SITAKUSAMEHE

Leo nimekuomba uketi chini nikufunulie tena kwa mara nyengine jarada hili lenye kanuni zangu na muongozo muhimu kwa mchumba angu!

jarada hili lina kanuni Hamsini jiandae kujua leo nasoma kanuni ya ngapi maana mara ya kwanza nilikusomea kanuni ya Sita niliyoipa jina la NITAKUOA LAKINI SITASAIDIA NDUGU ZAKO!
hii leo nimepata mshawasha wakukusomea kanuni ya Kumi yenye kichwa cha habari chenye neno moja tu SITAKUSAMEHE.
kubwa na muhimu tambua kuwa nitakuoa kamwe sitaruhusu maneno yangu haya yakumbwe na kimbunga kiitwacho AHADI HEWA.

Nitahakikisha nakuoa na nasimamia furaha yako muda wote ndani ya ndoa yetu!

ule ukatili wa mwanaume kumpiga mkewe mpaka kumpa chongo kamwe sitauruhusu univae nakunilaghai, ukinikera nitakutandika na maneno yakukuonya na ukiendelea nakucharaza na dua yenye maombi mazito kwa mola wangu nina imani kupitia yeye aibu yakuniudhi nakunikaraisha itakuvaa na utaona haya kunipa mateso mtoto wa mwanamke mwenzio.

yote nitayafanya mchumba kuhakikisha unajivunia mimi kuwa mumeo, lakini mchumba naomba uzingatie neno hili kuwa SITAKUSAMEHE.
ndio Aaziz wangu sitakusamehe kamwe kwa jaribio lolote lile utakalolifanya lakusaliti ndoa yetu!

naomba niseme tena kwa msisitizo SITAKUSAMEHE, nimezungumza na moyo wangu mara kadhaa na kuuliza swali hilo je nitafanya nn siku nikibaini mke wangu anauza hadhina yangu kwa wengine.

nafsi ikanikemea eti niache ujinga wakufikiria vitu vibaya vitanitokea kwenye ndoa yangu.

moyo wangu ukatabasamu uliposikia onyo hilo kutoka katika Nafsi na mpaka kesho sijui tabasamu lile la moyo lilikuwa la dhihaka ama dharau, maana moyo nao kwa kiburi, we acha tu!

nakumbuka akili ndio ilinifuta machozi yakukemewa ikajaribu kunieleza kuwa nipo sahihi kuwaza kitu kile maana siku hizi tunaoa nafsi zenye tamaa na zisizojua kuridhika ni nini.

ni vema kujiuliza je ni nini nitafanya siku nikibainisha kwa macho yangu mke wangu anagawa bidhaa yangu ya thamani.

kabla ya kuwaza hilo niliwaza makosa mengine ambayo nayo mnh ni mtihani kwakweli lkn hili lakusalitiwa ni fedheha ambayo jibu lilikuja
moja tu SITAKUSAMEHE.

kusema sitakusamehe haimaanishi kuwa nitakuua, nitakudhuru au kukunyasa kwa namna yoyote ile, naapa nitajizuia kutenda jinai ya aina yoyote ile ila tu utakuwa umevunja kabisa mkataba wa uaminifu kwangu na ule upendo wote utageuka chuki na sitakuwa tayari kuongea nawewe tena kuhusu mapenzi.

lugha zetu zitakuwa ni lugha gongana maana sitakuelewa kwa chochote kile labda tu tuongelee masuala mengine kabisa lakini sio upendo wala kuhusu ndoa yetu.

Sitakusamehe nakuapia sababu wewe ni mzinifu kama wazinifu wengine na haustahili kunichafua kwa janaba lako la uasherati wakusaliti ndoa yako,utapaswa upite njia yako nami uniache nikijongea kwa njia yangu taratiibu huku nikiuguza majeraha uliyonipa.

tambua na ujue sitakusamehe hakika na hata nikikwambia nimekusamehe haitamaanisha kuwa nitaendelea kuwa nawewe!

sitakusamehe sababu nimimi ndio nitakuwa wakwanza kuvaa vazi la uaminifu pindi tu nitakapoikanyaga ardhi ya ndoa.

michepuko nitainyari, nitaipiga kumbo nakuiweka nyuma yangu, sitatabasamu wala kumchekea mtu yoyote atakayenikonyeza nakuonesha dalili yakunitaka.

nitaimba wimbo wa NIMEOA NAMUHESHIMU MKE WANGU, zaidi nitakariri nakukirudia mara kwa mara kibwagizo chake chenye maneno adhimu ya SITAKI KUMSALITI MKE WANGU.
hakika nakuambia nitakuwa muaminifu mno ili ikitokea umenisaliti neno langu hili SITAKUSAMEHE lisiyumbe kimsimamo.

kuna mengi katika Jarida langu hili lakini leo nimewasilisha neno hili SITAKUSAMEHE ili usje ukasema eti nimeshikiwa akili na wanafiki wasiokupenda.

tutabaki tunasalimiana, hata shida tutasaidiana lkn litakapokuja suala la usaliti uliotenda kwangu tambua kuwa SITAKUSAMEHE.

zaidi nitamuachia Mungu na nitalia nae kila siku iitwayo leo akuadhibu kwa kosa hilo maana mimi sio mtoa hukumu mzuri kama alivyo yeye.

"kuna haja yakutenda wema kwa mwengine ili nafsi imsute siku atakakapokukosea"

BIN ZONGO

WAPINGA SIMULIZI 2

Wapinga simulizi wanapatwa na taharuki baada ya tukio la ajabu kutokea katika eneo walilokusanyika.

mwenyekiti alichomoka kama mshale na hata sijui aliwezaje kumruka katibu wake mtu mwenye sharubu nyingi kuwahi kutokea duniani.

wote waliweza kujimudu nakukimbia kunusuru roho zao lkn tatizo lilikuwa kwa mtu mnene kuliko wote waliokusanyika pale.

wakati akiwa anajiandaa kuamka ili akamvamie mwenyekiti ghafla akahisi anavamiwa na kitu kizito mgongoni.

kitu hiki ndicho kilichozua taharuki eneo lile, kilikuwa ni mithiri ya kinyamkera, masikini bonge wawatu alitoa yowe la woga akiomba msaada.

watu wote walishachanguka katika eneo lile ni bonge tu ndio alibaki, hata mkewe hakujali kabisa kuhusu mumewe.

alikimbia mbali kabisa kila mmoja alihakikisha anamuacha mwenzake umbali mrefu sio wanawake wala wanaume, sio watoto wala wakubwa, vijana na wazee woote kwa pamoja waligeuka wanariadha.

ni bonge tu ndio alibaki anagaragara pale chini huku lile zigo mithili ya kinyamkera likiwa limemg‘ang'ania.

kuna lugha ya woga alikuwa akiizungumza mtu mnene sjui ni lugha gani masikini ya Mungu lakini ilifanana sana na lugha za kibantu hasa za wenyeji wa Tanzania ukanda wa kusini.

kikao cha wapinga simulizi kiliingiliwa na kinyamkera kilichodondoka kutoka juu yamti.

ndio, kinyamkera kile kilikuwa kimefungwa ndani ya fuko kuuu kuu la safleti, kama ni mtu basi alikuwa ni mfupi mno kimo cha mfuko ule.

hakuonekana sura wala miguu, sehemu pekee ya viungo vyake iliyokuwa huru ilikuwa ni mikono, ambayo aliitumia kumkamata barabara mtu mnene.

baba wa watu alipiga mayowe ya woga alilama eti anakufa, sauti yake ya woga na kilio alichokuwa akikitoa kilifanya sauti za watu wakicheka kutoka juu ya mtu isikike.

ni hapa ndipo ilipobainika kuwa juu ya ule mti wa muembe kulikuwa na watu vijana wawili watukutu, waliokuwa wamedhamiria kuwaharibia kikao wapinga simulizi.

" Povu muachie aende zake" alisikika moja ya vijana kutoka juu ya mti huku sauti yake ikiambatana na kicheko, kile kinyamkera kilichokuwa kinamgaragaza bonge wawatu pale chini kikamuachia, masikini bonge wawatu alipata shida kuamka nakukimbia na hata alipoweza alipiga myereka mara tatu.

mwili ulikuwa ni tatizo kwake katika suala la kukimbia.

huku nyuma kile kitu mfano wa kinyamkera kikavua yale masafleti, loh! alikuwa ni mtu, mtoto miaka kama kama kumi na tano hivi, alionekana akicheka mno baada yakumuona mtu mnene akikimbia nakuanguka.

walikuwa wapo watatu wenzake wawili walishuka kutoka juu yamti nakuambatana nae kucheka.

walikuwa ni watoto watukutu, siku ile walidhamiria kuwakomoa wapinga Simulizi kutokana na kutumia uwanja wao wa kuchezea mpira kuendeshea vikao vyao.

"ile ndio dawa yao, alisikia dogo mmoja huku akisogelea meza kuu nakukaa sehemu aliyokuwa amekaa mwenyekiti mpiga miayo.

"povu baba ako alikuwa kakaa hapa, na koti lako kubwaaa" alisikika yule dogo akimuonesha yule mtoto aliyekuwa amevaa kama kinyamkera,

"duh ila mshkaji mwambie baba ako apungeze kula, ule unene utamuua, hahahaa"

maongezi yao haya ndio yalidhirisha kuwa watoto wale mmoja baba yake ni yule mwenyekiti mtu mweusi mwenye bonge la koti na mwengine baba yake ni yule mtu mnene.

"sema yote tisa kumi mwenzetu baba ako mwambie awe anakaza sauti"

Alisikika yule mtoto aliyeitwa Povu, wote walimgeukia mwenzao ambaye alikuwa ndio mrefu kuliko wote wakaanza kucheka pamoja.

mwengine akaongezea

"Duh na ile kofia kwa juu tulikuwa tunaona kipara chake, af wakamuondolea kiti hahaaa"

hakika watoto hawa watatu walikuwa watukutu mno, Hawakujali kuharibu kikao cha watu.
 wao walikuwa wakijadili nakucheka walichokiona kwenye kikao kile.

wapinga simulizi kila mmoja alirejea nyumbani kwake, hakuna aliyetaka hata kurudi katika eneo lile la kikao.
wengi walihusisha kiluchotokea na imani za kishikirikina,

mtu bonge alifika kwake bila kuuliza kitu akaanza kuandika talaka kwa mkewe eti kwanini amemuacha peke yake kwenye hatari, pengine isingekuwa majirani kumsihi sana asifanye hivyo labda angetimiza adhma yale hiyo, na nikatika ugomvi wake huu ndipo alipochomekea suala la kumuhisi mkewe anatembea na mwenyekiti wa wapinga simulizi.

huku nyuma watoto walikuwa wakipongezana hasa akili yao waliyotumia kutokuitana majina yao halisi.

walijua wangejulikana halafu ingekuwa tatizo kwao muda wakurejea nyumbani, ni hapa ndipo ilipoainika kuwa hata yule aliyeitwa POVU halikuwa jina lake halisi.

hakika hiki kweli ni kizazi cha fitna! tayari walishasambaza taarifa kwa wenzao kuwa mechi yao ipo kama kawaida, kwenye uwanja wao uleule.

hata walipokuja kukatazwa na wazazi wao wasiutumie ule uwanja sababu una mambo ya kichawi hawakujali sababu wao walijua sio uchawi ni kazi yao ya utukutu walioufanya.

TAMATI.....

CHIZI MAFANIKIO SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA.....
_Mama yake Salim anaingia chumbani kumsalimia mwanae anamkuta amelala usingizi wa kifo, hakutaka kuamini kabisa kuwa Salim amefariki lakini ukweli ulikuwa huo maana hakuweza kuamka hata walipofanya juhudi zakumuamsha_

SASA ENDELEA...

Haikuwa rahisi kuamini kuwa Salim amefariki dunia, maswali mengi magumu yalikatiza kichwani mwa mama yake..

wengi ilibidi waamini kuwa labda chanzo cha kifo chake ni kushambuliwa na Jef,

hata walipoufikisha hospitali mwili ule wa marehemu hakuna kilichobainika kumuua Salim.

ukweli wa kifo ni ukweli ambao hakuna ambaye yupo tayari kuukubali hasa aliyekufa awe na mahusiano ya dhati nawewe.

Salim alikuwa ni kijana mdogo sana umri wa miaka 27 pekee anafariki ndani ya siku nne tu tangu atoke uingereza kusoma.

wengi waliguswa na msiba huu lakini Bi Getrude aliguswa zaidi, aliamini chanzo cha kifo cha kijana yule ni mwanae Jef.

alilia sana na aliumia pia.

alishiriki kwa hali na mali katika msiba wa Salim na alionekana kuguswa zaidi na msiba ule na zaidi alimuomba sana Mungu isipite chuki kati ya familia zile mbili.

* * *

kujitoa kwake na kuguswa na msiba ule kulitoa faraja kubwa pia kwa familia ya kina Salim, hawakupata nafasi yakujenga chuki.

walizoeana na kuimarisha mahusiano yao. muda mwingi Bi getrude alikuwa nyumbani kwa kina Salim akimfariji mwanamke mwenzie, alitambua maumivu yakuondokewa na mtoto hasa kijana mkubwa kama Salim.

Ni majuma kadhaa yalipita tangu shughuli za msiba zipite bado ukaribu wa Bi getrude na mama yale Salim uliimarika.

"nafikiri Salim alidhamiria kumsaidia mwenzie, siku ile ya msiba wake nilikuta karatasi flani ameandika, zinahusu matatizo yanayomkabili Jef"

majuma kadhaa kupita baada ya kifo cha Salim siku moja alizungumza hivi mama yake, alimueleza mama yake Jef kabla yakumuagiza mwanae mwengine wa mwisho kuleta zile karatasi, yeye aliitwa Sophy.

haikuchukua muda mwingi sana mpaka karatasi zile kuletwa.

na ni sekunde chache pia zilitumika mpaka zoezi lakuanza kuzipitia karatasi zile kuanza.

'Msongo wa mawazo ya namna gani utafanikisha malengo yako na magumu unayopitia wakati mwengine huwa chanzo cha mtu kurukwa na akili.

utamgundua mwenye tatizo hili kwa kumsikiliza nini anatamka mara kwa mara na anajichukuliaje.

tafsiri ya alichokuwa nacho Jef ni matokeo ya kile alichokuwa anakiwaza nakukitamani muda mwingi.

changamoto na vikwazo vya kumfikisha anapopataka bila shaka ndio chanzo cha jef kuwa vile.

kuthibitisha utafiti huu wa awali ni lazima kuzungumza na watoto ambao anaamini yeye ni wafanyakazi wenzake."

Katatasi ile iliandikwa kwa kiingereza lakini tafsiri yake ilikuwa ni maneno hayo hapo juu.

walibaki wakitazamana mama yake salim pamoja na mama yake Jef.

siku ile Mama yake salim anaisoma hakuelewa sana sababu ya ile lugha SALIMU aliyoitumia ila pale walivyorejea kuisoma pamoja na mama yake Jef waliweza kutambua sababu mama yake Jef aling'amua vema lugha ile.

kufika hapa ghafla Mama yake Salum akashindwa kuvumilia taswira ya mwanae, upole wake na heshima aliyo nayo vikamrejea kwa pamoja.

ni yeye salim ndiye alikuwa mkombozi wake baada ya kupambana kumsomesha mpaka kidato cha sita na alipofaulu vizuri masomo yake alama zake zikamfanya afadhiliwe na serikali kwenda kusoma nje.

ni hapa ndipo ndoto yake ya kumsomesha mwanae ili aje kuwa daktari bingwa wa matatizo ya afya ya akili ikatimia.

Salim alihitaji kazi hiyo sababu ya historia mbaya aliyoisikia kuhusu baba yale mzazi Mzee Gondo Salim ambaye alijimaliza mwenyewe kwa kujiua sababu ya matatizo ya akili.

ni salim pekee ndiye ambaye alikuwa tumaini la mama yake. tumaini lakuja kumsaidia majukumu yakusomesha wadogo zake na kumuhudumia mama yake.

leo hii Salim hayupo tena! alijikuta akilia mfululizo mama yake Salim na ndipo hapa alipompa nafasi Ibilisi apenyeze sumu yake iitwayo uchonganishi.

wazo la isingekuwa Jef pengine Salim angekuwa bado yungali hai likaanza kupita kichwani mwake, tsunami la chuki taratibu likaanza kupenya kichwani mwake.....

"niache sitaki kabisa kubembelezwa nawewe nimesema niache" alifoka Mama Salim, huku akimsukuma vibaya Bi getrude nakuanguka sakafuni kama zigo la pumba.

mama yake Salim hakujali, alikimbilia chumbani huku akiendelea kulia.

"upo wakati ambao shetani huutu
mia kutujaribu, na ni wakati huo ndio ambao imani yako inapimwa" BIN ZONGO

INAENDELEA....

Watsap simulizi-0782181862

WAPINGA SIMULIZI :1


Idadi kubwa ya watu wake kwa waume, wazee kwa watoto, wasichana kwa wavulana.

eneo ni porini ni nyasi tu ndio zimesambaa kote, watu hawa wamekaa chini ya mti wa muembe.

mwenyekiti wa mkutano wao alikuwa ni mfupi kuliko wote waliokuwa pale.

alivaa koti kubwa kuliko kimo chake, hakuwa na kipaza sauti hivyo alilazimika kuipaza sauti yake isikike kuwafikia watu wote waliokusanyika pale.

watu wakiwa makini kumsikiliza ghafla jamaa fulani ambaye mwili wake ulikuwa mkubwa (mnene) akasikika akipumua kwa nguvu jambo lililozua tafurani na watu kuguna nakupoteza umakini wakumsikiliza mwenyekiti wao.

hali ya hewa ilibadilika ghafla katika eneo lile, jamaa bonge huku akiona aibu akajikuta akijikaza kuamka ili aombe radhi lakini kabla yakufanikisha zoezi hilo alijikuta akipumua tena mfululizo tena kwa sauti kuu iliyopenya masikioni mwa wote waliokusanyika pale, masikini ya Mungu mtu mnene yule sijui alishiba maharagwe mpaka yakamfanya ashindwe kujizuia kupumua hovyo nakuharibu hali ya hewa.

baadhi ya watu waliokuwa pale walianza kucheka kwa sirisiri lakini mwisho wakashindwa kujizuia wakajikuta wanaangua kicheko kikubwa akiwemo mwenyekiti wa kikao kile.

mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa karibu na yule mtu mnene alijikuta akiingiwa na aibu, aliyekuwa akichekwa ni mume wake. alijisikia aibu sana alitamani ardhi ipasuke aingie ndani.

"jamani basi yaishe tuendeleeni na kikao..!" alisikika mwenyekiti akizungumza na watu wote wakakaa kimya kumsikiliza.

"lengo lakukusanyika hapa nikutafuta namna yakuzidhoofisha simulizi, nasikia wanasema zinaishi inawesekana kuna ukweli maana nimezitafutia sumu ya panya nikazinywesha lakini wapi bado zinahema na wala hazionekani kuwa na dalili yakufa...bila shaka wote hapa tuliopo ni wapinga simulizi sasa kila mmoja atoe maoni yake..."

alipaza sauti mwenyekiti yule ambaye meno yale yalikuwa meupe sana hivyo kumfanya akizungumza angalau aonekane kutokana na kuwa mweusi kuliko ulivyo mkaa.

"mnh huyu nae mwenyewe mweusi bado akajivika koti jeusi watu wengine hawajijui loh"

 alijisemea nafsini mwanamke mmoja ambaye alikaa pembeni kabisa akifuatilia kikao cha Wapinga Simulizi.

watu sasa walikuwa wamenyoosha vidole wakionekana kila mmoja ana shauku yakutoa maoni ya namna gani nzuri yakudhoofisha Simulizi.
mwenyekiti akiwa makini kuchagua nani aanza kuzungumza ndani yake alikuwa akijisemea " hawa watu wangejua hapa kuwa nina njaa tangu asubuhi sijala hata wasingenipa uenyekiti"

alijisemea hivi huku akisindikizwa na miayo ya njaa huku yeye mwenyewe akilazimisha ionekane ni uchovu.

"acha nichague wanawake wazuri wazuri tu, mijianaume najifanya kama siioni" alijisemea tena mwenyekiti huku akimchagua mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa katikati ya kundi la watu.

mwanamke yule alisimama alikuwa amesuka mtindo wa haraka niwahi maarufu kama nywele za msibani chini alivaa kandambili kuubwa kuliko miguu yake. alisimama kwa mbwembwe akilazimisha kuonekana mzuri kwa kusimama akijitingisha ilhali mwili wenyewe hakujaaliwa yaani alipendelewa mifupa zaidi ya nyama.

sauti yake ndio iliwashangaza watu zaidi hakuna aliyetegemea kuwa mwanamke yule angekuwa na sauti nzito kama mwanaume.

mbaya zaidi alizungumza kwa jazba kama mtu angekuwa hamuoni angesema aneyezungumza ni mwanaume.

