kwanini unataka kunipa dhambi yakukuwazia vibaya rafiki yangu wa damu?
kwanini unataka kununua bure kabisa ubaya usio na faida yoyote ule?
Eti kwanini |
niambie basi kwanini lakini unajaribu kuipima roho yangu ukionesha kupinga kuwa mimi ni mwema kwako?
kwanini unanilipa malipo ambayo sistahili kulipwa na rafiki niliyemuhifadhi kwenye chumba kilicho jirani na ndugu zangu!
kwanini unaupa sababu ulimi wangu utamani kutamka maneno yaliyo na lawama kwako!
jipe muda basi utafakari tena labda pengine umekosea ulichokipanga kwangu tafadhali sana tafakari na ujisahihishe sababu wapo ambao nahisi wanastahili kunifanyia hivi lakini sio wewe!
nakupa nafasi tafakari naamini utaona kuwa sistahili kutendewa hivi nawewe!
sononeko langu litakugharimu, hivyo ndio naamini sababu ukatili wakulipiza ovu sijafundishwa naongozwa na imani ya kwamba utalipwa kwa matendo yako!
Nashukuru kwakutokuwa mkamilifu kwangu sababu umenifanya nitumie sanaa kuelezea hisia zangu! ila upatapo ujumbe huu naomba sana nafsi yako ikusute na uikaribie toba!.
bado sijakushutumu wala kukuhukumu kilicho na utayari nafsini mwangu ni msamaha wa bure kabisa sababu nami sijakamilika pengine baada ya hapa naweza kufanya uliyo nifanyia kwa mwengine ingawa kwa jinsi ninavyojisikia nitakesha nikiomba nisimtendee mwenzangu haya ulioyatenda kwangu.
ingawa ni dhahiri kabisa NIMEKUSAMEHE sababu muumbaji ni MUNGU sisi binaadamu ni wamiliki tu na hatuna silaha yakutosha kulinda alivyotugawia muda wowote huweza kutupa nakutunyang'anya akipenda.
Bado nafsi yangu inayumbishwa na simanzi lakutokuamini pengine labda utanisaidia kuondoa kadhia hii ulinijibu KWANINI RAFIKI YANGU UMEGEMUA GOME LA UTU WANGU KWAKO?.
"Maswali unayojiuliza nakujijibu kuhusu ujumbe huu ndio adhma yangu kama mwandishi" Bin Zongo
kwanini???