BLOGU YAKASIRIKA



mwisho wa mwezi wa saba 2016 harakati na shamra shamra zakuandaa uzinduzi wa blogu ya SIMULIZI ZINAISHI (ommyzongo.blogspot.com) zikiwa zimefana kweli kweli,

watu wenye kuitakia heri blogu hiyo wakishiriki vema kuitangaza siku ya uzinduzi kila mmoja kwa nafasi yake, ajabu blogu yenyewe yanuna!

yakasirika nakuhoji kwanini imetelekezwa! hakuna simulizi mpya inayoandikwa yapaza sauti yake ikifoka eti kwanini juhudi zimeongezwa katika kutangazwa kwake nakufanya watu wengi waitembelee nakuifunua kwa kuigeuza geuza, wakiishangaa kwanini izunduliwe!

inahoji kwanini nguvu isingeenda sambamba na kupostiwa SIMULIZI MPYA, yasema imechoka kutazamwa ikiwa haina jipya, yaona hauna haja uzinduzi kama yenyewe haipatilizwi.

naishangaa hii blogu nakosa kitu sahihi chakuiambia nataka niishutumu haina shukurani lakini nasita sababu upande mwengine naiona inaongea maneno ya kweli.

ni kweli juhudi ziliegemea sana kwenye kuutangaza uzinduzi wa blogu badala kupost simulizi mpya.

blogu yasema wageni wengi wanaitembelea wakiishangaa kwani hiyo blogu ina nini kipya mpaka izinduliwe, yasema yaona aibu sababu haina jipya la lakuwajibu.

Naionea huruma Blogu yasema kwa hasira huku ikilia kwa uchungu ikituhumu wamiliki hasa BIN ZONGO kuwa anaidhalilisha.

maneno sahihi yakuituliza blogu hii ni haya yafuatayo, kama hayatasaidia basi tena kutakuwa hakuna namna.

"blogu tulia, ukilia waniliza, hasira hasara, usinune hupendezi, uzinduzi ndiyo heshima yako yapasa ulijue hili, zitaheshimika SIMULIZI ZAKO hata ukiwa kaburini, ikifika tarehe yako watu watakumbuka amini na wataliita jina lako na mashada pomoni.

blogu wewe tulia lengo ni ujulikane, watu kukutembelea ndio lengo usibane, twawataka watu mia kwa siku wapishane maelfu kuwahesabia ndio lengo usinune.

31 tarehe simulizi itabaki mwezi wa saba aisee kichwani haisahauliki, haikuwa mwaka juzi wala jana hukumbuki!? ila leo ipo hivi shukuru usidhihaki.

mwaka kesho ukifika tutakumbuka hakika tutaenzi uzinduzi na kupika wali mbuzi, tutatafuna viazi na kuusaza mchuzi hatutaita uzinduzi bali SIKU YA SIMULIZI.

itaenda mwishowe kalenda ikujue vijukuu vitaenzi huu wetu uzinduzi vitaiita hii tarehe ni siku ya SImulizi nawe utapata jina la heshima siku zote.

blogu acha jazba kuwa mpole habiby usikabwe na kijiba ukashindwa vumilia.

hii nayo ni simulizi wewe kuninunia naiandika kama hivi na watu kuwatumia wauone wako uchizi kukataa kuzinduliwa...

31 july 2016 SIKU YA UZINDUZI WA ommyzongo.blogspot.com ( historia imeandikwa)

"kwa namna simulizi zilivyo na umuhimu duniani ingekuwa uwezo wangu kila mwisho wa mwezi wa saba ingekuwa SIKU YA SIMULIZI" Bin Zongo

UKWELI NI HUU

Kama utaamua unichukie sababu ya ukweli huu ni sawa tu sababu najua nyie mabinti mnapenda kudanganywa!

mtu hata kama hujapendeza ukiambiwa umependeza ndio furaha unacheka meno yote yanaonekana.

mimi mwenzio leo sitaki kusimamia uongo acha nionje chachu ya ukweli.

mwenzako mimi jina langu ni kama nilivyokutajia pale mwanzo, ninae mchumba na ni mzuri kushinda wewe!

nampenda sana na hivi sasa tupo katika hatua za mwisho kabisa zakuoana yaani kwetu wanamjua na hata mimi kwao wananijua vizuri na wamebariki sisi kuwa mwili mmoja.

lengo lakukusimamisha wewe nikukwambia kuwa nimekutamani sana! vazi lako la kishenzi na laana linaloonesha sehemu kubwa ya mwili wako limenifanya nitamani kuwa nawewe kwa muda mchache tu na tena kwa siri kubwa sababu haustahili kutambulishwa kwa yoyote si kwa ndugu wala rafiki zangu.

wote wanaonihusu ni wastaarabu sana bahati mbaya wakigundua natoka nawewe sidhani kama watanielewa wataniona nimepotoka!

Nitaongopa kwakweli nikikwambia nakupenda sababu nimpendae ana rangi yake ya asili wala hajajichubua kama wewe! sa ntakupendaje!? kusema kweli umenitamanisha tu na sijui kwanini kadiri ninavyoongea nawewe iyo tamaa yenyewe inaisha kwa mbali umbo lako la mchoro linaonekana vizuri sana ila ukifika karibu unagundua kuwa halina tofauti na wengine walioweka michina kisha ikawaporomoka!

dah samahani bwana nimeahirisha sitaki tena kuna sauti ina niambia ndani yangu kuwa nilichotamani kwako kimeonwa na wengi na nina mashaka wao sio wakweli walikuongopea wanakupenda na jinsi unavyoonekana muongo muongo umeshawakubalia wengi nahisi tamaa yangu mbele mauti..kwaheri dada sema kabla hujaondoka

chukua hii pesa kiasi nenda kanunua vitu vifuatavyo..

kwanza kabisa kanunue khanga pale dukani ujistiri mana ni dhahiri unaizuga tu jamii kuwa umevaa nguo lakini ukweli kabisa upo mtupu.

Pili kanunue maji hata yale maji safi kanunue unawe uso wako mana hayo ma makeup uliyoyarundika usoni hayana tofauti na mwanasesere!

mikope kama dodoki nahisi kope zako ulizoumbwa nazo zinakupendeza zaidi kuliko hayo uliyoyaweka usiku unaweza kumfanya mtoto aote.
futa kabisa iyo mirangi yako mdomoni nahisi kioo kilikuongopea hujapendeza hata kidogo upo kama sanamu lakuchorwa au zombi mla damu!

nahisi kuna haja yakutafuta ushungi uuvae kichwani mana hiyo minywele ya kughushi inazidi kuzinyonya akili zako ulizozaliwa nazo nahisi ukiendelea kesho utatembea na kufuli pekee.

kiasi cha pesa kilichobaki wahi hospitali mapema mana Vipodozi vinakasirikia ngozi yako naviona usoni vinaanza kutema sumu ya kansa na hii miale ya jua utazeeka mapema walahi.

Ngoja tu niseme kweli nilivyokuwa mbali nilikutamani ila nimekukaribia kuongea nawe nimegundua tamaa zangu zimepotea njia!

uafrika umeukimbia uzungu nao umekukataa yani upo kama Mzimu wa Sokwe!

"Napenda tamaduni za afrika, Nampenda mwanamke wakiafrika, Napenda kila kitu cha mwafrika! najivunia uafrika" Bin Zongo
Ukweli Ni Huu

WE BINTI BWANA


Sitothubutu kusema huna akili ingawa matendo yako yananithibitishia hilo.

kwanza tulipendana,
pili tukazoeana,
tatu tukakerana
hatimaye tukaachana.

mazoea yakaniadhibu,
nikakumbuka ukaribu,
nikarejea kwa aibu,
kuomba uje unitibu,
mashaallah hukunighilibu,
ukarudi kwangu tabibu.

maisha yakaendelea,
penzi kiraka nikizoea,
baadae nikagundua,
ni adha nimeikaribia
dharau nimejijengea,
upuuzi nimeurejea.

kitu kimoja hujajua,
mie ni yule wa mwanzo.
sifai kulumangiwa,
kuteswa kwangu tatizo,
Kamwe sitofurahia,
kugeuzwa chotezo.
maneno yangu rejea,
mimi sio wa mchezo,
kamwe sitokurudia,
huu ni msisitizo.

Huu moyo ni mashine,
hukoboa na kusaga.
moyo wangu usiupime,
usitake kuuiga,
kulifuga pakashume,
bora kusugua gaga..
unyayo wako ung'ae,
na wengine wataiga.

ni heri nikose vyote,
kuliko ile heshima.
sina sababu yoyote,
kwako wewe kusimama.
umenivua nguo zote,
muungwana nachutama.
likiisha jua lote,
gizani ntasimama.
ntajistiri chochote,
nafsi yangu itatuama.

utenzi umenijia
bila ya kudhamiria,
faraja kukuimbia,
moyoni najivunia,
hasira zanikimbia,
maumivu kadhalika.
lakini nakuambia,
utakuja nikumbaka.