"kwakweli siwapendi sana hawa watu wa simulizi,wananinkera kuanzia chini yao mpaka juu yao, nawachukia sana"

aling'aka mwanamama yule huku kitaalamu akiwa hajazungumza kitu chamaana hata kimoja, alizunguka tu kwa maneno meengi lkn akiwa na maana moja tu kuwa Hazipendi Simulizi Zinazoishi.

katika kuonesha wote waliokuwa pale akili zao zilifanana walijikuta wanampigia makofi kwa wingi.

na mwenyekiti bila kujua kuwa alichouliza hakijajibiwa alijikuta anamruhusu mwanamama yule kukaa baada yakuthibitisha kuwa amemaliza kuchangia.

"vizuri sana haya mwengine mwenye mawazo yakudhoofisha si....." kabla mwenyekiti hajamaliza kuzungumza yule mwanadada mwenye sautu nzito alisimama tena akidai eti amesahau kitu muhimu chakuzungumza, watu wote wakanyamaza nakumgeukia.

"katika simulizi Kuna kale kadada kutoka nyanda za kati kanajiita Wendo yaani sikapendi kanajiona kazuuuri kutwa mitandaoni na picha picha zao za Simulizi, yaani bahati yake me simu yangu mbovu yakuingia huko fesibuku!"

alizungumza tena yule mwanamama huku pia bado akiwa hajachangia njia yakudhoofisha Harakati za Simulizi lkn bahati mbaya hakuna pia aliyegundua hili wote walijikuta wakipiga makofi wakimsifia amechangia vizuri.

"haya asante kwa kuchangia kaa chini mwengine aamke achangie" aliamrisha mwenyekiti huku akipiga miayo mara kwa mara.
safari hii aliamka mwanaume alikuwa amevaa kanzu nyeupe lakini ilibadilika rangi kutokana na kuchakaa na ilikuwa na viraka kila sehemu.

baraghashea aliyovaa ndio ilikuwa vituko zaidi ilirarukararuka kama imeshambuliwa na bomu, jamaa huyu alikuwa mrefu kiasi, mwembamba kwa umbo, pengine kutokana na urefu wake ndio maana watu walielekeza umakini wao kwake.
jamaa alianzakwa kusalimia
loh! ilikuwa ni ajabu sauti yake yaani ilikuwa nyembamba mno, kama ya kike.

ilistaajabisha sana maana mchangiaji wakwanza wakike alikuwa ana sauti nzito yakiume sasa huyu wakiume inakuaje awe na sauti nyembamba ya kike.

mwenyekiti akahisi anadharauliwa, bila hata kufikiri mara mbili akasimama akamuamrisha jamaa akae,

"ndugu yangu mwenyekanzu kama unaenda kwenye mualiko, tafadhali kaa chini hakikisha sauti yako inakuwa yakiume, nzito yakishababi kisha utazungumza. haiwezekani mwanaume uwe na sauti hiyo, eboo!!"

watu wote wakajikuta wanaangua kicheko, masikini baba wa watu mwenyekanzu akajikuta akikumbwa na huzuni na aibu ndani yake, mwenyekiti alimdhalilisha, alijiandaa kukaa chini huku akisikika akijikohoza kuweka koo lake vizuri, kumbe wakati anasimama kuna mtu aliondoa kiti alichokuwa amekalia hivyo jamaa yule wakanzu alijikuta anaanguka kama mzigo baada yakukosa pakukaa, ilikuwa ni bahati mbaya sana kwake maana hakutazama anapokaa,

ilikuwa ni ajabu sana yaani badala ya watu kumpa pole walijikuta wakimcheka baba wa watu.

muda huu mwenyekiti alikuwa akijipongeza kimoyoni "nimemuweza, halafu sijui imekuaje nikamruhusu mwanaume asimame.hapa ni mwendo wa wanawake tu" alijisemea hivi mwenyekiti bila kujua anazungumza kwa nguvu na sauti yake imesikika na katibu wake aliyekuwa amekaa nae meza kuu.

"hee kumbe ndio njama yako !?" alisema Katibu mtu mwenye sharubu nyingi kuwahi kutokea hapa duniani! alikuwa mfupi na kitambi chake cha pombe za kienyeji kilimfanya aonekane mfupi pengine labda angelikuwa mwembamba angelikuwa mrefu kidogo.

"njama? njama gani!?" alihamaki mwenyekiti hakutaka kabisa kuamini kuwa amesikika alichokuwa amedhamiria, macho yataharuki yalimtazama katibu wake wa masharubu.

" nimekusikia kuwa umepanga kuchagua wanawake tu hapa" alisema katibu safari hii kwa sauti kubwa iliyomfikia jamaa wakupumua, mtu bonge kuliko wote waliokuwako pale.

"ndio zake huyo, nina kesi nae mimi tena leo atanitambua" alisikika bonge akizungumza kutoka katikati ya watu, na tayari alikuwa ameamka na jazba, sijui hata alikuwa na mgogoro gani na mwenyekiti.

wakati hayo yakiendelea tifu zito liliibuka kwa jamaa wakanzu akiuliza ni nani aliyemtolea kiti mpaka kusababisha aanguke.

tafurani ikazuka katika eneo, utulivu na maelewano vikatoweka kwa kasi yaajabu sasa eneo la mkutano likageuka soko la kelele

na wakati hayo yakiendelea ghafla tukio la ajabu likatokea pale taharuki ikwakumba wote waliopo pale na kila mmoja akichanguka kuelekea upande wake ili mradi kunusuru roho yake.

NINI KIMETOKEA KATIKA KIKAO HIKI CHA WAPINGA SIMULIZI??

INAENDELEA.....

jiunge nasi
watsap simulizi: +255 782 181 862

Na.
BIN ZONGO
MR EXPERIENCE

SIMULIZI ZINAISHI...!

CHIZI MAFANIKIO: SEHEMU YA PILI

Ilipoishia...

 Jef anamvamia nakumuangusha Salim huku akimshambulia vibaya, watu wanazunguka eneo lile wakishangaa bila kutoa msaada_

sasa endelea.....

Haikuwa rahisi kwa Salim kujinasua pale chini, Jef alimdhibiti 'barabara' na asiweze hata kufurukuta.

"Ni miaka mingapi imepita tangu uingie mkataba na kampuni yangu? ulidhani utanitoroka milele, leo nimekukamata utanitambua! umeitia hasara ya mabilioni kampuni yetu!." haya ndio maneno aliyokuwa akiyasema Jef huku akimshambulia Salim.

watu waliofika eneo lile waliposhuhudia damu zinaruka ndipo walipopatwana taharuki lakini wengi wao waliogopa hata kusogea karibu mpaka alipojitokeza kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la mtaani Kinongo ndipo akajitosa kumzuia Jef asiendelee kumshambulia Mwenzie.

"we Jef nini unafanya!? pumbavu!. hebu muache mwenzio" alipaza sauti Kinongo huku akipata ujasiri wakumsogelea karibu Jef.

ajabu Jef hakuwa mbishi ghafla aliacha kumshambulia Salim akanyoosha mikono juu kama mtu aliyekuwa anajisalimisha kwa polisi.

maneno yake ndio yalishangaza watu zaidi.

"Mimi sina tatizo nanyinyi polisi hata mahakamani nipelekeni lakini naomba mzingatie utaratibu wakunikamata..yupo hapa mwanasheria wangu," alimnyooshea kidole moja ya watoto aliokuwa akicheza nae.

"nitaongozana na mwanasheria wangu mpaka kituoni lakini pia naomba nikabidhi kabisa ofisi kwa msaidizi wangu" kufika hapa Aliangaza huku na kule akimtafuta mtu na alipomuona mtoto mmoja wapo kati ya wale anaocheza nao akaendelea kuzungumza

"yule pale anaitwa Deo, Deo naelekea kituoni hakikisha kila kitu kinaenda sawa hapa ofisini."

aliagiza Jef, kwa mtu mgeni ilikuwa ni kichekesho kikubwa kile anachozungumza Jef .

watoto wale aliodai ndio wafanyakazi wake ndio alikuwa akicheza nao muda wote.

watu waliomfahamu Jef hawakumshangaa kabisa walikuwa wameshamzoea na mara zote alikuwa akijitamba kuwa yeye ni bosi.

Baada ya Jef kumuachia Salim huku akionekana anajitetea kwa polisi kinongo!. Salim alitumia nafasi hiyo kuamka pale chini na ni yeye mwenyewe ndiye aliyewahi kuvua shati lake jeupe kisha akalibandika haraka katika pembe ya paji lake la uso ambapo palikuwa panatoka damu mfululizo.

Kinongo alionekana amemzoea Jef hakuwa anamuogopa alimuamrisha aondoke arudi nyumbani.

kama kawaida kichwani mwa Jef alimtafsiri kinongo ni polisi hivyo akajibu.

"safi lazima ufuate sheria naenda nyumbani kuaga familia kisha utakuja kunikamata baadae"

wapo waliokuwa wakicheka kila Jef anapozungumza, nafikiri kutokana na wengi kumjua kuwa alikuwa ni mwendawazimu ndio maana walimuacha tu aondoke licha yakumshambulia Salim hadharani.

Salim alimshukuru Kinongo kisha akasimamisha bajaji akielekeza impeleke zahanati ya karibu kwa matibabu. alijeruhiwa kidogo eneo lile la usoni na damu zilizokuwa zikimtoka aliweza kuzizuia kwa muda kwa kutumia shati lake.

baada ya bajaji kuondoka ndipo watu wakaanza kusambaratika katika eneo lile. wengi walisikika wakielezea kustaajabishwa na tukio lile.

"huyu kijana hana kabisa kawaida yakushambulia watu sjui leo imekuaje hata!" walisikika baadhi ya kina mama walioshuhudia tukio lile.
* * *

Jef aliporudi nyumbani tayari taarifa zilishawafikia ndugu zake kuwa amemshambulia mtu,mwanzo hawakufahamu kabisa kuwa aliyeshambuliwa ni Salim. baadae wapojua bi Getrude alilaani sana lakini hakuwa na lakufanya.

alishiriki kujua maendeleo ya Salim na bahati nzuri Salim alikuwa ameshapata tiba na alishonwa mahali alipoumia kisha akatakiwa kurudu nyumbani.

Salim hakuwa na chuki kabisa na Jef alimchukulia kama hana hatia kutokana na hali yake.

na kutokana na tukio lile alijikuta tayari ana mwanzo mzuri sana wakubaini kinachomsumbua Jef.

aliporudi nyumbani kwao alipata nafasi yakuweka mikakati yake ya namna yakubaini kinachomsibu rafiki yake.

"nahitajika kuzungumza na watoto anaocheza nao, nafikiri watanisaidia sana" aliwaza Salim wakati akiwa amejipumzisha chumbani kwake huku akisikilizia maumivu kwa mbaali ya kichwa.

taarifa za awali juu ya alichokibaini kwa Jef kupitia jef mwenyewe na ndugu zake tayari alikuwa ameziandika kwenye karatasi yake na utaratibu wakukamilisha utafiti wake pia aliuweka.

kabla yakupitiwa na usingizi nakulala..usingizi ambao hakuna aliyebahatika kuweza kumuamsha hata mama yake mzazi aliyeingia mule ndani kumletea chakula na kumjulia hali.

ikuwa ni ngumu kuamini kuwa Salim alipoteza maisha.

INAENDELEA....

Na. Bin Zongo 

CHIZI MAFANIKIO ; SEHEMU YA 1


 MTUNZI :  BIN ZONGO

Jina Lake aliitwa Jef alikuwa ni mrefu kwa kimo umbo lililoshiba na sura yake haikuwa ya mzaha.

Maisha yake yalikuwa mtaani, nguo zake zilimtambulisha kwa yoyote kuwa hakuwa timamu kiakili.

alizoeleka kuongea peke yake na kujichekesha mwenyewe bila sababu ya msingi.

alikuwa ni mwendawazimu lakini uzuri wake hakuzuru watu wala kugombana nao yeye alipenda kuwachekea na kila gari na nyumba nzuri aliyoiona alijinasibu kuwa ni ya kwake.

alipenda sana kuzungumza na watoto wadogo ambao wengi walimzoea jef nakumfanya rafiki.

bila shaka wazazi wa watoto wale walithibitisha kuwa Jef hakuwa mwendawazimu wakudhuru watoto ndio maana wakawaacha watoto wao wacheze nae kutwa nzima ingawa pia walikuwepo wazazi waliokuwa wakihofia kuwaacha watoto wao na Jef. wakihisi kuwa ipo siku atazidiwa na uchizi awafanye kitu kibaya.

Pengine labda isingekuwa Rafiki yake jef aitwae Salim hata pia nisingepata lakusimulia kuhusu Jef.

ni Salim ambaye alijaribu kuelezea tatizo linalomkumba Jef, tatizo ambalo wazazi wake na hata mpenzi wake alipambana kulitatua sababu lilimuanza kimasihara sana na hakuna aliyedhani kama angefikia hatua ile.

hakuna Daktari aliyefanikiwa kujua chanzo cha Jef kuwa vile wengi walitoa maoni yao kuwa Jef amerogwa.

lakini hakuna aliyethibitisha hilo wala pia hakuna aliyejitokeza kumuagua!

Baada ya salim kuachana na Jef miaka zaidi ya tano alistaajabishwa sana na hali aliyomkuta nayo mwenzake huyo.

miaka yote hiyo Salim alikuwa yupo nje ya nchi akisomea masuala ya afya ya akili.

kumuona mtaani rafiki yake akirandaranda kama mbuzi wa albadili lilikuwa ni pigo kwake.

alikumbuka mengi aliyowahi kufanya naye enzi akiwa timamu.

siku ya kwanza Salim kujaribu kumfuata Jef ilikuwa ni hatari kubwa!

ni siku hiyo ndio ambayo Jef alizidi kchanganyikiwa!

ilikuwa hivii..

baada ya Salim kumdadisi mama yake na ndugu zake kuhusu hali ya rafiki yake aliamua kwenda nyumbani kwa kina Jef kuwajulia hali na kuwapa pole kwa matatizo yaliyomkuta kijana wao.

ni siku hii ndio ambayo mama yake Jef alilia sana baada ya kumuona Salim.

kijana wake alikuwa makamo sawa na Salim ilimuumiza kichwa sana kwann apatwe na matatizo yale.

Salim alifanya juhudi zakumfariji kabla yakuomba ruhusa yakwenda kumuona Jef lakini aliambiwa kuwa muda ule jef hataki kabisakukaa nyumbani anaaga anaenra kazini.

"hataki kabisa kukaa ndani hasa mida ya mchana ila jioni anarudi mwenyewe nyumbani" alisema kwa uchungu Bi Getrude ambaye ndie mama mzazi wa Jef.

