Bwana WOGA amekamata gazeti la serikali ya nchi yao anawasomea watoto wake na mkewe.
ukurasa wa juu kabisa wa gazeti lile uliandikwa "SERIKALI YAENDELEA KUTANGAZA VITA DHIDI YA MAENDELEO YA BINADAMU"
Mzee WOGA alisoma kwa furaha habari ile bashasha la tabasamu lilipamba uso wake wenye hila na wivu dhidi ya mafanikio ya mwanadamu.
serikali ya nchi yao ilitangaza vita zaidi dhidi ya harakati za binadamu kuyafikia mafanikio.
gazeti lile liliandika mbinu zitakazotumika kufanikiwa kushinda vita ile, miongoni mwa waliokuwa makini kusikiliza habari ile ni mke wa bwana WOGA aliyefahamika kwa jina la Bi.HOFU.
alikuwa ni mtu wa aina yake upole wake ulitiwa nakshi na wivu usio na msingi uliojidhihirisha usoni mwake kupitia pua yake ilioyotota vijasho na Inaelezwa kuwa hata chakula chake kilikuwa cha karaha sababu ya umoto pengine labda ile dhana ya wivu huweza kuashiriwa na umoto wa chakula upikacho ilijidhihirisha kupitia Bi HOFU.
usiogope |
wao hawakuwa na umbile maalumu na pia hawakuwahi hata siku moja kujitokeza mbele ya upeo wa macho ya mwanadamu yoyote hivyo Kusababisha wasijulikane hasa wapoje lkn walijaaliwa uwezo wakuishi ndani ya nafsi ya mwanadamu na kumjengea jumba la woga hasa anapotaka kujaribu kuonesha uwezo wake ama kupiga hatua za maendeleo, woga hujitokeza bila hata papara na taratibu hujichanganya na akili ya mwanadamu nakujenga sauti ya upole ambayo hujirudia mara nyingi ikitamka maneno kama haya "WEWE HUWEZI" "ACHA HIYO,WATAKUCHEKA" Na maneno mengine mengi kama haya.
hizo ndio hila za bwana na Bi hofu, huleta ugonjwa wa ajabu sana duniani, ugonjwa wakutojiamini kwa kuhofia kujaribu kukanyaga au kupita kwenye daraja linaloelekea kwenye ndoto zako!
mara zote serikali inayowaongoza kina woga imekuwa na kisirani cha visasi na kuleta sintofahamu ya udhaifu mkuu katika maamuzi ya mwanadamu hasa maamuzi yenye tija katika maisha yake.
Nimemega kwa usiri mipango yao na mipango hiyo inapangwa kila uchwao na jamii wanayoishi kina Bi Hofu...lengo lakumega siri hii ni ili wewe ujishtukie kuwa unatakiwa ukatafutie dawa kauoga kanakokuzingira nakukufanya usite kutimiza mipango yako!
umeshajiuliza ni kwanini ujipe sababu za kushindwa katika kila jambo? kwanini mipango yako mizuri haiamii kwenye vitendo? kwanini wengine wameweza walipojaribu na hivi sasa unawaita wenye mafanikio? eti umeshajiuliza unachoogopa ni nini?
waliofanikiwa katika dunia hii ni wale walioshindwa mara kadhaa katika maisha yao lkn mafanikio yao yaliletwa na imani kuwa wanaweza kujaribu tena na hata waliposhindwa walijaribu tena natena na mwisho wakaweza, hawakuogopa kuchekwa wala kitu chochote nafikiri waliusuta uoga tena suto la majivu ya moto..
woga ukaona haya na ukakaa mbali kabisa na harakati zao!
woga hauna lolote katika maisha yetu zaidi yakuturudisha nyuma.
Usiogope, ukitafuta sana katika dunia hii utagundua wapo ambao wana mapungufu na hawakufikii wewe kwa chochote lakini wamefanikiwa! wamewezaje unadhani!? walijiamimi na wakaamini wanaweza.
usiogope jaribu chochote kinachokuelekeza kwenye mafanikio mradi kiwe na utu na kisiharibu sheria zetu!