Posts

Showing posts from 2018

RUDI KWA MAMA

Image
Na. Omar Zongo Wino huu uliomwagika umeandikwa Na yatima asiye Na baba wala mama! Mwenye machungu ya kumbukumbu kila atazamapo picha za wazazi wake! Mwenye tamaa yakuzungumza Na mama kumwambia anampenda! Nakushauriana na baba jinsi dunia inavyokwenda. Leo wino wangu umebeba dhamira yakukumbusha urudi kwa Mama. Usiseme hakuna sababu yamsingi yakwenda kumsalimia mama! Ukifanyacho kinakupa riziki, mafanikio na utajiri lakini vitu hivyo ni vichungu siku utakapokuwa huwaoni wazazi wako. Siku watakapokuwa mbali Na upeo wa macho yako! Siku nawewe utakapokuwa yatima. Rudi kwamama! Nenda kamwambie unampenda sana! Kaseme nae yote yakwako naumsikilize yote yakwake. Hakikisha anafarijika kwa uwepo wako! Usitoe hata dakika akahisi upweke! Akahisi umemtenga nakuzipa thamani kazi zako au watu wako wengine ulionao. Kumbuka wao wanakuona wamuhimu, mwenye nguvu Na wathamani! Kwasababu ya juhudi za wazazi wako. Walikesha nawewe ulipokuwa unawasumbua ukilia usiku kucha enzi ...

'Watu'

Image
Kwa tabu sana Mzee alijisogeza juu ya kitanda nakulaza shingo yake kwenye mto. Uchovu wa maradhi ulimdhoofisha vyakutosha, macho yake yaliashiria kukata tamaa, lakini alijikaza kiume. Alinitazama Na kisha akasema. "Ilikuwa ni siku ambayo kila mtu alinisema vibaya nakunizungumzia vibaya, lawama za kila rangi nilipakwa, Hakuna aliyejuwa niwapi nimeelekea nawewe, ulikuwa bado mchanga kabisa. Nimimi pekee ndio nilijua dhamira yakutoroka nawewe siku ile, Kwakweli Siku ile nilikuwa naingojea kwa hamu sana ifike sababu nilidhamiria kuzungumza nawewe. Nilitoroka nawewe nikaenda mbali kidogo Na nyumba yetu, Ulikuwa una siku 40 tu tangu uzaliwe, nafikiri ndio maana watu walinishangaa sana kuondoka nawewe, tena bila kuwaaga. Nilienda nawewe mahala nilipopajua mwenyewe, Ninachoshukuru nikwamba nilichodhamiria kilifanikiwa. Nilizungumza yote na naamini uliyasikia maana hata kawaida yako yakulia siku ile sikuiona kabisa. Ulinyamaza tuli kana kwamba ulikuwa mkubwa kumbe n...

Tafakari Wengine

Image
Muda mwingi hua unautumia kutafakari mazuri yako huku ukihitaji kusifiwa, hua unatamani kuongelewa wewe tu, unatamani kuonekana  Na wote wanaokuzunguka wasifu nakukuheshimu.  Ni nadra sana mtu kutoa nafasi yakutafakari wengine, hivi ndivyo tulivyoumbwa, tumeumbwa na umimi. Unajiona Bora kuliko wengine, wewe ndio unajiona mwenye akili, busara Na ushauri mzuri unaweza kutokea kwako. Ni ajabu sana tabia hii Na kwa vile ni asili ya kuumbwa kwako sina lawama katika hilo Ila leo nataka utenge muda kutafakari wengine, kuona vipawa vyao, nafasi yao, akili zao Na tamaa zao. Ndio, Anza sasa kumfikiria mtu wako wakaribu, ana umuhimu gani kwako. Acha kuwaza wewe tu ndio mwenye umuhimu kwake. Jiulize maswali ya Je ni vipi ingekuwa kama yeye asingekuwepo. Tuanze Na msaidizi wako wa kazi za ndani. Yeye anafua nguo zako, anakupikia, anakufanyia usafi wa nyumba n.k. Acha kiburi chakusema hata kama asingekuwepo ungetafuta mwengine fikiria kuna watu duniani wanatafuta msa...

Mpumbavu 'Shida'

Image
Huna stara, vazi lako ni fedheha, aibu hata huna waadhirisha wazee. Mpumbavu shida. Wafanya mtu awe lofa penye sio aseme ndio, mjinga baradhuli huna utu ata chembe. Ujio wako ni waghafla, hodi kwenu hujafunzwa, harufu yako inatesa pua zote ni madonda. Mpumbavu shida. Kwani kwenu wapi!?? Bosi wako wewe nani, ujio wako washetani ama una baraka za Mungu!? Eti!!, wapendelea nini kwenye maisha ya watu, mbona king'ang'anizi kwenye majumba ya watu!!. Ujira wako upi, kumdhalilisha baba, umefaidika nini kumuandama mama!?? Eti mpumbavu shida!! Nani kakuagiza kwangu, ina maana umeshamalizana na mke wa jirani yangu?? Nani kakupa kiburi,  Shida kuandama watu, hata laana za wahenga shida hazijakupata!! Acha ya mbaraka mwishehe kuna laana ya babu yangu, ulimuandama mpaka kifo shida kweli baradhuli. Okey shida! Keti chini puuza maneno yangu. Zungumza nami Leo nani kakuagiza!?? Kama rushwa nikupe uwaache watu huru! Waache watoto wetu, waache wazazi wetu, waache viong...

Nachora Picha

Image
Hata kama sio mzuri kwenye kuchora lakini Leo naanza rasmi kuchora picha. Picha ya kusisimua, Picha yenye kupendeza, Picha niipendayo, Leo rasmi naichora. Kwanza ile nyumba yangu nnayoiota kila siku. Naanza kuchora kiwanja eneo flani tulivu, upepo flani mwanana, uwanja wake mkubwa. Nachora eneo la kuogelea, eneo lakupumzikia, eneo lakuchezea Na eneo la hifadhi ya ndege Na wanyama Nawachora wanyama, ndege na miti mingi nawaweka humu ndani katika eneo Lao maalum. Nauchora uzio mrefu wa nyumba yangu, nauwekea umeme kuilinda nyumba yangu. Nachora mageti mengi nawaweka Na walinzi nayachora Na magari mazuri ya kila aina nayaweka kwenye 'parking' ya kwenye hii nyumba yangu. Nachora picha ya ndani ya vyumba vya nyumba yangu, kila chumba choo ndani ni nzuri picha yangu.. Rangi flani za amani zinapamba nyumba yangu, ukumbi mkubwa ndani yapendeza nyumba yangu. Nachora samani zote zifaazo ndani, tena zile zakisasa zenye mvuto wa juu. Naichora bahari eneo la mbele...

USIJIELEZEE SAAANA!

Image
We jamaa!! Umerudi home mapema kabla ya mpenzi wako, umekuta nguo zako Na za mkeo zimeanikwa nje!! Umeamua kuanua ili uziingize ndani!! Bila kujua unaanua nguo ya ndani ya jirani yako(wakike), unaingiza ndani. Dakika chache tu jirani yako anagonga mlango, unamkaribisha anaingia, Anaulizia nguo yake kama umeondoa kwenye kamba bahati mbaya, Unamwambia asubiri umuangalize, Ametoka kuoga yuko Na khanga moja tu. Unamlaani shetani, unaingia chumbani nakuanza kuchangua manguo uliyoanua! Unaiona nguo ya ndani ya rangi ya pinki. Unatoka nayo fasta, ili isiwe msala, unamkabidhi. Anatoka nje mara paaap, uso kwa uso na mwanamke wako anatoka kazini. Wivu wa mapenzi unamvaa mkeo, anatazama jirani alivyonona Na khanga moja, anajiaminisha kabisa kuwa ametoka kutenda dhambi Na wewe!! Khanga moja, imeloa!! Mbaya zaidi mkononi kashika nguo ya ndani!! Hata ni mimi nisingeelewa!! Mkeo analianzisha pale nje, anamshukia Na mineno mikali jirani yenu. Jirani mpole,  hajibu...

This Iz My Sister

Image
Na. OMAr ZONGo Hey niaje, naitwa Jayvny, kwetu tumezaliwa wawili tu, mimi na dada 'angu, yeye anaitwa Jackline. Tumepishana miaka sita mimi nayeye!!, tunapendana sana mimi na dada angu licha ya yakwamba tumetofautiana baba. Nataka kukupa kitu chakujifunza Leo kutoka kwa dada 'angu. Sitakwambia amepitia mangapi mpaka kumuita shujaa kwenye Andiko hili ila nitakwambia kuhusu Moyo wake wa chuma. 2014 terehe 01, mwezi wa 11, ndio siku tulimpoteza mama etu, nikiwa Na umri wa miaka 16. Mama aliondoka ghafla duniani, hakupata hata nafasi yakusema 'kwaherini wanangu'. Alituacha mimi Na dada 'angu tukiwa wakiwa, tena wapweke wenye donda kubwa la maumivu ya kifo cha mama etu mpendwa. Nakumbuka kifo cha bimkubwa kilinifanya nilie sana, nilipoteza fahamu. Nakumbuka nilipozinduka nikajikuta nimelala chumbani, kichwa changu kikiwa juu ya mapaja ya dada. Nilifumbua macho kuangaza humu ndani, vilio vya chini chini vilisikika kutoka kwa watu wengi waliomo humu...

Dunia ni jinsia Gani??

Image
Nawaza natafakari, kichwani hoja lukuki!!! Naugua na maswali dunia jinsia gani?? Yakike au kiume, dunia ni dini gani?? Kabila lake mchaga, mnyamwezi au mhehe?? Dunia asili Ipi Iraq ama brazil?? Mwenyeji wa bara lipi afrika ama ulaya?? Dunia yajua nini swahili ama Arab?? Chakula chake ni kipi ni wanga au mafuta?? Yote Mie nayawaza ila kubwa ni hili. DUNIA JINSIA GANI??? Jinsia yake ni KE au ni ME semeni!! Ina hila za kike wakati mwengine huringa! Lakini msimamo wake ni dume, umeikuta na utaiacha. Dunia ina magumu, harakati za kibabe! Tabia hii ni dume, ila utamu wakike. Imehifadhi mengi viumbe aina zote, sifa hii yakike twaitambua wote lakini mbona ni kali yatesa viumbe wake, mwanaume baradhuli hii ni sifa yake.. Dunia kama ni kike kwanini yapendelea, upendo wa mwanamke kotekote waenea. Au tuseme kidume ndio yake jinsia ila mbona pakashume yalea mpaka wambea. Dunia kama ni mama mbona huruma haina, haya tuseme ni baba matunzo yake yawapi?? Kama ni mke iseme ...

Dear tomorrow

Image
Mambo vipi?? Nataka kusema nawewe, imenilazimu kufanya ivo sababu ya hofu uliyoijenga kwa mdogo wangu Sam! Maneno yake mengi kukuhusu ameyaelezea acha nimnukuu "bro, natamani kujua vipi itakuwa kesho yangu, natamani kuona mahali nitakapoanguka, Na jee nitasimama kuendelea Na safari au ndio basi tena, kipi kitajiri kesho nijiandae nacho...nawaza sana!!" Mwisho wakunukuu!! Dear tomorrow!!  Kipi nikupe ili unimegee siri, Je ukifika yatanitokea yaliyonitokea Jana au wewe utakuja namengine mapya!? Je utakuja Na vazi liitwalo huzuni au utaniletea zawadi ya furaha? utasimamia ndoto yangu vema au utaiacha iende Na maji. Nataka dawa ya wanafiki, wazandiki, wachawi waliojificha kwenye mwamvuli wa wema, sasa niambie utakuja Na ufumbuzi wa kuwajua au ndio bado nitaendelea kuishi nao nikidhani ni watu kumbe majitu. Dear tomorrow, nakuwaza mpaka nakonda! Je utakuja Na maradhi yakunilaza au uzima wakuniimarisha?? Utasema namimi kwa upole au utanikemea kwa jazba! Ukija ...

MASWALI Unayojiuliza

Image
 NA Majibu niliyokuandalia!! No1. Nimesoma, nimemaliza nina vyeti smart sana!! Sasa kwanini sina kazi!?? Jibu lake: Kwasababu ulibweteka ukategemea elimu ikufanyie makubwa, ukasahau ulichosomea wenzako mamia wapo mtaani wamesomea!!! Hutaki kujiajiri wala kujitolea kufanya kazi bure, unaamini katika muujiza wakuitwa Na bosi uliyemtumia barua ya kazi!! Unahisi siku moja utakua meneja, kiongozi katika kampuni hiyo, unamuamini mganga aliyekutuma kuku, akakupa hirizi nakukuaminisha utapata kazi hivi karibuni. Shtuka, tafuta njia ya kujiajiri hiyo nafasi unayoitaka kuna mwenzako kaikalia Na amejizatiti kwelikweli mpaka umng'oe basi lazima uwe mzoefu zaidi yake, uwe Na ushawishi zaidi yake lakini zaidi uwe mchawi zaidi yake. Usiendelee kujiuliza swali hili acha sasa Na ubadili mtazamo. No2. Kwanini msichana akiwa Na mvuto sana nakosa ujasiri wakumtongoza!?? Jibu lake!! Kwasababu haujiamini, uzuri wake umefanikiwa kudhoofisha akili yako Na mara zote unajiambia "...

Mchamungu Maskani

Image
leo mcha Mungu nimekuja maskani umenizidi uchungu namkemea shetani enyi vijana wenzangu twendeni ibadani kwani wewe ninani mbona anaturushia stimu zipo kichwani wewe unatuzingua Ibada ndio kitu gani mbona sijakuelewa  Hili kweli nijanga vijana mwateketea Mungu anamipenda ndio mana mewajia punguzeni Maujinga shetani anawaponzea masela hili balaa maskani limeingia jamaa sijui ni njaa msikie anachoongea oyah hebu ambaa tusije kukuchengua huruma nawaonea enyi vijana wenzangu nawaomba zingatia nasaa hizi zakwangu nyakati zimewadia anawahitaji Mungu Mungu ndio kitu gani lini ulimuona akija mambo ya kizamani maskani toa kioja Mungu wetu mjani kamatia pafu piga Mungu awasamehe hamjui mlisemalo shetani tumkemee hatapata atakalo acheni niwaombe enyi mabarobaro shika adabu yako muombee mama ako hatutaki sera zako ni hora uende zako sura ka mbwa koko fanya usepe zako. maarifa ndio hamna basi pokeeni yangu nafanya kila namna kuwaokoa w...

MARIA & CONSOLATHA : KILELE CHA HUZUNI

Image
Na. Omar Zongo Nimekaa juu ya kichuguu, katika kilele cha mlima wa huzuni, naangaza chini kutazama mandhari ya kijani kinachopamba msitu wa Mauti uliopakana na kijiji cha Majonzi kilichopo pembezoni kabisa mwa Taifa huru Tanzania. Nimelazimika kuja huku juu ya kilima kukaa kwa siku saba za maombelezo ya wadogo zangu, dada zangu, watanzania wenzangu wazalendo Maria Na Consolatha. Juu ya kichuguu cha mlima Huzuni, natafakari maisha ya mabinti hawa waliogusa mitima ya wengi afrika mashariki Na Duniani kwa ujumla. Nani asiyeguswa Na khabari za wadada hawa!!?? Tangu maisha yao ya utoto mpaka ukubwa wao wakishangaza watu Na Utashi wao wakung'amua mambo katika masomo yao Na ndoto kubwa zakulitumikia Taifa lao. Kuungana kwao ulikuwa ni umoja ulio Na nguvu ambao daima ulidhihirisha kuwa utengano ni udhaifu. Kama mapambano ya kupigania uhai yangelikuwa Na mafanikio naamini Consolatha Na Maria wangelikuwa washindi Na mpaka Leo wangekuwa miongoni Mwa tulio hai. Lakini sivyo!...

UONGO WA MAMA 'ANGU

Image
Ni Simulizi niliyoitohoa kutoka kwenye clip flani iv yakizungu. Nimeweka Utashi wangu ili kufikisha ujumbe kama uliokuwepo kwenye clip ile, sijacopy nikapaste, kuna vingi nimebadili kuleta uhalisia... Na. Omar Zongo "Usihuzunike, sihisi maumivu, najiona nina afadhali!" Huu ndio ulikuwa uongo wake wa mwisho kuniambia!! Baada ya hapo alifumba macho na hakuweza kufumbua tena. Roho yake ikaacha mwili! Leo ndio nakumbuka, mama yangu alikuwa Muongo, hata kabla ya siku hii ya mwisho. Nakumbuka, wakati mdogo, mara nyingi chakula chetu kidogo kinachopatikana, yeye alikuwa hali na alikuwa akisema  "nimeshiba kijana wangu, kula wewe ushibe!" Nilikuwa namshuhudia akiokoteza mifupa ya samaki niliyobakisha mimi. Hata nilipokuwa nikimbakishia minofu ya samaki alikataa kabisa akisema hapendi samaki!! Nilipoanza shule ya awali, ilimbidi afanye kazi mbilimbili ili aweze kumudu ada za shule. Hakupata muda wakupumzika! Mara zote nilipokuwa nikishtuka us...

ANDIKO TATA

Image
Na. Omar Zongo Hili ni andiko Tata tena tupu, linalosindikizwa na ala ya simanzi! Linajichora kwa kalamu ya ukiwa kwenye karatasi ya upweke. Andiko lenye nukta ya kilio na koma ya kukata tamaa!! Andiko lenye madoa ya machozi na uchakavu wa kilio. Mwandishi nimie mkiwa mwenye tamaa ya nuru, niliyesimama njia panda mbele kiza, nyuma miba, kulia moto, kushoto mamba mwenye njaa! Mwandishi mchovu mwenye akili ya majuto! Kosa langu silijui lakini najihisi nina hatia. Duniani wakumlaumu nadhani nimimi mwenyewe!!. Naandika ilhali nina uchovu ila kwa vile ukamilifu wa Andiko nautaka siachi kujihimu niendelee ingawa kwi kwi za kilio zanikosesha umakini. Ni ipi tamati ya Andiko!! Je ni kusagwa na meno ya mamba au kushambuliwa na ncha za miba??? Je, nikupata joto Kali la moto au kupotelea kizani!?? Ninani msaidizi katika hatua yangu ijayo??? Ninani mpatanishi wa mgogoro wa nafsi yangu!?? Je nimimi mwenyewe au kudra za Mungu!?? Je ni rafiki ambaye simuoni au ndugu aki...

NIONE KABLA SIJAZIKWA @Sauti ya Akwi

Image
Ijumaa tarehe 16 mwezi wa pili, 2018 Mpaka saa tatu usiku muda naenda kulala bado nilikuwa sijapata taarifa zozote kuhusu msichana aliyepigwa risasi Na polisi. Hii ni ajabu kwakweli!!! Ni kawaida yangu kabla yakulala kuvinjari mtandaoni kujua matukio muhimu yaliyo Na yanayoendea kujiri nchini kwangu Na kwengineko. Nashangaa kwanini sikuliona tukio hili Tanzia. Anyway namshukuru MUNGU huenda alitaka iwe hivyo ili usingizi wangu usiwe wa mang'am ng'am. Lakini inawezekana vipi mpaka saa nane usiku nashtuka naingia mitandaoni kuona yaliyojiri usiku bado nisione hili tukio!! Mpaka kesho nitaendelea kujiuliza kwanini tukio hili lilichelewa kunifikia. Nakumbuka usiku ule nilivinjari mtandaoni kutazama zaidi maandalizi ya uchaguzi mdogo kwenye jimbo la kinondoni, Dar es salaam na lile la Siha, Kilimanjaro pamoja na kata nane ambazo nazo zilikuwa na pengo la madiwani. Nakumbuka usiku ule zaidi nilifuatilia maagizo ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Kaijage. Aliku...

