kusema ni kujiumiza mwenyewe sababu mengi yamepita na kwangu yamebaki historia Sitasema kamwe kuwa ni mimi ndie nilikuwa chanzo chakuachana nawewe! sitasema sababu ni fedheha sio tu kwa ndugu zangu hata wazazi wako na mara ya mwisho kuongea na mama yako ni leo, sauti yake yaucheshi bado inaendelea kuniita mkwe sikuweza kumwambia kuwa umenifumania na umeumia sana na hautaki hata kuniona!
Sitasema kamwe |
Nimejaribu kungoja siku mbili zipite baada yatukio lile labda utarudi ama utapokea simu yangu lkn wapi, nasikia hutaki hata kusikia jina langu na kwasababu ya maumivu umeamua kuacha kazi nakuhama mji sijui unaishi wapi kwasasa!
Sitasema hata kwa bahati mbaya kwa marafiki zangu ambao wamezoea kukuita shemeji tena mbaya zaidi muda mchache uliopita nimesoma meseji ya Swahiba angu Sosi akiuliza kama hujambo mbona hupatikani kwenye simu eti anadai amekumbuka sana utani wako!
Siwezi kumwambia na Sitasema kuwa nimekukorofisha sababu ni aibu kubwa kwangu kumpoteza mwanamke wa heshima kama wewe! ni aibu sababu mahusiano ya wengine wengi yalikuwa yakienda kwa kuakisi mahusiano yetu iweje nimekuwa mjinga kiasi hiki mpaka kuhadaika na binti mwengine ambaye kimsingi hamfanani hata kidogo, yeye tulipokuwa tukikutana alikuwa anaomba pesa hata zisizo za msingi wakati wewe ulikuwa ukinishauri namna yakuongeza kipato kwa maisha yetu ya baadae. Dah! sio kwa aibu hii kwakweli!. naapa sitasema na kama nikifanikiwa kukutana nawe nitakuomba msamaha nakukusisitiza sana usije ukasema, nakiri ujana ni maji yamoto na haya yameniunguza, nimebabuka mwili mzima na sina wakumlaumu sababu kilicho niponza ni tamaa na ujinga wakutumia kitanda chako kusaliti Uaminifu wako kwangu!
nani nitakaeweza kumtazama nakumwambia kasoro yangu hii. na zaidi nakuwa kitanzini sababu ni mwezi mmoja tu umepita tangu ukute ujumbe mfupi kwa mdogo wako akiwasiliana nimimi nakusifia uhodari wangu kunako uwanja wa fundi seremala! ulidhihiri kuwa nimetoka na nduguyo lkn nikakupiga kiswahili ukanisamehe huku ukinisihi nisikuumize, nilishukuru Mungu msamaha huo huku nikiustaajabia moyo wako sababu kabla ya hapo uliwahi kunisamehe mikosa isiyo na idadi likiwemo lile lakunifuma bafuni nikiwa na mke wa jirani yangu Baba Emi. ulizuia mdomo wako usipayuke kujaza watu, ukatuhifadhi sana mimi na Mama Emi nakumbuka uliwahi sema aibu yako niyangu hivyo hutathubutu kunijazia watu na mwisho ukanisamehe! Sitasema haya sababu kuyasema haya nikujivua nguo mwenyewe! ingawa siachi kumuomba mungu nisije pata habari ya kwamba umejizuru huko ulipo. nahisi baraka zakujisahihisha zimenikumba sitahadaika na ujana tena rudi mchumba tuyajenge maisha.
sitasema naomba nawe usiseme sababu ni aibu kwakweli.
2 comments
commentsSimulizi sahihi kaka, keep focus ni muandishi bora.
ReplySimulizi sahihi kaka, keep focus ni muandishi bora.
Reply