Posts

Showing posts from 2017

MWANAMKENDEGE ; USHAIRI

Image
 hadith hadith njoo simulizi lake sikio naanza safisha koo nikupe langu tukio eneo nikariakoo sikujua mwanamkendege ushungi, umbo na guu mahabani kazamia kiunoni kichuguu moyoni nikaridhia yalonisibu makuu sikujua  mwanamkendege tabasamu lake lahaja nikaona njia nyeupe amejazia mapaja si mweusi si mweupe Radhia jina kataja sikujua  mwanamkendege lafudhi yake yalamu tamko lake murua midomo yake adhimu kicheko kajaaliwa kumbe mja haramu sikujua  mwanamkendege sikujua  mwanamkendege kuuza yake tabia ucheshi wake nizengwe pesa kushadadia ukiwa nacho twende mwanzoni sikutambua kwa miguu miwili nikazama nae hubani sikutaka subiri kumfikisha nyumbani kumbe ndumilakuwili sikujua  mwanamkendege alianzia kwa kaka ushemeji kukataa akasema anataka nayeye kuzima taa mwenzenu yamenifika sikujua  mwanamkendege ndugu kunihabarisha nimepotea gizani mie nikakanusha kwamba haiwezekani kaka uongo kazusha sikujua mwanam...

MUHIMU KUJUA @ukweli unaumbua

Image
Ukweli unapotaka kudhihirika kamwe hauwezi kuzuiliwa na nguvu ama utashi wowote alionao mwanadamu. amini nakwambia ukweli una nguvu adimu ambayo haizuiliwi kamwe na vitu kama Pesa, maneno mengi, cheo, huruma wala kujuana. Ukweli ni jambo la kuajabia maana lina 40 zake kama ilivyo kwa siku za mwizi. Ukweli unapotaka kudhihirika haupokei rushwa wala hongo tena humchagua yoyote hata awe ndio bingwa wa uongo siku hiyo hujikuta akianika sura ya ukweli mbele za watu. Ni ukweli pekee ndio ambao huruhusu wenyewe kufichwa lakini unapotaka kujidhihiri hujidhiri wenyewe kwa njia zake. ukweli jambo balaa ambalo nalistaajabia lilivyokaa! maana lenyewe ndio linaruhusu kukumbatiwa na waongo tena wakiruhusu vitu kama Chuki, Uadui, Mauaji, Ubinafsi, Rohombaya na choyo vivae vazi la Upendo, Urafiki, Wema na Kusaidiana na siku ukweli ukijiachia hubaki aibu kwa watu hao waongo. Mra nyingi sifa za ukweli huumiza na ndio maana wengi wetu hatupendi kusadiki mambo ya kweli mbaya zaidi tu...

Dear Septemba....

Image
 "Mwezi ambao nimezaliwa mimi, Mwezi ambao nauthamini, sijui kwanini hua unakuja nakuondoka mwezi huu, September"   Na. Omar Zongo   Unaelekea wapi mpendwa!? iweje unishushe hapa duniani kisha uniache kama hunijui! ninani mwenyeji wangu!? inamaana lengo lako nikunileta kisha unitelekeze!! Jibu lako la jana usiku wakati ukifungusha nguo zako bado nalifikiria eti "nitakomazwa na octoba, novemba na december" hivi mie nawajulia wapi watu hao! niwewe ndio umenileta hapa duniani niwewe ndio nimekuandika kwenye historia! niwewe ndio nakufahamu bosi wangu kwanini lakini unanifanyia hivi!! basi ungeniambia mapema kuwa lengo lako nikunishusha tu duniani halafu utaniacha! ndio ungeniambia namimi nikajiandaa kisaikolojia! nani atanidekeza kama wewe! nani atajua kuwa nimezaliwa katika moja ya siku zako! ninani atajua kuwa nina vinasaba vya baraka zako! hujisikii vibaya labda siku ile unanishusha duniani watu walishangilia kila mmoja akisema "Wak...

chuki shairi

Image
chuki imekuwa vazi,  limewakaa mwilini. kulivua kwao kazi, haling'oki mauongoni kama dunia twapita chuki ya kazi gani. imewakaa mwilini imetuwama nyoyoni. yajionyesha machoni, imegeuka miwani. kama dunia twapita chuki ya kazi gani. chuki pini nyembamba yapenya kotekote si baba wala mjomba atakuchuki yoyote kama dunia twapita chuki ya kazi gani chuki ikikuhadaa pigana kuiambaa ni jumba la karaha sio kiti chakukaa kama dunia twapita chuki ya kazi gani. chuki ina hila zote haingojei sababu ikukuzidia kete itakuvaa taabu hii dunia twapita chuki ya kazi gani dunia hii twapita hatutaishi dawamu litakufika gharika chuki haina nidhamu swali nakuswalika chuki ya kazi gani ulimwengu una adha njiaze kadha wakadha itakupata bughudha fakiri wakujifunza kama dunia twapita chuki ya kazi gani.

SHAIRI: JAWA

Image
"Ni baada tu ya rafiki yangu fulani wakati nipo chuo kuniomba nimuandikie utenzi kumuhusu, kila siku nilikuwa namuahidi nitamuandikia ila siku moja abra ikanishukia na tenzi nikamtungia...." Na. BIN ZONGO Jawa Malkia Zawadiwa Jaaliwa Jawa Tunukiwa pendelewa Zidishiwa Jawa kwani nani mtu gani, ana nini? jawa mwenye hadhi sio mpuzi ni azizi roho yake nyeupe theluji mithili yake sema nini akupe kilicho uwezo kwake haiba ni vazi lake stara jaala yake ucheshi sifa yake maringo hayapo kwake

Wa UBAVU WAKO

Image
Wazungu wanamuita  soulmate je unamjua mtu huyu? umeshakutana nae? unadhani yuko wapi?? anza sasa kumfikiria wa ubavu wako maana ni muhimu sana mtu huyu! kama umempata hewallah laa kama bado fanya hima umtafute mashariki na magharibi usiache akaendelee kuteseka nawe kuteseka kwa nyinyi watu kuishi mbalimbali. huyo ndiyo sahihi kwako, katika mahusiano yako ya urafiki, mapenzi mpaka ndoa. yeye ni muendelezo wa akili zako zinapogota kufikiri! yeye ni msaada wa dhati unapokwama katika hali yoyote! yeye nifaraja unapotokwa na machozi! amini nakwambia ni mtu aaziz sana huyu. hatoruhusu ulie! udhoofishwe na mawazo mabaya na ujihisi mpweke. atakufanya useme "kwanini sikumpata tangu mwanzo mtu huyu!" hata ujinga wake utakuwa ni burudani kwako! yote sababu ni ubavu wako umetokana na yeye wanaoamini uumbaji wa Adam na hawa watasadiki hili kwanini uendelee kuteseka na mtu ambaye hamuendani? kwako wewe moja jumlisha moja ni mbili kwake yeye ni kumi...

mtandaoni shairi

Image
 Na Bin Zongo karibu mtandaoni uyaone ya duniani karibu keti makini ujue nani ana nini bando la uhakika bando halina shaka insta kunafikika twitter nakadhalika simu yangu smart tabu tabu sipati maridadi internet karibuni tuchart naanza nae Kimambi Mage haeshi vitimbi leo kapost mengi post zake hupingi alaani serikali ina nyingi dosari viongozi dhoflehali insta kote zohari mateja wazodolewa polisi wanatakiwa mkuu kashaamua mkoa kusimamia apost vita vyaanza biashara tokomeza harakati ndo imeanza madawa kuyamaliza wengine niwapinzani wameanzisha tafrani eti mkuu hajulikani amesoma shule gani mengi ya mtandaoni hufurahisha moyoni eti mchungaji gani amezaa kwa kuzini yule na wimbo mpya huyu na demu mpya mondi kaibua jipya bifu limeanza upya

PANDE MBILI ZAZOZANA

Image
Pande moja imevaa gauni ishara ya mwanamke nyengine imetinga kanzu ishara ya mwanaume! moja ya kanzu yasema wake waharibifu uaminifu hawana wamejawa mapungufu. gauni lataharuki almanusura livuke lasema hayasadiki waume wanachosema wao ndio mamruki uaminifu hawana. kanzu yatetemeka mate kinywani yatoka maneno yaropoka waume wametukuka, wanawake kwa vibweka duniani wasifika. Gauni latabasamu kwa dharau na kiburi lasema huna nidhamu mwanaume baradhuli ukishaishiwa hamu mwanamke humjali hauna ubinadamu wanaume ni zohari. Kanzu yakunja ndita mijicho yachomoka, kukupiga sitosita hivi ndivyo yaropoka sema nami kwa nukta dharau sitazitaka. Mwanamke gauni asema sikuogopi sitoshuka chini maneno yangu silipi tena yana thamani wanaume ni makapi. kanzu yagadhibika busara yamtoka matusi aropoka gauni lamcheka. Bi Gauni : tukana utukanavyo ila habari unayo, hivyo ndvyo mlivyo waume mapoyoyo, hasira zenye ujazo ni mapungufu hayo. Bwana Kanzu : wanitafutia kesi mwanamke hayawani ...

USISAHAU CHANGAMOTO @UjanaMajiYamoto

Image
Na.  Omar Zongo Ishi nami kwa furaha ila tambua siku moja kuna karaha hivyo usisahau kujiandaa! Usisahau changamoto ambazo kwa jicho langu naziona zimejaa pomoni! kupendana angali vijana ni suala lamaana lina taadhima na kubwa heshima! lakini usisahau kuwa ujana ni laana, jumba la usahaulifu na upotofu na kwa taarifa yako wengi waliouvamia sasa hivi ni wafu! walio hai wanasubiri andiko litimie!, afya zao dhalili, wakenda kama walevi, wamedhoofu mwili, nguvu zao kumbukizi, kwao naona dalili ya kupoteza nguvu kazi, ni baya suala hii UJANA kweli maradhi. Usisahau changamoto ya kwanza kwetu Ni Ujana! tena hii ni ya Moto yapasa kuomba sana. tuvuke mito, vijito tukeshe kuombeana! kwenye baridi na joto tubaki tumeshikana. Tena tuache utoto laa sivyo tutaachana. Ujana ni changamoto naomba kumbuka sana! wengi eti tulizo wanasema lipo kwa wazee! eti "vijana mzozo bora tuwapotezee" mapenzi sio mchezo yanaumiza aisee! singeni khabari hizo mchumba uzireje...

USINIACHE MUNGU WANGU!

Image
Naandika kwa mtindo wa kuomba, maombi ambayo yametawaliwa na unyenyekevu na sura yangu ina dalili zote za kuonesha kuwa nina uhitaji wa ninachikiomba! tena sio uhitaji mdogo nina uhitaji mkubwa wa nikiombacho leo. Yupo mpumbavu mmoja, ambaye daima sura lake analikunja kwa jazba kila anaposikia nataja jina lako kwa unyenyekevu nakumuita yeye kwa kiburi tena nikimtukana kumuita Mwanakharamu. ni yeye ndiye ambaye ananitamani kuninyakua nakuniadhibu vikali, anatamani niwe mtumwa wake, ananiwinda kwa juhudi zake zote na hata siku moja hajachoka kunifatilia. ni huyu maaluni ndio leo amenifanya ninyooshe mikono yangu kwako nikiomba kwa unyenyekevu nikikusihi kamwe usiniache maana dude hili linanitamani leo kesho niwe rafiki ake. lengo lake nikuasi Mungu wangu na nifanye yale uloyakataza hakika nakuambia sijawahi kumpenda kiumbe huyu tangu nilipoijua dhamira yake kwangu. leo nina machache nataka kukwambia MUNGU wangu na nakuomba sana unipe msaada wako kwa kuniitiki...

MASIKINI "MSAMAHA" @thamani yako haipo!!

Image
uko wapi rafiki yangu msamaha, kusema kweli nimegundua leo kuwa haupo katika dunia hii maana mimi mwenyewe nimeshindwa kujisamehe mpaka muda huu kwa uzembe wakupoteza andiko langu la mwanzo. Na Omar Zongo Andiko langu lakwanza kukuhusu lilikuwa zuri lapendeza nililipamba kwa vazi la mafumbo juu yake nikalivika joho zuri la tenzi kisha nikalipulizia marashi yenye misamiati ya lugha adhimu ya kiswahili! ndio!! andiko kukuhusu wewe MSAMAHA nililipamba likawa kamili kwa kusomwa lakini sijui ninini masikini ya MUNGU ghafla bin vuu tsunami la teknolojia ya simu inayohitaji chaji kuwa pomoni muda wote likanivaa simu ikazima kabla ya andiko langu kukuhifadhi ukahifadhika. kwa namna ambavyo nilikupangilia ukapangika wallah naapa sikuwahi kupangilia vizuri andiko lolote kabla yako! nafsi ikiwa imejawa lawama yakutokuwa makini na chaji yangu nikakumbuka kujiomba msamaha na nilipofanya hivyo angalau nafsi ikawa huru lakini nikaja gundua kisasi na simu yangu hakikuniisha moyoni nil...

KESHO HAIJULIKANI @Ishi Ki kamilifu

Image
Na Omar Zongo Siku za mwisho kabla ya kifo chako nakiri niliona mabadiliko ya kitabia! ulipenda kukaa mwenyewe! upole ulikuvaa na hata chakula kilikuwa hakipandi jambo ambalo silakawaida kwako, kiukweli upweke niliuona kupitia macho yako na sijui kwanini nilikupuuza. leo natamani kujua nini chanzo cha wewe kuwa hivyo lakini sina namna yakusikia sauti yako ikinieleza. je ni hali ngumu ya maisha ulikosa dira na muongozo??? mimi sijui.. je ni mapenzi yalikuvuruga kiasi kwamba ukakosa ushauri wangu mimi kaka ako hivyo ukaamua kujimaliza??? hili pia mimi sijui wakati mwengine nawaza labda kutokuwa karibu tena nawewe tukibadilishana mawazo, kucheka na kutaniana ndio chanzo maana ni ukweli kuwa ulinizoea sana na ni mimi pekee ndio nilikuwa kaka na rafiki yako pia. bado hili nalo sina uhakika nalo pia. kwa ufupi nateseka kwa kutaka kujua kilichokufanya ukakatisha pumzi yako. sijui kwanini sikutilia maanani nilikupuuza uliponiomba kuzungumza nami hata sauti yako iki...

TWENDAPO WAZEE HAWATAKUWEPO!!!

Image
"Huko twendako, siku baada ya hizi nina uhakika wazee watakuwa viumbe adimu kuonekana katika sura ya dunia hii! sababu ni nyingi lakini chache kati ya hizo ndizo nitakazoziwekea mkazo katika andiko langu la leo!" Na Omar Zongo Baridi kali inayopuliza mwilini inasababisha mwili usisimke kwa woga vinyweleo visimame, hali hii ya hewa ni sababu tosha kwa wavivu kuvuta shuka hasa mishale hii ya asubuhi lakini kwangu ni tofauti, saa kumi kamili za alfajiri niko macho natafakari utashi wa MUNGU. tafakuri yangu hiyo inaenda sambamba na vitendo vyangu takatifu vyakujiandaa kwenda masjid kumsujudia mwenye dunia hii, mwenzenu imani yangu ni muislamu lakini namshukuru MUNGU sijawahi kukashifu imani za wengine. vitendo vyangu vya maandalizi yakujiweka safi kimwili na kiimani vinachukua kama dakika kumi na tano hivi, najipuliza marashi, navaa msuli wangu kwa kuukunja vema mkwiji, shati langu safi nililoliandaa kwa ajili ya swala ile kisha nalisindikizia na koti ku...

SAUTI YA MUNGU

Image
  Anaandika  Omar Zongo wakati mwengine ukiwaza sanaaaa utagundua kuwa hauna faida yoyote kwa mwenzio wala yeye hana faida yoyote kwako! ukiendelea kuwaza sanaa utagundua ni MUNGU pekee ndio mwenye faida kwenu wote, na ukiendelea kuwaza sanaa utagundua mnashobokeana, kufuatiliana kujuliana hali na kujaliana kutokana na Amri ya huyo  MUNGU ambaye ametuamrisha tupendane na ni dhambi kuchukiana. ukiwa unaendelea kuwaza sanaa utazidi kubaini kuwa anaekupuuza kutojali uwepo wako na kukupotezea hauna sababu yoyote yakumshobokea, kumfutalia nakumjali lakini ajabu ukiendelea kuwaza sanaa utagundua kuwa kufanya hivyo nikumuudhi MUNGU wako ambaye anakujali wewe kwa ukarimu mkuu! na niyeye ndiye aliyekuamrisha umpende adui yako! ukiwa hujachoka kuwaza utagundua kuwa kuna kitu kinaitwa uvumilivu kinahitajika sana ili uwende sawa na watu wote maana wameumbwa kwa mitihani usipoangalia unaweza ukaamka asubuhi moja nakuwatukana wote kwa kuwa hawana faida kwako! ukiwa unaendelea k...

NIHESHIMU MKE WANGU

Image
Unakumbuka maisha yako kabla sijakuoa?? ulikuwa hauna tofauti na bidhaa yakukodiwa ambayo ilikuwa ikitumiwa nakurudishwa ili mwengine aje aikodi tena. maisha yako yalikuwa na uhuru wakukudharaulisha. wapo wanaume wengi kama mimi walikufata nakukutumia bila hata kuwaza kuwa unastahili kuolewa. kitendo cha mimi leo kutimiza ahadi yangu nakukuoa kinatosha kabisa kufanya wewe uniheshimu. sio kama sijaona mapungufu yako au wewe ndio mwanamke mkalimilifu kuliko wote laa hasha! nimekuoa kwasababu nimeamua kukupokea kwa jinsi ulivyo so inatosha kabisa wewe kuniheshimu. kwani hujasikia fununu kuwa duniani wanawake mpo wengi kuliko wanaume sasa kwanini usione bahati kubwa kwako kuchaguliwa namimi nakuolewa eti huoni kuwa nastahili kuheshimiwa nawewe?? Niheshimu mke wangu sababu nahisi kuwa nimekuvisha stara nakukutofautisha na wanawake wengine wahuni wanaotumiwa nakuachwa kila siku, naamini kuwa hayo sio maisha mazuri yanayompendeza binti yeyote hivyo niheshimu mume wako ...

