'Watu'
Kwa tabu sana Mzee alijisogeza juu ya kitanda nakulaza shingo yake kwenye mto. Uchovu wa maradhi ulimdhoofisha vyakutosha, macho yake yaliashiria kukata tamaa, lakini alijikaza kiume. Alinitazama Na kisha akasema. "Ilikuwa ni siku ambayo kila mtu alinisema vibaya nakunizungumzia vibaya, lawama za kila rangi nilipakwa, Hakuna aliyejuwa niwapi nimeelekea nawewe, ulikuwa bado mchanga kabisa. Nimimi pekee ndio nilijua dhamira yakutoroka nawewe siku ile, Kwakweli Siku ile nilikuwa naingojea kwa hamu sana ifike sababu nilidhamiria kuzungumza nawewe. Nilitoroka nawewe nikaenda mbali kidogo Na nyumba yetu, Ulikuwa una siku 40 tu tangu uzaliwe, nafikiri ndio maana watu walinishangaa sana kuondoka nawewe, tena bila kuwaaga. Nilienda nawewe mahala nilipopajua mwenyewe, Ninachoshukuru nikwamba nilichodhamiria kilifanikiwa. Nilizungumza yote na naamini uliyasikia maana hata kawaida yako yakulia siku ile sikuiona kabisa. Ulinyamaza tuli kana kwamba ulikuwa mkubwa kumbe n...