Posts

NIMEZAMA TOPENI

Image
uvundo nausikia, karaha tupu puani. tope hili madhara, afya yangu hatiani. sinayo hamu yakula njaa ingali tumboni. ninani wakunitoa nimezama topeni! siwezi kujinasua tope limeniganda nashindwa kujiondoa,kihoro kimenipanda. masaa yanasogea joto lazidi kupanda tope lanizidia mwili wote waganda tope hili maajabu launguza mwili wangu nimepuuza ya babu na sasa majuto yangu ubishi ndio sababu wahaya mateso yangu, nani sasa wakutibu matope mwilini mwangu. sina wakumlaumu kadhia mejitakia tope hili lasumu nimezama kwa umbea! sinayo tena hamu, mecheza pata potea meupata ugumu kwa nnayojionea ombea yasikupate,utageuka msongo. niliambiwa ningoje nikaona ni porojo, nikauvaa mtope sasa wanipa kipigo zamishwa mwili wote iliyobaki ni shingo tope flani karaha, kulijua ni vibaya limejua kunihadaa bila soni wala haya chini yake nimekaa, siwezi tena kimbia maumivu majeraha nafsi yangu yajutia mwanzo niliona tamu kuchezea tope hili,  lilinikidhi na hamu, sikuiona shubir...

ASANTENI KWA HISTORIA

Image
"Zaidi ya miaka 50 tangu kufanyike mapinduzi matakatifu visiwani zanzibar, mapinduzi ambayo yamewaweka huru ndugu zetu visiwani humo, hakika historia ya zanzibar imejiandika vema kupitia wana mapinduzi wakiongozwa na Sheikh Abeid Aman Karume na wengine wengi kama vile Okelo na wengineo..leo naifurahia historia ya zanzibar na nawashukuru wanamapinduzi kwa kutuachia historia hii yenye funzo kubwa kwetu, funzo la uzalendo na ujasiri . Na Omar Zongo  Historia ilotukuka, historia ya heshima, historia isofutika, asanteni kwa historia. Meshika kitabu changu aliniachia babu, kitabu cha mapinduzi kina nyingi historia. Kitabu chanikumbusha niishi kwa uzalendo, maovu kuyaondosha nisimamie upendo, upendo wa watu wangu, upendo wa nchi yangu, upendo kwa taifa langu. Asanteni kwa historia. Historia yanifunza nisiishi kiunyonge mgeni nisomuelewa nimfukuze aende. Historia hii tamu, nzuri tena adimu, historia  adhimu, yanipenya kwenye damu. Historia yasema wenyeji walisimama, ha...

NIMEPATA PESA

Image
Na. BinZongo Shida shida sasa basi tayari ninazo pesa! Pesa nyingi za kuzidi sio zile za mawazo. Nabadilisha mavazi, chakula nikipendacho, magari ya kila rangi kampuni tofauti. Jumba langu ni 'palace' mtawala ndio mie Limezingirwa Na fensi, himaya kubwa ijue. Ulinzi imara sana, majambazi halahala! Mabaya mtayavuna mkija kifalafala. Niite bosi, tajiri we mwenyewe siunaona! Yajana siyakumbuki usije yataja tena. Dhiki ndio kitu gani! Habari zakizamani ukinitajia tena shtaka mahakamani. Kwasasa pesa ninayo mpenzi naomba nielewe maamuzi yafuatayo naomba uyatambue Nahisi haunifai, kuishi nawe aibu, japo tumetoka mbali ila sasa Tabutabu. Siwezi tumia nawe pesa hizi pomoni, nataka mtu mwengine nimuingize moyoni Sema nikupe nini ili tuachane leo, tusahau yazamani sasa nimepanda cheo. Umasikini enzi zetu utajiri zama nyengine. Pesa sasa zanitosha kumtafuta mwengine. Ongeza basi mvinyo tuendelee kuongea, hivi sasa nina meno natafuna hili penzi. Tafuta aina y...

