Masikini Taaluma yangu

MASIKINI TAALUMA YANGU!
haionekani chanzo chakukumbata maovu.

   Alikuja akitokea kusipojulikana lakini kutokana na Taadhima aliyo nayo alipokelewa na kila mmoja wetu na akaheshimika vilivyo kwa kusadiki kila alichosema.

Hatukua na uwezo wakung'amua kila lililojiri lakini kutokana na upeo aliojaaliwa  mgeni huyo aliweza kuwaeka chini wooote wakubwa kwa wadogo nakuwapa habari, kuwaelimisha na walipochoka hakusita kuwaburudisha kwa mtindo ulio mzuri ambao kamwe haukuathiri tamaduni wala maadili yetu,

alijijua nguvu aliyo nayo katika kujenga ama kubomoa mtazamo wa jamii hivyo mara zote alihakikisha anafikiri kabla yakusema.

pengine kutokana na hili ndio maana aliaminika sana na enzi hizo mimi mdogo niliamini yeye anajua kila kitu duniani hapa kumbe laa, hakua anajua bali alikuwa ni mfuatiliaji na alichunguza neno kabla yakuliibua kwa mapana yake.

Nakumbuka vema alikuja akiwa amejisitiri kwa vazi lililomficha vema maungo yake, alikuwa mwingi wa aibu katika kuzungumza uongo hivyo uongo ukajitenga nae kabisa, alikuwa makini sana katika kuongea maana alijijua kuwa angeweza kuleta vita palipo na amani na mapigano palipo na maelewano.

Aliishi nasi kwa upendo mno, alikuwa mtaratibu na alitushauri njia yakupita pale tuliposita kupiga hatua,

sina shaka anakuvutia sana mgeni huyu aitwae Taaluma Yangu, pengine hata ulitamani kuwa yeye, ajabu yake anayo njia yakukufanya uwe kama yeye, kwa hakika ameumbwa kwa namna yake.

Katika maisha yake duniani wapo ambao walitaka kumpima imani, walitaka kumuondoa kwenye njia aipitayo na msimamo aliyokuja nao, nina uhakika mpaka leo kama wangali hai wanajutia maamuzi yao au kama wamekufa wanatumikia adhabu zao kwa maana walisababisha damu za watu wengi sana kumwagika na mauaji yale yakapewa jina na bado yanakumbukwa mpaka kesho.

yalikuwa maujai ya watu wengi ni nani wakuweza kuifuta historia ile? lakini chanzo chake  kilikuwa ni watu kugeuka nakutaka kulazimisha mitazamo yao badala ya kuheshimu mtazamo wa mgeni Taaluma Yangu..

Masikini Taaluma yangu hii leo anapakwa shombo la kuipotosha jamii kimaadili, analazimishwa kutangaza tamaduni ambayo iliangamiza kabisa kizazi kimoja wapo enzi za kale.

pesa inalazimisha kuvua vazi la staha la Taaluma Yangu, inataka kuacha maungo yake wazi yachunguliwe na watoto na wakubwa, Masikini Taaluma yangu inalia kwa uchungu ikitamani kurudi itokapo.

Inajutia inapobaini kuwa inataka kufanywa chanzo cha kuidhinisha dhambi iliyopingwa na wazazi wetu ambao hawakutaka hata sekunde kujadili dhambi hiyo, ambayo ni chafu na aibu kwa walio na busara, Taaluma yangu inalalama nakusonona ikilaumu jinsi wanaoiendesha kutaka kusababis
inapaza sauti yake thabiti lakini sauti hiyo haitoki vema imezuiliwa na vumbi la uchafu wa pesa lakini ukiisikiliza kwa makini sauti yake inasema MIMI SIPO HIVYO MNAVYOTAKA NIWE, lakini ni nani wakuisikia sauti hii inayozibwa isisikike?

MASIKINI TAALUMA YANGU!

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »