unamuumiza sister angu bhana, dah! halafu samahani
Unamuumiza dada 'Angu |
Dada alifuruhi sana alipojua dhamira yako kuwa ni njema hutaki kumchezea unataka kumuoa lakini tambua kuwa hakuwa anajua kuwa kila tabia mbaya unayo na nina uhakika angejua asingetoa machozi ya furaha siku ile ya send Off pale kwenye ukumbi mkuubwa wa Majengo In kule Muheza Tanga.
Shem si niwewe ndio ulijifanya mwema kipindi unakuja kutoa posa kila jambo ulimuhusisha MUNGU na maneno kama Inshaallah ukiyatamka kila saa!
iweje hivi sasa hata dada nywele zimempauka zikitaka kuandamana kwa kukosa matunzo.
kumbuka hujamkuta ivo sista basi ruhusu hata aibu ikuingie!
Sitaki kuamini kabisa kuwa eti saivi ule uchamungu haupo tena loh! kweli wewe ni muigizaji siniwewe ndio ulikuwa ukitupa vifungu mbalimbali kutoka kwenye vitabu vya dini!!
Acha zako bhana shem unazingua kinoma kwa unayofanya kwa sister au kisa unajua kama ndio kwako keshajifia, watoto keshakuzalia na kila namna ushamtumia?.
yeye mwenzio hakujua hilo alijua akiolewa nawe atayaona anayofanyiwa mama etu na Dingi, watu wanasema wanaume wote baba mmoja mama mmoja ila wewe baba na mama yako itakuwa ni shetani yani mpaka kulisha familia umeweka zamu na sister.....sio poa!
Mimi kuwa mume Bora Nimejifunza kwa Mzee wangu yeye hakuwa kama wewe, mkewe aliponuna alienda nunua cd za Mzee Majuto ili acheke.
na alipoona amezingua alikuwa mwepesi kuomba msamaha na hata siku moja sikuona akikimbia majukumu yake kama mume! we mwenzetu vipi nasikia mzito mpaka kutoa ada za wajomba.
mbona lakini unajimudu tu kifedha shemeji au ndio kuna kimada amekudhibiti ndio mana dada angu unamuona dampo.
acha zako bhana me sifagilii wala nini pigo zako,
hiyo michozi inayomtoka sister tambua kuwa ikidondoka chini inatimua vumbi la lana.
mbona lakini unachafua sifa zetu vijana wa leo tuonekane wote makuzi we unadhani sister akikaa na mashoga zake anaongea nini kuhusu wanaume! achana na izo habari bhana tafsiri ya mwanaume kamili sio ubabe, wala kubadili wanawake kama nguo ili mwanamke akuone mwanaume kamili unapaswa kuijua thamani yake, kuiheshimu, kumjali na kuisimamia furaha!
unanisikia shem? hayo unayoyafanya unasababisha mpaka mchumba angu aanze kusita kuolewa nami akihisi ndoa ni ndoano na wanaume wote ni wanyama!
kama umenielewa fanya ivi sasa,
Rudi maskani, hujaacha pesa yamatumizi..mkeo kuna dera anatamani af amemis ule ucheshi na upendo wako uliomuonesha kabla hujamuoa..
nenda haraka ukatimize hayo mimi wiki ijayo nafunga shule nikija likizo nikute amani ndani ya nyumba yenu laa sivyo nitafanya juu chini nimlaghai mdogo wako yule wamwisho kwenu kuzaliwa, yule binti mpole mpole, akiingia kwenye kumi na nane zangu nahakikisha baadae namuoa kisha namfanyia unayomfanyia dada angu.
Tuone kama utafurahi!
Tafsiri ya misamiati iliyotumika
Sister - Dada
Bhana - Bwana
Ntakuchana - Nitakwambia ukweli
Send Off - Sherehe ya Kutambulishana ndugu wa pande mbili wa bwana harusi na bibi harusi
Shem - Kifupi cha neno shemeji
Inshaallah - Apendapo Mungu
Ivo - Hivyo
saivi - Sasa hivi
unazingua -Hautendi sawa
kinoma - Iliyopitiliza
keshajifia - amependa sana
Dingi - Baba
Sio Poa - Sio vizuri
Sifagilii - Sikubaliani
Pigo zako - Mwenendo/ tabia zako
Makuzi - Kutokueleweka
Dera - Gauni kuu kuu la wanawake
Amemis - Amekumbuka
Kumi na nane zangu - Himaya yangu
Ahsante kwa kusoma!
bin Zongo.