NATAMANI..


Natamani leo hii nyote mniulize nini natamani ningewajibu natamani mniulize nini natamani na pale ambapo mngeniuliza nini natamani ningewajibu natamani vijana wote tusio na ajira tuwe na kauli moja tu, kauli ambayo tunaizungumza kwa pamoja kwa nia moja na tamaa ya aina moja, kauli ambayo kwa wengine ingesikika kwa mvumo wa nguvu na ingeeleweka kwa kiswahili ikitamka maneno LAZIMA TUJIAJIRI!

kauli hii sina shaka ingeanza kwa kuchekwa na waliovimba matumbo kwa ajira za upendeleo, wanaokalia viti vya ajira huku wakiwa hawana vigezo vya kuajiriwa, wanaoona urahisi wa maisha kwa donge nono la Ajira liitwalo KUPEANA!
Natamani

ningeelezea vema tamaa yangu kwa vijana wenzangu wanaohangaika mtaani wanaokumbwa na mgogoro wa ndani wa nafsi zao huku wakijilaumu kwa kutumia muda mwingi darasani wakisoma kwa mategemeo ya kuiokota muda wowote ile funguo ya maisha!
ningetamani sote tuongee lugha ya aina moja inayoakisi maisha yakujiajiri kwa kuwa wabunifu nakujitahidi kuleta ufanisi kuwazidi walioridhika na unafuu wa maisha ya ganda la ndizi.


ningetamani sana mniulize ninachotamani kwakweli ningeelezea vingi sana vya maana kuhusu kugeuka nyuma nakuupa mgongo mlango wa ajira uliofungwa bila kujua ni lini utafunguliwa hata kwa bahati mbaya!


ningezungumza kwa hisia sana na mwisho ningewataka vijana wote tusio na ajira tusikate tamaa sababu muda nao umeumbwa na kificho mara nyingi huficha siku,saa na mwezi wa mtu kuweza kuyasimamia maisha yake nakuwasaidia na wengine hivyo tusiache kufanya kazi kwa bidii huku tukijua ni mkosi na laana kubwa kukata tamaa!


ningepata nafasi yakuulizwa nami ningeuliza kabla ya kujibu KWANINI UKATE tamaa!? lala,amka,tembea,kaa fanya chochote ukiamini kuwa MTAJI WA MASIKINI NI KUJITUMA KWAKE kwa nguvu, maarifa na kumtegemea MUNGU!.
Mwisho kabisa ningewashukuru kwa kuniuliza swali zuri.
huku nikiwaacha mkiyatafakari yale ambayo ningewajibu endapo mngeniuliza natamani nini

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »