Posts

Showing posts from July, 2016

BLOGU YAKASIRIKA

Image
mwisho wa mwezi wa saba 2016 harakati na shamra shamra zakuandaa uzinduzi wa blogu ya SIMULIZI ZINAISHI (ommyzongo.blogspot.com) zikiwa zimefana kweli kweli, watu wenye kuitakia heri blogu hiyo wakishiriki vema kuitangaza siku ya uzinduzi kila mmoja kwa nafasi yake, ajabu blogu yenyewe yanuna! yakasirika nakuhoji kwanini imetelekezwa! hakuna simulizi mpya inayoandikwa yapaza sauti yake ikifoka eti kwanini juhudi zimeongezwa katika kutangazwa kwake nakufanya watu wengi waitembelee nakuifunua kwa kuigeuza geuza, wakiishangaa kwanini izunduliwe! inahoji kwanini nguvu isingeenda sambamba na kupostiwa SIMULIZI MPYA, yasema imechoka kutazamwa ikiwa haina jipya, yaona hauna haja uzinduzi kama yenyewe haipatilizwi. naishangaa hii blogu nakosa kitu sahihi chakuiambia nataka niishutumu haina shukurani lakini nasita sababu upande mwengine naiona inaongea maneno ya kweli. ni kweli juhudi ziliegemea sana kwenye kuutangaza uzinduzi wa blogu badala kupost simulizi mpya. blogu yase...

UKWELI NI HUU

Image
Kama utaamua unichukie sababu ya ukweli huu ni sawa tu sababu najua nyie mabinti mnapenda kudanganywa! mtu hata kama hujapendeza ukiambiwa umependeza ndio furaha unacheka meno yote yanaonekana. mimi mwenzio leo sitaki kusimamia uongo acha nionje chachu ya ukweli. mwenzako mimi jina langu ni kama nilivyokutajia pale mwanzo, ninae mchumba na ni mzuri kushinda wewe! nampenda sana na hivi sasa tupo katika hatua za mwisho kabisa zakuoana yaani kwetu wanamjua na hata mimi kwao wananijua vizuri na wamebariki sisi kuwa mwili mmoja. lengo lakukusimamisha wewe nikukwambia kuwa nimekutamani sana! vazi lako la kishenzi na laana linaloonesha sehemu kubwa ya mwili wako limenifanya nitamani kuwa nawewe kwa muda mchache tu na tena kwa siri kubwa sababu haustahili kutambulishwa kwa yoyote si kwa ndugu wala rafiki zangu. wote wanaonihusu ni wastaarabu sana bahati mbaya wakigundua natoka nawewe sidhani kama watanielewa wataniona nimepotoka! Nitaongopa kwakweli nikikwambia nakupenda sababu n...

WE BINTI BWANA

Image
Sitothubutu kusema huna akili ingawa matendo yako yananithibitishia hilo. kwanza tulipendana, pili tukazoeana, tatu tukakerana hatimaye tukaachana. mazoea yakaniadhibu, nikakumbuka ukaribu, nikarejea kwa aibu, kuomba uje unitibu, mashaallah hukunighilibu, ukarudi kwangu tabibu. maisha yakaendelea, penzi kiraka nikizoea, baadae nikagundua, ni adha nimeikaribia dharau nimejijengea, upuuzi nimeurejea. kitu kimoja hujajua, mie ni yule wa mwanzo. sifai kulumangiwa, kuteswa kwangu tatizo, Kamwe sitofurahia, kugeuzwa chotezo. maneno yangu rejea, mimi sio wa mchezo, kamwe sitokurudia, huu ni msisitizo. Huu moyo ni mashine, hukoboa na kusaga. moyo wangu usiupime, usitake kuuiga, kulifuga pakashume, bora kusugua gaga.. unyayo wako ung'ae, na wengine wataiga. ni heri nikose vyote, kuliko ile heshima. sina sababu yoyote, kwako wewe kusimama. umenivua nguo zote, muungwana nachutama. likiisha jua lote, gizani ntasimama. ntajistiri chochote, nafs...

