Simulizi Zinazopatikana ndani ya jukwaa hili zote Zinaishi na lugha adhimu ya kiswahili ndio pumzi yake!
TAFAKARI,BURUDIKA, JIFUNZE,
AUDIO YA SIMULIZI JICHO VUMILIA
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Hii ni moja ya simulizi yangu BORA niliyoiteua kwa mwaka uliopitwa inaitwa JICHO VUMILIA, isikilize kwa sauti nikikusimulia kwa Utashi na weledi wa hali ya juu..
SEHEMU YA KWANZA ''Ni kawaida kwa hadithi nyingi pendwa kuwa na sehemu ya kwanza na sehemu ya pili na nyengine nyingi zenye mfululizo wa visa vya kusisimua, lakini ukweli wa mambo ni kuwa hali ni tofauti katika mapenzi, Hadith ya mapenzi inayonoga zaidi ni ile ya sehemu ya kwanza, ukiiharibu kwa kudhani kuwa utapata sehemu ya pili ni kosa kubwa sana ni sawa na ufa usioweza kurekebishika'' HII HADITH HAINA JINA INAITWA SEHEMU YA KWANZA NA SEHEMU YA PILI..... NI KISA CHA MAPENZI ..... Na Bin Zongo Mapenzi yamekolea hakuna aliyeona kero kwa mwenzie, kila mmoja anaishi kwa amani na hutabasamu kila wakati akikumbuka uwepo wa mwenzake. marafiki zao walikuwa wanawaona machizi mana walipokuwa mbalimbali kila mmoja alikuwa busy na simu yake akichart na mwenzake nakucheka cheka kila saa kama chizi mpya aliyepelekwa kituoni kwa matibabu. mapenzi yao yalikuwa yanavutia kama mapenzi ya kitabuni, yalifanya kila mmoja kati yao aone thamani yakuzaliwa kwake, nafs...
''Zawadi ni chachu ya mahusiano ya aina yoyote ile, mzawadie ulicho nacho yule ambaye unahisi ni sahihi kuzawadiwa nae, naamini tabasamu lake usoni ni ishara tosha yakufarijiwa na zawadi uliyompa, kuna aina nyingi za zawadi, lakini katika mapenzi Maneno matamu ni zaidi ya zawadi zote unazozijua wewe, waswahili huamini NENO HUUMBA......'' UTENZI WA MAHABA Na Bin Zongo leo nachana kifua nautoa moyo nje nataka kuyaachia yalo ndani uyaone si joto wala baridi ni wastani kipupwe leo nataka kuahidi ukweli wangu nikupe kupenda kama umbea masuto nastahili naapa sitokimbia majivu ntayakubali laa kupenda ni homa matibabu weka mbali nataka kuumwa homa joto mwili liwe kali mapenzi kama ugali mpunga mie wanini sitaitaka zohari mahindi weka chumbani kupenda jambo geni sijawahi kabla yako naapa kwa rahmani nafsi yangu mali yako mwenzako kwetu pwani kudekeza nimefunzwa kuoga nawe bafuni Tanga nimesisitizwa kupiga ni ukatili u...
MTUNZI : BIN ZONGO Jina Lake aliitwa Jef alikuwa ni mrefu kwa kimo umbo lililoshiba na sura yake haikuwa ya mzaha . Maisha yake yalikuwa mtaani, nguo zake zilimtambulisha kwa yoyote kuwa hakuwa timamu kiakili. alizoeleka kuongea peke yake na kujichekesha mwenyewe bila sababu ya msingi. alikuwa ni mwendawazimu lakini uzuri wake hakuzuru watu wala kugombana nao yeye alipenda kuwachekea na kila gari na nyumba nzuri aliyoiona alijinasibu kuwa ni ya kwake. alipenda sana kuzungumza na watoto wadogo ambao wengi walimzoea jef nakumfanya rafiki. bila shaka wazazi wa watoto wale walithibitisha kuwa Jef hakuwa mwendawazimu wakudhuru watoto ndio maana wakawaacha watoto wao wacheze nae kutwa nzima ingawa pia walikuwepo wazazi waliokuwa wakihofia kuwaacha watoto wao na Jef. wakihisi kuwa ipo siku atazidiwa na uchizi awafanye kitu kibaya. Pengine labda isingekuwa Rafiki yake jef aitwae Salim hata pia nisingepata lakusimulia kuhusu Jef. ni Salim ambaye alijaribu kuelezea ...
Comments
Post a Comment