ACHA!! USING'ANG'ANIE MAHUSIANO YALIYOISHA MUDA WAKE.
Kuanzisha mahusiano ya mapenzi sio dhambi wala jambo baya katika akili ya yeyote aliye timamu. Lakini ubaya unakuja jitokeza pale ambapo mnashindwana na kushindwa kuamini kama mmeshindwana hivyo kubaki mnavumiliana, mkikondeshana, kudharauliana, kutukanana, kupigana na wakati mwengine hata kuuana. Jifunze leo hapa kumuacha aende zake, kuitambua,kuiheshimu na kuitumia vizuri siku. Siku ya kuachana. Na. Omar zongo. Hakikisha muda wa kuachana ukifika unafanya hima muachane. Using'ang'anie bidhaa ambayo imefika tamati Yake ya matumizi. Hiyo tayari ni sumu kukuua si ajabu! Muda wa kuachana una dalili na upo dhahiri. Ukiona tu mambo yamebadilika, upendo umechujuka, taa imezimika, nakusihi ondoka. Hakuna Tena zile 'baby' na 'sweetheart' unaitwa kwa jina lako, au 'Apple' na 'Chocolate' ujue ndio mwisho wako. Kitendo cha 'text' kupungua, zile 'I miss you' kupotea na hakuna kujishtukia ujue muda umewadia. Muda wa kuchokana una nyingi tash...