Maamuzi kama ni yako,
 itakuwa afadhali,
ila kama ni tamaa yako,
umejipiga kabali,
mbeleni pumzi yako,
itakosa kuvinjari,
utageuka kituko,
mauti kukukabili
yatakupiga kikumbo
 yote sababu kiburi.

sithubutu tema lana,
sababu itakupata,
nilikupenda kwa sana,
iweje uje nitupa,
ama ndio uungwana,
kulipa baya kwa jema.
acha nisiseme sana,
 nitawapa lakusema,
wale wengi wafitina.
ubeti natamalai,maishani tutaonana
Yani we Binti.

KWANINI?

Ndugu kwanini kitu chakununua kwa pesa kisababishe uvunje uiminifu kwa mimi ambaye sina hata chembe ya nia mbaya nawewe!?

kwanini unataka kunipa dhambi yakukuwazia vibaya rafiki yangu wa damu?
kwanini unataka kununua bure kabisa ubaya usio na faida yoyote ule?

Eti kwanini
Eti kwanini unaruhusu tamaa yako isiyo na tafakuri ibomoe ukuta thabiti wa urafiki wetu wenye tija?

niambie basi kwanini lakini unajaribu kuipima roho yangu ukionesha kupinga kuwa mimi ni mwema kwako?

kwanini unanilipa malipo ambayo sistahili kulipwa na rafiki niliyemuhifadhi kwenye chumba kilicho jirani na ndugu zangu!

kwanini unaupa sababu ulimi wangu utamani kutamka maneno yaliyo na lawama kwako!

jipe muda basi utafakari tena labda pengine umekosea ulichokipanga kwangu tafadhali sana tafakari na ujisahihishe sababu wapo ambao nahisi wanastahili kunifanyia hivi lakini sio wewe!

nakupa nafasi tafakari naamini utaona kuwa sistahili kutendewa hivi nawewe!

sononeko langu litakugharimu, hivyo ndio naamini sababu ukatili wakulipiza ovu sijafundishwa naongozwa na imani ya kwamba utalipwa kwa matendo yako!

Nashukuru kwakutokuwa mkamilifu kwangu sababu umenifanya nitumie sanaa kuelezea hisia zangu! ila upatapo ujumbe huu naomba sana nafsi yako ikusute na uikaribie toba!.

bado sijakushutumu wala kukuhukumu kilicho na utayari nafsini mwangu ni msamaha wa bure kabisa sababu nami sijakamilika pengine baada ya hapa naweza kufanya uliyo nifanyia kwa mwengine ingawa kwa jinsi ninavyojisikia nitakesha nikiomba nisimtendee mwenzangu haya ulioyatenda kwangu.

ingawa ni dhahiri kabisa NIMEKUSAMEHE sababu muumbaji ni MUNGU sisi binaadamu ni wamiliki tu na hatuna silaha yakutosha kulinda alivyotugawia muda wowote huweza kutupa nakutunyang'anya akipenda.

Bado nafsi yangu inayumbishwa na simanzi lakutokuamini pengine labda utanisaidia kuondoa kadhia hii ulinijibu KWANINI RAFIKI YANGU UMEGEMUA GOME LA UTU WANGU KWAKO?.

"Maswali unayojiuliza nakujijibu kuhusu ujumbe huu ndio adhma yangu kama mwandishi" Bin Zongo

kwanini???

ILINICHUKUA MUDA KIDOGO

Kwa jicho la baba asiyekuwa na mipango thabiti na familia yake haiwezi kumchukua muda mrefu kama ilivyo nichukua mimi na hii yote ni sababu nilitaka muda wakujiridhisha,
kila nilipokuwa naiwaza familia yangu ilinipa wakati mgumu sana kuamua yupi ambaye atakufaa wewe na ukajivunia kweli kumuita mama.

kila mmoja leo hii humwambii kitu kuhusu mama yake na ukimwambia azungumze kitu kuhusu mzazi wake huyo ni lazima atakosa neno sahihi lakumwambia kudhihirisha upendo wake lkn ni ukweli kwamba sio mama wote wanaosifiwa na watoto wao ni wema ila kwa vile wamefanya tendo lakishujaa kwa kuwahifadhi tumboni nakuwatoa kwa uchungu nakuwazawadia upendo wa malezi ni lazima wawe wema kwao hata wakiwa wabaya kwa wenzao huu ni ukweli ulio dhahiri mwanangu achana na ule ukweli usiopendwa kuongelewa.

Ilinichukua Muda kidogo
mimi ilinichukua muda kumpata wakukuzaa sababu sikutaka awe mama kwako tu nilihitaii awe mama wa jamii.

nilihitaji pakitafutwa mfano wakuigwa angalau linyooshewe kidole hata vazi lake tu kama yeye mwenyewe hayupo, ilinichukua muda kidogo kumpata sababu dunia hii ya leo sio kama ya kina babu yako mzee Zongo ambaye alibahatika kumpata bibi yako Mariam kiulaini kabisa nakujiwekea historia yakuoa mwanamke wa shoka Ilinichukua muda mwanangu na ndio mana sitaacha kukusitiza umuheshimu sana mama yako sababu mimi mwenyewe huduma anazonipa ndizo zinafanya niwe baba bora na niipende kwa kuiota familia yangu! nimetoka nae mbali sana mama yako mpk kuamua wewe uzaliwe sio mchezo hata kidogo....ilichukua muda mwingi na ndio mana nitakuwa tayari umtaje yeye ukiulizwa kati ya mimi na yeye ni nani umpendae zaidi, nitakuwa tayari sababu mchango wa mama yako ni mkubwa ukilinganisha namimi nakumbuka enzi zile bado mdogo kabisa bosi wangu alinituma kikazi mkoa mwengine nilitaka sana kuwa nawe karibu muda wote lkn niliwaza maisha yetu bila ajira nikalazimika kukubali safari ile ya bosi ambayo hakunipa kwa ombi bali kwa amri, nikiwa safarini nilipata taarifa huku nyuma namna ambavyo ulimsumbua mama yako, nilisikia jinsi ulivyokamatwa na homa la ajabu Mungu wangu sijui lilikuwa ni n
ini lile, ulibadilika ukawa umekakamaa macho yalikutoka nikaja kujua baadae kuwa ulikuwa na mchango, siku mbili kama sio tatu ulikuwa ukilia na mama yako na ulipokesha bila kulala ulikesha nae. unaweza kunijulisha kwa hapa duniani ni nani kama mama yako?
sasa achana na hilo kuna kipindi nilikamatika kweli na maradhi nawe ukawa unaumwa katika familia yetu aliyekuwa mzima ni mama yako pekee, masikini ya mungu alipambana sana kutuhudumia nakuhakikisha uzima unarejea kwetu kwa tabasamu lake linalompendeza kila mwanadamu, Ilinichukua muda sana kumpata huyu mwanamke, nimemuokota katika dunia ya wanawake waovu lkn yeye alibandikwa bango liliandikwa MIMI SI MIONGONI MWAO.
maandishi hayo sikuweza kuyasoma vzr hata nilipokutana nae sababu yalichafuliwa na uchafu mkuu uitwao UTANDAWAZI ambao umewachafua sana wanawake nakuwafanya wanuke uvundo wa tamaduni za wazungu hivyo Manukato ya stara na nembo yakuvutia iliyonakshiwa na tamaduni za kiafrika ikiwemo maadili mema yamekaa mbali na wao.
Ilichukua Muda
Ilinichukua muda sana sababu sikuhitaji mshangao wako wenye taswira ya swali la NILIMPENDEA NINI MAMA YAKO.
nina hakika jibu tayari unalo..ni mwema sana hata nilipoamua kumuoa ni kama niliamua kuongeza ndugu mwengine kwenye familia yetu, mara zote alipolia ujue mimi ndio nilimliza na kilio chake kilikuwa ni bakora inayouma kweli moyoni mwangu na huniadhibu kwa pigo liitwalo majuto ya kwanini niitendee maovu nafsi isiyo na hata chembe ya uovu.
Ilinichukua muda sana kumpata mama yako lakini mara zote huwa nafarijika maana hata yeye huniambia kuwa ilimchukua muda sana kuamua kwa dhati kabisa mimi niwe baba yako! na nikweli mwanangu alinisumbua sana mpaka kunipa ridhaa yakuuendesha kwa upendo moyo wake!
nikisema niendelee kuelezea namna ambavyo ilinichukua muda nitatumia siku nyingi tu acha tu niishie hapa ila tambua ilinichukua muda sana kumpata mama yako.

TUSIDANGANYANE..!


Tusidanganyane Bwana!
Ifike mahali tusichukuliane kama watoto, tuheshimiane, tusidharauliane kwa uongo ulio dhahiri!.

Umetengana na mwenzako miaka zaidi ya tano, kuwasiliana nae kwa nadra sana tena ukimpigia ni salamu then anakuomba umcheki baadae coz muda ule yuko busy.

kinyonge unakata simu unamsikilizia baadae yenyewe hakucheck wala nini, unazuga kumpotezea unajikuta unampotezea kweli siku na mawiki kadhaa yanapita unapotimu mwezi anakupigia yeye na kwa bahati mbaya unakuwa busy hivyo nawe unampokelea kisha unamuomba akucheki baadae..

baadae hakucheki wala nini, masiku yanaisha miezi baadae mwaka na miaka.

alikuwa mkoani huko amerudi dar bila kukwambia kama zali siku mnakutana mkigombea gari la mbagala.

kinafki kabisa mnaanza kukumbatiana kila mmoja akionesha kummis mwenzake.

stori stori mnaanza kuongopena eti siku zote mlizokaa mbalimbali hakuna mechi yoyote ya nje iliyochezwa...! si uongo huu jamani!, tena uongo usiovaa nguo!.

mnajidanganya kwa vinywa ilhali kila mmoja wenu akijua kuwa ameshiriki mechi na kila aina ya timu..

ifike mahali TUSIDANGANYANE na sisemei kwa kuwa uongo ni dhambi na kesho mbinguni kuna moto la!, hofu yangu ni kuambukizana maradhi kizembe sababu sio wote wamezaliwa na tahadhari duniani, wengine ni wadhaifu sana utakuta akishadanganywa hivo anajiachia tu akijilazimisha kuufanya uongo uwe ni kupendwa.

Shtuka jamaa utajikuta unakuwa MZEE MPUMBAVU!.

Tusidanganyane dunia hii sio ya wachumba kuvumiliana Eti kukaa miaka mingiiii bila uhalifu kufanyika....

ruksa kudanganyana kwa midomo kisha tuthibitisha kwa vipimo kama kweli mwapendana.

ndio pimeni Maukimwi, magonorea, makaswende bila kusahau ma UTI halafu mambo mengine yafuate....TUSIDANGANYANE BWANA AGH!

Me sitaki kudanganywa!

"JIPENDE WEWE KWANZA DUNIANI UTAKUWA NI MWENYE FURAHA SABABU UTAJIFUNZA THAMANI YAKUWAPENDA NA WENGINE" bin Zongo

KALAMU YAGOMA

Napata wazo jipya nalitafakari kwa undani wake naona lafaa niliweke kwa maandishi ili walau liwafae na wengine maishani, katika kuumbwa kwangu vingi sana nimenyimwa ikiwemo choyo na ndio mana siweki ndani hata siku moja hadhina ya nikiandikacho nakigawa kwa wengine ili wakonge nyoyo nakulisha bongo zao pia!

sasa Nawezaje kuliweka wazo langu kimaandishi?

swali hili zuri lanifanya niikumbuke marafiki zangu kalamu na karatasi nakurupuka kuwafuata sababu jamaa zangu hawa hawakai mbali, makaazi yao ni mezani na yapo jirani kabisa na maskani yangu maarufu iitwayo Kitanda hatua si zaidi ya nne nafika mezani.

kwa mara ya kwanza kabisa nagundua tabia za jamaa zangu kalamu na karatasi, tabia ambazo siku zote kumbe wamezificha kwa usiri mioyoni mwao na leo ndio wameamua kuzidhihiri.

loh! ama kweli ya moyoni yaliyo na usiri usiombe yatoke kinywani unaweza ukaliona kaburi!

siku hii ndio niligundua kuwa kalamu siku zote inaigiza unyenyekevu lakini kumbe ndani yake ni jeuri na ina misimamo hasa ikiamua lakwake!
karatasi

kwa upande wa karatasi yeye ni binti mpole sana lakini nilibaini kuwa hana msimamo na mara zote hutegemea kalamu anachokisema ndicho yeye afuate!

tabia hii ya karatasi niliibaini leo wakati kalamu ikinipa makavu yangu karatasi yeye ilikuwa ikitabasamu kinafiki huku ikikosa ujasiri wakunitazama usoni nakupeperuka peperuka kana kwamba eneo lile lilikuwa na upepo.

kalamu haikunionea haya hata kidogo ilifunguka kwa hisia kali huku machozi ya hisia za hasira yakuonewa yakimiminika usoni mwake, jamani kalamu yanichimba !!

kwanza iligoma kabisa mimi kuishika ili niitumie kuandika wazo langu.
mwanzo nilidhani masikhara lakini ukweli ukawa ndio huo kalamu yanikatalia katakata,
yagoma kwa kisirani ikinihoji kwa ukali vipi naitumia malipo hayaonekani!

yafika mbali zaidi ikidai eti mimi ni tajiri iweje naitumia bila kuilipa posho.

naistaajabia hii kalamu leo imepatwa na nini..!!

yasema imetumika sana kuandika vitu vya mana lkn ufukura yanuka haioni chamaana..

kwahivyo leo imegoma inachohitaji ni neema, naibembeleza kwa huzuni walau ikubali naipa ukweli tupu taarifa tanabai, watu hawapendi soma maandishi hawathamini hivyo ninachokifanya nikutimiza tu nilichoagizwa duniani.

naipasha zaidi kwa kuiambia kuwa haata mimi najua niandikacho ni mali lakini nifanye nini na watu ni wabahiri.

huwa naingoja kesho labda mlango utafunguka lkn ni miyeyusho malipo nipatashika,

nafsi inasonona siijui yangu hatima najaribu kwenda kisasa lkn sipati mbivu

 naambulia tu misifa kipato ni maumivu.

naijuza kalamu kuwa sanaa bado ni kiza Tanzania haina nuru, na mimi sio wakwanza walikufa na ufukura wanafasihi mahiri,

 kipato kiliwatenga lakini hawakughairi waliendelea songa bila kutamalai

iweje nianze mimi leo hii kujinai kukichinja kikatili kipaji changu kukinai.

rafiki yangu kalamu endelea kupiga moyo konde endelea kumwaga wino usinigomee mwenzio utazidi kuniumiza.

wewe ndio rafiki pekee ambaye hunimaliza mawazo yanaponijia na hukimbiza huzuni inaponikaribia iweje leo wanitendea hivyo.

kwani siniwewe ndio ulikubaliana nami kuandika makala KUHUSU PESA na siniwewe ndio ulitia saini ukiunga mkono kuwa pesa zetu zipo mahali zitatufikia muda ukifika.

Iweje leo wanisaliti unageuka kuwa MAPENZI YA SASA waniacha kisa sikupi pesa! itafutie rangi hii fedheha walau hata isinifanye nichekwe na walimwengu pindi wakigundua ipo ndani yangu.

hakika leo umetonesha mahali ambapo hapajapona hata kidogo nawezaje kustahimili machozi haya.

Ni juzi tu Rafiki yangu Muda alilalama kuwa namtumia bure bila yeye kuona mafanikio yoyote mpaka leo ameniachia fumbo eti shauri zangu ipo siku ataniacha!

shemeji yenu nae haishi kunisema ati kila saa natumia kuandika kitu kisicho na faida kwangu na nina uhakika ni yeye ndiye kaja kuwatia ndimu ninyi leo hii mnigomee lakini iweje mshirikiane kunilaumu mie wakati ninyi ndio watu wakaribu ambao nawaamini!?

iweje leo hii mlivue vazi la ustahimilivu nakujivika kiburi kisicho kuwa na uungwana!

lengo lenu nini hasa mwataka nami nidanganyike kwa kuhisi pombe, bange na Madawa ya kulevya ndiyo vitanimaliza mawazo ya kukosa kufanikiwa kwa nikifanyacho!

kadri ninavyo zidi kuongea nawe kalamu nazidi kugundua sipaswi kukunyenyekea bali kukuropokea tu mana wewe na wenzako hamna nia njema hata kidogo na kwa taarifa yenu tu niwapashe wewe kalamu, wewe karatasi wewe muda na huyo mkaza angu mie ambaye ni shemeji yenu,

kalamu
mjue kuwa mimi sio kijana niliyeumbwa na tamaa yakutafuta faraja inayogharimu utu wangu sitaenda maskani kuvuta bange wala club kunywa pombe eti nipunguze mawazo.

Aliwahi sema kilembwe wangu SHAABAN ROBERT mwandishi ni mtu wa desturi ambaye haridhishwi na hasara wala haishi kwa kunywa ukungu nakula hewa.

Jamii hailijui hili nami sitataka kuwa mwanaharakati wakulipigania hili ila nitahakikisha napiga goti nasali nikisujudu kumuomba Mungu ili Thamani ya Maandishi iendelee kuonekana kwa kuizindua jamii katika tope la usingizi uitwao UJINGA

na utu wa Mwandishi utambulike kwa kupewa hadhi ya mtu pekee anayejitahidi kuvaa uhusika wa kila namna ili mradi kufikisha ujumbe kwa jamii.

Mwandis
hi yeye ni mwendawazimu sa nyengine, mwandishi huyu ni Kiongozi wakati fulani, Mwandishi yeye hudiriki kuhama katika mawazo yadunia hii kwa lengo moja tu lakuhakikisha anaibumburusha jamii nakuweza kufikiri tofauti.

