MWANAMKENDEGE ; USHAIRI

hadith hadith njoo simulizi lake sikio naanza safisha koo nikupe langu tukio eneo nikariakoo sikujua mwanamkendege ushungi, umbo na guu mahabani kazamia kiunoni kichuguu moyoni nikaridhia yalonisibu makuu sikujua mwanamkendege tabasamu lake lahaja nikaona njia nyeupe amejazia mapaja si mweusi si mweupe Radhia jina kataja sikujua mwanamkendege lafudhi yake yalamu tamko lake murua midomo yake adhimu kicheko kajaaliwa kumbe mja haramu sikujua mwanamkendege sikujua mwanamkendege kuuza yake tabia ucheshi wake nizengwe pesa kushadadia ukiwa nacho twende mwanzoni sikutambua kwa miguu miwili nikazama nae hubani sikutaka subiri kumfikisha nyumbani kumbe ndumilakuwili sikujua mwanamkendege alianzia kwa kaka ushemeji kukataa akasema anataka nayeye kuzima taa mwenzenu yamenifika sikujua mwanamkendege ndugu kunihabarisha nimepotea gizani mie nikakanusha kwamba haiwezekani kaka uongo kazusha sikujua mwanam...