Posts

Showing posts from 2019

Kifo chako kikitokea

Image
Kifo chako kikitokea, kitawashtua wanaokujua Na wengi watakulilia lakini zaidi watakaoumia ni wale walio karibu na wewe! Pia kwasasa upo hai,Wapo ambao unawakera nakuwaudhi lakini kwa unafki wao siku hiyo watasema kuwa wewe ni mtu mwema sana. Moja ya fikra zako muda huu upo hai ni labda siku ukifa mzigo wa majukumu yako ataubeba ndugu yako flani, kisa anakuchekea, anawafurahia watoto wako, mke au mume wako. Labda kisa mnasaidiana sana na ushamtendea mema mengi! Unajifariji huenda yeye atavaa viatu vyako, atawasomesha kwa moyo mmoja, atawaongoza nakuwafariji bila Tatizo. Sipingi hisia zako inawezekana zipo sahihi, lakini acha nikufikirishe tofauti kidogo! Tambua kuwa binaadamu tumeumbwa Na unafiki wa asili! Wengi wao waliokufa walijifariji kama wewe lakini matokeo yake watoto wao wanadhalilika, ni ombaomba Na wengine hawana ndoto tena. Au wengine walibahatika kulelewa lakini kwa dhiki Na masimango makubwa, makovu ya mateso waliyopitia wanayakumbuka hadi Leo. Ipo hivyo r...