Kalamu nakuacha sitakutumia mpaka utakapopenda mwenyewe lakini sitaacha kuandika ingawa sijui nitatumia mbinu gani na nakwambia hili ili utambue kuwa mimi muandishi nakamilisha kazi zangu nikitegemea uwezo wako!.

kaa tafakari umeandika vingapi mpaka leo hii tangu enzi zile zakina wilium walkspear, hivi duniani kuna pesa inayoweza kulipia kazi yako!

tafakari maneno yangu yakirudisha moyo wako nirejee uniombe msamaha tuendelee na kazi lakini mpaka hapa nimeshakusamehe.

Kwaheri!.

MAISHA YA FACEBOOK

Mtandao wa Facebook
Nilianza kwa kuhadithiwa na jamaa yangu flani ivi kwamba eti facebook kuna watoto wakali, marafiki wa kila aina na zaidi kuna kila aina ya swagg kutoka Facebook,
Dah! Alikuwa akinitamanisha mno enzi hizo me kushika smartphone ilikuwa ni ndoto kubwa mno, na ata computer sikuwa naweza kuitofautisha na luninga,
Basi dah nikajiona niko nyuma sana, nilijona mshamba, niliyepitwa na wakati, niliwavuta kichwani hao warembo wa facebook, nikaanza kuwajengea taswira hii!.
wana rangi nzuuri za kiafrika, mavazi adimu na adhimu yenye heshima na taadhima, sura zenye bashasha na tabasamu muda wote, wana haiba za kike na post zao zina alama ya upendo sababu niliamini upendo unaishi kwa wanawake.
Hizo zote zilikuwa ni taswira nilizojenga huku nikitamani kujiunga na ulimwengu huo wa facebook,
Masikini ya mungu tayari hata mke wangu nikapanga nitampata Facebook,
Marafiki nao nikawajengea taswira ya watu wema wasio na hata chembe ya chuki, wapole wasio na ubaguzi,
Sasa nikawa natamani kupata simu namimi nijiunge na facebook, maisha ni hatua, utakanyaga mchanga, tope mwisho utakanyaga lami, na ndivyo ikawa nilianza kutumia Nokia flani ivi ya tochi dah balaa sana ilikuwa napiga simu af mtu akipokea
namuuliza unanisikia??? Akinijibu ndio nakata simu kisha naanza kutafakari utaalamu wa wagunduzi wa mawasiliano!! Ikaenda ivo mpk nikapata namimi izi cm za kisasa asante mchina!!
Sasa nikaweza kujiunga na facebook nakumbuka aliniunganisha yuleyule jamaa yangu aliyekuwa akinipa taarifa za facebook.
Dah! Ilinichukua muda kuweza kutumia lkn Baadae nikaweza, na ndipo hapa nikaja kugundua kuwa facebook hata sivyo nilivyokuwa nadhani Mimi.
Kumbe watu ni walewale!!, Binaadamu wenye tabia hizihizi za kawaida,
WABAGUZI: wanabagua hata post za kulike, watu waku wa add na mengine mengi tu yakibaguzi.
WANACHUKI: wanachukia post hata ya mtu hawamjui.
WAIGIZAJI: wanajibadili majina yao, sura zao, makazi yao hata shughuli zao.
WACHOYO: mtu hata kulike post ya mwenzie anahisi kama anampa dola kadhaa zakimarekani na atatajirika.
Aisee nimejionea mengi sana na kujifunza mengi pia, nimeweza pia kufananisha maisha ya facebook na uhalisia wa maisha ya watu kawaida yaani ukiwa unapost kitu tambua kuwa kuna Rafiki zako wengi wanapost nao, na ukiwa unasubiria like na coment kwenye post yako hiyo na mwenzako anasubiria ivoivo pia,
Kwa uhalisia ni fundisho katika maisha yetu yaani ni vema UJIFUNZE KUTATUA MATATIZO YAKO MWENYEWE USISUBIRI MWENZAKO AKUTATULIE SABABU HATA YEYE YUKO ANAWAZA NAMNA GANI ATAYATATUA YAKWAKE.
haya ndio maisha ya facebook......

SITASEMA

Kama kuimba nitachoka nitashika kalamu kuandika Makala fupi na ilitokea sina chakuandika nitaingia watsap kwenye group langu ambalo member ni mimi peke yangu nakumbuka nililiunda group hili siku ile mama yangu anafariki hua nalitumia kuelezea hisia zangu hasa ninapovurugwa na haya maisha pamoja walimwengu, hua najifariji kuwa naongea na mama yangu! nitatumia group hili kupoteza muda mradi nisiseme sababu ni yamini nimeila na nafsi yangu kuwa sitasema.

kusema ni kujiumiza mwenyewe sababu mengi yamepita na kwangu yamebaki historia Sitasema kamwe kuwa ni mimi ndie nilikuwa chanzo chakuachana nawewe! sitasema sababu ni fedheha sio tu kwa ndugu zangu hata wazazi wako na mara ya mwisho kuongea na mama yako ni leo, sauti yake yaucheshi bado inaendelea kuniita mkwe sikuweza kumwambia kuwa umenifumania na umeumia sana na hautaki hata kuniona!
Sitasema kamwe

Nimejaribu kungoja siku mbili zipite baada yatukio lile labda utarudi ama utapokea simu yangu lkn wapi, nasikia hutaki hata kusikia jina langu na kwasababu ya maumivu umeamua kuacha kazi nakuhama mji sijui unaishi wapi kwasasa!

Sitasema hata kwa bahati mbaya kwa marafiki zangu ambao wamezoea kukuita shemeji tena mbaya zaidi muda mchache uliopita nimesoma meseji ya Swahiba angu Sosi akiuliza kama hujambo mbona hupatikani kwenye simu eti anadai amekumbuka sana utani wako!

Siwezi kumwambia na Sitasema kuwa nimekukorofisha sababu ni aibu kubwa kwangu kumpoteza mwanamke wa heshima kama wewe! ni aibu sababu mahusiano ya wengine wengi yalikuwa yakienda kwa kuakisi mahusiano yetu iweje nimekuwa mjinga kiasi hiki mpaka kuhadaika na binti mwengine ambaye kimsingi hamfanani hata kidogo, yeye tulipokuwa tukikutana alikuwa anaomba pesa hata zisizo za msingi wakati wewe ulikuwa ukinishauri namna yakuongeza kipato kwa maisha yetu ya baadae. Dah! sio kwa aibu hii kwakweli!. naapa sitasema na kama nikifanikiwa kukutana nawe nitakuomba msamaha nakukusisitiza sana usije ukasema, nakiri ujana ni maji yamoto na haya yameniunguza, nimebabuka mwili mzima na sina wakumlaumu sababu kilicho niponza ni tamaa na ujinga wakutumia kitanda chako kusaliti Uaminifu wako kwangu!

nani nitakaeweza kumtazama nakumwambia kasoro yangu hii. na zaidi nakuwa kitanzini sababu ni mwezi mmoja tu umepita tangu ukute ujumbe mfupi kwa mdogo wako akiwasiliana nimimi nakusifia uhodari wangu kunako uwanja wa fundi seremala! ulidhihiri kuwa nimetoka na nduguyo lkn nikakupiga kiswahili ukanisamehe huku ukinisihi nisikuumize, nilishukuru Mungu msamaha huo huku nikiustaajabia moyo wako sababu kabla ya hapo uliwahi kunisamehe mikosa isiyo na idadi likiwemo lile lakunifuma bafuni nikiwa na mke wa jirani yangu Baba Emi. ulizuia mdomo wako usipayuke kujaza watu, ukatuhifadhi sana mimi na Mama Emi nakumbuka uliwahi sema aibu yako niyangu hivyo hutathubutu kunijazia watu na mwisho ukanisamehe! Sitasema haya sababu kuyasema haya nikujivua nguo mwenyewe! ingawa siachi kumuomba mungu nisije pata habari ya kwamba umejizuru huko ulipo. nahisi baraka zakujisahihisha zimenikumba sitahadaika na ujana tena rudi mchumba tuyajenge maisha.

sitasema naomba nawe usiseme sababu ni aibu kwakweli.

ACHA NIKUDANGANYE

Mwenzako sijasoma sana! sijivunii kusema hivyo naumia lakini inanipasa tu nikwambie licha ya akili kuwa nazo nyingi lakini nguvu ya mapenzi katika umri mdogo ilinifanya shule niione ya nini na mapenzi ndio habari ya mjini!

Nikajikuta nasoma kwa ubabaishaji sana leo hii hapa natamani nipewe kipaza sauti chenye nguvu yakusikika maeneo mengi nchini Tanzania hasa kwa watoto washule ambao wazazi wao masikini kama alivyokuwa mama yangu mimi ningewakemea kwa sauti nakiwasihi wasome wasioge kamwe kwenye bahari ya huba kwani mawimbi yake yatawazamisha kwenye tope la ujinga na hata waweze kupuuza elimu ambayo ni muongozo thabiti!

mimi sijasoma sana na ndio mana leo nalalama sababu sitaweza kukuthibitishia kisomi kwa kukuletea tafiti nilizofanya zikakuonesha kuwa MAPENZI HUDUMU KUTOKANA NA UONGO!

lakini huo ndio ukweli, bila uongo mahaba hayana uhai!
kabla sijakuelezea hisia zangu kuwa nakupenda nakumbuka nilimsikia rafiki yako akisema kuwa wewe unavutiwa sana na kijana mcha Mungu, na ndipo hapo nami nikaanza kubeba lozari na biblia huku salamu yangu popote hasa mahala ulipo ikiwa ni "Bwana yesu asifiwe"

ukweli ni mapenzi yangu tu mazito juu yako lakini mimi sio mkristo kabisa! unafiri ningefanyaje sasa ili kuuridhisha moyo wangu ambao unaniamrisha kila siku nikupende! ilikuwa ni lazima nikudanganye.

mimi pekee mtaani kwetu ndio nilikuwa mgeni na mtu pekee kuanza kuzoeana nae ni MPOLE kumbe wewe hupatani kabisa na MPOLE pamoja na marafiki zake nilipokuja kujua hili nikaachana kabisa na MPOLE nikaunga urafiki na MUONGEAJI ingawa ukweli ni kwamba mimi sikumfurahia kabisa MUONGEAJI na marafiki zake sababu mara zote walipenda kuzungumza mambo kuwahusu wao lakini ningefanyaje ilibidi siku ile yakwanza kuongea nawewe nikwambie kuwa wenzangu mimi ni MUONGEAJI na wenzake nalikumbuka tabasamu lako ulilonipa baada yakusikia kua mimi ni miongoni mwa kampani ya MUONGEAJI nafsi yangu ilinisuta sababu huo sio ukweli lkn ningefanyaje sasa kama sio kutumia uongo huo.

nakumbuka siku ile hata tabia niliiga ya MUONGEAJI mara zote nilijisifia na kujiongelea na ndipo nilipofanikiwa kuziteka hisia zako Uongo wangu ulinifanya nikupate, Acha tu nikuongopee sababu uongo kwa sasa ni mbinu kuu katika mapenzi nami sipo tayari kukupoteza!

nidanganye nawe usije ukaniambia ukweli sababu nimevutiwa nawe kwa umbo, rangi na ongea yako kumbe ukweli hivi vyote sio vyako! umbo lako lakweli nimeliona kwenye picha zako za shule ya sekondary kumbe hili umenunua kwa mchina asante kwa kunidanganya, nimeridhika! haitoshi rangi yako kumbe ni muafrika kabisa lkn kutokana namimi nimeharibiwa na tamthilia za kizungu nikajikuta nataka mweupe na nilipokuona nikaona nimepata kumbe ni uongo wako mama, hongera.

Acha Nikudanganye 





uongo wako umefanikiwa kununua upendo wangu! asante kwa kunidanganya ingawa nina shaka akija mkweli katika hili nitakuacha! sikuchukii nazidi kukupenda lkn tambua uongo wako unachangia sana kukupenda kwangu mana nasikia ulikuwa una lafudhi ya kigogo kilichochanganyika na kiswahili lkn tangu ujue wanaume umekuwa ukitudanganya kwa kuongea kwa maringo kiswahili ukichanganya na kiingereza, vijana tukikaa tunasifia kuwa una swagg basi nazidi kukupenda ingawa nafikiria sana itakuwaje siku ukitakiwa uwe wewe na usitudanganye tena na lugha za wengine!

naomba ridhaa mchumba tupitishe uongo uwe ndio ngao ya penzi letu sababu ni unafiki kujifanya hatudanganyani wakati penzi letu linazidi kuimarika kila uchwao kutokana na kuongopeana kwetu.

ni mimi ndio nilijifanya nimefiwa na babu yangu mzee Ally kule udigoni kwetu sababu ilikuwa ni sherehe yako yakuzaliwa nami sikuwa hata na pesa yakukuzawadia hata pipi sa unadhani ningefanyaje kama sio kumuua babu yangu kwa mara ya pili maana alishafariki miaka miiiingi iliyopita.

nashukuru ulinielewa nawe ukanidanganya
umeahirisha party kumbe ukweli ulifanya kwa mtindo wa kwenda mziki na mashosti zako! uongo umesababisha tuone tunathaminiana kwakweli....naomba tuendelee kudanganyana kwakweli sababu sitakuwa tayari kuusikia ukweli wa kwamba siku ile ulitoka na bosi wako wakati me ulishaniambia siku ile mlikuwa busy sana ofisini kwenu na hakukuwa na mwanaume mlikuwa wasichana tupu na bosi wenu alikuwa nje ya nchi kikazi...

NAOMBA UAMINI UONGO WANGU MCHUMBA KAMA NIFANYAVYO ILI KUDUMISHA PENZI LETU LIFIKE MBALI NA IKIBIDI TUOANE.

SHEM UNAMUUMIZA SISTER 'ANGU

Haikuwa na maana tu wewe kuzaliwa mwanaume mwenye mvuto halafu usijue majukumu yako..

unamuumiza sister angu bhana, dah! halafu samahani
Unamuumiza dada 'Angu
najua wewe ni mswahili safi na mara nyingi hutupendi vijana kwa kuchanganya maneno ya kihuni na ya kiingereza kene sentensi za kiswahili lakini leo mimi ili kuonesha msisitizo ntakuchana kwa kuchanganya maneno yote hata ya kidigo mradi ujue unaniumizia dada!

Dada alifuruhi sana alipojua dhamira yako kuwa ni njema hutaki kumchezea unataka kumuoa lakini tambua kuwa hakuwa anajua kuwa kila tabia mbaya unayo na nina uhakika angejua asingetoa machozi ya furaha siku ile ya send Off pale kwenye ukumbi mkuubwa wa Majengo In kule Muheza Tanga.

Shem si niwewe ndio ulijifanya mwema kipindi unakuja kutoa posa kila jambo ulimuhusisha MUNGU na maneno kama Inshaallah ukiyatamka kila saa!

 iweje hivi sasa hata dada nywele zimempauka zikitaka kuandamana kwa kukosa matunzo.

kumbuka hujamkuta ivo sista basi ruhusu hata aibu ikuingie!

Sitaki kuamini kabisa kuwa eti saivi ule uchamungu haupo tena loh! kweli wewe ni muigizaji siniwewe ndio ulikuwa ukitupa vifungu mbalimbali kutoka kwenye vitabu vya dini!!

Acha zako bhana shem unazingua kinoma kwa unayofanya kwa sister au kisa unajua kama ndio kwako keshajifia, watoto keshakuzalia na kila namna ushamtumia?.

yeye mwenzio hakujua hilo alijua akiolewa nawe atayaona anayofanyiwa mama etu na Dingi, watu wanasema wanaume wote baba mmoja mama mmoja ila wewe baba na mama yako itakuwa ni shetani yani mpaka kulisha familia umeweka zamu na sister.....sio poa!

Mimi kuwa mume Bora Nimejifunza kwa Mzee wangu yeye hakuwa kama wewe, mkewe aliponuna alienda nunua cd za Mzee Majuto ili acheke.
na alipoona amezingua alikuwa mwepesi kuomba msamaha na hata siku moja sikuona akikimbia majukumu yake kama mume! we mwenzetu vipi nasikia mzito mpaka kutoa ada za wajomba.

mbona lakini unajimudu tu kifedha shemeji au ndio kuna kimada amekudhibiti ndio mana dada angu unamuona dampo.
acha zako bhana me sifagilii wala nini pigo zako,

hiyo michozi inayomtoka sister tambua kuwa ikidondoka chini inatimua vumbi la lana.

mbona lakini unachafua sifa zetu vijana wa leo tuonekane wote makuzi we unadhani sister akikaa na mashoga zake anaongea nini kuhusu wanaume! achana na izo habari bhana tafsiri ya mwanaume kamili sio ubabe, wala kubadili wanawake kama nguo ili mwanamke akuone mwanaume kamili unapaswa kuijua thamani yake, kuiheshimu, kumjali na kuisimamia furaha!

unanisikia shem? hayo unayoyafanya unasababisha mpaka mchumba angu aanze kusita kuolewa nami akihisi ndoa ni ndoano na wanaume wote ni wanyama!

kama umenielewa fanya ivi sasa,

Rudi maskani, hujaacha pesa yamatumizi..mkeo kuna dera anatamani af amemis ule ucheshi na upendo wako uliomuonesha kabla hujamuoa..

nenda haraka ukatimize hayo mimi wiki ijayo nafunga shule nikija likizo nikute amani ndani ya nyumba yenu laa sivyo nitafanya juu chini nimlaghai mdogo wako yule wamwisho kwenu kuzaliwa, yule binti mpole mpole, akiingia kwenye kumi na nane zangu nahakikisha baadae namuoa kisha namfanyia unayomfanyia dada angu.

Tuone kama utafurahi!