Salim aliumia sana kwa hali aliyomuona nayo mama yake Jef na taarifa alizopewa kuhusu Rafiki yake.

alijikuta anajiambiza mwenyewe kuwa ni lazima amsaidie Jef.

aliondoka nyumbani pale akiwa ana mawazo lukuki na nafsi yake ilimwambia kuwa anapaswa kutumia utaalamu wake aliosomea ili kumsaidia mwenzake.

wakati akikatiza mtaani nyumba tano kutoka nyumbani kwa kina Jef ghafla mbele akaona rundo la watoto wakiimba nakukimbizana na kijana ambaye alipomtazama kwa makini alimtambua kuwa ni Jef rafiki yake.

alijikuta akipigwa na butwaa nakumeza funda kubwa la mate huku akisimama kumtazama Jef, huruma ilimuingia, kumbukumbu za miaka kadhaa nyuma waliyokuwa wakisoma wote ikamrejea.

alimuona mawazoni Jef mwenye nidhamu, msafi mwenye akili na anayejipenda, Jef ambaye alikuwa tofauti kabisa na yule anayemuona mbele akiwa anacheza na watoto.

kwa hatua za tahadhari na umakini Salim alijongea kumsogelea Jef na watoto waliokuwa sasa wamekaa kwenye jumba bovu wakicheza nakucheka.

nafikiri nia ya Jef ilikuwa ni nzuri sana, alipanga kuyaaminisha macho yake kuwa kweli anayemuona ni Jef au amemfananisha.

lakini dhamira yake hiyo iliibua utata mkubwa sana pale Jef alipomuona Salim.

kwa mara ya kwanza tangu Jef awehuke siku hii ndio alionesha hasira yake.

kitendo cha kumuona Salim tu anamtazama kilikuwa ni kitendo cha kero kwake.

masikini ya MUNGU sijui alitafsiri nini kichwani mwake aliamka ghafla akawasukuma watoto waliokuwa wanamdandia dandia nakucheza nae. kisha akamsogelea Salim.

huku Salim akiwa amepigwa na butwaa kwa tukio hilo ghafla alishangaa akivamiwa nakuangushwa chini kama mzigo.

ilikuwa ni hatari Jef alianza kumshambulia kwa mawe na ngumi hila woga wala huruma.

wengi wapita njia walikuwa bado wameduwaa wasijue lakufanya mpaka pale walipoanza kushuhudia damu zikiruka kwa kasi kutoka pale chini.

ni dhahiri SALIM alikuwa yupo katika hatari ya kuuliwa wakati watu wakijishauri kumuokoa.

INAENDELEA....

UJUMBE WA YATIMA

Tumefanikiwa kuwatembelea wadogo zetu(YATIMA)

Ni wenye furaha na amani yaani kwa mara ya kwanza tupoziona sura zao mioyo yetu ilipiga magoti kuwaombea kwa MUNGU wasimamizi wa kituo kinachotumika kuwalea.

tumefanikiwa kuzungumza nao nakubadilishana nao mawazo watoto hawa na kwa usiri nafsi zao na zetu zikafanya kikao chasiri.

kikao ambacho hakikuhitaji kadamnasi ya watu, na kiliweza kutumia dakika 120 pekee kufika tamati.


Baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Tatima Fund Group katika picha ya pamoja na Vijana kutoka Katika Simulizi zinaishi Blog




nafsi zao zilipata uhuru kuzungumza mengi katika kikao hicho lakini mwisho zilitupa ujumbe tuufikishe kwa hadhira ya watu ambao ni wanajamii.

ujumbe ambao ulianza kuzungumzwa na mtoto mdogo umri miaka saba nakujazwa nyama za maneno nakaka zake aliokutana nao katika kituo kile wakiwa na jina la YATIMA.

anasema ndoto ya mafanikio ni sehemu inayoishi ndani yake na inakuwa kila uchwao ikijenga tamaa ya siku moja kuja kuitimiza.

anasema ndoto yake imekuwa ikibadilika kila siku iitwayo leo maana juzi aliota simanzi baada ya kugundua hana baba wala mama na jana akaota faraja baada ya kujikuta analelewa katika kituo na watoto wenzake na anasema anaamini usiku wa leo ataota mafanikio yake licha ya kwamba usingizi utakaoleta ndoto Ghiyo utatokana na kitanda kizuuri kiitwacho MSAADA kutoka kwa jamii.

"Ni ujumbe nawafikishia ningali bado nikiwa MCHANGA MAANA LEO PIA NI TAREHE YAKUZALIWA KWANGU MIAKA KAMA 25 nyuma.

Nitawezaje kupunguza maneno waliyonituma niwafikishie yatima wenzangu?" BIN ZONGO

ni wao ndio wamesema kuwa jamii ikiwatandikia vema kitanda hicho cha msaada wa hali na mali ni rahisi kwao kulala unono nakuota MAFANIKIO YAO.

wanasema mfano wa msaada wa hali
ambao wanahitaji wao ni jamii angalau kutenga muda nakuwa nao nakuwapa njia na mawazo ya vp wanaweza kufikia malengo yao.

msaada wa hali wanaouhitaji wao ni faraja, huruma nakutosahaulika, wanahitaji kukukumbukwa nakutoonekana wana tofauti na watoto wengine wenye baba na mama zao wanaoishi majumba ya kifahari wakikesha kubadili movie na games zakila namna.

wanasema msaada wa mali sio lazima majumba na pesa mkawagawie bali chochote kidogo kitawafariji na kuwapa sababu zakutojiona wapweke.

Nashukuru kwa kuwafikishia machache ambayo nafsi zao zilizungumza na nafsi zetu WANASIMULIZI zikatuagiza tuwafikishie wanajamii.

"NI FARAJA YA JAMII PEKEE INAHITAJIKA KWA YATIMA MAANA NI WAO WALIOKOSA FARAJA YA WAZAZI" Bin Zongo