Posts

Showing posts from January, 2018

NIMEZAMA TOPENI

Image
uvundo nausikia, karaha tupu puani. tope hili madhara, afya yangu hatiani. sinayo hamu yakula njaa ingali tumboni. ninani wakunitoa nimezama topeni! siwezi kujinasua tope limeniganda nashindwa kujiondoa,kihoro kimenipanda. masaa yanasogea joto lazidi kupanda tope lanizidia mwili wote waganda tope hili maajabu launguza mwili wangu nimepuuza ya babu na sasa majuto yangu ubishi ndio sababu wahaya mateso yangu, nani sasa wakutibu matope mwilini mwangu. sina wakumlaumu kadhia mejitakia tope hili lasumu nimezama kwa umbea! sinayo tena hamu, mecheza pata potea meupata ugumu kwa nnayojionea ombea yasikupate,utageuka msongo. niliambiwa ningoje nikaona ni porojo, nikauvaa mtope sasa wanipa kipigo zamishwa mwili wote iliyobaki ni shingo tope flani karaha, kulijua ni vibaya limejua kunihadaa bila soni wala haya chini yake nimekaa, siwezi tena kimbia maumivu majeraha nafsi yangu yajutia mwanzo niliona tamu kuchezea tope hili,  lilinikidhi na hamu, sikuiona shubir...

ASANTENI KWA HISTORIA

Image
"Zaidi ya miaka 50 tangu kufanyike mapinduzi matakatifu visiwani zanzibar, mapinduzi ambayo yamewaweka huru ndugu zetu visiwani humo, hakika historia ya zanzibar imejiandika vema kupitia wana mapinduzi wakiongozwa na Sheikh Abeid Aman Karume na wengine wengi kama vile Okelo na wengineo..leo naifurahia historia ya zanzibar na nawashukuru wanamapinduzi kwa kutuachia historia hii yenye funzo kubwa kwetu, funzo la uzalendo na ujasiri . Na Omar Zongo  Historia ilotukuka, historia ya heshima, historia isofutika, asanteni kwa historia. Meshika kitabu changu aliniachia babu, kitabu cha mapinduzi kina nyingi historia. Kitabu chanikumbusha niishi kwa uzalendo, maovu kuyaondosha nisimamie upendo, upendo wa watu wangu, upendo wa nchi yangu, upendo kwa taifa langu. Asanteni kwa historia. Historia yanifunza nisiishi kiunyonge mgeni nisomuelewa nimfukuze aende. Historia hii tamu, nzuri tena adimu, historia  adhimu, yanipenya kwenye damu. Historia yasema wenyeji walisimama, ha...

NIMEPATA PESA

Image
Na. BinZongo Shida shida sasa basi tayari ninazo pesa! Pesa nyingi za kuzidi sio zile za mawazo. Nabadilisha mavazi, chakula nikipendacho, magari ya kila rangi kampuni tofauti. Jumba langu ni 'palace' mtawala ndio mie Limezingirwa Na fensi, himaya kubwa ijue. Ulinzi imara sana, majambazi halahala! Mabaya mtayavuna mkija kifalafala. Niite bosi, tajiri we mwenyewe siunaona! Yajana siyakumbuki usije yataja tena. Dhiki ndio kitu gani! Habari zakizamani ukinitajia tena shtaka mahakamani. Kwasasa pesa ninayo mpenzi naomba nielewe maamuzi yafuatayo naomba uyatambue Nahisi haunifai, kuishi nawe aibu, japo tumetoka mbali ila sasa Tabutabu. Siwezi tumia nawe pesa hizi pomoni, nataka mtu mwengine nimuingize moyoni Sema nikupe nini ili tuachane leo, tusahau yazamani sasa nimepanda cheo. Umasikini enzi zetu utajiri zama nyengine. Pesa sasa zanitosha kumtafuta mwengine. Ongeza basi mvinyo tuendelee kuongea, hivi sasa nina meno natafuna hili penzi. Tafuta aina y...