KWANINI?

Image
Ndugu kwanini kitu chakununua kwa pesa kisababishe uvunje uiminifu kwa mimi ambaye sina hata chembe ya nia mbaya nawewe!? kwanini unataka kunipa dhambi yakukuwazia vibaya rafiki yangu wa damu? kwanini unataka kununua bure kabisa ubaya usio na faida yoyote ule? Eti kwanini Eti kwanini unaruhusu tamaa yako isiyo na tafakuri ibomoe ukuta thabiti wa urafiki wetu wenye tija? niambie basi kwanini lakini unajaribu kuipima roho yangu ukionesha kupinga kuwa mimi ni mwema kwako? kwanini unanilipa malipo ambayo sistahili kulipwa na rafiki niliyemuhifadhi kwenye chumba kilicho jirani na ndugu zangu! kwanini unaupa sababu ulimi wangu utamani kutamka maneno yaliyo na lawama kwako! jipe muda basi utafakari tena labda pengine umekosea ulichokipanga kwangu tafadhali sana tafakari na ujisahihishe sababu wapo ambao nahisi wanastahili kunifanyia hivi lakini sio wewe! nakupa nafasi tafakari naamini utaona kuwa sistahili kutendewa hivi nawewe! sononeko langu litakugharimu, hivyo ndio na...

ILINICHUKUA MUDA KIDOGO

Image
Kwa jicho la baba asiyekuwa na mipango thabiti na familia yake haiwezi kumchukua muda mrefu kama ilivyo nichukua mimi na hii yote ni sababu nilitaka muda wakujiridhisha, kila nilipokuwa naiwaza familia yangu ilinipa wakati mgumu sana kuamua yupi ambaye atakufaa wewe na ukajivunia kweli kumuita mama. kila mmoja leo hii humwambii kitu kuhusu mama yake na ukimwambia azungumze kitu kuhusu mzazi wake huyo ni lazima atakosa neno sahihi lakumwambia kudhihirisha upendo wake lkn ni ukweli kwamba sio mama wote wanaosifiwa na watoto wao ni wema ila kwa vile wamefanya tendo lakishujaa kwa kuwahifadhi tumboni nakuwatoa kwa uchungu nakuwazawadia upendo wa malezi ni lazima wawe wema kwao hata wakiwa wabaya kwa wenzao huu ni ukweli ulio dhahiri mwanangu achana na ule ukweli usiopendwa kuongelewa. Ilinichukua Muda kidogo mimi ilinichukua muda kumpata wakukuzaa sababu sikutaka awe mama kwako tu nilihitaii awe mama wa jamii. nilihitaji pakitafutwa mfano wakuigwa angalau linyooshewe kidole hat...

TUSIDANGANYANE..!

Image
Tusidanganyane Bwana! Ifike mahali tusichukuliane kama watoto, tuheshimiane, tusidharauliane kwa uongo ulio dhahiri!. Umetengana na mwenzako miaka zaidi ya tano, kuwasiliana nae kwa nadra sana tena ukimpigia ni salamu then anakuomba umcheki baadae coz muda ule yuko busy. kinyonge unakata simu unamsikilizia baadae yenyewe hakucheck wala nini, unazuga kumpotezea unajikuta unampotezea kweli siku na mawiki kadhaa yanapita unapotimu mwezi anakupigia yeye na kwa bahati mbaya unakuwa busy hivyo nawe unampokelea kisha unamuomba akucheki baadae.. baadae hakucheki wala nini, masiku yanaisha miezi baadae mwaka na miaka. alikuwa mkoani huko amerudi dar bila kukwambia kama zali siku mnakutana mkigombea gari la mbagala. kinafki kabisa mnaanza kukumbatiana kila mmoja akionesha kummis mwenzake. stori stori mnaanza kuongopena eti siku zote mlizokaa mbalimbali hakuna mechi yoyote ya nje iliyochezwa...! si uongo huu jamani!, tena uongo usiovaa nguo!. mnajidanganya kwa vinywa ilhali kil...

KALAMU YAGOMA

Image
Napata wazo jipya nalitafakari kwa undani wake naona lafaa niliweke kwa maandishi ili walau liwafae na wengine maishani, katika kuumbwa kwangu vingi sana nimenyimwa ikiwemo choyo na ndio mana siweki ndani hata siku moja hadhina ya nikiandikacho nakigawa kwa wengine ili wakonge nyoyo nakulisha bongo zao pia! sasa Nawezaje kuliweka wazo langu kimaandishi? swali hili zuri lanifanya niikumbuke marafiki zangu kalamu na karatasi nakurupuka kuwafuata sababu jamaa zangu hawa hawakai mbali, makaazi yao ni mezani na yapo jirani kabisa na maskani yangu maarufu iitwayo Kitanda hatua si zaidi ya nne nafika mezani. kwa mara ya kwanza kabisa nagundua tabia za jamaa zangu kalamu na karatasi, tabia ambazo siku zote kumbe wamezificha kwa usiri mioyoni mwao na leo ndio wameamua kuzidhihiri. loh! ama kweli ya moyoni yaliyo na usiri usiombe yatoke kinywani unaweza ukaliona kaburi! siku hii ndio niligundua kuwa kalamu siku zote inaigiza unyenyekevu lakini kumbe ndani yake ni jeuri na ina misimamo ...

MAISHA YA FACEBOOK

Image
Mtandao wa Facebook Nilianza kwa kuhadithiwa na jamaa yangu flani ivi kwamba eti facebook kuna watoto wakali, marafiki wa kila aina na zaidi kuna kila aina ya swagg kutoka Facebook, Dah! Alikuwa akinitamanisha mno enzi hizo me kushika smartphone ilikuwa ni ndoto kubwa mno, na ata computer sikuwa naweza kuitofautisha na luninga, Basi dah nikajiona niko nyuma sana, nilijona mshamba, niliyepitwa na wakati, niliwavuta kichwani hao warembo wa facebook, nikaanza kuwajengea taswira hii!. wana rangi nzuuri za kiafrika, mavazi adimu na adhimu yenye heshima na taadhima, sura zenye bashasha na tabasamu muda wote, wana haiba za kike na post zao zina alama ya upendo sababu niliamini upendo unaishi kwa wanawake. Hizo zote zilikuwa ni taswira nilizojenga huku nikitamani kujiunga na ulimwengu huo wa facebook, Masikini ya mungu tayari hata mke wangu nikapanga nitampata Facebook, Marafiki nao nikawajengea taswira ya watu wema wasio na hata chembe ya chuki, wapole wasio na ubaguzi, Sa...

SITASEMA

Image
Kama kuimba nitachoka nitashika kalamu kuandika Makala fupi na ilitokea sina chakuandika nitaingia watsap kwenye group langu ambalo member ni mimi peke yangu nakumbuka nililiunda group hili siku ile mama yangu anafariki hua nalitumia kuelezea hisia zangu hasa ninapovurugwa na haya maisha pamoja walimwengu, hua najifariji kuwa naongea na mama yangu! nitatumia group hili kupoteza muda mradi nisiseme sababu ni yamini nimeila na nafsi yangu kuwa sitasema. kusema ni kujiumiza mwenyewe sababu mengi yamepita na kwangu yamebaki historia Sitasema kamwe kuwa ni mimi ndie nilikuwa chanzo chakuachana nawewe! sitasema sababu ni fedheha sio tu kwa ndugu zangu hata wazazi wako na mara ya mwisho kuongea na mama yako ni leo, sauti yake yaucheshi bado inaendelea kuniita mkwe sikuweza kumwambia kuwa umenifumania na umeumia sana na hautaki hata kuniona! Sitasema kamwe Nimejaribu kungoja siku mbili zipite baada yatukio lile labda utarudi ama utapokea simu yangu lkn wapi, nasikia hutaki hata kusikia...

