Nikajikuta nasoma kwa ubabaishaji sana leo hii hapa natamani nipewe kipaza sauti chenye nguvu yakusikika maeneo mengi nchini Tanzania hasa kwa watoto washule ambao wazazi wao masikini kama alivyokuwa mama yangu mimi ningewakemea kwa sauti nakiwasihi wasome wasioge kamwe kwenye bahari ya huba kwani mawimbi yake yatawazamisha kwenye tope la ujinga na hata waweze kupuuza elimu ambayo ni muongozo thabiti!
mimi sijasoma sana na ndio mana leo nalalama sababu sitaweza kukuthibitishia kisomi kwa kukuletea tafiti nilizofanya zikakuonesha kuwa MAPENZI HUDUMU KUTOKANA NA UONGO!
lakini huo ndio ukweli, bila uongo mahaba hayana uhai!
kabla sijakuelezea hisia zangu kuwa nakupenda nakumbuka nilimsikia rafiki yako akisema kuwa wewe unavutiwa sana na kijana mcha Mungu, na ndipo hapo nami nikaanza kubeba lozari na biblia huku salamu yangu popote hasa mahala ulipo ikiwa ni "Bwana yesu asifiwe"
ukweli ni mapenzi yangu tu mazito juu yako lakini mimi sio mkristo kabisa! unafiri ningefanyaje sasa ili kuuridhisha moyo wangu ambao unaniamrisha kila siku nikupende! ilikuwa ni lazima nikudanganye.
mimi pekee mtaani kwetu ndio nilikuwa mgeni na mtu pekee kuanza kuzoeana nae ni MPOLE kumbe wewe hupatani kabisa na MPOLE pamoja na marafiki zake nilipokuja kujua hili nikaachana kabisa na MPOLE nikaunga urafiki na MUONGEAJI ingawa ukweli ni kwamba mimi sikumfurahia kabisa MUONGEAJI na marafiki zake sababu mara zote walipenda kuzungumza mambo kuwahusu wao lakini ningefanyaje ilibidi siku ile yakwanza kuongea nawewe nikwambie kuwa wenzangu mimi ni MUONGEAJI na wenzake nalikumbuka tabasamu lako ulilonipa baada yakusikia kua mimi ni miongoni mwa kampani ya MUONGEAJI nafsi yangu ilinisuta sababu huo sio ukweli lkn ningefanyaje sasa kama sio kutumia uongo huo.
nakumbuka siku ile hata tabia niliiga ya MUONGEAJI mara zote nilijisifia na kujiongelea na ndipo nilipofanikiwa kuziteka hisia zako Uongo wangu ulinifanya nikupate, Acha tu nikuongopee sababu uongo kwa sasa ni mbinu kuu katika mapenzi nami sipo tayari kukupoteza!
nidanganye nawe usije ukaniambia ukweli sababu nimevutiwa nawe kwa umbo, rangi na ongea yako kumbe ukweli hivi vyote sio vyako! umbo lako lakweli nimeliona kwenye picha zako za shule ya sekondary kumbe hili umenunua kwa mchina asante kwa kunidanganya, nimeridhika! haitoshi rangi yako kumbe ni muafrika kabisa lkn kutokana namimi nimeharibiwa na tamthilia za kizungu nikajikuta nataka mweupe na nilipokuona nikaona nimepata kumbe ni uongo wako mama, hongera.
Acha Nikudanganye |
naomba ridhaa mchumba tupitishe uongo uwe ndio ngao ya penzi letu sababu ni unafiki kujifanya hatudanganyani wakati penzi letu linazidi kuimarika kila uchwao kutokana na kuongopeana kwetu.
ni mimi ndio nilijifanya nimefiwa na babu yangu mzee Ally kule udigoni kwetu sababu ilikuwa ni sherehe yako yakuzaliwa nami sikuwa hata na pesa yakukuzawadia hata pipi sa unadhani ningefanyaje kama sio kumuua babu yangu kwa mara ya pili maana alishafariki miaka miiiingi iliyopita.
nashukuru ulinielewa nawe ukanidanganya
umeahirisha party kumbe ukweli ulifanya kwa mtindo wa kwenda mziki na mashosti zako! uongo umesababisha tuone tunathaminiana kwakweli....naomba tuendelee kudanganyana kwakweli sababu sitakuwa tayari kuusikia ukweli wa kwamba siku ile ulitoka na bosi wako wakati me ulishaniambia siku ile mlikuwa busy sana ofisini kwenu na hakukuwa na mwanaume mlikuwa wasichana tupu na bosi wenu alikuwa nje ya nchi kikazi...
NAOMBA UAMINI UONGO WANGU MCHUMBA KAMA NIFANYAVYO ILI KUDUMISHA PENZI LETU LIFIKE MBALI NA IKIBIDI TUOANE.