Jef anamvamia nakumuangusha Salim huku akimshambulia vibaya, watu wanazunguka eneo lile wakishangaa bila kutoa msaada_
sasa endelea.....
Haikuwa rahisi kwa Salim kujinasua pale chini, Jef alimdhibiti 'barabara' na asiweze hata kufurukuta.
"Ni miaka mingapi imepita tangu uingie mkataba na kampuni yangu? ulidhani utanitoroka milele, leo nimekukamata utanitambua! umeitia hasara ya mabilioni kampuni yetu!." haya ndio maneno aliyokuwa akiyasema Jef huku akimshambulia Salim.
watu waliofika eneo lile waliposhuhudia damu zinaruka ndipo walipopatwana taharuki lakini wengi wao waliogopa hata kusogea karibu mpaka alipojitokeza kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la mtaani Kinongo ndipo akajitosa kumzuia Jef asiendelee kumshambulia Mwenzie.
"we Jef nini unafanya!? pumbavu!. hebu muache mwenzio" alipaza sauti Kinongo huku akipata ujasiri wakumsogelea karibu Jef.
ajabu Jef hakuwa mbishi ghafla aliacha kumshambulia Salim akanyoosha mikono juu kama mtu aliyekuwa anajisalimisha kwa polisi.
maneno yake ndio yalishangaza watu zaidi.
"Mimi sina tatizo nanyinyi polisi hata mahakamani nipelekeni lakini naomba mzingatie utaratibu wakunikamata..yupo hapa mwanasheria wangu," alimnyooshea kidole moja ya watoto aliokuwa akicheza nae.
"nitaongozana na mwanasheria wangu mpaka kituoni lakini pia naomba nikabidhi kabisa ofisi kwa msaidizi wangu" kufika hapa Aliangaza huku na kule akimtafuta mtu na alipomuona mtoto mmoja wapo kati ya wale anaocheza nao akaendelea kuzungumza
"yule pale anaitwa Deo, Deo naelekea kituoni hakikisha kila kitu kinaenda sawa hapa ofisini."
aliagiza Jef, kwa mtu mgeni ilikuwa ni kichekesho kikubwa kile anachozungumza Jef .
watoto wale aliodai ndio wafanyakazi wake ndio alikuwa akicheza nao muda wote.
watu waliomfahamu Jef hawakumshangaa kabisa walikuwa wameshamzoea na mara zote alikuwa akijitamba kuwa yeye ni bosi.
Baada ya Jef kumuachia Salim huku akionekana anajitetea kwa polisi kinongo!. Salim alitumia nafasi hiyo kuamka pale chini na ni yeye mwenyewe ndiye aliyewahi kuvua shati lake jeupe kisha akalibandika haraka katika pembe ya paji lake la uso ambapo palikuwa panatoka damu mfululizo.
Kinongo alionekana amemzoea Jef hakuwa anamuogopa alimuamrisha aondoke arudi nyumbani.
kama kawaida kichwani mwa Jef alimtafsiri kinongo ni polisi hivyo akajibu.
"safi lazima ufuate sheria naenda nyumbani kuaga familia kisha utakuja kunikamata baadae"
wapo waliokuwa wakicheka kila Jef anapozungumza, nafikiri kutokana na wengi kumjua kuwa alikuwa ni mwendawazimu ndio maana walimuacha tu aondoke licha yakumshambulia Salim hadharani.
Salim alimshukuru Kinongo kisha akasimamisha bajaji akielekeza impeleke zahanati ya karibu kwa matibabu. alijeruhiwa kidogo eneo lile la usoni na damu zilizokuwa zikimtoka aliweza kuzizuia kwa muda kwa kutumia shati lake.
baada ya bajaji kuondoka ndipo watu wakaanza kusambaratika katika eneo lile. wengi walisikika wakielezea kustaajabishwa na tukio lile.
"huyu kijana hana kabisa kawaida yakushambulia watu sjui leo imekuaje hata!" walisikika baadhi ya kina mama walioshuhudia tukio lile.
* * *
Jef aliporudi nyumbani tayari taarifa zilishawafikia ndugu zake kuwa amemshambulia mtu,mwanzo hawakufahamu kabisa kuwa aliyeshambuliwa ni Salim. baadae wapojua bi Getrude alilaani sana lakini hakuwa na lakufanya.
alishiriki kujua maendeleo ya Salim na bahati nzuri Salim alikuwa ameshapata tiba na alishonwa mahali alipoumia kisha akatakiwa kurudu nyumbani.
Salim hakuwa na chuki kabisa na Jef alimchukulia kama hana hatia kutokana na hali yake.
na kutokana na tukio lile alijikuta tayari ana mwanzo mzuri sana wakubaini kinachomsumbua Jef.
aliporudi nyumbani kwao alipata nafasi yakuweka mikakati yake ya namna yakubaini kinachomsibu rafiki yake.
"nahitajika kuzungumza na watoto anaocheza nao, nafikiri watanisaidia sana" aliwaza Salim wakati akiwa amejipumzisha chumbani kwake huku akisikilizia maumivu kwa mbaali ya kichwa.
taarifa za awali juu ya alichokibaini kwa Jef kupitia jef mwenyewe na ndugu zake tayari alikuwa ameziandika kwenye karatasi yake na utaratibu wakukamilisha utafiti wake pia aliuweka.
kabla yakupitiwa na usingizi nakulala..usingizi ambao hakuna aliyebahatika kuweza kumuamsha hata mama yake mzazi aliyeingia mule ndani kumletea chakula na kumjulia hali.
ikuwa ni ngumu kuamini kuwa Salim alipoteza maisha.
INAENDELEA....
Na. Bin Zongo