UONGO WA MAMA 'ANGU

Ni Simulizi niliyoitohoa kutoka kwenye clip flani iv yakizungu. Nimeweka Utashi wangu ili kufikisha ujumbe kama uliokuwepo kwenye clip ile, sijacopy nikapaste, kuna vingi nimebadili kuleta uhalisia... Na. Omar Zongo "Usihuzunike, sihisi maumivu, najiona nina afadhali!" Huu ndio ulikuwa uongo wake wa mwisho kuniambia!! Baada ya hapo alifumba macho na hakuweza kufumbua tena. Roho yake ikaacha mwili! Leo ndio nakumbuka, mama yangu alikuwa Muongo, hata kabla ya siku hii ya mwisho. Nakumbuka, wakati mdogo, mara nyingi chakula chetu kidogo kinachopatikana, yeye alikuwa hali na alikuwa akisema "nimeshiba kijana wangu, kula wewe ushibe!" Nilikuwa namshuhudia akiokoteza mifupa ya samaki niliyobakisha mimi. Hata nilipokuwa nikimbakishia minofu ya samaki alikataa kabisa akisema hapendi samaki!! Nilipoanza shule ya awali, ilimbidi afanye kazi mbilimbili ili aweze kumudu ada za shule. Hakupata muda wakupumzika! Mara zote nilipokuwa nikishtuka us...