Sitothubutu kusema huna akili ingawa matendo yako yananithibitishia hilo.
kwanza tulipendana,
pili tukazoeana,
tatu tukakerana
hatimaye tukaachana.
mazoea yakaniadhibu,
nikakumbuka ukaribu,
nikarejea kwa aibu,
kuomba uje unitibu,
mashaallah hukunighilibu,
ukarudi kwangu tabibu.
maisha yakaendelea,
penzi kiraka nikizoea,
baadae nikagundua,
ni adha nimeikaribia
dharau nimejijengea,
upuuzi nimeurejea.
kitu kimoja hujajua,
mie ni yule wa mwanzo.
sifai kulumangiwa,
kuteswa kwangu tatizo,
Kamwe sitofurahia,
kugeuzwa chotezo.
maneno yangu rejea,
mimi sio wa mchezo,
kamwe sitokurudia,
huu ni msisitizo.
Huu moyo ni mashine,
hukoboa na kusaga.
moyo wangu usiupime,
usitake kuuiga,
kulifuga pakashume,
bora kusugua gaga..
unyayo wako ung'ae,
na wengine wataiga.
ni heri nikose vyote,
kuliko ile heshima.
sina sababu yoyote,
kwako wewe kusimama.
umenivua nguo zote,
muungwana nachutama.
likiisha jua lote,
gizani ntasimama.
ntajistiri chochote,
nafsi yangu itatuama.
utenzi umenijia
bila ya kudhamiria,
faraja kukuimbia,
moyoni najivunia,
hasira zanikimbia,
maumivu kadhalika.
lakini nakuambia,
utakuja nikumbaka.
Maamuzi kama ni yako,
itakuwa afadhali,
ila kama ni tamaa yako,
umejipiga kabali,
mbeleni pumzi yako,
itakosa kuvinjari,
utageuka kituko,
mauti kukukabili
yatakupiga kikumbo
yote sababu kiburi.
sithubutu tema lana,
sababu itakupata,
nilikupenda kwa sana,
iweje uje nitupa,
ama ndio uungwana,
kulipa baya kwa jema.
acha nisiseme sana,
nitawapa lakusema,
wale wengi wafitina.
ubeti natamalai,maishani tutaonana
Yani we Binti. |