KALAMU YAGOMA

Napata wazo jipya nalitafakari kwa undani wake naona lafaa niliweke kwa maandishi ili walau liwafae na wengine maishani, katika kuumbwa kwangu vingi sana nimenyimwa ikiwemo choyo na ndio mana siweki ndani hata siku moja hadhina ya nikiandikacho nakigawa kwa wengine ili wakonge nyoyo nakulisha bongo zao pia!

sasa Nawezaje kuliweka wazo langu kimaandishi?

swali hili zuri lanifanya niikumbuke marafiki zangu kalamu na karatasi nakurupuka kuwafuata sababu jamaa zangu hawa hawakai mbali, makaazi yao ni mezani na yapo jirani kabisa na maskani yangu maarufu iitwayo Kitanda hatua si zaidi ya nne nafika mezani.

kwa mara ya kwanza kabisa nagundua tabia za jamaa zangu kalamu na karatasi, tabia ambazo siku zote kumbe wamezificha kwa usiri mioyoni mwao na leo ndio wameamua kuzidhihiri.

loh! ama kweli ya moyoni yaliyo na usiri usiombe yatoke kinywani unaweza ukaliona kaburi!

siku hii ndio niligundua kuwa kalamu siku zote inaigiza unyenyekevu lakini kumbe ndani yake ni jeuri na ina misimamo hasa ikiamua lakwake!
karatasi

kwa upande wa karatasi yeye ni binti mpole sana lakini nilibaini kuwa hana msimamo na mara zote hutegemea kalamu anachokisema ndicho yeye afuate!

tabia hii ya karatasi niliibaini leo wakati kalamu ikinipa makavu yangu karatasi yeye ilikuwa ikitabasamu kinafiki huku ikikosa ujasiri wakunitazama usoni nakupeperuka peperuka kana kwamba eneo lile lilikuwa na upepo.

kalamu haikunionea haya hata kidogo ilifunguka kwa hisia kali huku machozi ya hisia za hasira yakuonewa yakimiminika usoni mwake, jamani kalamu yanichimba !!

kwanza iligoma kabisa mimi kuishika ili niitumie kuandika wazo langu.
mwanzo nilidhani masikhara lakini ukweli ukawa ndio huo kalamu yanikatalia katakata,
yagoma kwa kisirani ikinihoji kwa ukali vipi naitumia malipo hayaonekani!

yafika mbali zaidi ikidai eti mimi ni tajiri iweje naitumia bila kuilipa posho.

naistaajabia hii kalamu leo imepatwa na nini..!!

yasema imetumika sana kuandika vitu vya mana lkn ufukura yanuka haioni chamaana..

kwahivyo leo imegoma inachohitaji ni neema, naibembeleza kwa huzuni walau ikubali naipa ukweli tupu taarifa tanabai, watu hawapendi soma maandishi hawathamini hivyo ninachokifanya nikutimiza tu nilichoagizwa duniani.

naipasha zaidi kwa kuiambia kuwa haata mimi najua niandikacho ni mali lakini nifanye nini na watu ni wabahiri.

huwa naingoja kesho labda mlango utafunguka lkn ni miyeyusho malipo nipatashika,

nafsi inasonona siijui yangu hatima najaribu kwenda kisasa lkn sipati mbivu

 naambulia tu misifa kipato ni maumivu.

naijuza kalamu kuwa sanaa bado ni kiza Tanzania haina nuru, na mimi sio wakwanza walikufa na ufukura wanafasihi mahiri,

 kipato kiliwatenga lakini hawakughairi waliendelea songa bila kutamalai

iweje nianze mimi leo hii kujinai kukichinja kikatili kipaji changu kukinai.

rafiki yangu kalamu endelea kupiga moyo konde endelea kumwaga wino usinigomee mwenzio utazidi kuniumiza.

wewe ndio rafiki pekee ambaye hunimaliza mawazo yanaponijia na hukimbiza huzuni inaponikaribia iweje leo wanitendea hivyo.

kwani siniwewe ndio ulikubaliana nami kuandika makala KUHUSU PESA na siniwewe ndio ulitia saini ukiunga mkono kuwa pesa zetu zipo mahali zitatufikia muda ukifika.

Iweje leo wanisaliti unageuka kuwa MAPENZI YA SASA waniacha kisa sikupi pesa! itafutie rangi hii fedheha walau hata isinifanye nichekwe na walimwengu pindi wakigundua ipo ndani yangu.

hakika leo umetonesha mahali ambapo hapajapona hata kidogo nawezaje kustahimili machozi haya.

Ni juzi tu Rafiki yangu Muda alilalama kuwa namtumia bure bila yeye kuona mafanikio yoyote mpaka leo ameniachia fumbo eti shauri zangu ipo siku ataniacha!

shemeji yenu nae haishi kunisema ati kila saa natumia kuandika kitu kisicho na faida kwangu na nina uhakika ni yeye ndiye kaja kuwatia ndimu ninyi leo hii mnigomee lakini iweje mshirikiane kunilaumu mie wakati ninyi ndio watu wakaribu ambao nawaamini!?

iweje leo hii mlivue vazi la ustahimilivu nakujivika kiburi kisicho kuwa na uungwana!

lengo lenu nini hasa mwataka nami nidanganyike kwa kuhisi pombe, bange na Madawa ya kulevya ndiyo vitanimaliza mawazo ya kukosa kufanikiwa kwa nikifanyacho!

kadri ninavyo zidi kuongea nawe kalamu nazidi kugundua sipaswi kukunyenyekea bali kukuropokea tu mana wewe na wenzako hamna nia njema hata kidogo na kwa taarifa yenu tu niwapashe wewe kalamu, wewe karatasi wewe muda na huyo mkaza angu mie ambaye ni shemeji yenu,

kalamu
mjue kuwa mimi sio kijana niliyeumbwa na tamaa yakutafuta faraja inayogharimu utu wangu sitaenda maskani kuvuta bange wala club kunywa pombe eti nipunguze mawazo.

Aliwahi sema kilembwe wangu SHAABAN ROBERT mwandishi ni mtu wa desturi ambaye haridhishwi na hasara wala haishi kwa kunywa ukungu nakula hewa.

Jamii hailijui hili nami sitataka kuwa mwanaharakati wakulipigania hili ila nitahakikisha napiga goti nasali nikisujudu kumuomba Mungu ili Thamani ya Maandishi iendelee kuonekana kwa kuizindua jamii katika tope la usingizi uitwao UJINGA

na utu wa Mwandishi utambulike kwa kupewa hadhi ya mtu pekee anayejitahidi kuvaa uhusika wa kila namna ili mradi kufikisha ujumbe kwa jamii.

Mwandis
hi yeye ni mwendawazimu sa nyengine, mwandishi huyu ni Kiongozi wakati fulani, Mwandishi yeye hudiriki kuhama katika mawazo yadunia hii kwa lengo moja tu lakuhakikisha anaibumburusha jamii nakuweza kufikiri tofauti.

Kalamu nakuacha sitakutumia mpaka utakapopenda mwenyewe lakini sitaacha kuandika ingawa sijui nitatumia mbinu gani na nakwambia hili ili utambue kuwa mimi muandishi nakamilisha kazi zangu nikitegemea uwezo wako!.

kaa tafakari umeandika vingapi mpaka leo hii tangu enzi zile zakina wilium walkspear, hivi duniani kuna pesa inayoweza kulipia kazi yako!

tafakari maneno yangu yakirudisha moyo wako nirejee uniombe msamaha tuendelee na kazi lakini mpaka hapa nimeshakusamehe.

Kwaheri!.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »