MARIA & CONSOLATHA : KILELE CHA HUZUNI

Na. Omar Zongo Nimekaa juu ya kichuguu, katika kilele cha mlima wa huzuni, naangaza chini kutazama mandhari ya kijani kinachopamba msitu wa Mauti uliopakana na kijiji cha Majonzi kilichopo pembezoni kabisa mwa Taifa huru Tanzania. Nimelazimika kuja huku juu ya kilima kukaa kwa siku saba za maombelezo ya wadogo zangu, dada zangu, watanzania wenzangu wazalendo Maria Na Consolatha. Juu ya kichuguu cha mlima Huzuni, natafakari maisha ya mabinti hawa waliogusa mitima ya wengi afrika mashariki Na Duniani kwa ujumla. Nani asiyeguswa Na khabari za wadada hawa!!?? Tangu maisha yao ya utoto mpaka ukubwa wao wakishangaza watu Na Utashi wao wakung'amua mambo katika masomo yao Na ndoto kubwa zakulitumikia Taifa lao. Kuungana kwao ulikuwa ni umoja ulio Na nguvu ambao daima ulidhihirisha kuwa utengano ni udhaifu. Kama mapambano ya kupigania uhai yangelikuwa Na mafanikio naamini Consolatha Na Maria wangelikuwa washindi Na mpaka Leo wangekuwa miongoni Mwa tulio hai. Lakini sivyo!...