MWANAMKENDEGE ; USHAIRI

Image
 hadith hadith njoo simulizi lake sikio naanza safisha koo nikupe langu tukio eneo nikariakoo sikujua mwanamkendege ushungi, umbo na guu mahabani kazamia kiunoni kichuguu moyoni nikaridhia yalonisibu makuu sikujua  mwanamkendege tabasamu lake lahaja nikaona njia nyeupe amejazia mapaja si mweusi si mweupe Radhia jina kataja sikujua  mwanamkendege lafudhi yake yalamu tamko lake murua midomo yake adhimu kicheko kajaaliwa kumbe mja haramu sikujua  mwanamkendege sikujua  mwanamkendege kuuza yake tabia ucheshi wake nizengwe pesa kushadadia ukiwa nacho twende mwanzoni sikutambua kwa miguu miwili nikazama nae hubani sikutaka subiri kumfikisha nyumbani kumbe ndumilakuwili sikujua  mwanamkendege alianzia kwa kaka ushemeji kukataa akasema anataka nayeye kuzima taa mwenzenu yamenifika sikujua  mwanamkendege ndugu kunihabarisha nimepotea gizani mie nikakanusha kwamba haiwezekani kaka uongo kazusha sikujua mwanam...

MUHIMU KUJUA @ukweli unaumbua

Image
Ukweli unapotaka kudhihirika kamwe hauwezi kuzuiliwa na nguvu ama utashi wowote alionao mwanadamu. amini nakwambia ukweli una nguvu adimu ambayo haizuiliwi kamwe na vitu kama Pesa, maneno mengi, cheo, huruma wala kujuana. Ukweli ni jambo la kuajabia maana lina 40 zake kama ilivyo kwa siku za mwizi. Ukweli unapotaka kudhihirika haupokei rushwa wala hongo tena humchagua yoyote hata awe ndio bingwa wa uongo siku hiyo hujikuta akianika sura ya ukweli mbele za watu. Ni ukweli pekee ndio ambao huruhusu wenyewe kufichwa lakini unapotaka kujidhihiri hujidhiri wenyewe kwa njia zake. ukweli jambo balaa ambalo nalistaajabia lilivyokaa! maana lenyewe ndio linaruhusu kukumbatiwa na waongo tena wakiruhusu vitu kama Chuki, Uadui, Mauaji, Ubinafsi, Rohombaya na choyo vivae vazi la Upendo, Urafiki, Wema na Kusaidiana na siku ukweli ukijiachia hubaki aibu kwa watu hao waongo. Mra nyingi sifa za ukweli huumiza na ndio maana wengi wetu hatupendi kusadiki mambo ya kweli mbaya zaidi tu...

Dear Septemba....

Image
 "Mwezi ambao nimezaliwa mimi, Mwezi ambao nauthamini, sijui kwanini hua unakuja nakuondoka mwezi huu, September"   Na. Omar Zongo   Unaelekea wapi mpendwa!? iweje unishushe hapa duniani kisha uniache kama hunijui! ninani mwenyeji wangu!? inamaana lengo lako nikunileta kisha unitelekeze!! Jibu lako la jana usiku wakati ukifungusha nguo zako bado nalifikiria eti "nitakomazwa na octoba, novemba na december" hivi mie nawajulia wapi watu hao! niwewe ndio umenileta hapa duniani niwewe ndio nimekuandika kwenye historia! niwewe ndio nakufahamu bosi wangu kwanini lakini unanifanyia hivi!! basi ungeniambia mapema kuwa lengo lako nikunishusha tu duniani halafu utaniacha! ndio ungeniambia namimi nikajiandaa kisaikolojia! nani atanidekeza kama wewe! nani atajua kuwa nimezaliwa katika moja ya siku zako! ninani atajua kuwa nina vinasaba vya baraka zako! hujisikii vibaya labda siku ile unanishusha duniani watu walishangilia kila mmoja akisema "Wak...

chuki shairi

Image
chuki imekuwa vazi,  limewakaa mwilini. kulivua kwao kazi, haling'oki mauongoni kama dunia twapita chuki ya kazi gani. imewakaa mwilini imetuwama nyoyoni. yajionyesha machoni, imegeuka miwani. kama dunia twapita chuki ya kazi gani. chuki pini nyembamba yapenya kotekote si baba wala mjomba atakuchuki yoyote kama dunia twapita chuki ya kazi gani chuki ikikuhadaa pigana kuiambaa ni jumba la karaha sio kiti chakukaa kama dunia twapita chuki ya kazi gani. chuki ina hila zote haingojei sababu ikukuzidia kete itakuvaa taabu hii dunia twapita chuki ya kazi gani dunia hii twapita hatutaishi dawamu litakufika gharika chuki haina nidhamu swali nakuswalika chuki ya kazi gani ulimwengu una adha njiaze kadha wakadha itakupata bughudha fakiri wakujifunza kama dunia twapita chuki ya kazi gani.