muda mwengine unajilaumu sana kwa maamuzi yako uliyoyaamua mwenyewe unamkumbuka mpenzi wako uliye achana nae unajutia makosa yako na kila ukijitahidi uwe sawa unashindwa...unadhani kwanini!?
jibu ni kwasababu umeshawahi kuomba msamaha mara moja au zaidi kwa wale ulio wakosea au kwa MUNGU wako lakini hata siku moja hujawahi kufikiria kujiomba msamaha wewe mwenyewe!
tunajikosea sana sisi na nafsi zetu lakini tumekuwa wapuuzaji wakujiomba msamaha huku tukiona kuwaomba msamaha wengine ndio dawa. sio kweli chukua muda sasa baada kusoma ujumbe huu ujiombe msamaha.
ulishawahi kuahidi nafsi yako ipo siku utakuwa fulani katika dunia hii lakini ndoto hizo hujazianza kuzitimiza, ni wazi umejikosea sana kujidanganya ni muda wako kujiomba msamaha.
ulishamuahidi mtu kuwa utakuwa nae maishani hutamuacha kamwe lakini sasa hivi penzi lenu hilo ni simulizi zinazoishi tambua kuwa hujamkosea yeye tu hata wewe umejikosea na hautaacha kujutia uongo huo kama hautajiomba msamaha!
jiombe msamaha uwe huru.
ipe nafsi yako nafasi ya pili, ni tiba itakayofanya uwe huru maishani! usiendelee kusononeka kwa kujiona mkosaji.
Jiombe Msamaha |
umezaliwa Masikini na ukaiahidi nafsi yako kuwa hautakufa masikini lakini mpaka sasa bado unapuuzia kujituma nakusimamia
ndoto zako ni wazi umejikosea sana. jiombe msamaha.
sema...
ewe nafsi, mimi sio mkamilifu,
usinighasi, kwa yangu mapungufu,
nipe nafasi, nifanye ulinganifu,
yale maasi, yageuke ukamilifu,
nibaki hasi, kama chanya ina upungufu.
huu wasiwasi, utoweke bila tifu.
Jiombe msamaha rafiki usiendelee kujihisi una hatia kwa makosa yalopita ni dawa zaidi ya muarobaini kujiomba msamaha kwa dhati kabisa mpaka uhakikishe nafsi yako imeridhia kukusamehe na ahidi kutorudia tena makosa yako.
ishi na watu vizuri kumbuka mtu akikutendea wema wewe ukirudisha maovu hata kwa bahati mbaya hujamkosea tu huyo mtu bali hata nafsi yako, na itakusuta katika maisha yako yote mpaka utakapokiri umekosa nayo itakusamehe.
Jiombe msamaha usiwe mtumwa wa nafsi yako mwenyewe tafuta uhuru wakujiomba msamaha nakujisamehe.
katika maisha yangu nimeshajikosea sana kwa kuwaumiza wengine bila sababu za msingi niliteseka sana mpaka nilipogundua kujiomba msamaha nakujipa nafasi nyengine katika maisha yangu.
Ewe nafsi yangu naomba sana unisamehe, nayaona mapungufu yangu na yananizomea mpaka naona haya.
nisamehe kwakweli siwezi kukamilika kwa furaha bila ya msamaha wako.
naahidi nitajiweka mbali na makosa haya yanayoigasi himaya yako. ungana nami kwa nia njema tuogelee pamoja katika bahari ya amani.