WARAKA WA JPM

Huu ni waraka wa kufikirika wa Hayati John Pombe Magufuli, Rais awamu ya tano wa Tanzania ambaye alifariki dunia usiku wa tarehe 17 march mwaka 2021... Muandishi wa waraka huu ni Omar Zongo Kutokea Eneo ambalo wanaenda waliokufa tumepokea waraka huu. Waraka wa JPM. Anasema.... Ndugu zangu watanzania, ile siku ambayo roho yangu iliusaliti mwili wangu, ilikuwa ndio siku ya kwanza ya mimi na ninyi kutenganishwa katika ulimwengu huu wa Roho na Mwili. Sikuwa na namna yoyote ya kupinga rungu la malaika mtoa roho, ninachoshukuru ni kwamba udongo umeudhibiti mwili wangu lakini Roho yangu ingali hai hata kupata uwezo wa kuyaona yanayoendelea Duniani, lakini zaidi kuwaandikia waraka huu. Nimelazimika kuuandika waraka huu kwa sababu nyingi lakini kubwa ni hili tendo linalotarajiwa kujiri hivi karibuni Tendo la kuuaga mwaka uliogharimu maisha yangu. Najua nimesaliti kiapo cha Uongozi, kwa kuwaacha kabla ya muda, lakini ningewezaje kupinga mapenzi yake Mungu. Katika waraka w...