nalijua hili na wala sina haja yakuelezea sana labda tu kuongezea nikwamba hata nikitoka na washkaji zangu mavazi yangu yakawaida sana jamaa wanakuwa wamependeza na hii ni mara zote sio tu siku moja moja, najijua sina mvuto ndio mana pia napaza sauti nikikunyooshea kidole nakukwambia NAKULAUMU WEWE!
Nakumbuka siku ile mimi na rafiki zangu tunaingia mlimani city wewe na rafiki zako mnatoka, mmependeza zaidi wewe unaonekana kuwazidi wenzio hasa umbile lako la mchoro, sura yako ya haiba na mavazi yako ambayo nakiri yalitiwa dosari na usasa lkn kwavile mwenyewe wakisasa sikuzingatia hilo nilibaki nikijiambiza "hakika amependeza yule dada"
nilijiambiza hivo huku nikikubaliana na hali yangu kuwa siwezi kumiliki mrembo kama wewe labda rafiki zangu yeyote yule sababu wao walikuwa na nyota za wadada, wasichana walijigonga kwao vibaya na nilikuwa nimeshazoea wasichana wazuri kuwaita shemeji sababu hata kipesa jamaa zangu niliwaita "kaka".
pale yenyewe mlimani city niliwasindikiza wao walikuwa wanajiandaa na safari ya nje ya nchi kula bata!.
Nakulaumu wewe sabau haya yote mimi nayajua na nilikushangaa sana siku ile uliponisimamisha mimi nakuwaacha wao, uling'ata kucha, ukanikonyeza kabla yakuniomba namba!.
nakumbuka nilitaka kuondoka nikihisi unanichora kumbe masikini ya mungu ulinipenda kweli!
nakumbuka rafiki zako walitaka kukuacha lkn wewe haukujali ulichohitaji ni mawasiliano yangu.
Nakulaumu wewe na wala usijali utafahamu tu kwann hili rundo la lawama nalishusha kwako, nakumbuka ulinitamkia wewe unanipenda na hata nilipokujibu nakupenda pia nilikuwa bado nina hisia kuwa unanidhihaki, nilijihoji sana iweje msichana uliye na neema ya urembo unipende kituko mimi!.
Nakulaumu wewe! |
ulinionesha penzi ambalo lilikuwa geni kwangu nikastaajabu, iweje nisikamatike kimahaba tanga nije nikamatike dar!
ukanipa heshima ya mume huku ukiongelea kila saa suala la mimi kukuoa loh! Mimi huyu nikuoe wewe!! utani gani huu unaniletea!? nilikuwa siachi kujiuliza.
ilichukua muda kukuzoea kwakweli nilikuwa mtumwa wa fikra zangu mwenyewe ingawa baadae
nikakuzoea...! nikakuona wakawaida,
lile wazo la kwamba mimi sio aina yako nikaliona la kijinga na rafiki zako waliokuwa wakikusema nikahisi nao wananitaka,
nikaanza kuwatongoza lkn walinikatalia wote tena mbaya zaidi walikuwa wanakuja kukwambia huku wakikucheka nakukusihi uniache sabahu sifanani nawewe, hukuwa unawajali!
hakika mapenzi ni uchizi! uliendelea kunipenda hata nilipoanza jeuri nakukuongelea maneno ya shombo we ulizidi kukolea nami haukuchizika hata kidogo na wenye nazo walokufata kila uchwao wewe uliapa kufa nami.
nakulaumu wewe sababu ulinifanya nijisahau kuwa nimekupata kwa bahati, ukanipa kiburi hata nilipotaka kuachana nawe ukawa unatishia kujiua ama kweli kILA SHETANI NA MBUYU WAKE.
najutia sasa na nakulaumu sababu kero zangu zilipozidi ukaamua kuniacha nakwenda kwa jamaa aliyekuwa akikuonesha heshima niliyokunyima,
jamaa alikuwa akikubembeleza kituoko mimi nilipokuliza, jamaa aliwaza kukuoa wakati mimi nikifurahia kukuchezea nakukuburuza kama mzoga, ulikuwa una haki yakuniacha lakini tambua kuwa imekuwa chanzo chakurudiwa na ufahamu wangu.
nimegundua sasa kuwa mimi si chochote hata na hata kama ingetokea siku ile mimi ndio nakupenda wewe usingenikubali hata kidogo sababu sina sababu ya wewe kuwa namimi,
nafikiri ulinipenda kwa dhati, haukupenda pesa sababu ni ukweli kwamba pesa sina, wala hukunipenda mvuto sababu ni wazi kuwa mvuto sijajaliwa lakini ajabu sana niliyasahau haya nikajiona mimi ndio mimi handsome boy, kidume.
kumbe kituko kama walivyokuwa wakiniita wenzio nilijishau sababu ya upendo wako nikajiongopea kuwa kama wewe umeweza kunipenda basi naweza kumpata yoyote yule nae akanipenda NAKULAUMU WEWE, kwann unifanye nijisahau nijione nina pesa kumbe ulikuwa unajipendezesha mwenyewe, nijione nina mvuto kumbe ni upendo tu na mara zote upendo hauna desturi yakutaka kujua sababu!
NAKULAUMU WEWE SABABU UMENIFANYA NIJIONGOPEE!
nakiri mimi ni mjinga na huu ujinga ndio unanituma nikulaumu wewe!
"Mapenzi ni zaidi ya ukifikiriacho, ukipendwa pendeka. Usije ukamlaumu mwenzio siku moja akiweza kukuacha!"