ACHA NIKUDANGANYE

Image
Mwenzako sijasoma sana! sijivunii kusema hivyo naumia lakini inanipasa tu nikwambie licha ya akili kuwa nazo nyingi lakini nguvu ya mapenzi katika umri mdogo ilinifanya shule niione ya nini na mapenzi ndio habari ya mjini! Nikajikuta nasoma kwa ubabaishaji sana leo hii hapa natamani nipewe kipaza sauti chenye nguvu yakusikika maeneo mengi nchini Tanzania hasa kwa watoto washule ambao wazazi wao masikini kama alivyokuwa mama yangu mimi ningewakemea kwa sauti nakiwasihi wasome wasioge kamwe kwenye bahari ya huba kwani mawimbi yake yatawazamisha kwenye tope la ujinga na hata waweze kupuuza elimu ambayo ni muongozo thabiti! mimi sijasoma sana na ndio mana leo nalalama sababu sitaweza kukuthibitishia kisomi kwa kukuletea tafiti nilizofanya zikakuonesha kuwa MAPENZI HUDUMU KUTOKANA NA UONGO! lakini huo ndio ukweli, bila uongo mahaba hayana uhai! kabla sijakuelezea hisia zangu kuwa nakupenda nakumbuka nilimsikia rafiki yako akisema kuwa wewe unavutiwa sana na kijana mcha Mungu, na ndip...

SHEM UNAMUUMIZA SISTER 'ANGU

Image
Haikuwa na maana tu wewe kuzaliwa mwanaume mwenye mvuto halafu usijue majukumu yako.. unamuumiza sister angu bhana, dah! halafu samahani Unamuumiza dada 'Angu najua wewe ni mswahili safi na mara nyingi hutupendi vijana kwa kuchanganya maneno ya kihuni na ya kiingereza kene sentensi za kiswahili lakini leo mimi ili kuonesha msisitizo ntakuchana kwa kuchanganya maneno yote hata ya kidigo mradi ujue unaniumizia dada! Dada alifuruhi sana alipojua dhamira yako kuwa ni njema hutaki kumchezea unataka kumuoa lakini tambua kuwa hakuwa anajua kuwa kila tabia mbaya unayo na nina uhakika angejua asingetoa machozi ya furaha siku ile ya send Off pale kwenye ukumbi mkuubwa wa Majengo In kule Muheza Tanga. Shem si niwewe ndio ulijifanya mwema kipindi unakuja kutoa posa kila jambo ulimuhusisha MUNGU na maneno kama Inshaallah ukiyatamka kila saa!  iweje hivi sasa hata dada nywele zimempauka zikitaka kuandamana kwa kukosa matunzo. kumbuka hujamkuta ivo sista basi ruhusu hata aibu ikuin...

JIOMBE MSAMAHA

Image
Unadhani ni kwanini nafsi yako inajilaumu sana unajiona mpweke, hujiamini na wakati mwengine unadiriki hata kutamani siku zirudi nyuma urudi katika hatua fulani uliyowahi kuipitia...eti unadhani ni kwanini? muda mwengine unajilaumu sana kwa maamuzi yako uliyoyaamua mwenyewe unamkumbuka mpenzi wako uliye achana nae unajutia makosa yako na kila ukijitahidi uwe sawa unashindwa...unadhani kwanini!? jibu ni kwasababu umeshawahi kuomba msamaha mara moja au zaidi kwa wale ulio wakosea au kwa MUNGU wako lakini hata siku moja hujawahi kufikiria kujiomba msamaha wewe mwenyewe! tunajikosea sana sisi na nafsi zetu lakini tumekuwa wapuuzaji wakujiomba msamaha huku tukiona kuwaomba msamaha wengine ndio dawa. sio kweli chukua muda sasa baada kusoma ujumbe huu ujiombe msamaha. ulishawahi kuahidi nafsi yako ipo siku utakuwa fulani katika dunia hii lakini ndoto hizo hujazianza kuzitimiza, ni wazi umejikosea sana kujidanganya ni muda wako kujiomba msamaha. ulishamuahidi mtu kuwa utakuwa nae mai...

NAKULAUMU WEWE..

Image
Nakumbuka nilitoka na wenzangu mlimani city, ni mimi pekee katika marafiki zangu ndio sijengi mvuto kwa yeyote wala pia sina uwezo wakumfanya mtu ahamasike namimi ata walau atamani kunisalimia.. nalijua hili na wala sina haja yakuelezea sana labda tu kuongezea nikwamba hata nikitoka na washkaji zangu mavazi yangu yakawaida sana jamaa wanakuwa wamependeza na hii ni mara zote sio tu siku moja moja, najijua sina mvuto ndio mana pia napaza sauti nikikunyooshea kidole nakukwambia NAKULAUMU WEWE! Nakumbuka siku ile mimi na rafiki zangu tunaingia mlimani city wewe na rafiki zako mnatoka, mmependeza zaidi wewe unaonekana kuwazidi wenzio hasa umbile lako la mchoro, sura yako ya haiba na mavazi yako ambayo nakiri yalitiwa dosari na usasa lkn kwavile mwenyewe wakisasa sikuzingatia hilo nilibaki nikijiambiza "hakika amependeza yule dada" nilijiambiza hivo huku nikikubaliana na hali yangu kuwa siwezi kumiliki mrembo kama wewe labda rafiki zangu yeyote yule sababu wao walikuwa na ny...

INATOSHA..

Image
Kusema neno hilo nalazimika licha ya kwamba bado nahitajika, uwezo wangu sasa watambulika, lkn kusitisha nahitajika, neno lifaalo INATOSHA na hapa mbele nukta naweka. mafundisho yangu yangali hai,  niloyatoa yanatosha tamalai, huu mkono wapunga wasema bai,  tutakutana nafsi yangu ikifurahi. nipasayo kukugawia ni mengi sana, ila wanadamu waso na mana, wanaweza kujigea kwa mapana, Inatosha kisha kukimbia mbali sana. Inatosha ipo siku takutana. najua mpo mtakaojali , na wengine mtanyari, iweje niahirishe safari, wakati bado ningali hai. watakaoponda ni wengi pia,  sababu ya chuki kwa hii rupia,  hawajui kama MUNGU alonigea,  kusitisha hii safari kaniambia. Ipo siku mtamuhitaji Bin Zongo mkihitaji story zake za mafumbo  ila unafki wenu utageuka fimbo,  utawachapa pande zote za mgongo. inatosha kwa leo nasema basi, nitarudi tena nikipata chance,  kwa kizungu kwa kiswahili ni nafasi, Inatosha jamani Nasema basi.

Jicho Vumilia

Image
Jicho Vumilia Jicho langu mwenzio naamini kuwa wewe ndio kipimo cha utu wangu usipokuwa mvumilivu  utanifanya niwe mtu wa ajabu sana, nilo jisitiri kwa vazi zuuri la staha lakini nanuka uvundo wa fedheha. Jicho langu wewe, ni wewe ambaye huona kwanza kabla unachokiona hakijajadiliwa na ubongo nakupenya moyoni. Jana nilipita barabarani nikaona Gari, kwa hakika nisingejua kama ni zuri gari lile bila wewe kulitazama, jicho siunakumbuka vizuri kama ulikiponza kidole changu cha mguu sababu nilijikwaa kwa kushangaa gari lile. basi sawa nilifurahi wewe kutenda uwezo uliopewa na mola wako lakini ilikuwaje mpaka ukatazama sana mpaka akili ikajenga mvuto wa hali ya juu wa gari lile,nikabaki naumia moyoni sababu sina hata shilingi moja yakuweza kununua gari lile. nikapiga moyo konde nakuendelea na safari huku nikifariji moyo kwamba ipo siku nitakuja kumiliki gari lile. hatua si chini ya kumi na Tano, mbele nikiwa nimeongozana nawe jicho ukisimama kama bakora inayoniongoza nie...

NATAMANI..