Tafsiri ya misamiati iliyotumika

 Sister - Dada

Bhana - Bwana

Ntakuchana - Nitakwambia ukweli

Send Off - Sherehe ya Kutambulishana ndugu wa pande mbili wa bwana harusi na bibi harusi

Shem - Kifupi cha neno shemeji

Inshaallah - Apendapo Mungu

Ivo - Hivyo

saivi - Sasa hivi

unazingua -Hautendi sawa

kinoma  - Iliyopitiliza

keshajifia - amependa sana

Dingi - Baba

Sio Poa - Sio vizuri

Sifagilii - Sikubaliani

Pigo zako - Mwenendo/ tabia zako

Makuzi - Kutokueleweka

Dera - Gauni kuu kuu la wanawake

Amemis - Amekumbuka

Kumi na nane zangu - Himaya yangu

Ahsante kwa kusoma!
bin Zongo.

JIOMBE MSAMAHA

Unadhani ni kwanini nafsi yako inajilaumu sana unajiona mpweke, hujiamini na wakati mwengine unadiriki hata kutamani siku zirudi nyuma urudi katika hatua fulani uliyowahi kuipitia...eti unadhani ni kwanini?

muda mwengine unajilaumu sana kwa maamuzi yako uliyoyaamua mwenyewe unamkumbuka mpenzi wako uliye achana nae unajutia makosa yako na kila ukijitahidi uwe sawa unashindwa...unadhani kwanini!?

jibu ni kwasababu umeshawahi kuomba msamaha mara moja au zaidi kwa wale ulio wakosea au kwa MUNGU wako lakini hata siku moja hujawahi kufikiria kujiomba msamaha wewe mwenyewe!

tunajikosea sana sisi na nafsi zetu lakini tumekuwa wapuuzaji wakujiomba msamaha huku tukiona kuwaomba msamaha wengine ndio dawa. sio kweli chukua muda sasa baada kusoma ujumbe huu ujiombe msamaha.

ulishawahi kuahidi nafsi yako ipo siku utakuwa fulani katika dunia hii lakini ndoto hizo hujazianza kuzitimiza, ni wazi umejikosea sana kujidanganya ni muda wako kujiomba msamaha.

ulishamuahidi mtu kuwa utakuwa nae maishani hutamuacha kamwe lakini sasa hivi penzi lenu hilo ni simulizi zinazoishi tambua kuwa hujamkosea yeye tu hata wewe umejikosea na hautaacha kujutia uongo huo kama hautajiomba msamaha!

jiombe msamaha uwe huru.

ipe nafsi yako nafasi ya pili, ni tiba itakayofanya uwe huru maishani! usiendelee kusononeka kwa kujiona mkosaji.
Jiombe Msamaha

umezaliwa Masikini na ukaiahidi nafsi yako kuwa hautakufa masikini lakini mpaka sasa bado unapuuzia kujituma nakusimamia
ndoto zako ni wazi umejikosea sana. jiombe msamaha.

sema...

ewe nafsi,  mimi sio mkamilifu,
usinighasi, kwa yangu mapungufu,
nipe nafasi, nifanye ulinganifu,
yale maasi, yageuke ukamilifu,
nibaki hasi, kama chanya ina upungufu.
huu wasiwasi, utoweke bila tifu.

Jiombe msamaha rafiki usiendelee kujihisi una hatia kwa makosa yalopita ni dawa zaidi ya muarobaini kujiomba msamaha kwa dhati kabisa mpaka uhakikishe nafsi yako imeridhia kukusamehe na ahidi kutorudia tena makosa yako.

ishi na watu vizuri kumbuka mtu akikutendea wema wewe ukirudisha maovu hata kwa bahati mbaya hujamkosea tu huyo mtu bali hata nafsi yako, na itakusuta katika maisha yako yote mpaka utakapokiri umekosa nayo itakusamehe.

Jiombe msamaha usiwe mtumwa wa nafsi yako mwenyewe tafuta uhuru wakujiomba msamaha nakujisamehe.

katika maisha yangu nimeshajikosea sana kwa kuwaumiza wengine bila sababu za msingi niliteseka sana mpaka nilipogundua kujiomba msamaha nakujipa nafasi nyengine katika maisha yangu.

Ewe nafsi yangu naomba sana unisamehe, nayaona mapungufu yangu na yananizomea mpaka naona haya.

nisamehe kwakweli siwezi kukamilika kwa furaha bila ya msamaha wako.

naahidi nitajiweka mbali na makosa haya yanayoigasi himaya yako. ungana nami kwa nia njema tuogelee pamoja katika bahari ya amani.

NAKULAUMU WEWE..

Nakumbuka nilitoka na wenzangu mlimani city, ni mimi pekee katika marafiki zangu ndio sijengi mvuto kwa yeyote wala pia sina uwezo wakumfanya mtu ahamasike namimi ata walau atamani kunisalimia..

nalijua hili na wala sina haja yakuelezea sana labda tu kuongezea nikwamba hata nikitoka na washkaji zangu mavazi yangu yakawaida sana jamaa wanakuwa wamependeza na hii ni mara zote sio tu siku moja moja, najijua sina mvuto ndio mana pia napaza sauti nikikunyooshea kidole nakukwambia NAKULAUMU WEWE!

Nakumbuka siku ile mimi na rafiki zangu tunaingia mlimani city wewe na rafiki zako mnatoka, mmependeza zaidi wewe unaonekana kuwazidi wenzio hasa umbile lako la mchoro, sura yako ya haiba na mavazi yako ambayo nakiri yalitiwa dosari na usasa lkn kwavile mwenyewe wakisasa sikuzingatia hilo nilibaki nikijiambiza "hakika amependeza yule dada"

nilijiambiza hivo huku nikikubaliana na hali yangu kuwa siwezi kumiliki mrembo kama wewe labda rafiki zangu yeyote yule sababu wao walikuwa na nyota za wadada, wasichana walijigonga kwao vibaya na nilikuwa nimeshazoea wasichana wazuri kuwaita shemeji sababu hata kipesa jamaa zangu niliwaita "kaka".

pale yenyewe mlimani city niliwasindikiza wao walikuwa wanajiandaa na safari ya nje ya nchi kula bata!.
Nakulaumu wewe sabau haya yote mimi nayajua na nilikushangaa sana siku ile uliponisimamisha mimi nakuwaacha wao, uling'ata kucha, ukanikonyeza kabla yakuniomba namba!.

nakumbuka nilitaka kuondoka nikihisi unanichora kumbe masikini ya mungu ulinipenda kweli!
nakumbuka rafiki zako walitaka kukuacha lkn wewe haukujali ulichohitaji ni mawasiliano yangu.

Nakulaumu wewe na wala usijali utafahamu tu kwann hili rundo la lawama nalishusha kwako, nakumbuka ulinitamkia wewe unanipenda na hata nilipokujibu nakupenda pia nilikuwa bado nina hisia kuwa unanidhihaki, nilijihoji sana iweje msichana uliye na neema ya urembo unipende kituko mimi!.

Nakulaumu wewe!
nakumbuka vzr niwewe ndie ulieanza kunifanya nipendeze kwa kunizawadia mavazi mazuri na kuniandaa kabla hatujatoka kwenda popte, nakumbuka sana ulivyogombana na marafiki zako mara kadhaa walipokuuliza unanipendea nini, masikini ya mungu walikuwa wanaona kama mimi nilivyokuwa naamini kuwa wewe hautoshani namimi.

ulinionesha penzi ambalo lilikuwa geni kwangu nikastaajabu, iweje nisikamatike kimahaba tanga nije nikamatike dar!

ukanipa heshima ya mume huku ukiongelea kila saa suala la mimi kukuoa loh! Mimi huyu nikuoe wewe!! utani gani huu unaniletea!? nilikuwa siachi kujiuliza.

ilichukua muda kukuzoea kwakweli nilikuwa mtumwa wa fikra zangu mwenyewe ingawa baadae
nikakuzoea...! nikakuona wakawaida,
lile wazo la kwamba mimi sio aina yako nikaliona la kijinga na rafiki zako waliokuwa wakikusema nikahisi nao wananitaka,

nikaanza kuwatongoza lkn walinikatalia wote tena mbaya zaidi walikuwa wanakuja kukwambia huku wakikucheka nakukusihi uniache sabahu sifanani nawewe, hukuwa unawajali!

hakika mapenzi ni uchizi! uliendelea kunipenda hata nilipoanza jeuri nakukuongelea maneno ya shombo we ulizidi kukolea nami haukuchizika hata kidogo na wenye nazo walokufata kila uchwao wewe uliapa kufa nami.

nakulaumu wewe sababu ulinifanya nijisahau kuwa nimekupata kwa bahati, ukanipa kiburi hata nilipotaka kuachana nawe ukawa unatishia kujiua ama kweli kILA SHETANI NA MBUYU WAKE.

najutia sasa na nakulaumu sababu kero zangu zilipozidi ukaamua kuniacha nakwenda kwa jamaa aliyekuwa akikuonesha heshima niliyokunyima,

jamaa alikuwa akikubembeleza kituoko mimi nilipokuliza, jamaa aliwaza kukuoa wakati mimi nikifurahia kukuchezea nakukuburuza kama mzoga, ulikuwa una haki yakuniacha lakini tambua kuwa imekuwa chanzo chakurudiwa na  ufahamu wangu.

nimegundua sasa kuwa mimi si chochote hata na hata kama ingetokea siku ile mimi ndio nakupenda wewe usingenikubali hata kidogo sababu sina sababu ya wewe kuwa namimi,

nafikiri ulinipenda kwa dhati, haukupenda pesa sababu ni ukweli kwamba pesa sina, wala hukunipenda mvuto sababu ni wazi kuwa mvuto sijajaliwa  lakini ajabu sana  niliyasahau haya  nikajiona mimi ndio mimi handsome boy, kidume.

 kumbe kituko kama walivyokuwa wakiniita wenzio nilijishau sababu ya upendo wako nikajiongopea kuwa kama wewe umeweza kunipenda basi naweza kumpata yoyote yule nae akanipenda NAKULAUMU WEWE,  kwann unifanye nijisahau nijione nina pesa kumbe ulikuwa unajipendezesha mwenyewe, nijione nina mvuto kumbe ni upendo tu na mara zote upendo hauna desturi yakutaka kujua sababu!

NAKULAUMU WEWE SABABU UMENIFANYA NIJIONGOPEE!

 nakiri mimi ni mjinga na huu ujinga ndio unanituma nikulaumu wewe!

"Mapenzi ni zaidi ya ukifikiriacho, ukipendwa pendeka. Usije ukamlaumu mwenzio siku moja akiweza kukuacha!"

INATOSHA..


Kusema neno hilo nalazimika
licha ya kwamba bado nahitajika,
uwezo wangu sasa watambulika,
lkn kusitisha nahitajika,
neno lifaalo INATOSHA na hapa mbele nukta naweka.

mafundisho yangu yangali hai,
 niloyatoa yanatosha tamalai,
huu mkono wapunga wasema bai,
 tutakutana nafsi yangu ikifurahi.

nipasayo kukugawia ni mengi sana,
ila wanadamu waso na mana,
wanaweza kujigea kwa mapana,
Inatosha
kisha kukimbia mbali sana.
Inatosha ipo siku takutana.

najua mpo mtakaojali ,
na wengine mtanyari,
iweje niahirishe safari,
wakati bado ningali hai.

watakaoponda ni wengi pia,
 sababu ya chuki kwa hii rupia,
 hawajui kama MUNGU alonigea,
 kusitisha hii safari kaniambia.

Ipo siku mtamuhitaji Bin Zongo
mkihitaji story zake za mafumbo
 ila unafki wenu utageuka fimbo,
 utawachapa pande zote za mgongo.

inatosha kwa leo nasema basi,
nitarudi tena nikipata chance,
 kwa kizungu kwa kiswahili ni nafasi,
Inatosha jamani Nasema basi.

Jicho Vumilia

Jicho Vumilia
Jicho langu mwenzio naamini kuwa wewe ndio kipimo cha utu wangu usipokuwa mvumilivu  utanifanya niwe mtu wa ajabu sana, nilo jisitiri kwa vazi zuuri la staha lakini nanuka uvundo wa fedheha.

Jicho langu wewe, ni wewe ambaye huona kwanza kabla unachokiona hakijajadiliwa na ubongo nakupenya moyoni.

Jana nilipita barabarani nikaona Gari, kwa hakika nisingejua kama ni zuri gari lile bila wewe kulitazama, jicho siunakumbuka vizuri kama ulikiponza kidole changu cha mguu sababu nilijikwaa kwa kushangaa gari lile.

basi sawa nilifurahi wewe kutenda uwezo uliopewa na mola wako lakini ilikuwaje mpaka ukatazama sana mpaka akili ikajenga mvuto wa hali ya juu wa gari lile,nikabaki naumia moyoni sababu sina hata shilingi moja yakuweza kununua gari lile.

nikapiga moyo konde nakuendelea na safari huku nikifariji moyo kwamba ipo siku nitakuja kumiliki gari lile.
hatua si chini ya kumi na Tano, mbele nikiwa nimeongozana nawe jicho ukisimama kama bakora inayoniongoza niendapo ghafla ukatulia kumtazama msichana wa haiba, mwenye mvuto usio semeka..nakumbuka vema shingo yake uliiona wewe kama ni ndefu mithili ya twiga, mpole kama mnyama huyo na hata mwendo wake ulikuwa ni kama mnyama huyo pia.

rangi yake yakiafrika ambayo uliiona wewe ilifanya mpaka moyo uende mbio ukijiambiza kuwa yule ni malkia wa kiafrika.

alivaa mavazi ya asili na nywele zake zilionekana kuwa na chuki na madawa yakuunguza nywele, sababu alikuwa amesuka kawaida sana, alisuka mnyoosho lakini nywele zake zilishiba rangi nyeusi na ziliniwiri kichwani.

Jicho wewe, jicho wewe! ulisita kabisa kuhama nakutazama kwengine, ulituwama kwa binti wa watu mpaka alipokuja jamaa ambaye dhahiri alionekana ni mchumba wake, ni wewe ndio uliona namna ambavyo jamaa yule alimtandika bakora za mabusu na kumkumbatia kwa hisia, huku nafsi za wote zikionekana kufurahia kukutana kwao.

ni wewe jicho ndio ulinifanya nione wivu nakutonesha kidonda cha moyo wangu ambacho kiliwekwa na mpenzi aliyenighilibu nakuniacha mpweke huku akienda kwa vijana wenzangu wenye kuvaa chepeo na nguo mlegezo,huku masikioni wakijipamba kwa hereni na kuzungumza kwa kupindisha mdomo wenyewe wakiita swagg.

Ni wewe jicho, ambaye licha ya kuona madhara uliyoyakabidhi kwa nafsi yangu kwa kukumbushia upweke bado ukaenda kushuhudia chumba cha mwenyeji wangu niliyekuwa namfata.

Jicho wewe!
ni kweli kile chumba kilikuwa kizuri mashaallah! lakini haikuwa vema wewe kutazama kwa hisia hadi kujenga tamaa ndani ya moyo wangu, niwewe ndiye ambaye ulifanya nikashusha thamani chumba changu kwa kukiona si lolote!
Jicho kuwa na ustahimilivu, tazama kidogo utosheke, utaendelea kunipa maumivu hadi lini, mwenzio sio vyote uvionavyo nina uwezo navyo. Kuwa na Uvumilivu tafadhali


NATAMANI..


Natamani leo hii nyote mniulize nini natamani ningewajibu natamani mniulize nini natamani na pale ambapo mngeniuliza nini natamani ningewajibu natamani vijana wote tusio na ajira tuwe na kauli moja tu, kauli ambayo tunaizungumza kwa pamoja kwa nia moja na tamaa ya aina moja, kauli ambayo kwa wengine ingesikika kwa mvumo wa nguvu na ingeeleweka kwa kiswahili ikitamka maneno LAZIMA TUJIAJIRI!

kauli hii sina shaka ingeanza kwa kuchekwa na waliovimba matumbo kwa ajira za upendeleo, wanaokalia viti vya ajira huku wakiwa hawana vigezo vya kuajiriwa, wanaoona urahisi wa maisha kwa donge nono la Ajira liitwalo KUPEANA!
Natamani

ningeelezea vema tamaa yangu kwa vijana wenzangu wanaohangaika mtaani wanaokumbwa na mgogoro wa ndani wa nafsi zao huku wakijilaumu kwa kutumia muda mwingi darasani wakisoma kwa mategemeo ya kuiokota muda wowote ile funguo ya maisha!
ningetamani sote tuongee lugha ya aina moja inayoakisi maisha yakujiajiri kwa kuwa wabunifu nakujitahidi kuleta ufanisi kuwazidi walioridhika na unafuu wa maisha ya ganda la ndizi.


ningetamani sana mniulize ninachotamani kwakweli ningeelezea vingi sana vya maana kuhusu kugeuka nyuma nakuupa mgongo mlango wa ajira uliofungwa bila kujua ni lini utafunguliwa hata kwa bahati mbaya!


ningezungumza kwa hisia sana na mwisho ningewataka vijana wote tusio na ajira tusikate tamaa sababu muda nao umeumbwa na kificho mara nyingi huficha siku,saa na mwezi wa mtu kuweza kuyasimamia maisha yake nakuwasaidia na wengine hivyo tusiache kufanya kazi kwa bidii huku tukijua ni mkosi na laana kubwa kukata tamaa!


ningepata nafasi yakuulizwa nami ningeuliza kabla ya kujibu KWANINI UKATE tamaa!? lala,amka,tembea,kaa fanya chochote ukiamini kuwa MTAJI WA MASIKINI NI KUJITUMA KWAKE kwa nguvu, maarifa na kumtegemea MUNGU!.
Mwisho kabisa ningewashukuru kwa kuniuliza swali zuri.
huku nikiwaacha mkiyatafakari yale ambayo ningewajibu endapo mngeniuliza natamani nini