NIMEZAMA TOPENI

Image
uvundo nausikia, karaha tupu puani. tope hili madhara, afya yangu hatiani. sinayo hamu yakula njaa ingali tumboni. ninani wakunitoa nimezama topeni! siwezi kujinasua tope limeniganda nashindwa kujiondoa,kihoro kimenipanda. masaa yanasogea joto lazidi kupanda tope lanizidia mwili wote waganda tope hili maajabu launguza mwili wangu nimepuuza ya babu na sasa majuto yangu ubishi ndio sababu wahaya mateso yangu, nani sasa wakutibu matope mwilini mwangu. sina wakumlaumu kadhia mejitakia tope hili lasumu nimezama kwa umbea! sinayo tena hamu, mecheza pata potea meupata ugumu kwa nnayojionea ombea yasikupate,utageuka msongo. niliambiwa ningoje nikaona ni porojo, nikauvaa mtope sasa wanipa kipigo zamishwa mwili wote iliyobaki ni shingo tope flani karaha, kulijua ni vibaya limejua kunihadaa bila soni wala haya chini yake nimekaa, siwezi tena kimbia maumivu majeraha nafsi yangu yajutia mwanzo niliona tamu kuchezea tope hili,  lilinikidhi na hamu, sikuiona shubir...

ASANTENI KWA HISTORIA

Image
"Zaidi ya miaka 50 tangu kufanyike mapinduzi matakatifu visiwani zanzibar, mapinduzi ambayo yamewaweka huru ndugu zetu visiwani humo, hakika historia ya zanzibar imejiandika vema kupitia wana mapinduzi wakiongozwa na Sheikh Abeid Aman Karume na wengine wengi kama vile Okelo na wengineo..leo naifurahia historia ya zanzibar na nawashukuru wanamapinduzi kwa kutuachia historia hii yenye funzo kubwa kwetu, funzo la uzalendo na ujasiri . Na Omar Zongo  Historia ilotukuka, historia ya heshima, historia isofutika, asanteni kwa historia. Meshika kitabu changu aliniachia babu, kitabu cha mapinduzi kina nyingi historia. Kitabu chanikumbusha niishi kwa uzalendo, maovu kuyaondosha nisimamie upendo, upendo wa watu wangu, upendo wa nchi yangu, upendo kwa taifa langu. Asanteni kwa historia. Historia yanifunza nisiishi kiunyonge mgeni nisomuelewa nimfukuze aende. Historia hii tamu, nzuri tena adimu, historia  adhimu, yanipenya kwenye damu. Historia yasema wenyeji walisimama, ha...

NIMEPATA PESA

Image
Na. BinZongo Shida shida sasa basi tayari ninazo pesa! Pesa nyingi za kuzidi sio zile za mawazo. Nabadilisha mavazi, chakula nikipendacho, magari ya kila rangi kampuni tofauti. Jumba langu ni 'palace' mtawala ndio mie Limezingirwa Na fensi, himaya kubwa ijue. Ulinzi imara sana, majambazi halahala! Mabaya mtayavuna mkija kifalafala. Niite bosi, tajiri we mwenyewe siunaona! Yajana siyakumbuki usije yataja tena. Dhiki ndio kitu gani! Habari zakizamani ukinitajia tena shtaka mahakamani. Kwasasa pesa ninayo mpenzi naomba nielewe maamuzi yafuatayo naomba uyatambue Nahisi haunifai, kuishi nawe aibu, japo tumetoka mbali ila sasa Tabutabu. Siwezi tumia nawe pesa hizi pomoni, nataka mtu mwengine nimuingize moyoni Sema nikupe nini ili tuachane leo, tusahau yazamani sasa nimepanda cheo. Umasikini enzi zetu utajiri zama nyengine. Pesa sasa zanitosha kumtafuta mwengine. Ongeza basi mvinyo tuendelee kuongea, hivi sasa nina meno natafuna hili penzi. Tafuta aina y...