
kuthibitisha utafiti huu wa awali ni lazima kuzungumza na watoto ambao anaamini yeye ni wafanyakazi wenzake."
Katatasi ile iliandikwa kwa kiingereza lakini tafsiri yake ilikuwa ni maneno hayo hapo juu.
walibaki wakitazamana mama yake salim pamoja na mama yake Jef.
siku ile Mama yake salim anaisoma hakuelewa sana sababu ya ile lugha SALIMU aliyoitumia ila pale walivyorejea kuisoma pamoja na mama yake Jef waliweza kutambua sababu mama yake Jef aling'amua vema lugha ile.
kufika hapa ghafla Mama yake Salum akashindwa kuvumilia taswira ya mwanae, upole wake na heshima aliyo nayo vikamrejea kwa pamoja.
ni yeye salim ndiye alikuwa mkombozi wake baada ya kupambana kumsomesha mpaka kidato cha sita na alipofaulu vizuri masomo yake alama zake zikamfanya afadhiliwe na serikali kwenda kusoma nje.
ni hapa ndipo ndoto yake ya kumsomesha mwanae ili aje kuwa daktari bingwa wa matatizo ya afya ya akili ikatimia.
Salim alihitaji kazi hiyo sababu ya historia mbaya aliyoisikia kuhusu baba yale mzazi Mzee Gondo Salim ambaye alijimaliza mwenyewe kwa kujiua sababu ya matatizo ya akili.
ni salim pekee ndiye ambaye alikuwa tumaini la mama yake. tumaini lakuja kumsaidia majukumu yakusomesha wadogo zake na kumuhudumia mama yake.
leo hii Salim hayupo tena! alijikuta akilia mfululizo mama yake Salim na ndipo hapa alipompa nafasi Ibilisi apenyeze sumu yake iitwayo uchonganishi.
wazo la isingekuwa Jef pengine Salim angekuwa bado yungali hai likaanza kupita kichwani mwake, tsunami la chuki taratibu likaanza kupenya kichwani mwake.....
"niache sitaki kabisa kubembelezwa nawewe nimesema niache" alifoka Mama Salim, huku akimsukuma vibaya Bi getrude nakuanguka sakafuni kama zigo la pumba.
mama yake Salim hakujali, alikimbilia chumbani huku akiendelea kulia.
"upo wakati ambao shetani huutu
mia kutujaribu, na ni wakati huo ndio ambao imani yako inapimwa" BIN ZONGO
INAENDELEA....
Watsap simulizi-0782181862