Usiogope

Familia kuubwa ya bwana na Bibi WOGA  imekaa nje ya bustani ya kaya yao katika eneo lisilojulikana ni wapi hasa katika ulimwengu huu.
Bwana WOGA amekamata gazeti la serikali ya nchi yao anawasomea watoto wake na mkewe.
ukurasa wa juu kabisa wa gazeti lile uliandikwa "SERIKALI YAENDELEA KUTANGAZA VITA DHIDI YA MAENDELEO YA BINADAMU"
Mzee WOGA alisoma kwa furaha habari ile bashasha la tabasamu lilipamba uso wake wenye hila na wivu dhidi ya mafanikio ya mwanadamu.
serikali ya nchi yao ilitangaza vita zaidi dhidi ya harakati za binadamu kuyafikia mafanikio.
 gazeti lile liliandika mbinu zitakazotumika kufanikiwa kushinda vita ile, miongoni mwa waliokuwa makini kusikiliza habari ile ni mke wa bwana WOGA  aliyefahamika kwa jina la Bi.HOFU.
alikuwa ni mtu wa aina yake upole wake ulitiwa nakshi na wivu usio na msingi uliojidhihirisha usoni mwake kupitia pua yake ilioyotota vijasho na Inaelezwa kuwa hata chakula chake kilikuwa cha karaha sababu ya umoto pengine labda ile dhana ya wivu huweza kuashiriwa na umoto wa chakula upikacho ilijidhihirisha kupitia Bi HOFU.
usiogope
tumbo lake lilikuwa na rutuba na aliweza pata uzazi wa kike na kiume huku watoto wote wakike wakipewa majina ya MASHAKA na wakiume wakiitwa WASIWASI, watoto wao wote walirithi tabia na mienendo ya wazazi pamoja na jamii yao, walikuwa na chuki na mafanikio ya binaadamu licha ya kwamba walikuwa na utofauti mkubwa sana na binadamu.

wao hawakuwa na umbile maalumu na pia hawakuwahi hata siku moja kujitokeza mbele ya upeo wa macho ya mwanadamu yoyote hivyo Kusababisha wasijulikane hasa wapoje lkn walijaaliwa uwezo wakuishi ndani ya nafsi ya mwanadamu na kumjengea jumba la woga hasa anapotaka kujaribu kuonesha uwezo wake ama kupiga hatua za maendeleo, woga hujitokeza bila hata papara na taratibu hujichanganya na akili ya mwanadamu nakujenga sauti ya upole ambayo hujirudia mara nyingi ikitamka maneno kama haya "WEWE HUWEZI" "ACHA HIYO,WATAKUCHEKA" Na maneno mengine mengi kama haya.

hizo ndio hila za bwana na Bi hofu, huleta ugonjwa wa ajabu sana duniani, ugonjwa wakutojiamini kwa kuhofia kujaribu kukanyaga au kupita kwenye daraja linaloelekea kwenye ndoto zako!
mara zote serikali inayowaongoza kina woga imekuwa na kisirani cha visasi na kuleta sintofahamu ya udhaifu mkuu katika maamuzi ya mwanadamu hasa maamuzi yenye tija katika maisha yake.
Nimemega kwa usiri mipango yao na mipango hiyo inapangwa kila uchwao na jamii wanayoishi kina Bi Hofu...lengo lakumega siri hii ni ili wewe ujishtukie kuwa unatakiwa ukatafutie dawa kauoga kanakokuzingira nakukufanya usite kutimiza mipango yako!
umeshajiuliza ni kwanini ujipe sababu za kushindwa katika kila jambo? kwanini mipango yako mizuri haiamii kwenye vitendo? kwanini wengine wameweza walipojaribu na hivi sasa unawaita wenye mafanikio? eti umeshajiuliza unachoogopa ni nini?
waliofanikiwa katika dunia hii ni wale walioshindwa mara kadhaa katika maisha yao lkn mafanikio yao yaliletwa na imani kuwa wanaweza kujaribu tena na hata waliposhindwa walijaribu tena natena na mwisho wakaweza, hawakuogopa kuchekwa wala kitu chochote nafikiri waliusuta uoga tena suto la majivu ya moto..

woga ukaona haya na ukakaa mbali kabisa na harakati zao!
woga hauna lolote katika maisha yetu zaidi yakuturudisha nyuma.
Usiogope, ukitafuta sana katika dunia hii utagundua wapo ambao wana  mapungufu na hawakufikii wewe kwa  chochote lakini wamefanikiwa! wamewezaje unadhani!? walijiamimi na wakaamini wanaweza.
usiogope jaribu chochote kinachokuelekeza kwenye mafanikio mradi kiwe na utu na kisiharibu sheria zetu!

Tazama Tabasamu la Shaaban Robert

Kutazama sehemu ya kwanza ya Simulizi Zinaishi usiache kutembelea Youtube Chanel yetu kwa jina hilo hilo simulizi zinaishi link yakuitazama barua tuliyomuandikia Nguli huyo wa kiswahili ni hii hapa
https://www.youtube.com/watch?v=Z_RBWRZLqwE

Masikini Taaluma yangu

MASIKINI TAALUMA YANGU!
haionekani chanzo chakukumbata maovu.

   Alikuja akitokea kusipojulikana lakini kutokana na Taadhima aliyo nayo alipokelewa na kila mmoja wetu na akaheshimika vilivyo kwa kusadiki kila alichosema.

Hatukua na uwezo wakung'amua kila lililojiri lakini kutokana na upeo aliojaaliwa  mgeni huyo aliweza kuwaeka chini wooote wakubwa kwa wadogo nakuwapa habari, kuwaelimisha na walipochoka hakusita kuwaburudisha kwa mtindo ulio mzuri ambao kamwe haukuathiri tamaduni wala maadili yetu,

alijijua nguvu aliyo nayo katika kujenga ama kubomoa mtazamo wa jamii hivyo mara zote alihakikisha anafikiri kabla yakusema.

pengine kutokana na hili ndio maana aliaminika sana na enzi hizo mimi mdogo niliamini yeye anajua kila kitu duniani hapa kumbe laa, hakua anajua bali alikuwa ni mfuatiliaji na alichunguza neno kabla yakuliibua kwa mapana yake.

Nakumbuka vema alikuja akiwa amejisitiri kwa vazi lililomficha vema maungo yake, alikuwa mwingi wa aibu katika kuzungumza uongo hivyo uongo ukajitenga nae kabisa, alikuwa makini sana katika kuongea maana alijijua kuwa angeweza kuleta vita palipo na amani na mapigano palipo na maelewano.

Aliishi nasi kwa upendo mno, alikuwa mtaratibu na alitushauri njia yakupita pale tuliposita kupiga hatua,

sina shaka anakuvutia sana mgeni huyu aitwae Taaluma Yangu, pengine hata ulitamani kuwa yeye, ajabu yake anayo njia yakukufanya uwe kama yeye, kwa hakika ameumbwa kwa namna yake.

Katika maisha yake duniani wapo ambao walitaka kumpima imani, walitaka kumuondoa kwenye njia aipitayo na msimamo aliyokuja nao, nina uhakika mpaka leo kama wangali hai wanajutia maamuzi yao au kama wamekufa wanatumikia adhabu zao kwa maana walisababisha damu za watu wengi sana kumwagika na mauaji yale yakapewa jina na bado yanakumbukwa mpaka kesho.

yalikuwa maujai ya watu wengi ni nani wakuweza kuifuta historia ile? lakini chanzo chake  kilikuwa ni watu kugeuka nakutaka kulazimisha mitazamo yao badala ya kuheshimu mtazamo wa mgeni Taaluma Yangu..

Masikini Taaluma yangu hii leo anapakwa shombo la kuipotosha jamii kimaadili, analazimishwa kutangaza tamaduni ambayo iliangamiza kabisa kizazi kimoja wapo enzi za kale.

pesa inalazimisha kuvua vazi la staha la Taaluma Yangu, inataka kuacha maungo yake wazi yachunguliwe na watoto na wakubwa, Masikini Taaluma yangu inalia kwa uchungu ikitamani kurudi itokapo.

Inajutia inapobaini kuwa inataka kufanywa chanzo cha kuidhinisha dhambi iliyopingwa na wazazi wetu ambao hawakutaka hata sekunde kujadili dhambi hiyo, ambayo ni chafu na aibu kwa walio na busara, Taaluma yangu inalalama nakusonona ikilaumu jinsi wanaoiendesha kutaka kusababis
inapaza sauti yake thabiti lakini sauti hiyo haitoki vema imezuiliwa na vumbi la uchafu wa pesa lakini ukiisikiliza kwa makini sauti yake inasema MIMI SIPO HIVYO MNAVYOTAKA NIWE, lakini ni nani wakuisikia sauti hii inayozibwa isisikike?

MASIKINI TAALUMA YANGU!