NIONE KABLA SIJAZIKWA @Sauti ya Akwi

Ijumaa tarehe 16 mwezi wa pili, 2018 Mpaka saa tatu usiku muda naenda kulala bado nilikuwa sijapata taarifa zozote kuhusu msichana aliyepigwa risasi Na polisi. Hii ni ajabu kwakweli!!! Ni kawaida yangu kabla yakulala kuvinjari mtandaoni kujua matukio muhimu yaliyo Na yanayoendea kujiri nchini kwangu Na kwengineko. Nashangaa kwanini sikuliona tukio hili Tanzia. Anyway namshukuru MUNGU huenda alitaka iwe hivyo ili usingizi wangu usiwe wa mang'am ng'am. Lakini inawezekana vipi mpaka saa nane usiku nashtuka naingia mitandaoni kuona yaliyojiri usiku bado nisione hili tukio!! Mpaka kesho nitaendelea kujiuliza kwanini tukio hili lilichelewa kunifikia. Nakumbuka usiku ule nilivinjari mtandaoni kutazama zaidi maandalizi ya uchaguzi mdogo kwenye jimbo la kinondoni, Dar es salaam na lile la Siha, Kilimanjaro pamoja na kata nane ambazo nazo zilikuwa na pengo la madiwani. Nakumbuka usiku ule zaidi nilifuatilia maagizo ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Kaijage. Aliku...