MWENYE SIFA HIZI AJE!!!

Image
Awe na kinywa tulivu chenye ulimi asali, neno lake tulizo sauti yake gitaa. umbo lake pambo, mvuto kwa jicho langu, rangi ladha tamu si mweupe si mweusi! lafudhi yake wimbo lahaja iwe ya pwani, sikio lipumbazike aniitapo jina. aniduwaze na mwendo mithili yake hapana kaumbwa kwa mapambo na Mungu wa sifa njema. upole tabia yake si binti wa pekepeke imani vazi lake hofu kwa Mungu wake. kajaaliwa midomo unene wa kitumbua jicho lake legevu MUNGU kalipaka kungu. nijione Adamu naye ndiye Hawa Wangu tena anipe faraja tabasamu lake afya. Ngozi yake mboga wala sio yakughushi mchicha na matembele si maji wala mchina. kauli yake dira, upole ndo vazi lake wala hawezi kuzira subira tabia yake. roho yake imani, uchamungu matendo yake, adui yake shetani tumaini lake MUNGU. mwenye sifa hizi nani namgojea afike simtaki hayawani akija nifilisike. sitaki jibu dhalili eti nimuumbe mwenyewe naahidi kumsubiri hata kama yu tumboni. akijue kiswahili maneno yake matamu, kizungu sist...

JUNIOR

Image
 "Sikuwahi kusimulia kisa cha kweli nikakiruhusu kusomwa na watu pengine hii inaweza kuwa simulizi yangu ya kwanza yenye ukweli ndani yake, ni zawadi kwa ndugu yangu Ramadhan Madebe ambaye kwa asilimia kubwa amechangia ukamilifu wa simulizi hii....ni sehemu ndogo pekee ndio yakubuni lakini mengi yana ukweli....." JUNIOR SEHEMU YA KWANZA Niliona wivu sana baada ya rafiki yangu kupewa jina na dada yako, yeye aliitwa mwinjuma lakini alimbeza jina lake hilo na akasema kuwa anapendeza zaidi akiitwa Geminus! Leo ndio nagundua kuwa aina ya familia bora kama ilivyo ya kwenu ndiyo huwaaribu watoto nakuwafanya wayachukie majina ya Kiswahili kutokana na wao kukesha wakitazama filamu za kizungu na kihispania. Hata kama muhusika mkuu katika filamu ya kizungu akitokea anaitwa Zongo, mradi ni mzungu na anacheza vizuri kwenye nafasi yake basi jina hilo linaweza kuwa ni jina zuri kuliko yote duniani. Kiukweli licha ya kuwa akili yangu ndogo lakini imebaini kuwa hili ...

UMESAHAULIKA BABA WA KISWAHILI

Image
Imekuwa ni desturi yangu kuenzi harakati zako kila siku hasa kipindi ambacho ni kumbukizi ya kifo chako mithili yakuzima kwa mshumaa uliokuwa ukimulika fasihi andishi yenye tija na akili kubwa kwa miongo kadhaa sasa yaani tangu na baada ya kifo chako. Baba wa kiswahili, Shaaban Robert  (kuzaliwa 1 January 1909 – kufa 20 June 1962) Nionacho leo kuhusu kuenzi mchango wako ni USAHAULIFU MKUU, kiukweli UMESAHAULIKA BABA WA KISWAHILI!  Anasimulia Omar Zongo  Naona aibu kusema kuwa natamani ule utashi wako walau ungeuacha sehemu kisha ukaniagiza hata ndotoni nikauchukue niutumie kuendeleza falsafa zako na utamu wa Kiswahili uliopo ndani yako. Nasikitika ninapogundua kuwa 20 june wakati unafariki ulikusanya kila kilicho chako nakuelekea nacho kaburini, sitaki kusema kuwa hilo limetokea kutokana na uchoyo wako laa hasha ila nakulaumu kwanini hukutaka kumuachia mtu arithi angalau robo ya unguli wako wa kutumia vema hii lugha Kiswahili katika maandishi. Ni...