Image
Natamani leo hii nyote mniulize nini natamani ningewajibu natamani mniulize nini natamani na pale ambapo mngeniuliza nini natamani ningewajibu natamani vijana wote tusio na ajira tuwe na kauli moja tu, kauli ambayo tunaizungumza kwa pamoja kwa nia moja na tamaa ya aina moja, kauli ambayo kwa wengine ingesikika kwa mvumo wa nguvu na ingeeleweka kwa kiswahili ikitamka maneno LAZIMA TUJIAJIRI! kauli hii sina shaka ingeanza kwa kuchekwa na waliovimba matumbo kwa ajira za upendeleo, wanaokalia viti vya ajira huku wakiwa hawana vigezo vya kuajiriwa, wanaoona urahisi wa maisha kwa donge nono la Ajira liitwalo KUPEANA! Natamani ningeelezea vema tamaa yangu kwa vijana wenzangu wanaohangaika mtaani wanaokumbwa na mgogoro wa ndani wa nafsi zao huku wakijilaumu kwa kutumia muda mwingi darasani wakisoma kwa mategemeo ya kuiokota muda wowote ile funguo ya maisha! ningetamani sote tuongee lugha ya aina moja inayoakisi maisha yakujiajiri kwa kuwa wabunifu nakujitahidi kuleta ufa...

Usiogope

Image
Familia kuubwa ya bwana na Bibi WOGA  imekaa nje ya bustani ya kaya yao katika eneo lisilojulikana ni wapi hasa katika ulimwengu huu. Bwana WOGA amekamata gazeti la serikali ya nchi yao anawasomea watoto wake na mkewe. ukurasa wa juu kabisa wa gazeti lile uliandikwa "SERIKALI YAENDELEA KUTANGAZA VITA DHIDI YA MAENDELEO YA BINADAMU" Mzee WOGA alisoma kwa furaha habari ile bashasha la tabasamu lilipamba uso wake wenye hila na wivu dhidi ya mafanikio ya mwanadamu. serikali ya nchi yao ilitangaza vita zaidi dhidi ya harakati za binadamu kuyafikia mafanikio.  gazeti lile liliandika mbinu zitakazotumika kufanikiwa kushinda vita ile, miongoni mwa waliokuwa makini kusikiliza habari ile ni mke wa bwana WOGA  aliyefahamika kwa jina la Bi.HOFU. alikuwa ni mtu wa aina yake upole wake ulitiwa nakshi na wivu usio na msingi uliojidhihirisha usoni mwake kupitia pua yake ilioyotota vijasho na Inaelezwa kuwa hata chakula chake kilikuwa cha karaha sababu ya umoto pengine labda ile dha...

Tazama Tabasamu la Shaaban Robert

Image
Kutazama sehemu ya kwanza ya Simulizi Zinaishi usiache kutembelea Youtube Chanel yetu kwa jina hilo hilo simulizi zinaishi link yakuitazama barua tuliyomuandikia Nguli huyo wa kiswahili ni hii hapa https://www.youtube.com/watch?v=Z_RBWRZLqwE

Masikini Taaluma yangu

Image
MASIKINI TAALUMA YANGU! haionekani chanzo chakukumbata maovu.    Alikuja akitokea kusipojulikana lakini kutokana na Taadhima aliyo nayo alipokelewa na kila mmoja wetu na akaheshimika vilivyo kwa kusadiki kila alichosema. Hatukua na uwezo wakung'amua kila lililojiri lakini kutokana na upeo aliojaaliwa  mgeni huyo aliweza kuwaeka chini wooote wakubwa kwa wadogo nakuwapa habari, kuwaelimisha na walipochoka hakusita kuwaburudisha kwa mtindo ulio mzuri ambao kamwe haukuathiri tamaduni wala maadili yetu, alijijua nguvu aliyo nayo katika kujenga ama kubomoa mtazamo wa jamii hivyo mara zote alihakikisha anafikiri kabla yakusema. pengine kutokana na hili ndio maana aliaminika sana na enzi hizo mimi mdogo niliamini yeye anajua kila kitu duniani hapa kumbe laa, hakua anajua bali alikuwa ni mfuatiliaji na alichunguza neno kabla yakuliibua kwa mapana yake. Nakumbuka vema alikuja akiwa amejisitiri kwa vazi lililomficha vema maungo yake, alikuwa mwingi wa aibu katika kuzun...